Nadia Mukami afunguka kutengana na Arrow Boy

Nadia Mukami afunguka kutengana na Arrow Boy

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami amefunguka kuhusu madai ya kutengana na baba ya mtoto wake Arrow Bwoy. Katika mahojiano na Mungai Eve, Nadia amesema kuwa alitengana na Arrow Bwoy baada ya kulemewa na mambo mengi ambayo yalitokea katika maisha yake katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. “Imekuwa moja ya miaka mbaya zaidi kwangu. Mungu amenibariki na pia nimepitia changamoto kwa viwango sawa. Nimepitia mengi, mambo yanaweza kuwa makubwa na inaweza kufikia mahali ukavunjika,” alisema. Aidha amewasuta watu ambao walidai alikuwa akifanya kiki kwa ajili ya kutangaza biashara yake mpya ya urembo iliyofunguliwa jijini Nairobi mapema wiki hii. “Haiwezi kuwa mbinu ya kutangaza biashara. Iliikuwa ni sadfa tu. Watu wanaoweza kunielewa wanajua kwamba nimeolewa hivi majuzi, nimepata mtoto na inaweza kulemea mtu, utapanga virago, ni mambo mengi,” alisema Msanii huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema licha ya kutengana na baba ya motto wake bado wanasaidia majukumu ya kuwalea motto wao, Haseeb Kai ikizingatiwa kuwa bado wanaisha katika nyumba moja. Lakini pia amezungumzia ishu ya Eric Omondi kumkosoa kwa kushindwa kuwekeza kwenye suala la branding katika mitandao ya kijamii kwa kusema kuwa amejifunza kitu kwenye kauli ya Omondi na atalifanyia kazi suala hilo. Kauli ya Nadia Mukami imekuja mara baada ya kuzindua biashara yake iitwayo ‘Nadia’s Nailbar & Beauty Parlor’ ambayo itahusika na masuala yote ya urembo. Akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa Nadia’s Nailbar & Beauty Parlor’, nadia alisema uzinduzi wa biashara yake hiyo ni moja kati ya ndoto ambazo amekuwa akitamani kufanikisha katika maisha.

Read More
 Nadia Mukami mbioni kuzindua biashara yake mpya

Nadia Mukami mbioni kuzindua biashara yake mpya

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Nadia Mukami anatarajiwa kuzindua biashara mpya katikati mwa jiji la Nairobi kando ya barabara ya Koinange mwishoni mwa wiki. Mwimbaji huyo maarufu na mtunzi wa nyimbo ametumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza habari hiyo njema kwa wafuasi wake wakati akizindua nembo rasmi ya saloon yake  ya urembo ambayo itakuwa inatoa huduma zake katika duka la jumla la Deluxe Mall. Mashabiki wengi wamempongeza kwa hatua hiyo kubwa, wengine wakiulizia kama wanaweza pata kazi ambapo wengi wameahidi kuunga mkono biashara yake. Huu umekuwa mwaka mzuri kwa Nadia, ambaye amekuwa akivunja vizingiti katika tasnia ya muziki kwa kujiboresha kwa kila njia inayoweza. Mapema mwaka huu, alisaini msanii wake wa kwanza Latinoh, chini ya Seven Creative Hub, lebo yake ya muziki. Hii ni baada ya kutangaza kwamba anataka kupanua himaya yake kwa kusaini msanii mpya

Read More
 Nadia Mukami athibitisha kuachana na Arrow Boy

Nadia Mukami athibitisha kuachana na Arrow Boy

Staaa wa muziki nchini Nadia Mukami amethibitisha kutengana na mwanamuziki mwenzake Arrow Bwoy. Katika taarifa ambayo aliichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nadia alibainisha kuwa yeye na mzazi huyo mwenzake hawajakuwa pamoja kwa muda mrefu sasa. aidha alikiri kuwa ameshindwa kabisa kuendelea kudanganya kuhusu uhusiano wao kwa watu wengi ambao hawakuwa na ufahamu kuhusu kutengana kwao. “Ili tu kuwafafanulia watu wanaojaribu kubook mimi na Arrow Bwoy, nimeishiwa na uwongo. Hatujakuwa pamoja kwa muda, tuliachana,” Nadia Mukami aliandika kwenye Instastory yake leo Alhamisi. Hata hivyo Nadia amesisitiza kuwa ni kweli ameachana na Arrow Boy na hatumii suala hilo kutafuta kiki kama wengi wanavyodhani kwa kuwa tayari ana jina kubwa kwenye muziki nchini Kenya. Nadia Mukami na Arrow Boy wamekuwa wapenzi kwa muda sasa na kwa pamoja wamebarikiwa kumpat motto mmoja aitwaye Haseeb Kai.

Read More
 Nadia Mukami afunguka juu ya mpango wa kupata mtoto wa pili

Nadia Mukami afunguka juu ya mpango wa kupata mtoto wa pili

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Nadia Mukami amefichua kuwa hana mpango wa kupata mtoto mwingine hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram akimjibu shabiki aliyetaka kujua ni lini atampata mtoto wake wa pili, Nadia amesema kwa sasa hajajiandaa kisaikolojia kupata uja uzito mwingine huku akisisitiza kuwa atafanya hivyo labda miaka mitano ijayo. “Labda baada ya miaka mitano, sitaki saa hii! Eh ni kujitolea pakubwa sana,” Mukami alisema. Nadia kwa sasa ni mama ya mtoto mmoja aitwaye Kai aliyepata na mchumba wake Arrow Boy miezi minane iliyopita.

Read More
 Nadia Mukami atangaza kuja na jambo lake kubwa mwezi Desemba

Nadia Mukami atangaza kuja na jambo lake kubwa mwezi Desemba

Hitmaker wa Maombi, msanii Nadia Mukami ametangaza kuwa ana jambo lake kubwa la kufungia mwaka. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema mwezi Desemba mwaka huu ana shughuli ambayo atazindua kwa ajili ya mashabiki zake. “Launching Something this December,” Aliandika insta-story Hata hivyo haijajulikana ni nini hasa msanii huyo atazindua ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wamehoji huenda ni mipango ya kuachia Album yake mpya ambayo juzi kati alitusanua kuwa itaingia sokoni mapema mwaka 2023.

Read More
 Nadia Mukami kuachia Album yake mpya mwaka 2023

Nadia Mukami kuachia Album yake mpya mwaka 2023

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami ametangaza rasmi ujio wa album yake mpya na ya kwanza katika muziki wake. Kupitia ukurasa wake wa instagram amesema yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya kukamilisha album yake mpya ambayo itaingia sokoni mapema mwaka 2023. “I am working on my Album! The best thing I can do is starve my fans just a little bit! Early Next year, y’all getting an Album!Sending Love to my Fans! kaNadians!”. Aliandika Mara ya mwisho Nadia Mukami kuwabariki mashabiki na kazi ilikuwa miezi sita iliyopitia alipoachia Bundle of Joy EP yenye jumla ya mikwaju 4 ya moto.

Read More
 Nadia Mukami afunguka chanzo cha kuzinyoa nywele zake

Nadia Mukami afunguka chanzo cha kuzinyoa nywele zake

Msanii nyota nchini Nadia Mukami amefunguka sababu za kunyoa nywele zake pindi alipojifungua mtoto wake wa kwanza na Arrow Bwoy. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nadia amesema alichukua maamuzi hayo kutokana na nywele zake kukatika kila mara alipokuwa anamnyonyosha mtoto wake. Katika hatua nyingine ametoa wito kwa mashabiki zake wamuombee wakati huu yupo mbioni kukata uzito kutoka kilo 67 hadi 60 ili aweze kurejesha muonekano wake wa awali kabla ya kujifungua. Kauli yake imekuja siku moja mara baada ya kukiri kuteswa na unene uliopitiliza kiasi cha kumfanya kuingiwa na uoga wa kuchapisha video pamoja na picha kwenye mitandao yake ya kijamii.

Read More
 Nadia Mukami atangaza kuingia gym kupunguza mwili wake

Nadia Mukami atangaza kuingia gym kupunguza mwili wake

Baada ya kusemwa sana mitandaoni kuwa amenenepa kupita kiasi na kupoteza mvuto tangu ajifungue mtoto wake wa kwanza na Arrow Boy, msanii Nadia Mukami ameamua kuingia gym kwa ajili ya kupunguza mwili wake. Nadia Mukami amechukua hatua hiyo kutokana na baadhi ya wasanii wenzake pamoja na mashabiki wake kutopendezwa na unene wake kwani unamfanya kuonekana kituko kwenye jamii. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nadia amekiri kuteswa na unene kiasi cha kuingiwa na uoga wa kuchapisha picha au video zake kwenye mitandao ya kijamii huku akiapa kufanya mazoezi makali ambayo yatamsaidia kukata uzito wa mwili wake kutoka kilo 67 hadi 60. Hata hivyo, baada ya kuanza mazoezi magumu , watu wengi wamempongeza Nadia Mukami kwa hatua hiyo huku baadhi ya mashabiki wakisema wanasubiri kumuona msanii huyo akirejesha muonekano wake wa awali lakini asijikondeshe kupita kiasi.

Read More
 NADIA MUKAMI ADOKEZA UJIO WA EP YA PAMOJA NA ARROW BWOY

NADIA MUKAMI ADOKEZA UJIO WA EP YA PAMOJA NA ARROW BWOY

Mwanamuziki Nadia Mukami amedokeza kuja na EP ya pamoja na mchumba wake Arrow Boy kwa sababu wamekuwa na muendelezo mzuri wakuachia nyimbo kali.   Kwenye mahojiano hivi karibuni Nadia amesema wana nyimbo nyingi ambazo hazijatoka ambapo amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kupokea EP yao ya pamoja ambayo ameitaja kuwa moto wa kuotea mbali.   Katika hatua nyingine ametupasha kuhusu maendeleo ya album yake mpya kwa kusema kwamba album yake hiyo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika na itakuwa ya kitofauti sana kwani itaangazia safari yake ya maisha kabla na baada ya umaarufu.   Hitmaker huyo “Maombi” amesema album hiyo ilipaswa kutoka mapema mwaka huu lakini kutokana na yeye kushikika na majukumu ya malezi aliamua kuachia EP iitwayo Bundle of Joy ambayo ilikuwa mahsusi kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya mtoto.

Read More
 NADIA MUKAMI AONYA WATOTO WA KIKE DHIDI YA ATHARI ZA MIMBA YA MAPEMA

NADIA MUKAMI AONYA WATOTO WA KIKE DHIDI YA ATHARI ZA MIMBA YA MAPEMA

Msanii nyota nchini Nadia Mukami ametoa angalizo kwa watoto wa kike kuwa wangalifu kabla ya kuchukua maamuzi ya kupata uja uzito. Nadia amesema wanawake kwa asilimia kubwa ndio hubeba majukumu ya kumlea mtoto ikilinganishwa na wanaume, hivyo wanapaswa kujipanga kisaikolojia kukabiliana na changamoto za kuwa mzazi ikiwemo mabadiliko ya kimwili na kimuonekano. Katika hatua nyingine Nadia Mukami amesema kuwa kutokana na changamoto zinazowakumba akina mama wachanga kwenye masuala ya malezi ana mpango wa kushirikiana na mume wake Arrow Boy kuja na podcast ambayo itakuwa mahsusi kwa ajili ya kuhamasisha vijana kuhusu athari za mimba ya utotoni.

Read More
 NADIA MUKAMI AFIKISHA SUBSCRIBERS LAKI 5 YOUTUBE

NADIA MUKAMI AFIKISHA SUBSCRIBERS LAKI 5 YOUTUBE

Nyota wa muziki nchini Nadia Mukami amefanikiwa kufikisha idadi ya subscribers laki 5 kwenye mtandao wa Youtube. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nadia Mukami amewashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia kazi zake huku akiwataka wakae mkao wa kula kupokea wimbo wake mpya. “Thank you for Half a Million Subscribers!!! (500k)I have the realest Fanbase aka KaNadians God bless you all! New Music Loadingggg……” Ameandika. Channel ya youtube ya Nadia Mukami ilifunguliwa rasmi Mei 19 mwaka 2017 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 63.4 huku ikiwa na jumla ya subscribers 500, 000.

Read More
 ARROW BOY AMKINGIA KIFUA NADIA MUKAMI KWA KUKOSOLEWA MTANDAONI

ARROW BOY AMKINGIA KIFUA NADIA MUKAMI KWA KUKOSOLEWA MTANDAONI

Msanii nyota nchini Arrow Boy ameshindwa kuvumilia watu wanaomkosoa baby mama wake Nadia Mukami kutokana na mavazi aliyovalia juzi kati kwenye onesho lake huko Meru. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Arrow Boy ameshangazwa namna watu wanavyomshambulia Nadia Mukami kwenye mitandao ya kijamii kwa mambo yasiokuwa na msingi huku akisema kuwa huenda ni mafanikio ya msanii huyo  ndio imepelekea baadhi ya watu kuanza kumchukia. “Watu huku nje roho zao zimejaa machungu just ready to explode like a time bomb….Why too much hate?” Ameandika Instagram. Hitmaker huyo wa Enjoy amesema watu waache kumuonea Nadia Mukami wivu kwenye  muziki wake kwa kuwa anazidi kuandika historia ya kipekee ambayo hajawahi fikiwa na msanii yeyote wa kike nchini. “As you keep hating, others are making history….Tuseme tu ukweli which female artist in Kenya has pulled a move @NadiaMukami pulled over the weekend in Meru since Kenya izaliwe? Hakuna…”  Ameongeza Arrow Boy

Read More