Mr Nice Amkosoa Dudu Baya kwa Kuwatukana Wasanii Wakongwe
Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Mr. Nice amemshambulia kwa maneno mazito Dudu Baya. Hii imekuja kufuatia tabia ya Dudu Baya ya kuwasema vibaya wasanii wenzake, jambo ambalo limeonekana kumkera Mr. Nice. Kupitia mitandao yake ya kijamii Mr. Nice amemtuhumu Dudu Baya kwa kutumia lugha chafu na kudhalilisha wasanii wenzake bila sababu. Ameonya kuwa endapo ataendelea na mwenendo huo wa kuwatusi na kuwadhalilisha wenzake, anaweza kuambulia kipigo. Amesema licha ya Dudu Baya kumpiga miaka kadhaa iliyopita, alichagua kumsamehe, lakini sasa anashangazwa na madai mapya ya msanii huyo kwamba hajawahi kushindwa kwenye vita. Amefichua kuwa Dudu Baya aliwahi kupigwa na kikosi cha mizinga hadi kuvuliwa suruali mbele ya watu. Hata hivyo Mr. Nice amemtaka Dudu Baya kuomba msamaha kwa kile alichodai ni kuiba pesa za kanisa, akisema laana ya kitendo hicho ndiyo inamfanya leo kumtukana mama wa mtoto wake.
Read More