Gravity Omutujju Amaliza Urafiki na King Saha kwa Uchungu Mwingi

Gravity Omutujju Amaliza Urafiki na King Saha kwa Uchungu Mwingi

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini Uganda, Gravity Omutujju, amezungumza kwa mara ya kwanza kwa kina kuhusu kuvunjika kwa urafiki wake na mwanamuziki King Saha, akifichua kuwa hana tena uhusiano wowote naye. Wawili hao walikuwa marafiki wa karibu kwa muda mrefu na walishirikiana katika kibao kilichopata umaarufu kiitwacho “Winner”. Hata hivyo, uhusiano wao uliingia doa mwezi Septemba mwaka jana baada ya King Saha kusherehekea hadharani kufeli kwa tamasha la Gravity, kitendo kilichomvunja moyo na kumwacha na maumivu makali. Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Gravity alisema wazi kuwa hana nia ya kurejesha urafiki huo, licha ya kutokuwa na chuki ya moja kwa moja. “Sina ugomvi naye, lakini si rafiki yangu tena. Sitaki kuwa na uhusiano wowote naye. Tulikuwa marafiki wa dhati, lakini niliumia sana kwa alichokifanya. Siwezi kumsamehe, wala kusahau,” alieleza kwa hisia. Kauli hiyo imezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii, ambapo mashabiki wameonyesha hisia mseto, wengine wakisikitishwa na kuvunjika kwa urafiki huo, huku baadhi wakimuunga mkono Gravity kwa msimamo wake. Ingawa haijulikani iwapo wawili hao wataweza kusameheana na kurejesha urafiki wao wa zamani, kwa sasa, dalili zote zinaonyesha kuwa mlango huo umefungwa kabisa.

Read More
 King Saha aahirisha tamasha lake kutokana na matatizo ya kiafya

King Saha aahirisha tamasha lake kutokana na matatizo ya kiafya

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha ameripotiwa kuahirisha tamasha lake la muziki ambalo lilipaswa kufanyika siku ya wapendanao duniani, Februari 14 mwaka 2023. Duru za kuaminika zidai kuwa mratibu wa tamasha hilo, Promota Musa Kavuma maarufu KT Promotions, pamoja na King Saha walianda mkutano wa faragha ambapo kwa kauli moja waliridhia kuahirisha tamasha hilo hadi pale itakapotangazwa tena. “Haitatokea. Imeahirishwa,” msemaji wa KT Promotions, Eddie Ssendi alithibitisha. Mabadiliko ya Tamasha la King Saha yamehusishwa na hali ya kiafya ya msaniii huyo ambaye alishauriwa na madaktari apumzike kabla ya kuanza tena shughuli zake za muziki.

Read More
 King Saha amshukuru Chameleone kwa kusimama naye wakati wa matatizo

King Saha amshukuru Chameleone kwa kusimama naye wakati wa matatizo

Mwanamuziki King Saha ni mwingi wa shukran kwa kitendo cha Jose Chameleone kutumbuiza kwenye shows zake alizokuwa ameratibu kutoa burudani kwa mashabiki zake. King saha ambaye aliruhusiwa kuondoka katika hospitali ya Nakasero wiki iliyopita ambako alikuwa amelazwa, amefarijika na ukarimu waBosi huyo wa Leone Island kumkingia kifua alipokuwa kwenye matatizo ambapo amemtaja kuwa mtu mwema kuwahi kutokea nchini Uganda kwa upande wa wasanii. “Namshukuru Chameleone kwa ukarimu wake. Namheshimu sana kwa kunifanyia shows zangu nilipokuwa nimelazwa hospitalini,” alisema. King Saha kwa sasa amechukua mapumziko kwenye muziki wake kwa ajili ya kuiweka afya yake sawa kabla ya kuanza shughuli zake rasmi.

Read More
 King Saha akanusha madai ya kutumia mihadarati.

King Saha akanusha madai ya kutumia mihadarati.

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha amejitenga na madai yaliyoibuliwa na Bebe Cool kuwa anatumia mihadarati. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema alihasi matumizi ya dawa za kulevya miaka mingi iliyopita baada ya kugundua kuwa inaathari afya yake. Hitmaker huyo wa “Zakayo”, ameanika tusiyojua kuhusu Bebe Cool kwa kusema kuwa msanii huyo anatumia bangi pamoja na miraa huku akiongeza kuwa alimfunza jinsi ya kutumia dawa za kulevya kipindi cha nyuma. Hata hivyo ametishia kumshambulia Bebe Cool iwapo hataacha tabia ya kumchafulia jina kwenye vyombo vya habari kwa kusema kuwa ana nyimbo nyingi ambazo zipo studio kwa ajili kuanika maovu yote ambayo bosi huyo wa Gagamel amekuwa akifanya kwa siri. King Saha ambaye juzi kati aliondoka hospitalini ambako alikuwa amelazwa baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana, atasalia nyumbani kwa wiki mbili zijazo kwa ajili kujiweka sawa kiafya.

Read More
 Niko tayari kutumbuiza katika shoo zote za King Saha hadi atakapopata nafuu- Chameleone

Niko tayari kutumbuiza katika shoo zote za King Saha hadi atakapopata nafuu- Chameleone

Msanii mashuhuri kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amejitolea kujaza nafasi ya mwanamuziki King Saha katika shoo zake zote alizokuwa ameratibiwa kutumbuiza  hadi atakapopata afueni. Katika mahojiano hivi karibuni, Chameleone amesema yuko tayari kuwapa burudani mashabiki wake bure bila malipo. Bosi huyo wa Leone Island ameeleza kuwa tayari ameanza mazungumzo na meneja wa King Saha aitwaye Mukasa ili kufanikisha hilo. “Sasa hivi mdogo wangu King Saha hayuko vizuri kiafya na tayari nimempigia simu meneja wake, Mukasa kuhusu pendekezo langu. Nitatumbuiza kwenye shoo zake vya alizopewa nafasi bila bila malipo. Huu ni wakati ambao anahitaji wema wetu,” alisema Chameleone. King Saha aliruhusiwa kwenda nyumbani siku ya Jumanne kutoka hospitali ya Nakasero ambapo alishauriwa na madaktari kupumzika kabla ya kuanza tena shughuli zake za muziki.

Read More
 King Saha aripotiwa kulazwa hospitalini

King Saha aripotiwa kulazwa hospitalini

Msanii kutoka King Saha ameripotiwa kulazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali moja nchini nchini Uganda. Hii ni baada ya picha yake kusambaa mtandaoni zikimuonesha akiwa kwenye kitanda cha hospitali akiipambania afya yake. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Uganda, chanzo cha ugonjwa wake haijawekwa wazi ila mashabiki wanaendelea kumtumia salamu za pole apate afueni ya haraka. Ikumbukwe Juzi kati King Saha aligonga vichwa vya habari nchini Uganda baada ya mtangazaji wa radio Brian Mulondo kumtolea uvivu, akimtaka azingatie masuala ya usafi kutokana na harufu mbaya anayotoa mwilini mwake. Ni madai ambayo yalikaririwa na Bebe Cool ambaye alidai kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa akitoa wito kwa vyombo vya habari kuungana naye kwenye kampeini ya kubadili maisha ya King Saha ambaye kwa mujibu wake ni mraibu wa dawa za kulevya.

Read More
 Waandishi wa nyimbo za Bebe Cool ni bandia – King Saha

Waandishi wa nyimbo za Bebe Cool ni bandia – King Saha

Mwanamuziki King Saha ameibuka na kuwachana watu wanaomuanndikia Bebe Cool nyimbo kwa kusema kwamba hawana vipaji kwenye masuala ya uandishi. Kwenye mohajiano yake hivi karibuni King Saha amesema Bebe Cool amewekeza mamilioni ya pesa kwa waandishi wa nyimbo ilhali kazi zake zinachuja haraka. Aidha ameenda mbali Zaidi na kujinadi kuwa huwa anaandika nyimbo 5 kwa mwaka na zote zinaisha kuwa kubwa zaidi kwenye tasnia ya Afrika Mashariki. Baadhi ya waandishi wa nyimbo wanaofanya kazi kwa ukaribu na Bebe Cool ni  pamoja na Yese Oman Rafiki na Ronnie On Dis One. Utakumbuka Bebe Cool na King Saha hawajakuwa na maelewano mazuri kwa muda mrefu na ugomvi wao ulianza kipindi ambacho Bebe Cool alimshauri hitmaker huyo wa Zakayo aachane na matumizi ya mihadarati kwa kuwa itampoteza kimuziki. Tangu wakati King Saha amekuwa akimrushia vijembe Bebe Cool kila mara anapopata nafasi kwenye mahojiano yake mbali mbali.

Read More
 KING SAHA AJITANGAZA RASMI MPYA WA UMA, AJIONGEZA WALINZI

KING SAHA AJITANGAZA RASMI MPYA WA UMA, AJIONGEZA WALINZI

Mwanamuziki kutoka Uganda King Saha amejiongezea usalama baada ya kujitangaza rais mpya wa chama cha wanamuziki Uganda. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Zakayo” amesema amechukua hatua hiyo kutokana na wadhfa huo wa urais kumweka kwenye hatari ya kushambuliwa na wahuni. Msanii huyo aidha amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kwamba alikodisha walinzi kwa hofu ya kushambulia na hasimu wake Bebe Cool ambaye wamekuwa kwenye bifu kwa muda sasa. King Saha alijitangaza kuwa rais wa chama wa wanamuziki uganda baada ya Cindy Sanyu ambaye ni rais wa sasa wa UMA kuendelea na majukumu yake akidai kuwa kuna pengo la uongozi katika chama hicho.

Read More
 KING SAHA AMPA ZA USO BEBE COOL, ADAI NI MCHAWI

KING SAHA AMPA ZA USO BEBE COOL, ADAI NI MCHAWI

Mwanamuziki kutoka Uganda King Saha ameibuka na kumtuhumu msanii mwenzake  Bebe Cool kuwa nii mshirikina. Katika perfomance yake juzi kati King Saha amesema Bebe Cool amekuwa akitumia uchawi kuwashusha wasanii wengine. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Zakayo” amesema hatua ya Bebe Cool kutumia nguvu za giza ni kwa ajili ya kubaki kwa muda mrefu kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda bila kuchuja. Utakumbuka King Saha amekuwa akirushiana maneno makali na Bebe Cool tangu bosi huyo wa Gagamel amshauri aachane na matumizi ya dawa za kulevya mwaka wa 2021.

Read More
 ALLAN HENDRICK AAPA KUANIKA MAOVU YA KING SAHA

ALLAN HENDRICK AAPA KUANIKA MAOVU YA KING SAHA

Msanii Allan Hendrik ameahidi kuanika siri nzito kuhusu baba mzazi wa King Saha iwapo hatoacha kumshambulia baba yake Bebe Cool. Katika mahojiano yake hivi karibuni Hendrick amesema amefanya utafiti na amegundua baadhi ya maovu ambayo baba mzazi wa king saha anajihusisha nayo. Msanii huyo amesema atamuaibisha King Saha akikataa kumtukana bebe cool licha ya baba yake huyo kumpuza kwa muda kwa muda. “I have done my research and discovered some dirty things about his father. I’ll go personal if he refuses to chill my dad. He keeps attacking him despite of ignoring him,” amesema Hendrik. Allan Hendrik tayari ameshaachia nyimbo mbili mbili zinazomtolea uvivu King Saha ambaye amekuwa akimshambulia Bebe Cool kwenye mahojiano mbali mbali. Utakumbuka juzi kati Bebe Cool alimpa ruhusa mwanae huyo apambane na wanaomkosoa kwenye mitandao ya kijamii.

Read More
 EDDY KENZO AAPA KUMALIZA UGOMVI WA KING SAHA NA BEBE COOL

EDDY KENZO AAPA KUMALIZA UGOMVI WA KING SAHA NA BEBE COOL

Staa wa muziki nchini Uganda,Eddy Kenzo amefichua kuwa ugomvi unaoendelea kati ya Bebe Cool na King Saha unamchukiza. Katika mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amesema wasaniii wanapaswa kuacha kutupiana maneno makali mtandaoni na badala yake waungane kwa ajili kuupeleka muziki wĂ  Uganda kimataifa. “I hate the negativity in this industry. I don’t like artists who fight each other. We don’t need a divided industry. We need to grow first and conquer the international market,” Amesema Eddy kenzo ameahidi kuwaleta pamoja King Saha na Bebe Cool ambao wamekuwa kwenye bifu kwa muda mrefu kwa kuwa ni marafiki zake. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Nsimbudde” ameeleza kuwa tasnia ya muziki nchini Uganda bado ni changa hivyo wasanii wanapaswa kuelekeza nguvu zao kubuni njia za kuingiza kipato na kutoa muziki mzuri badala kupigana vita. “I will work to unite the two because I speak to both. Artists ought to know our industry is still young, we should unite and fight brokenness instead of fighting one another,”  Ameongeza King Saha na Bebe Cool wamekuwa kwenye ugomvi tangu bebe cool amshauri aachane na matumizi ya dawa za kulevya la sivyo atapotea kimuziki. King Saha alikasirisha na kauli hiyo ambapo amekuwa akimchana Bebe Cool kwenye mahojiano mbali mbali na hata akaachia disstrack iitwayo Zakayo ambayo inalenga bossi huyo wa Gagamel. Eddy Kenzo kipindi cha nyuma alikuwa kwenye ugomvi na Bebe Cool lakini baadae wakakuja wakamaliza tofauti zao ambapo kwa sasa wana uhusiano mzuri wa kufanya kazi pamoja.        

Read More
 KING SAHA MBIONI KUFUNGA NDOA MBELE YA HASIMU WAKE BEBE COOL

KING SAHA MBIONI KUFUNGA NDOA MBELE YA HASIMU WAKE BEBE COOL

Inaonekana Ugomvi wanamuziki King Saha na Bebe Cool kutoka uganda hautamalizika hivi karibuni. Hii ni baada ya king saha kuibuka na kumtolea uvivu msanii mwenzake Bebe Cool akidai atafanya harusi mbele ya msanii huyo licha ya kuwa anamzidi kiumri. Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha amesema ni aibu kwa mtu kama Bebe Cool kutohalalisha ndoa yake kwa njia ya harusi ikizingatiwa kuwa ana umri mkubwa kumshinda. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Zakayo” amesema atafunga harusi hivi karibuni mara baada ya ujenzi wa nyumba yake kukamilika. King Saha amesema licha ya kuwa ana mpango wa kuhalalisha ndoa yake hivi karibuni, hatamweka wazi mke wake kwa umma kwa faida ya amani yake ya akili. “Bebe Cool was singing when I was in P.1. He is a very old man but stuck in the skin of a young man. I’m sure even my wedding will come before his. I will wed my wife immediately after completing my house,” Amesema King Saha Mjengo wa kifahari wa King Saha umekamilika kwa asilimia 80 na nyumba yake hiyo ipo maeneo ya Nakawuka, katika wilaya ya Wakiso nchini Uganda.

Read More