Marioo Ajivunia Kuleta Sound Mpya Afrika Mashariki
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Marioo, amesema anajivunia kuwa miongoni mwa wasanii walioweza kuleta sound mpya katika ukanda wa Afrika Mashariki, hatua ambayo imemuwezesha kutengeneza hits kadhaa. Akizungumza na Mpasho akiwa nchini Kenya, Marioo amesema kuwa sound aliyotumia kwenye nyimbo zake “Oluwa,” “Hahaha,” na “Dunia” zinafanana kwa sababu zimetengenezwa kwa mtindo mmoja aliouamini tangu mwanzo. Kwa mujibu wake, uamuzi wa kusimamia sound hiyo ulimsaidia kutoa hit tatu mfululizo. Marioo amesema mafanikio hayo yamempa imani kubwa kuwa yeye ndiye aliyeileta sound hiyo kwa mara ya kwanza katika soko la muziki la Afrika Mashariki, akisisitiza kuwa kujiamini na ubunifu ndivyo nguzo kuu za mafanikio yake. Kauli ya Marioo imeendelea kuzua gumzo miongoni mwa wadau wa muziki, wengi wakimtaja kama msanii mwenye maono mapya na mchango mkubwa katika mabadiliko ya sound ya Bongo Fleva na muziki wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
Read More