Mwijaku: Diamond Aliiba Nyota ya Kassim Mganga Usiku wa Valentine
Mdau wa burudani Mwijaku amezua mjadala mkali mitandaoni baada ya kudai kuwa msanii wa Bongofleva Kassim Mganga ameisha kimuziki kufuatia tukio la Diamond Platnumz kubusu viatu vyake akiwa jukwaani usiku wa Valentine’s. Akizungumza kupitia majukwaa ya kijamii, Mwijaku amedai kuwa tukio hilo halikuwa la kawaida, akisema Diamond alitumia fursa hiyo kuiba nyota ya mafanikio ya msanii huyo. Katika hatua nyingine, Mwijaku amemtaja Jay Melody akisema aliwahi kuibiwa nyota kwa njia kama hiyo, jambo ambalo amedai mpaka sasa imeathiri muziki wa mkali huyo wa ngoma ya Sugar. Mwanamitandao huyo hakuishia hapo, ameenda mbali zaidi na kufichua kuwa kitendo cha Jay Melody kuonekana kususia kumpa mkono Diamond jukwaani katika hafla ya Garravallentines ilikuwa ni ishara ya kujingika kiimani.
Read More