Nadia Mukami Apinga Madai ya Kuhamasisha Uasherati Kupitia Wimbo wa Woza Woza

Nadia Mukami Apinga Madai ya Kuhamasisha Uasherati Kupitia Wimbo wa Woza Woza

Staa wa muziki kutoka Kenya, Nadia Mukami, amepinga vikali madai yanayotembea mtandaoni kuwa wimbo wake mpya uitwao Woza Woza unahamasisha uasherati katika jamii. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Nadia amesema kuwa wasanii wa kike hukumbwa na hukumu kali zaidi ikilinganishwa na wanaume wanapotoa kazi zinazogusa mada nyeti katika jamii. Ameeleza kuwa mara nyingi wanaume huachwa huru kuimba kuhusu masuala mbalimbali bila kulaumiwa, huku wanawake wakishambuliwa kwa vigezo vya maadili. Nadia amesisitiza kuwa kama msanii, ana uhuru wa kuimba na kuwasilisha ujumbe unaoakisi uhalisia wa kijamii, hisia na maisha ya kila siku. Ameongeza kuwa muziki ni jukwaa la kueleza fikra tofauti na si lazima kila wimbo umfurahishe kila mtu. Mwimbaji huyo amewataka mashabiki na wakosoaji kuheshimu ubunifu wa wasanii na kuelewa kuwa sanaa ina nafasi ya kuibua mijadala, kuelimisha na kuburudisha kwa wakati mmoja.

Read More
 Nadia Mukami Atangaza Mshindi wa Woza Challenge

Nadia Mukami Atangaza Mshindi wa Woza Challenge

Msanii wa muziki nchini Kenya, Nadia Mukami, ametangaza rasmi mshindi wa Woza Challenge iliyotikisa mitandao ya kijamii kwa wiki kadhaa. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Nadia amesema haikuwa kazi rahisi kumchagua mshindi kutokana na ubunifu mkubwa ulioonyeshwa na washiriki wengi, lakini hatimaye Paida Mitumba aliibuka kidedea. Kwa mujibu wa Nadia, video ya Paida Mitumba ilivutia umakini mkubwa na kufikisha watazamaji zaidi ya milioni 3 kwenye mitandao wa Tiktok, jambo lililoifanya ionekane wazi miongoni mwa video nyingi zilizoshiriki kwenye changamoto hiyo. Nadia Mukami amewashukuru kwa dhati mashabiki walioshiriki Woza Challenge, akisema ushiriki wao umechangia pakubwa mafanikio ya wimbo huo na kuonesha nguvu ya mashabiki wa muziki Afrika Mashariki. Wakati huohuo, video ya wimbo wa Woza inaendelea kufanya vizuri sokoni na kwa sasa inashika nafasi ya kwanza kwenye YouTube Kenya, licha ya madai kutoka kwa baadhi ya wadau wa mitandao kwamba Nadia alitumia sehemu ya wimbo wa msanii wa Tanzania Zuchu kwenye kazi hiyo. Hata hivyo, madai hayo hayajazuia Woza kuendelea kupendwa na kusikilizwa kwa wingi na mashabiki.

Read More
 Nadia Mukami Ashindwa Kuficha Furaha Baada ya Wimbo Wake Kushika Namba Moja YouTube Kenya

Nadia Mukami Ashindwa Kuficha Furaha Baada ya Wimbo Wake Kushika Namba Moja YouTube Kenya

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Nadia Mukami, ameshindwa kuficha furaha yake baada ya wimbo wake mpya Woza kushika nafasi ya kwanza kwenye chati ya YouTube Trending Kenya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nadia amewashukuru mashabiki wake pamoja na Mungu kwa mafanikio hayo makubwa, akieleza kuwa mapenzi na sapoti ya mashabiki ndiyo yameufikisha wimbo huo kileleni kwa muda mfupi. Katika ujumbe wake, Nadia pia ametangaza kuwa ataandaa “dera party” Ijumaa hii kusherekea mafanikio ya Woza. Amewaalika mashabiki wake kupendekeza sehemu nzuri itakayofaa kufanyika sherehe hiyo, akisema angetamani kusherekea pamoja nao. Video ya wimbo Woza iliachiwa rasmi Disemba 11, na ndani ya siku nne pekee tayari imefanikiwa kukusanya zaidi ya views laki tatu kwenye YouTube, jambo linaloonesha ukubwa wa mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki wake.

Read More
 Nadia Mukami Akanusha Kuiba Ubunifu wa Zuchu na Kutumia Kwenye Wimbo Wake Mpya

Nadia Mukami Akanusha Kuiba Ubunifu wa Zuchu na Kutumia Kwenye Wimbo Wake Mpya

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Nadia Mukami, ameweka wazi msimamo wake kufuatia madai yaliyosambaa mitandaoni kwamba wimbo wake mpya Woza ulinakiliwa au kusampuliwa kutoka kwa msanii wa Tanzania, Zuchu. Akizungumza kuhusu suala hilo, Nadia amesisitiza kuwa Woza haujanakiliwa wala kusampuliwa kutoka kwa wimbo wowote wa Zuchu. Ameeleza kuwa kilichofanyika ni yeye na mtayarishaji wake, Teknixx, kuamua kutumia mtindo wa sauti unao-trend kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa Nadia, mdundo huo si mali ya msanii mmoja bali ni mtindo wa muziki unaotumiwa na wasanii wengi wa kikanda wanaotaka kwenda na mwelekeo wa soko la sasa. Ameongeza kuwa wasanii wengi kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wakitumia aina hiyo ya sauti bila kuhusishwa na wizi wa kazi za wengine. Msanii huyo amesisitiza kuwa ubunifu katika muziki hubadilika kulingana na wakati, na ni jambo la kawaida kwa wasanii kukumbatia mitindo mipya ili kubaki relevant katika tasnia inayobadilika kwa kasi.

Read More
 Nadia Mukami Aikosoa Orodha ya WCB Kuhusu Wasanii wa Kike Wanaotazamwa Zaidi YouTube

Nadia Mukami Aikosoa Orodha ya WCB Kuhusu Wasanii wa Kike Wanaotazamwa Zaidi YouTube

Mwanamuziki kutoka Kenya Nadia Mukami ameikosoa lebo ya WCB Wasafi kwa kumwacha nje ya orodha ya wasanii wa kike kutoka Afrika Mashariki wenye watazamaji wengi zaidi kwenye YouTube. Nadia, ambaye kwa sasa ana zaidi ya watazamaji milioni 118 kwenye chaneli yake, ameeleza kuwa orodha hiyo ni batili na haina uhalali kwa sababu haijazingatia takwimu zake ambazo zinamweka miongoni mwa wasanii wanaoongoza katika ukanda huu. Katika ujumbe wake, ameonesha kutoridhishwa na kile alichokitaja kama kupuuzwa kwa mchango wake katika muziki wa Afrika Mashariki, akisisitiza kuwa juhudi zake na ukuaji wa chaneli yake haviwezi kupuuzwa katika tathmini kama hiyo. Aidha, Nadia ametoa wito kwa mashabiki wake kuendelea kuiunga mkono safari yake ya kutimiza lengo la kufikisha wafuatiliaji milioni moja kwenye chaneli yake ya Youtube. Tukio hili limezua mjadala mpana mtandaoni, mashabiki wengi wakitafsiri hatua ya Nadia kama mwito kwa wadau wa muziki kutambua takwimu halisi na mchango wa wasanii wa kike wanaotoka nje ya lebo kubwa za muziki katika kanda ya Afrika Mashariki.

Read More
 Nadia Mukami na Arrow Bwoy Wakaribisha Mtoto wa Pili

Nadia Mukami na Arrow Bwoy Wakaribisha Mtoto wa Pili

Msanii maarufu wa muziki wa Kenya, Nadia Mukami, na mchumba wake ambaye pia ni mwanamuziki, Arrow Bwoy, wametangaza kwa furaha ujio wa mtoto wao wa pili, wakimpa jina Ameer Kiyan. Kupitia mitandao ya kijamii, wawili hao walishiriki habari hizo njema pamoja na picha ya kumshukuru Mungu kwa zawadi hiyo mpya katika familia yao. Ujio wa Ameer Kiyan unakuja takribani miaka miwili baada ya wawili hao kupata mtoto wao wa kwanza, Haseeb Kai, aliyezaliwa Machi 2022. Mashabiki na wasanii wenzao wamemiminika kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kuwapongeza, wakipongeza hatua hiyo mpya katika maisha yao. Nadia na Arrow Bwoy wamekuwa wakishirikiana sio tu kimuziki bali pia kimaisha, na mara kadhaa wameeleza hadharani jinsi familia yao ilivyo kipaumbele . Tukio hili linaongeza ukurasa mwingine wa furaha kwenye safari yao ya pamoja, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona kama ujio wa Ameer Kiyan utaathiri kwa namna yoyote mwelekeo wa muziki wa wawili hao maarufu.

Read More
 Nadia Mukami Atoa Kauli Nzito Kuhusu Single Mothers

Nadia Mukami Atoa Kauli Nzito Kuhusu Single Mothers

Staa wa muziki, Nadia Mukami, amefunguka ya moyoni kuhusu unyanyapaa unaowakumba kina mama wanaolea watoto wao pekee yao (single mothers). Kupitia mitandao ya kijamii, Nadia ameeleza masikitiko yake kuhusu namna jamii imezoea kuwaelekezea lawama wanawake hao, huku ikiwapuuza kabisa wanaume waliokimbia majukumu yao ya malezi (deadbeat dads). Amebainisha kuwa sababu za mwanamke kuwa mama mlezi mmoja ni nyingi na halali, zikiwemo unyanyasaji wa majumbani, vifo vya waume, talaka, kutelekezwa, pamoja na uraibu wa dawa za kulevya au pombe kwa wenza wao. Ingawa amekiri kuwa si wanawake wote ni wakamilifu na baadhi huonyesha tabia zisizofaa katika co-parenting, Nadia amesisitiza kuwa lawama hazifai kuelekezwa kwa mwanamke pekee. Ametoa wito kwa jamii kujikita katika kutafuta suluhisho badala ya kuhukumu upande mmoja tu. Ujumbe wake huo umetambuliwa na wengi kama sauti ya matumaini kwa mamia ya kina mama wanaopitia hali hiyo kimya kimya. Mashabiki na wafuasi wake wamesifu msimamo wake wa kuthubutu kulizungumzia suala hilo kwa uwazi na kwa mtazamo wa huruma. Katika kuendeleza ujumbe huo, Nadia anatarajiwa hivi leo kuachia wimbo wake mpya “Single Mother”, ambao umetajwa kuwa sehemu ya harakati zake za kuangazia maisha na changamoto za mama mlezi mmoja kupitia muziki.

Read More
 Wasanii Wapaza Sauti Kufuatia Kujeruhiwa kwa Arrow Bwoy na Polisi Wakati wa Maandamano ya Amani

Wasanii Wapaza Sauti Kufuatia Kujeruhiwa kwa Arrow Bwoy na Polisi Wakati wa Maandamano ya Amani

Tukio la kujeruhiwa kwa msanii mashuhuri wa muziki wa Kenya, Arrow Bwoy, na polisi wakati wa maandamano ya amani limezua taharuki kubwa mitandaoni na kusababisha wasanii wenzake kuibua hisia kali za hasira na kukemea ukatili wa polisi. Arrow Bwoy alikuwa ameungana na rapa maarufu Khaligraph Jones pamoja na raia wengine katika maandamano ya kupinga ukatili wa vyombo vya usalama. Hata hivyo, maandamano hayo yaliishia kwa vurugu baada ya polisi kuwatawanya waandamanaji kwa kutumia mabomu ya machozi na nguvu kupita kiasi, hali iliyomwacha Arrow Bwoy amejeruhiwa. Khaligraph Jones alilalamikia tukio hilo kupitia mitandao ya kijamii, akisema kwa uchungu kuwa waandamanaji walikuwa wakifanya maandamano kwa amani, lakini walishambuliwa na polisi waliokuwa wakifyatua mabomu ya machozi moja kwa moja kwao. Alisema kitendo hicho ni mfano tosha wa ukatili wa polisi unaopaswa kukomeshwa mara moja. “Unapofanya maandamano ya amani halafu wanaanza kukupiga risasi za mabomu ya machozi… Kukomesha ukatili wa polisi nchini Kenya ni muhimu sana. #RespectTheOGs,”  Alielezea kwa uchungu Khaligraph Jones, ambaye alikuwa sambamba na Arrow Bwoy wakati wa maandamano hayo. Naye mchumba wa Arrow Bwoy na mama wa mtoto wake, Nadia Mukami, alionekana kuguswa sana na tukio hilo. Kupitia ujumbe alioutuma mtandaoni, aliandika kwa hasira kuwa polisi hawapaswi kumshika baba wa mtoto wake na kutaka ukatili huo ukome mara moja. “Nyinyi mafala msimguse baba watoto wangu!!!! #EndPoliceBrutality Nimejam ata!!!!!,” Aliandika kwa hasira Instagram. Kauli za wasanii hao zimeungwa mkono na maelfu ya mashabiki na wakenya wa kawaida, huku wengi wakitumia mitandao ya kijamii kulaani hatua ya polisi kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji wa amani. Hashtag kama #EndPoliceBrutality na #RespectTheOGs zimeendelea kutrendi huku wito ukitolewa kwa serikali kuwajibisha maafisa waliohusika. Tukio hili limezua mjadala mpana kuhusu haki ya kuandamana na uhuru wa kujieleza nchini Kenya, huku wasanii wakionyesha kuwa wako tayari kusimama na wananchi kupigania haki na mabadiliko katika jamii.

Read More
 Nadia Mukami Afichua Mpango wa Kufunga Kizazi Baada ya Mtoto wa Pili

Nadia Mukami Afichua Mpango wa Kufunga Kizazi Baada ya Mtoto wa Pili

Mwanamuziki maarufu wa Kenya, Nadia Mukami, ameweka wazi mpango wake wa kufunga kizazi (tubal ligation) baada ya kujifungua mtoto wake wa pili. Kupitia mahojiano yake hivi karibuni, Nadia alisema kuwa tayari amefikiria kwa kina kuhusu maamuzi ya uzazi na anahisi kuwa watoto wawili ni wa kutosha kwake. “Nikipata mtoto wangu wa pili, nafunga kabisa. Sina mpango wa kuzaa tena baada ya hapo,” alisema Nadia kwa uwazi. Nadia Mukami na mpenzi wake Arrow Bwoy tayari ni wazazi wa mtoto mmoja, na wawili hao wamekuwa wakionyesha maisha yao ya kifamilia kwa uwazi kupitia mitandao ya kijamii. Hata hivyo, Nadia sasa anaweka mipango thabiti ya kuhakikisha anadhibiti idadi ya watoto kwa namna anayoihisi inamfaa kiafya na kimaisha. Uamuzi wake umeibua mjadala mkubwa mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa kuchukua msimamo wa wazi kuhusu afya ya uzazi, na wengine wakijadili suala hilo kwa mtazamo wa kijamii na kidini. Nadia Mukami anaendelea kuwa sauti muhimu si tu katika muziki, bali pia kwenye mijadala ya kijamii kuhusu afya ya wanawake na maamuzi ya uzazi. Kwa sasa, mashabiki wake wanaendelea kumuunga mkono huku wakisubiri kwa hamu kazi zake mpya na hatua zake za kibinafsi.

Read More
 Nadia Mukami Afunguka Sababu ya Kuahirisha Harusi Yake na Arrow Bwoy

Nadia Mukami Afunguka Sababu ya Kuahirisha Harusi Yake na Arrow Bwoy

Msanii maarufu wa muziki wa Kenya, Nadia Mukami, amefichua kwamba yeye na mchumba wake, Arrow Bwoy, walilazimika kuahirisha harusi yao baada ya kugundua kwamba walikuwa wanatarajia mtoto wao wa pili. Kupitia mahojiano ya hivi karibuni, Nadia ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Overdose’ alieleza kuwa walikuwa tayari wameweka mikakati yote muhimu kwa ajili ya tukio hilo maalum, lakini ujio wa mtoto mpya uliwalazimu kuahirisha harusi hiyo. “Tulikuwa tumepanga kila kitu, lakini sasa tumelazimika kuifuta,” alisema Nadia kwa huzuni lakini pia kwa matumaini. Ingawa mashabiki wengi walikuwa na matarajio makubwa ya kushuhudia harusi hiyo ya wanamuziki wawili maarufu, Nadia alisisitiza kuwa afya na ustawi wa familia yao ni jambo la kipaumbele kwa sasa. Hata hivyo, hakufunga mlango wa uwezekano wa harusi hiyo kufanyika siku za usoni Nadia na Arrow Bwoy, ambao walimpokea mtoto wao wa kwanza mwaka wa 2022, wamekuwa wakiendelea kudumisha uhusiano wao wa kimapenzi hadharani huku wakishirikiana pia katika kazi za muziki.

Read More
 Nadia Mukami akanusha madai ya kufadhiliwa kufungua Saloon

Nadia Mukami akanusha madai ya kufadhiliwa kufungua Saloon

Msanii Nadia Mukami amejitokeza na kukanusha madai kwamba Saloon iliyozinduliwa hivi karibuni imefadhiliwa na mdhamini, na kwamba yeye ni wakala tu wa kutangaza Saloon hiyo. Akizungumza na Nairobi news, Nadia amefichua kuwa saloon iliyofunguliwa mwezi Disemba 2022 ni jasho lake na timu yake inaweza kuthibitisha hilo. “Siku zote watu watanikosoa kwa njia mbaya, wengine watadai nimedhaminiwa lakini ni timu yangu tu na wale walio karibu nami wanaelewa mapambano niliyopitia kuzindua saloon hii,” Nadia alisema akijibu madai hayo. Msanii huyo amesimulia mapambano aliyopitia akijaribu kutafuta fedha za kufungua biashara hiyo na kuwatolea uvivu wanaodai kuwa yeye sio mmiliki halisi wa saloon hiyo kwa kusema kuwa mradi huo ulimgharimu zaidi ya shilingi milioni 1.2 za Kenya na zote zilitokana na fedha za akiba. “Kwa wale wanaofuata kile ninachofanya, wananiona nikifanya shows, juzi nilifanya moja na Safaricom na nililipwa vizuri. Nimekuwa nikifanya kazi na EABL kwa muda mrefu zaidi. Namaanisha kwa nini mtu afikirie siwezi kumudu gharama ya kuanzisha biashara kama hiyo?” Mwanamuziki huyo alisema akionekana kukerwa na madai ya walimwengu. Hata hivyo amewaambia mashabiki zake kwamba licha ya kutotoa vibao vingi mwaka 2022, ana mengi ya kufanya mwaka huu ikiwemo kuachia Album mpya.

Read More
 Nadia Mukami afunguka kutengana na Arrow Boy

Nadia Mukami afunguka kutengana na Arrow Boy

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami amefunguka kuhusu madai ya kutengana na baba ya mtoto wake Arrow Bwoy. Katika mahojiano na Mungai Eve, Nadia amesema kuwa alitengana na Arrow Bwoy baada ya kulemewa na mambo mengi ambayo yalitokea katika maisha yake katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. “Imekuwa moja ya miaka mbaya zaidi kwangu. Mungu amenibariki na pia nimepitia changamoto kwa viwango sawa. Nimepitia mengi, mambo yanaweza kuwa makubwa na inaweza kufikia mahali ukavunjika,” alisema. Aidha amewasuta watu ambao walidai alikuwa akifanya kiki kwa ajili ya kutangaza biashara yake mpya ya urembo iliyofunguliwa jijini Nairobi mapema wiki hii. “Haiwezi kuwa mbinu ya kutangaza biashara. Iliikuwa ni sadfa tu. Watu wanaoweza kunielewa wanajua kwamba nimeolewa hivi majuzi, nimepata mtoto na inaweza kulemea mtu, utapanga virago, ni mambo mengi,” alisema Msanii huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema licha ya kutengana na baba ya motto wake bado wanasaidia majukumu ya kuwalea motto wao, Haseeb Kai ikizingatiwa kuwa bado wanaisha katika nyumba moja. Lakini pia amezungumzia ishu ya Eric Omondi kumkosoa kwa kushindwa kuwekeza kwenye suala la branding katika mitandao ya kijamii kwa kusema kuwa amejifunza kitu kwenye kauli ya Omondi na atalifanyia kazi suala hilo. Kauli ya Nadia Mukami imekuja mara baada ya kuzindua biashara yake iitwayo ‘Nadia’s Nailbar & Beauty Parlor’ ambayo itahusika na masuala yote ya urembo. Akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa Nadia’s Nailbar & Beauty Parlor’, nadia alisema uzinduzi wa biashara yake hiyo ni moja kati ya ndoto ambazo amekuwa akitamani kufanikisha katika maisha.

Read More