KRG THE DON AWATOLEA UVIVU WASANII WA MBOGI GENJE KWA KUDAI WIMBO WA ZIBLE NI WAO

KRG THE DON AWATOLEA UVIVU WASANII WA MBOGI GENJE KWA KUDAI WIMBO WA ZIBLE NI WAO

Mwanamuziki wa dancehall nchini KRG The Don amenyosha maelezo kuhusu umiliki wa wimbo wa Zible aliowashirisha wasanii wa kundi la Mbogi Genje baada ya kundi hilo kudai kuwa KRG aliiba ubunifu wao. Katika mahojiano yake hivi karibuni KRG The Don amesema wasanii wa Mbogi Genje hawakugharamia chochote kwenye mchakato wa kuandaa wimbo huo, hivyo hawana haki ya kudai mirabaha ya wimbo wa Zible. KRG The Don amewatolea uvivu wasanii wa Mbogi Genje kwa kutumia lugha isiyokuwa na mashiko kuwasilisha ujumbe kwa mashabiki, kitu ambacho amedai kuwa imekuwa kizingiti kwa muziki wao kusikilizwa na watu wa umri wote katika jamii. Hitmaker huyo wa “Full kishunzi” amepuzilia mbali madai ya wasanii wa Mbogi Genje kuwa walimuandikia wimbo wa zible kwa kusema kwamba madai hayo hayana msingi wowote kwani alihusika pakubwa kuandika wimbo huo bila usaidizi wa mtu yeyote. Kauli ya KRG The Don imekuja mara baada ya wasanii wa kundi la mbogi genje kumtuhumu kuwa alishindwa kuwalipa alipowashirikisha kwenye wimbo wake uitwao Zible ambapo walienda mbali zaidi na kusema kwamba wao ndio walihusika kwa asilimia moja kwenye uandishi wa wimbo huo.

Read More
 KRG THE DON ASHAMBULIWA MTANDAONI KISA KUTIA NIA YA KUJIUNGA NA SIASA ZA UCHAGUZI MKUU NCHINI KENYA

KRG THE DON ASHAMBULIWA MTANDAONI KISA KUTIA NIA YA KUJIUNGA NA SIASA ZA UCHAGUZI MKUU NCHINI KENYA

Walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamemshambulia mwanamuziki wa dancehall nchini KRG The Don mara baada ya msanii huyo kuomba ushauri awanie kiti gani cha kisiasa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9. Kupitia instagram page yake KRG The Don alidai kuwa amekuwa akipokea shinikizo kutoka kwa marafiki zake wa karibu kujiunga na siasa. Sasa kupitia uwanja wa comment wa post yake mashabiki wamemtolea uvivu Krg The Don wakisema kuwa hapaswi kuwania kiti chochote cha kisiasa kwani hana  kabisa vigezo vya kuwa kiongozi. Haikushia hapo wameenda mbali zaidi na kumshauri KRG The Don aendelee kufanya muziki wa Gengetone huku wengine wakidai kuwa msanii huyo anajaribu kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye media ikizingatiwa kuwa muziki umemshinda.

Read More
 MENEJA WA KUNDI LA MBOGI GENJE AMVUA NGUO KRG THE DON KISA KUWAADA WAKENYA

MENEJA WA KUNDI LA MBOGI GENJE AMVUA NGUO KRG THE DON KISA KUWAADA WAKENYA

Meneja wa kundi la Mbogi Genje Eastlando President amemtolea uvivu msanii KRG The Don kwa madai ya kuwadanganya wakenya kuwa yeye ndiye mmliki wa ukumbi wa burudani wa Casavara. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Eastlando president amesema kuwa mmiliki halisi waCasavara ni msanii wa dancehall kutoka jamaica Konshens ila KRG amepewa kazi ya kuipromote ukumbi huo wa starehe. Eastlando President ameenda mbali kumtaka KRG aache suala la kujigamba na badala ajifunze kuwa heshimu watu wengine kwani pesa ambazo analipwa na konshens zimempa kiburi. Kauli ya Eastlando president imekuja mara baada ya KRG The Don kushindwa kuwalipa wasanii wa kundi la Mbogi Genje pesa zao baada ya kuwashirikisha kwenye wimbo wake uitwao Zible ambao ulikuwa umefutwa kwenye mtandao kwa madai ya hakimiliki.

Read More
 WIMBO MPYA WA MSANII KRG THE DON WAFUFTWA YOUTUBE KWA MADAI YA HAKIMILIKI

WIMBO MPYA WA MSANII KRG THE DON WAFUFTWA YOUTUBE KWA MADAI YA HAKIMILIKI

Mwanamuziki KRG The Don amepata pigo baada ya wimbo wake uitwao Zible aliyomshirikisha msanii wa kundi la Mbogi Genje, Guzman kuondolewa kwenye mtandao wa Youtube kwa madai ya hakimiliki. Kulingana na ujumbe ambao KRG alishare kwenye ukurasa wake wa instagram wimbo huo ulifutwa na msanii chipukizi aitwaye Zoja K Worldwide ambaye anadai kuwa KRG alisample mdundo wake na akautumia kwenye wimbo wake , Zible na Guzman wa Mbogi Genje. Hitmaker huyo wa “Giddem” amewakosoa washindani wake akidai kuwa wanauone  muziki wake wivu huku akiwataka mashabiki zake wawe na subra wakati huu uongozi wake unaifanyia kazi  suala la kurejesha wimbo wake wa zible kwenye mtandao wa youtube. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na krg wakidai kuwa msanii huyo huenda msanii huyo amefuta wimbo huo mwenyewe ili azungumziwe kwenye mitandao ya kijamii ikizingatiwa kuwa amekuwa akipenda kujihusisha sana na kiki.

Read More
 KRG THE DON ATANGAZA KUWASAJILI WASANII WAPYA KWENYE LEBO YAKE YA FAST CASH GROUP MUSIC

KRG THE DON ATANGAZA KUWASAJILI WASANII WAPYA KWENYE LEBO YAKE YA FAST CASH GROUP MUSIC

Msanii wa muziki wa dancehall nchini KRG The Don ametangaza mpango wa kuwasajili wasanii wapya kwenye lebo ya muziki ya Fast Cash Group music. Kupitia ukurasa wake wa instagram KRG The Don amewataka mashabiki zake wamuunganishe na wasanii wenye vipaji kwenye muziki kwani lebo ya fast cash Group ipo tayari kuwasaidia kimuziki. Hata hivyo amewataka mashabiki na wasanii chipukizi waendelee kufuatilia mitandao ya kijamii ya Fast Cash Group kwa lebo hiyo itatoa tamko rasmi hivi karibuni ya kufanikisha mchakato mzima wa kuwasajili wasanii. “Lebo ya muziki ya Fast Cash Group ina habari njema kwa wasanii wachanga wenye vipaji kama unamjua msanii ambaye ana kipaji mwaambie kwamba lebo ya Fast Cash Group ipo tayari kumsaidia kimuziki ila kwa sasa endeleeni kufuatilia Fast Cash Group music kupitia mitandao yetu ya kijamii mwaka huu tuna mazuri kwa ajili yenu” amesema KRG The Don kupitia Instagram page yake. Utakumbuka lebo ya muziki ya Fast Cash Group ambayo makao yake makuu yapo South B jijini Nairobi ilizinduliwa miaka saba iliyopita na  KRG The Don  kwa ajili ya kurekodi kazi za wasanii na muziki wake mwenyewe.

Read More
 KRG THE DON ADAI ALIHUSIKA KWENYE UDUKUZI WA AKAUNTI YA INSTAGRAM YA MWANABLOGU EDGAR OBARE

KRG THE DON ADAI ALIHUSIKA KWENYE UDUKUZI WA AKAUNTI YA INSTAGRAM YA MWANABLOGU EDGAR OBARE

Mwanamuziki kutoka Kenya KRG The Don amedai kwamba yeye ndiye aliifuta akaunti mpya ya instagram ya mwanablogu mwenye utata nchini humo Edgar Obare. Kupitia instagram page yake KRG ameandika ujumbe wa kejeli kwenda kwa wafuasi wa Edgar Obare kwa kusema kwamba alikuwa ametishia kuifuta akaunti ya mwanablogu huyo ya Instagram ila watu walichukulia kama mzaha. “I had said i will delete BNNKE for this planet they though I was joking” ..alisema  KRG The Don kupitia Instagram yake. Hata hivyo wafuasi wa KRG The Don wameonekana kutofauti kimawazo na msanii huyo kwa kusema kwamba wanamjua aliyedukua akaunti ya Instagram ya Edgar Obare. Utakumbuka KRG The Don aliingia kwenye ugomvi na Edgar Obare baada ya mwanablogu huyo kuchapisha taarifa akihoji kuwa utajiri wa mwanamuziki huyo umetokana na biashara ya ulanguzi wa pesa ambayo amekuwa akifanya kwa muda. Akaunti ya kwanza ya Instagram ya Edgar Obare ilifutwa mara baada ya mwanablogu huyo kuwa kero kwa mastaa mbali mbali nchini kwa kuanika maovu yao yote kupitia ukurasa wake huo. Jaribio lake la kuirejesha akaunti yake ya kwanza ya Instagram iligonga mwamba na ndipo akafungua akaunti nyingine ambayo juzi kati  ilidukuliwa na mtu asiyejulikana ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wanahoji kuwa ni mchekeshaji Jalang’o ndiye alidua akaunti  hiyo kwani hajakuwa na maelewano mazuri na Edgar Obare.

Read More
 KRG THE DON ATHIBITISHA UJIO WA KOLABO YAKE NA MKALI WA DANCEHALL KUTOKA JAMAICA KONSHENS

KRG THE DON ATHIBITISHA UJIO WA KOLABO YAKE NA MKALI WA DANCEHALL KUTOKA JAMAICA KONSHENS

Habari nzuri kwa mashabiki wa muziki nchini ni kwamba tutarajie muda wowote ujio wa Collabo kati ya mwanamuziki KRG The Don na Star wa muziki wa dancehall duniani Konshens. Kupitia insta story ya KRG The Don kwenye mtandao wa Instagram ameshare taarifa hiyo nzuri kwa mashabiki na wadau wa muziki nchini kwa kuthibitisha kuwa tayari wawili hao wamefanya kazi ya pamoja. Endapo collabo hiyo itatoka itamfanya KRG The Don kuwa msanii wa pili nchini baada ya Ethic Entertainment kufanya kazi ya pamoja na mwanamuziki huyo nyota kutoka Jamaica. Itakumbukwa kwenye mkesha wa kuamkia mwaka mpya 2022 Konshens alipiga shoo ya kufa mtu kwenye onesho la NRG Wave Concert, shoo ambayo iliyoaacha wapenzi wa muziki mzuri wa dancehall wakitaka burudani zaidi kutoka mkali huyo

Read More
 SAKATA LA NDOA YA MSANII KRG THE DON LACHUKUA SURA MPYA

SAKATA LA NDOA YA MSANII KRG THE DON LACHUKUA SURA MPYA

Sakata la ndoa ya msanii KRG The Don  na mkewe Linah wanjiru linaendelea kuwaka moto. Mtandao wa Nairobi gossip umeripoti kwamba, Linah Wanjiru ameorodhesha kiasi ambacho anataka alipwe na KRG The Don baada ya kuachana.  Linah amesema anahitaji kiasi cha shillingi elfu 350  za kenya kwa mwezi kwa ajili ya matunzo yaani Spousal Support. Linah ambaye amezaa motto mmoja na KRG The Don, anayatolea macho mamilioni ya pesa ya msanii huyo wa muziki ambapo pia amemtaka amlipie ada ya mawakili wake kwa ajili ya mchakato mzima wa kufungua shauri la talaka miezi michache iliyopita.

Read More
 KRG THE DON AFUNGUA SHAURI LA TALAKA MAHAKAMANI

KRG THE DON AFUNGUA SHAURI LA TALAKA MAHAKAMANI

Msanii wa muziki wa dancehall nchini KRG The Don amefungua shauri la talaka mahakamani dhidi ya mke wake Linah Wanjiru, shauri hilo limefunguliwa katika Mahakama ya Milimani Jijini Nairobi. KRG ameweka wazi hilo kupitia instagram page yake baada ya kupost  nyaraka za kisheria kuhusiana na mchakato wa talaka na kusindikiza na caption inayosomeka “kwa wale waliyokuwa wanachukulia kwa mzaha, poleni” Hitmaker huyo Giddem alifunga ndoa na mke wake huyo mwaka wa 2014 na wamejaliwa kupata wawili kwa pamoja. Hatua ya KRG kufungua shauri la talaka dhidi mke wake inakuja siku chache baada ya kumsuta vikali mke wake huyo kwa madai ya kujihusisha sana na anasa na kusahau kuwahudumia watoto wao.

Read More
 KRG THE DON ATHIBITISHA KUACHANA NA BABY MAMA WAKE.

KRG THE DON ATHIBITISHA KUACHANA NA BABY MAMA WAKE.

Baada ya uvumi wa wiki kadhaa,  Msanii wa muziki wa Dancehall nchini KRG The Don hatimaye amethibitisha kuwa yeye na mke wake sio wapenzi tena. KRG ameweka wazi hilo kupitia Instagram page yake baada ya kupost picha ya mke wake huyo na kusindikiza na caption inayoashiria kuwa wameachana rasmi. Hitmaker huyo “Giddem” amemsuta vikali mke wake huyo kwa madai ya kujihusisha sana na anasa na kusahau kuwahudumia watoto wao. KRG pia ametumia fursa hiyo kukanusha madai yanayosambaa kwenye mitandao kuwa alitoka nje ya ndoa yake na ndio maana uhusiano wake na Baby mama wake ulivunjika. Hata  hivyo, bado haijabainika kama kuna ukweli wowote kuhusu stori za wawili hao kuachana ila kwa sasa wamefuta picha zote walizowahi kupiga wakiwa pamoja kwenye mtandao wa Instagram.

Read More