KING SAHA AFUNGUKA SABABU ZA KUFELI KWA MIPANGO YA KUFUFUA KUNDI LA GOODLYF CREW

KING SAHA AFUNGUKA SABABU ZA KUFELI KWA MIPANGO YA KUFUFUA KUNDI LA GOODLYF CREW

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha amefunguka sababu za kundi la Goodlife Crew kushindwa kurudi kwenye muziki licha ya mashabiki kushinikiza achukue nafasi ya marehemu, Mozey Radio. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni King Saha amesema licha ya kufanya majaribio ya kufufua kundi hilo kwa kuachia ngoma mbili na member wa Goodlife, Weasel Manizo imekuwa vigumu kwao kufanya kazi pamoja kutokana na kila mmoja kushikika na shughuli zake za kimuziki. King saha ambaye anafanya poa na ngoma yake iitwayo Sivaawo amesema jambo hilo limesambaratisha juhudi ya kuirudisha kundi la Goodlife Crew kwenye ramani ya muziki Afrika Mashariki, hivyo wamekubaliana na Weasel Manizo kwamba watakuwa wanaachia ngoma pindi tu  mashabiki watakapohitajia. Utakumbuka baada ya kifo cha MozeyR mwaka wa 2018 mashabiki wengi wa muziki nchini Uganda walimtaka King Saha achukue nafasi ya radio,kwenye kundi la Goodlife ambapo tuliona King Saha akifanya nyimbo mbili pamoja na Weasel, ambazo ni Mpa Love na Tubikole kama njia ya kujaribu kufufua kundi hilo. Licha ya Nyimbo hizo kupata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki  wawili hao wamekuwa kwenye harakati zake za kufanya muziki kama wasanii wa kujitegemea

Read More
 KING SAHA ATANGAZA KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA, AWASHAURI VIJANA KUJITENGA NA DAWA HIZO

KING SAHA ATANGAZA KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA, AWASHAURI VIJANA KUJITENGA NA DAWA HIZO

Inaonekana mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha ameanza kuwa mtu mwema hii ni baada ya kukiri hadharani kuwa ameachana kabisa na matumizi ya mihadarati. Katika  mahojiano yake hivi karibuni King Saha amethibitisha kuacha kutumia madawa ya kulevya na badala yake amehamua kuelekeza nguvu zake zote kwenye suala la kuiweka mwili wake sawa na pia kuboresha muziki wake ambao umekuwa ukisuasua katika siku za hivi karibuni. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sala Pulesa” amewashauri vijana kujitenga na masuala ya kutumia dawa za kulevya kwani matumizi ya dawa hizo ni hatari kwa maisha ya binadamu. Utakumbuka mwaka wa 2020 Bebe Cool alimshauri King Saha aache suala la kutumia  mihadarati kwani inaathiri kazi zake za muziki lakini msanii huyo hakupokea vyema ushauri huo ambapo alienda mbali zaidi na kumshambulia bebe cool kwa kusema kuwa anamuonea wivu hivyo hapaswi kuingilia maisha yake.

Read More