Krg The Don ajitolea kumsaidia Director wa video za muziki nchini Kenya Tiger Mind Vision

Krg The Don ajitolea kumsaidia Director wa video za muziki nchini Kenya Tiger Mind Vision

Mwanamuziki wa dancehall nchini Krg The Don ameamua kujitolea kumsaidia mwongozaji wa video nchini Tiger Mind Vision ambaye anadaiwa kuwa hana makaazi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Krg the Don amewataka watu walio na ukaribu na Tiger Mind Vision wawasiliane naye ili aweze kufanikisha mchakato mzima wa kumsaidia. “Someone put me in contact wirth Dir, Tyga or Tell him to come to Casavera lounge from 4pm We see how we can help”, Ameandika instastory. Kauli ya Bosi huyo wa Cash group Entertainment inakuja mara baada ya Picha za Tiger Motions kusambaa mtandaoni akiwa anaisha maisha ya uchochole kutokana na kukosa makaazi ya kuishi. Utakumbuka Tiger Motion ni moja kati ya waongozaji wa video za muziki nchini aliyeacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini kupitia video za nyimbo kama Mama ya Bahati, Lala Salama ya Willy Paul, Ndio yako ya Gloria Muliro, Tenda Wema ya Ringtone na nyingine nyingi.

Read More
 KRG THE DON AKANUSHA TUHUMA ZA KUFANYA BIASHARA YA ULANGUZI WA PESA

KRG THE DON AKANUSHA TUHUMA ZA KUFANYA BIASHARA YA ULANGUZI WA PESA

Msanii asiyeishiwa na matukio kila leo kutoka Kenya KRG The Don amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa anajihusisha na biashara ya ulanguzi wa pesa bandia (Wash Wash). Akipiga stori na Mpasho hitmaker huyo wa “Wano” amesema madai hayo hayana ukweli wowote bali yaliibuliwa na watu wanaomuonea wivu kutokana na mafanikio ambayo ameyapata akiwa na umri mdogo. Bosi huyo wa Cash Group Entertainment amesema anamiliki biashara mbali mbali ambazo zinamuingizia kipato ambacho kinafadhili maisha yake ya kifahari. Hata hivyo amemalizia kwa kusema kuwa utajiri wake wa sasa umechangiwa pakubwa na hatua ya yeye kuwakimbia marafiki wabaya ambao kipindi cha nyuma alikuwa anatumia nao pesa kiholela kwa kujihusisha na vitendo vya anasa.

Read More
 KRG THE DON AAMBULIA MATUSI MTANDAONI KISA BEI YA MAFUTA

KRG THE DON AAMBULIA MATUSI MTANDAONI KISA BEI YA MAFUTA

Mwanamuziki KRG The Don amejipata pabaya kwenye mitandao ya kijamii baada ya wakenya kumshambulia kwa madai ya kuwavunjia heshima kutokana na hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya mafuta. Kwenye ujumbe wake aliochapisha kwenye mtandao wa Instaram KRG aliwataka wakenya waache kulalamika kuhusu bei ya mafuta kupanda ikizingatiwa kuwa wengi wao hawamiliki magari yanayohitaji bidhaa hiyo muhimu. Hakuishi hapo alienda mbali zaidi na kuwaponda wakenya kwa kusema kuwa kulalamika kwao kumewafanya watu kuhisi wanapitia maisha magumu wakati sio kweli. “Unalalamika mafuta imepanda na hauna gari? Sisi watu tuko na 6.3L engine na German machines hatulalamiki. Unalalamika na unatembea na slippers yako na footsubishi? Nyinyi ndio mnafanya nchi ikae ni kama watu wanateseka na watu hawateseki.” Ameandika Sasa ujumbe huo umeonekana kuwakera watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wameshushia kila aina matusi msanii huyo huku wakisema bei ya mafuta inamuathiri kila mkenya bila kuzingatia utajiri alionao. Hata hivyo wamemalizia kwa kumtaka KRG The Don aanze kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji katika jamii kama kweli ana utajiri mkubwa badala ya kuisha maisha ya kuigiza kwenye mitandao ya kijamii. Utakumbuka juzi kati Serikali ya rais William Ruto iliondoa ruzuku ya mafuta kwa sababu imekuwa haiwasaidii raia wa Kenya wanaoendelea kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha

Read More
 KRG THE DON AWEKA WAZI THAMANI YA UTAJIRI WAKE

KRG THE DON AWEKA WAZI THAMANI YA UTAJIRI WAKE

Msanii asiyeishiwa na vituko kila leo Krg the Don amejigamba kuwa ana utajiri wa kima cha kati ya shillingi billioni 6 na 8 za Kenya. Katika mahojiano yake bosi huyo Cash Group Entertainment amesema katika kipindi cha miaka kumi ijayo thamani ya mali yake itakuwa imeongezeka hadi shillingi trillioni moja za Kenya kwani anazidi kuwekeza kwenye nyanja mbali mbali itakakayomuingizia kipato zaidi. KRG ambaye anafanya vizuri na singo yake mpya “Wano” amesema mafanikio makubwa ambayo ameyapata akiwa na umri mdogo ndio yamewafanya baadhi ya watu kuanza kumchukia na hata kumzushia tuhuma za uongo mitandaoni, jambo ambalo amedai alitamkatisha tamaa kwenye suala la kujitafutia riziki na kuishi maisha yake ya kifahari. Utakumbuka katika siku za hivi karibuni utajiri wa msanii huyo umekuwa ukitiliwa shaka huku wengi wakihoji kwamba huenda chanzo cha utajiri wake umetokana na yeye kushiriki kwenye biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya madai ambayo amekuwa akipuzilia mbali.

Read More
 NDOA YA KRG THE DON NA MKEWE LINAH WANJIRU LAFIKIA KIKOMO

NDOA YA KRG THE DON NA MKEWE LINAH WANJIRU LAFIKIA KIKOMO

Ndoa ya Krg The Don na mke wake Linah Wanjiru imevunjika rasmi baada ya miaka 8. Hii ni kufuatia mahakama kutangaza rasmi kwamba Krg anaweza kuendelea na maisha yake ya U-single. Pia mahakama hiyo imeliondoa jina la Krg kwenye majina matatu ya Linah Wanjiru  baada ya mchakato wa talaka kukamilika wiki hii. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Krg ameshabiki hatua hiyo ya mahakama akisema kwamba watashirikiana kutoa matunzo kwa watoto wao huku akimtakia kila la heri aliyekuwa mke wake Linah Wanjiru kwenye maisha yake mapya. Ikumbukwe, wawili hao wamedumu kwenye ndoa kwa takribani miaka 8 na wamebarikiwa kupata watoto wawili.

Read More
 KRG THE DON ADOKEZA KUANZA ZIARA YA MUZIKI NJE YA KENYA

KRG THE DON ADOKEZA KUANZA ZIARA YA MUZIKI NJE YA KENYA

Msanii wa dancehall nchini KRG The Don amefunguka tusiyoyajua kuhusu muziki wake. Katika mahojiano yake hivi karibuni amesema alilazimika kusitisha ziara yake ya muziki nje ya Kenya kwa sababu migogoro iliyokuwa inazingira ndoa yake mapema mwaka huu. Hitmaker huyo wa Ushasema amesema kwa sasa ametatua changamoto zilizokuwa zinamuandama kipindi cha nyuma, hivyo yupo mbioni  kuanza kufanya ziara yake ya kimuziki kimataifa. Katika hatua nyingine amewachana wasanii wa nyimbo za injili nchini waache unafiki na badala yake waugeukia muziki wa kidunia ambao una pesa nyingi. KRG amesema hayo alipotua nchini akitokea Sudan Kusini ambako alienda kutumbuiza kwenye moja ya show aliyokuwa amealikwa wikiendi hii iliyopita.

Read More
 KRG THE DON AWAPA SOMO MASHABIKI ZAKE

KRG THE DON AWAPA SOMO MASHABIKI ZAKE

Msaniii Krg the Don ametoa angalizo kwa mashabiki zake kutofuata au kuamini kile anachokiweka mtandaoni. Katika mahojiano hivi karibu bosi huyo Cash Group Entertainment amesema hayuko mtandaoni kuwafurahisha au kuwashauri watu, hivyo wasichukulie kwa uzito kila kitu anachokiandika mtandaoni kwani inaweza kuwasababishia matatizo. Kauli ya Krg The Don imekuja mara baada ya watu kumkosoa mtandaoni kufuatia kitendo chake cha kuweka hadharani taarifa ya mpesa yake inayoonesha kuwa ametumia kiasi cha shillingi millioni 10 za Kenya katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Hatua hiyo ilikosolewa na wengi wakimtaka Krg The Don aache kuwapotosha vijana kwa kuwafanya wajiingize kwenye visa vya uhalifu kwa ajili ya kujipatia kipato.

Read More
 KRG THE DON AONYESHA JEURI YA PESA KWA MASHABIKI

KRG THE DON AONYESHA JEURI YA PESA KWA MASHABIKI

Msanii wa muziki wa dancehall nchini Krg The Don ameamua kutuonyesha jeuri ya pesa anazozitolea jasho kila kuchao kwenye shughuli zake za kibiashara. Kupitia instastory kwenye mtandao wa instagram Krg ameshare taarifa ya mpesa yake inayoonesha kuwa ametumia kiasi cha shillingi millioni 10 za Kenya katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Katika taarifa yake hiyo amebainisha kuwa kwa wastani anatumia takriban millioni 1.6 kwa mwezi kwenye matumizi yake ya binafsi jambo ambalo limezua gumzo mtandaoni miongoni mwa wakenya. Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wamemtaka Krg The Don aache kuwapotosha vijana kwa kuwafanya wajiingize kwenye visa vya uhalifu kwa ajili ya kujipatia kipato huku wengine wakionekana kumtolea uvivu msanii huyo kwa madai ya kutumia suala hilo kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni.

Read More
 KRG THE DON AWAJIA JUU VIJANA WANAOTUMIA SHENG NCHINI KENYA

KRG THE DON AWAJIA JUU VIJANA WANAOTUMIA SHENG NCHINI KENYA

Mwanamuziki KRG the Don amewatolea uvivu vijana wanaotumia lugha ya Sheng yenye maneno yasiyoeleweka nchini Kenya. Kulingana na KRG, kundi la vijana wanaotumia lugha hiyo ni malimbukeni ambao wana fikra za kikoloni. “Hiyo ni ujinga, hiyo ni primitivity of the highest order! …iko sheng ile poa… You are going backwards !… ata kama mtu alikua anataka kukuambia anakupenda umuambie nakulombotov, si anaenda kama stima…,” Krg amesema kwa masikitiko. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Ushasema” amewataka vijana wajifunze mambo yatakayowasaidia maishani badala ya kutumia lugha isiyokuwa na mashiko kwenye jamii. “Hizo vitu vijana wametoka sijui wamevuta gum…wanaamka wanaanza kuongea vitu sasa ata ukiulizwa hizo vitu…itawasaidia nini?  Utatoka na hiyo vitu uende utafute kazi gani ? Mi naoana hiyo ni kama kurudi reverse kwa Maisha. Kwa sababu badala ujue lugha yenye unaeza kuongea, Ata si afadhali ujifunze kiChinese… Ukiongea Kichenese, sa hizi watu karibu 1. Something billion wananongea Kichenese, unaeza enda ata china ukafanya kazi ,sasa ukianza kuongea vitu yenye ni wewe na beshtee yako munaelewa,”…Amesema KRG Kauli yake imekuja mara baada ya msanii Jeshi Jinga na Madocho kuingia kwenye bifu ya ni nani hasa ndiye muasisi wa lugha bora ya sheng nchini Kenya. Sheng ni lugha legevu isiyozingatia kanuni za kisarufi ambayo mara nyingi huzungumzwa na vijana wengi nchini Kenya kwa kuchanganya Kiswahili na Kingereza pamoja na lugha za ndani vile Kikuyu,Kijaluo na nyingine nyingi.

Read More
 KRG THE DON AFUFUA BIFU YAKE NA KUNDI LA SAILORS GANG

KRG THE DON AFUFUA BIFU YAKE NA KUNDI LA SAILORS GANG

Msanii wa  muziki nchini KRG The Don amefufua tena bifu yake na wasanii wa sailors gang siku chache baada msanii wa kundi hilo Cocos Juma kudai kuwa lebo ya Black Market Records imesambaratisha muziki wao. Kupitia ukurasa wake wa instagram KRG The Don amesema aliwaonya wasanii wa sailors gang kuhusu muziki wao lakini walimchukulia poa huku akienda mbali zaidi na kusema kwamba tamaa ya kutaka maisha ya haraka ndio imewaponza wasanii hao jambo ambalo analodai lilipelekea kuingia mkataba na lebo ya Black Market Records ambayo iliwapoteza kimuziki. Bosi huyo wa Cash group Entertainment amedai masaibu yanayowaandama wasanii wa Sailors ni kutokana na kiburi waliowaonyesha wadau wa muziki nchini kipindi walipata umaarufu kubwa kwenye tasnia ya muziki nchini. Hata hivyo amewataka wasanii wa Sailors Gang kuwaomba msamaha watu waliowadharau kipindi cha nyuma ili njia zao zianze kufunguka Ikumbukwe KRG The Don na Sailors Gang waliachia  wimbo  wa pamoja uitwao “Nyandus” mwaka wa 2019 lakini lilopokuja suala la kutayarisha video walizozana kuhusiana na ishu ya malipo  na hivyo  ikasambaratisha  mpango wa kuiachia video  rasmi ya wimbo huo.

Read More
 KRG THE DON AZINDUA MAISHA POA APP INAYOJIHUSISHA NA MICHEZO YA KUBASHIRI

KRG THE DON AZINDUA MAISHA POA APP INAYOJIHUSISHA NA MICHEZO YA KUBASHIRI

Mwanamuziki wa Dancehall kutoka Kenya, KRG The Don amezindua programu ya simu inayojihusisha na michezo ya kubashiri iitwayo Maisha POA App, inayolenga kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi. Katika mkao na wanahabari KRG The Don amesema app hiyio ambayo inapatikana Google Playstore kwa watumiaji wa mfumo wa Android itatoa fursa kwa vijana kujishindia shillingi millioni 1.2 kwa siku. Msanii huyo amesema mtumiaji atatakiwa kulipa shillingi 100 kujiandikisha na kadri mtu anavyozidi kujiandikisha anajitengeneza mazingira ya kushinda pesa taslimu kupitia droo ambayo itafanyika kila siku. Hata hivyo KRG amewakikishia mashabiki zake pamoja na wakenya kwamba app hiyo imeidhinishwa na bodi inayodhibiti michezo ya kubashiri nchini, hivyo haihusiki kivyovyote na masuala ya kuwatapeli watu. Maisha Poa ni app ambayo ipo chini ya kampuni ya Pepe Mtanii ambayo inalenga kuwasaidia vijana kuboresha maisha yao kupitia michongo mbali mbali.

Read More
 BIFU LA KRG THE DON NA KUNDI LA MBOGI GENJE LACHUKUA SURA MPYA

BIFU LA KRG THE DON NA KUNDI LA MBOGI GENJE LACHUKUA SURA MPYA

Inaonekana bifu ya Mbogi Genje na Krg The Don haitapoa hivi karibuni hii ni baada ya wasanii wa kundi hilo kuibuka na kumchana Krg The Don kutokana na kauli aliyotoa majuzi kuwa wasanii wa mbogi genje ni wasanii wa mashinani. Wakiwa kwenye moja ya Interview wasanii hao wakiongozwa na Militant wamesema Krg The Don aache kujipiga kifua kuwa ni msanii wa kimataifa wakati ana idadi ndogo ya wafuasi kwenye mitandao kustream muziki duniani huku wakisema kama kweli Krg The Don angekuwa na pesa angewalipa baada ya kufanya nao kolabo kupitia wimbo wa Zible. Wasanii hao wa Mbogi Genje wameenda mbali zaidi na kusema kuwa hawana muda wa kupishana na Krg The Don ila hawakufurahishwa na hatua ya msanii huyo kukiuka mkataba wa maelewano kuhusu umiliki wa wimbo wa Zible baada ya kupakia video ya wimbo huo kwenye Youtube channel yake bila ridhaa yao. Mapema wiki Krg The Don aliibuka na kuwachana wasanii Mbogi Genje kuwa hawakugharamia chochote kwenye mchakato wa kuandaa audio na video wa wimbo wa Zible,  hivyo hawana haki ya kudai umiliki wa wimbo huo. Hii ni baada ya mbogi genje kudai kuwa Krg The Don aliwasiliti baada ya kukiuka mkataba wa maelewano kuhusu umiliki wa wimbo wa Zible alipoahamua kupakia video wa wimbo huo kwenye channel yake ya youtube bila idhini yao

Read More