BEBE COOL AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU BIFU YA KING SAHA NA ALLAN HENDRICK.

BEBE COOL AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU BIFU YA KING SAHA NA ALLAN HENDRICK.

Bebe Cool amekuwa kwenye kiwanda cha muziki Afrika Mashariki kwa kipindi cha miaka 20 bila kupoa. Ni moja kati ya wasanii wakongwe ambao wakiongea chochote kila mtu kwenye tasnia muziki nchini Uganda anamsikiliza licha ya maisha yake kuandamwa na kashfa nyingi. Msaniii huyo ametoa wito kwa kijana yake Allan Hendrik na King Saha wajitenge na vita vya maneno na badala yake wafanya muziki mzuri Hitmaker huyo wa Gyenvudde amesema wawili hao wanapaswa kuelekeza nguvu zao zote kwenye muziki kwani kutupia maneno makali mtandaoni kutawapoteza kimuziki huku akitoa angalizo kwa King Saha aache kutumia dawa za kulevya. “They have time to be productive because they are still young. They should focus on releasing music, they shouldn’t go after one another. I just want to  King Saha stay away from drugs,” Amesema kwenye mahojiano yake hivi karibuni. Mapema wiki hii , Allan Hendrick alithibitisha kuwa hana ugomvi wowote na King Saha licha ya wimbo wake uitwao  ‘matayo’ kuonekana kumlenga moja kwa moja msanii huyo.

Read More
 KING SAHA AMJIBU KISOMI ALLAN HENDRICK

KING SAHA AMJIBU KISOMI ALLAN HENDRICK

Mwanamuziki kutoka Uganda King Saha amethibitisha kuwa hawezi mujibu kijana wa Bebe Cool Allan Hendrick ambaye alimshambulia kupitia wimbo uitwao Matayo ambao aliuachia jumatatu wiki iliyopita. Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha ameeleza adui yake ni Bebe Cool na sio mwanae Allan Hendrick. Msanii huyo amesema Allan Hendrick anatumia jina lake kutafuta umaarufu. “Sitamjibu Hendrick kwa kuwa sijui nia yake. Labda anataka wamzungumzie kwenye vyombo vya habari ila nina shida na Zakayo ambaye Baba yake mzazi”,Alijibu alipoulizwa atoe maoni kuhusu wimbo wa Matayo wake Allan Hendrick. Hata hivyo Hendrick amesisitiza kuwa wimbo wa Matayo ni mahususi kwa ajili ya King Saha na kila kijana ambaye ameathirika na matumizi ya dawa za kulevya

Read More
 KING SAHA KUSUSIA UCHAGUZI WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA UMA

KING SAHA KUSUSIA UCHAGUZI WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA UMA

Hitmaker wa ngoma ya “Zakayo”, Msanii King Saha amehapa kususia uchaguzi wa Chama cha Wanamuziki nchini Uganda kama chama hicho hakitatumia mfumo wa kawaida wakupanga foleni kwenye vituo vya kupiga kura. Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha ameonesha kutofurahishwa na maandalizi ya uchaguzi huo kwa kusema kwamba huenda uongozi wa chama cha UMA unalenga kuiba kura. “Covid-19 iliisha, tunaweza tumia mfumo wa kawaida wakupanga foleni kwenye vituo vya kupiga kura. Nitaambia wafuasi wangu wasusie uchaguzi kama utafanyika kwa njia ya SMS”, Alisema kwenye mahojiano yake Uchaguzi wa Chama cha Wanamuziki nchini Uganda unatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu Mei 23 kwa njia ya SMS ambapo wapiga kura watatumia namba maalum kumpigia kura mgombea wa chaguo lao.  

Read More
 KING SAHA APINGA UCHAGUZI WA CHAMA CHA UMA KUFANYWA KWA NJIA YA KIDIJITALI.

KING SAHA APINGA UCHAGUZI WA CHAMA CHA UMA KUFANYWA KWA NJIA YA KIDIJITALI.

Mwanamuziki King Saha amepinga uchaguzi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA kufanyika kwa njia ya kidijitali. Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha amesema uchaguzi wa chama hicho unapaswa kufanya kwa njia ya kupiga foleni kwenye vituo vya kupigia kura ikizingatiwa kuwa kanuni za kudhibiti msambao wa virusi vya covid-19 zilisitishwa a na serikali. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Zakayo” amesema kuwa huenda uchaguzi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda hukakumbwa na dosari nyingi ikizingatiwa kuwa sajili ya wapiga kura aliyopewa juzi kati haina baadhi ya majina ya wasanii watakaoshiriki uchaguzi  wa chama hicho. Hata hivyo amesema licha ya zoezi la kuwasajili wapigari kura kukamilika wiki 3 zilizopita baado mchakato wa kuwaandikisha  wasanii unaoendesha nyuma ya pazia kitu ambacho amedai huenda ni njema ya Cindy na timu yake kumuibia kura. Utakumbuka uchaguzi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA utafanyika Mei 23 mwaka huu ambaopo King Saha anatarajiwa kumenyana na rais wa sasa wa chama hicho Cindy Sanyu

Read More
 KING SAHA AFUNGUKA KUPATA SHINIKIZO ZA KUJIUNGA NA SIASA

KING SAHA AFUNGUKA KUPATA SHINIKIZO ZA KUJIUNGA NA SIASA

Mwanamuziki kutoka Uganda King Saha amefichua kuwa watu wake wa karibu wameanza kumpa shinikizo za kujiunga na siasa. Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha amesema “Nina majirani ambao kila mara wananisukuma nijiunge na siasa, lakini bado nafakiria juu suala hilo. Huwezi jua, siku moja naweza kuwa mbunge,” King Saha ambaye anagombea wadhfa wa urais katika chama cha wanamuziki nchini uganda UMA huenda anatumia fursa hiyo kujenga misingi yake ya kisiasa ya siku za usoni. Utakumbuka baada ya Bobi Wine kufanya makubwa katika ulingo wa siasa, wanamuziki wengi kutoka Uganda wamekuwa wakijaribu kufuata nyayo zake.

Read More
 KING SAHA AZIDI KUMLILIA BEBE COOL KUUNGA MKONO AZMA YAKE YA KUWA RAIS WA UMA

KING SAHA AZIDI KUMLILIA BEBE COOL KUUNGA MKONO AZMA YAKE YA KUWA RAIS WA UMA

Mwanamuziki King Saha, ambaye anatajwa kuwa Rais ajaye wa Chama cha Wanamuziki nchini Uganda (UMA) ametoa rai kwa msanii mwenzake Bebe Cool kumuunga mkono kwenye azma ya kuwa rais wa wasanii nchini humo kwa sababu ni amekuwa mtu mwema katika jamii. Katika mahojiano na MwanaYouTube mmoja nchini uganda, King Saha ameelezea maisha yake yamebadilika kwa miaka ya hivi karibuni na, yuko tayari kuongoza na kutetea maslahi ya wasanii kupitia chama cha UMA. Mwimbaji huyo amefichua kuwa hajazungumza na Bebe Cool kwa muda mrefu ila anataka wafanye kazi pamoja kwa manufaa ya tasnia ya muziki nchini uganda. King Saha amesema Bebe Cool atakuwa balozi wa kumaliza matumizi ya mihadarati miongoni mwa vijana iwapo atashinda uchaguzi ujao wa chama cha wanamuziki nchini uganda. Utakumbuka Bebe Cool juzi kati alipinga azma ya King Saha kuwa rais wa chama cha wasanii chini Uganda kwa kuwa msanii huyo amekuwa akitumia mihadarati na hivyo hana vigezo vya kuwaongoza wasanii.

Read More
 KING SAHA: NITAKUBALI NIKISHINDWA KWENYE UCHAGUZI WA CHAMA CHA WASANII UGANDA

KING SAHA: NITAKUBALI NIKISHINDWA KWENYE UCHAGUZI WA CHAMA CHA WASANII UGANDA

Mwanamuziki kutoka uganda King Saha amethibitisha kuwa atakubali matokeo ya uchaguzi iwapo atashindwa na Cindy Sanyu katika uchaguzi ujao wa Chama cha Wanamuziki wa Uganda (UMA). Akiongea katika mahojiano na YouTuber mmoja nchini uganda, King Saha ameeleza kuwa hatarajii kama kutakuwa na wizi wa kura kwa kuwa anaamini uchaguzi utakuwa wa huru na haki. “Siasa ni mchezo, kuna kushinda na kushindwa. Nitakubali matokeo ikiwa mchakato wa uchaguzi utakuwa huru na wa haki. Lakini nina matumaini, nitashinda,” alisema katika mahojiano na YouTube mmoja nchini uganda. King Saha anachuana na mwimbaji mwenzake Cindy Sanyu kuwania urais wa Chama cha Wanamuziki wa Uganda.

Read More
 KING SAHA AFUNGUKA KUFANYA KAZI NA SERIKALI YA UGANDA

KING SAHA AFUNGUKA KUFANYA KAZI NA SERIKALI YA UGANDA

Msanii nyota kutoka Uganda King Saha amefunguka na kudai kwamba yuko tayari kufanya kazi na serikali ya nchini hiyo iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa muungano wa Wanamuziki nchini uganda (UMA). Mkali huyo wa ngoma ya “Sivaawo” ameeleza katika mahojiano ya hivi karibuni kuwa ili muungano huo unufaike ni lazima uongozi wa UMA ushirikiane na watekelezaji wa sera. King Saha amesema ana uhakika kwamba uhusiano mzuri na serikali utaleta manufaa kwenye tasnia ya muziki nchini uganda. “Nitashirikiana na kila mtu ana nia njema ya kuboresha tasnia yaa muziki, hata serikali kwa sababu wao ndio watunga sera. Tunahitaji serikali ijumuishe kila mtu katika tasnia sio watu wachache tu,” alisema kwenye mahojiano na YouTuber  mmoja mwishoni mwa juma lilopita . Utakumbuka King Saha anatarajiwa kupambana na rais wa sasa wa muungano wa wasanii nchini Uganda Cindy Sanyu kwenye uchaguzi wa muungano huo ambao utafanyika hivi karibuni.

Read More
 KING SAHA KUMCHAGUA BEBE COOL KUWA MSHAURI WAKE UMA

KING SAHA KUMCHAGUA BEBE COOL KUWA MSHAURI WAKE UMA

Msanii nyota nchini Uganda King Saha amedai kwamba atamchagua Bebe Cool kuwa mshauri wake pindi atakapochaguliwa kuwa rais wa muungano wa wanamuziki nchini humo. Katika mkao na wanahabari King Saha amesema atafanya kazi na wasanii wote bila upendeleo licha ya baadhi yao kupinga azma yake ya kuwa rais wa muungano wa wasanii nchini Uganda. Utakumbuka juzi kati Bebe cool alimponda sana king saha kwa kusema kwamba hana vigezo vya kuwaongoza wasanii kutokana na kuathirika na uraibu wa dawa za kulevya. Mapema wiki hii King saha aliidhinishwa kuwa mmoja wa wagombea wa urais wa muungano wa wasanii nchini Uganda ambapo anatarajiwa kuachuana na Daddy Andre pamoja na Cindy Sanyu ambaye kwa sasa ni rais wa muungano huo.

Read More
 KING SAHA AMJIBU BEBE COOL KWA KEJELI BAADA YA KUPINGA AZMA YAKE YA KUWA RAIS WA MUUNGANO WA WASANII UGANDA

KING SAHA AMJIBU BEBE COOL KWA KEJELI BAADA YA KUPINGA AZMA YAKE YA KUWA RAIS WA MUUNGANO WA WASANII UGANDA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha amejibu madai yaliyoibuliwa na Bebe Cool kuwa hana vigezo vya kuuongoza muungano wa wasanii nchini humo kutokana na kuathirika pakubwa na matumizi ya dawa za kulevya. Kupitia mitandao yake ya kijamii King Saha ameshare video ya Bebe Cool akimzungumzia vibaya na kuweka caption ya kumshukuru kwa kejeli huku akisema kwamba endapo atachaguliwa kama rais wa muungano wa wasanii nchini Uganda atamhudumia msanii huyo bila ubaguzi licha ya kumpinga vikali kwenye azma yake ya kuwa kiongozi wa wasanii. King saha ambaye juzi kati alitangaza kuwania wadhfa wa urais kwenye muungano wa wanamuziki nchini uganda anatarajiwa kuchuana na rais wa sasa wa muungano huo Cindy Sanyu kwenye uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya ambao utafanyika hivi karibuni. Tayari aliyekuwa rais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda Ykee Benda ameunga mkono azma ya King Saha kuwa rais wa muungano huo kwa kusema kwamba anastahili wadhfa huo licha ya kutokuwa maadili mema kama baadhi ya watu wanavyosema mitandaoni.

Read More
 KING SAHA AKIRI KUTUMIA BANGI KWA WINGI KIPINDI CHA KORONA

KING SAHA AKIRI KUTUMIA BANGI KWA WINGI KIPINDI CHA KORONA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha ameingia kwenye headlines mara baada ya kukiri hadharani kuwa alitumia sana bangi kwa wingi kipindi cha corona. Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha amesema asingetumia bangi kwa wingi angeshafariki kitambo au angeshambukizwa virusi vya korona kwani kwa mujibu wake dawa hizo alizitumia kujikinga na hadharani. Kauli ya King Saha imekuja mara baada ya kuwaonya vijana mapema mwaka huu kujitenga na matumizi ya mihadarati kwani ina athari kubwa kwenye maishani yao. Utakumbuka King Saha amekuwa akitajwa kama mmoja wa wasanii wanaotumia sana mihadarati nchini Uganda jambo ambalo lilipelekea msanii Bebe Cool kumuonya hadharani kuacha matumizi ya mihadarati la sivyo atapoteza mweelekeo kwenye muziki wake.

Read More
 KING SAHA AFUNGUKA SABABU ZA KUFELI KWA MIPANGO YA KUFUFUA KUNDI LA GOODLYF CREW

KING SAHA AFUNGUKA SABABU ZA KUFELI KWA MIPANGO YA KUFUFUA KUNDI LA GOODLYF CREW

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha amefunguka sababu za kundi la Goodlife Crew kushindwa kurudi kwenye muziki licha ya mashabiki kushinikiza achukue nafasi ya marehemu, Mozey Radio. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni King Saha amesema licha ya kufanya majaribio ya kufufua kundi hilo kwa kuachia ngoma mbili na member wa Goodlife, Weasel Manizo imekuwa vigumu kwao kufanya kazi pamoja kutokana na kila mmoja kushikika na shughuli zake za kimuziki. King saha ambaye anafanya poa na ngoma yake iitwayo Sivaawo amesema jambo hilo limesambaratisha juhudi ya kuirudisha kundi la Goodlife Crew kwenye ramani ya muziki Afrika Mashariki, hivyo wamekubaliana na Weasel Manizo kwamba watakuwa wanaachia ngoma pindi tu  mashabiki watakapohitajia. Utakumbuka baada ya kifo cha MozeyR mwaka wa 2018 mashabiki wengi wa muziki nchini Uganda walimtaka King Saha achukue nafasi ya radio,kwenye kundi la Goodlife ambapo tuliona King Saha akifanya nyimbo mbili pamoja na Weasel, ambazo ni Mpa Love na Tubikole kama njia ya kujaribu kufufua kundi hilo. Licha ya Nyimbo hizo kupata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki  wawili hao wamekuwa kwenye harakati zake za kufanya muziki kama wasanii wa kujitegemea

Read More