Mwanahabari na mchanganuzi wa masuala ya burudani, Mwijaku, ameibuka rasmi kumtetea msanii Harmonize katika sakata linaloendelea kati ya Konde Boy na Baba Levo, huku akisema kuwa kauli za Harmonize zinapaswa kuheshimika kama sheria ndani ya tasnia ya muziki.
Kupitia ujumbe wake mzito, Mwijaku amesema kuwa anamfahamu vyema Harmonize, na kwamba kwa msanii huyo kufikia hatua ya kusema yale yaliyo Moyoni, basi kuna jambo kubwa limefika mwisho. Ametaka watu waachane na shobo zinazodhoofisha brand ya msanii huyo na badala yake waheshimu misimamo yake.
Ameeleza kuwa kuna wasanii ambao hawawezi kupelekwa pelekwa na mitazamo ya watu wengine kama vibaraka wa mwambino wanaomramba miguu, akimaanisha wale wanaojipendekeza kwa baadhi ya vigogo wa muziki ili kupata nafasi au kutengeneza kiki.
Mwijaku amesema wazi kuwa kauli za Harmonize hazipaswi kupuuzwa, akizilinganisha na katiba ya nchi au kanuni za chama kikuu cha upinzani, akizipa jina la utani Konde Statment Sharia, ishara ya uzito anaouona katika msimamo wa msanii huyo.