NADIA MUKAMI: MIMI SIO MTU WA KIKI, KIKI ZINANIFUATA ZENYEWE

NADIA MUKAMI: MIMI SIO MTU WA KIKI, KIKI ZINANIFUATA ZENYEWE

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami amefunguka na kudai kuwa yeye siyo mtu wa kupenda kiki kama baadhi ya watu wanavyodai kupitia mitandao ya kijamii. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Nadia Mukami amesema yeye haitaji kiki ili kazi zake ziweze kufanya vizuri, tofauti na wasanii wengi wa kizazi kipya. Hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” amedai vitu vingi anavifanya katika hali ya kawaida lakini vinakuzwa na media hali ambayo amedai kwake haoni kama ni tatizo kwani ataendelea kutoa muziki mzuri bila kujihusisha na kiki. Nadia Mukami amekuwa akitawala mitandao ya kijamii kila kukicha kutokana na vituko vyake huku watu wakidhani huenda akawa anapanga kufanya matukio ya namna hiyo ili azungumziwe kwenye vyombo vya habari.

Read More
 NADIA MUKAMI AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UJA UZITO WAKE NA ARROW BOY

NADIA MUKAMI AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UJA UZITO WAKE NA ARROW BOY

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami ameshindwa kuvumilia kinachoendelea mtandaoni kuhusu uja uzito wake na Arrow boy. Kupitia video aliyoishare kwenye ukurasa wake wa instagram Nadia Mukami amedokeza kuwa alipoteza uja uzito wake mwishoni mwa mwaka wa 2021. Hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” amesema licha ya kupoteza uja uzito wake aliahuma kutoweka wazi habari hiyo mbaya kwa umma. Hata hivyo amemtolea uvivu Jalang’o kwa  madai ya kusema kuwa hataomba msamaha kwa hatua ya kuanika uja uzito wake akiwa redioni akisema kwamba kitendo hicho sio cha kingwana.. Kauli ya Nadia Mukami imekuja mara baada ya Jalang’o kutangaza redio kuwa anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mchumba wake Arrow Boy hivi karibuni. Jambo ambalo lilimkasirisha Arrow Boy ambapo alitumia instastory kumuonya Jalang’o akome kuingilia maisha yake na nadia mukami. Kutokana na hilo Jalang’o alimjibu Arrow Boy kwa kusema kwamba atakoma kuzungumzia maisha yao na hajutii kuweka wazi uja uzito wa Nadia Mukami.

Read More
 ARROW BOY AMVUA NGUO JALANG’O, AMTAKA AACHE KUFUATILIA MAISHA YAKE NA NADIA MUKAMI

ARROW BOY AMVUA NGUO JALANG’O, AMTAKA AACHE KUFUATILIA MAISHA YAKE NA NADIA MUKAMI

Staa wa muziki nchini Arrow Boy kwa mara nyingine amekanusha tetesi za mchumba wake Nadia Mukami kuwa na uja uzito wake. Hii ni baada ya mchekeshaji Jalang’o kwenye kipindi cha Jalas and Kamene in the morning kinachoruka kupitia Kiss 100 kusisitiza kuwa Nadia Mukami ni mjamzito na alithibitisha hilo wakati wapenzi wawili hao walimtembelea kijiji kwao. Jalango alienda mbali zaidi na kumshauri Nadia Mukami aache ishu ya kuficha uja uzito kwa umma kwani hivi karibuni itajulikana tu. Sasa akijibu hilo Arrow Boy kupitia instastory ameandika ujumbe unaosomeka “2022 Wanaume Tupunguze Mshene Bana biashara Haikuhusu achana nayo Kabisa shugulika na maisha yako” ujumbe ambao umetafsiri kumlenga moja kwa moja Jalang’o. Juzi kati Nadia Mukami aliripotiwa kuwa na uja uzito wa Arrow Boy hii ni baada ya kuonekana akitumbuiza kwenye show moja akiwa amevalia mavazi makubwa jambo ambalo liliwafanya wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” ni mjamzito. Hata hivyo Nadia Mukami kupitia Instagram page yake amenyosha maelezo kwa kupost picha ambayo imezima kabisa tetesi za kuwa na uja uzito.

Read More
 NADIA MUKAMI KUMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA HIVI KARIBUNI

NADIA MUKAMI KUMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA HIVI KARIBUNI

Msanii nyota nchini Nadia Mukami ametangaza kumtambulisha msanii wake mpya chini lebo ya muziki ya Sevens Creative hub mwanzoni mwa mwaka wa 2022. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema atamsaini msanii wake mpya chini ya Seven Creative Hub mwezi Januari mwaka wa 2022 ambapo amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kumpokea msanii huyo ambaye pia ataachia video ya wimbo wake mpya ambayo amemshirikisha baada ya utambulisho wake. This January I am introducing my New artist and our First video together Drops!!! Are you ready???? @sevenscreative_hub..ameandika Nadia Mukami kupitia Instagram page yake. Hata hivyo hajaweka wazi jinsia ya msanii huyo ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wamehoji huenda msanii huyo akawa Slyvia Ssaru ambaye kipindi cha nyuma alinukuliwa kwenye instagram yake akisema mwakani atasainiwa na lebo ya Sevens Creative hub ambayo inamilikiwa na Nadia Mukami. Haikushia mbali zaidi na kuwataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea ujio mpya kwani ataachia rasmi Extended Playlist yake baada ya kuingia ubia wa kufanya kazi na Sevens Creative hub.

Read More
 MUONEKANO WA NADIA MUKAMI WAZUA  GUMZO MTANDAONI, ADAIWA ANA UJA UZITO WA ARROW BOY

MUONEKANO WA NADIA MUKAMI WAZUA GUMZO MTANDAONI, ADAIWA ANA UJA UZITO WA ARROW BOY

Nyota wa muziki nchini Nadia Mukami anadaiwa kushika ujauzito wa mpenzi wake Arrow Boy Uvumi huo umeanza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii kutokana na muendelezo wa picha na mavazi ambayo Nadia Mukami amekuwa akivaa kwa sasa. Kwanza kabisa ni picha aliyopiga na Arrow Boy ambayo inamuonesha  Nadia Mukami kuficha tumbo lake mbele ya camera jambo ambalo si kawaida yake. Haijaishia hapo, vazi ambalo  Nadia Mukami alilivaa juzi kati akimsuprise mpenzi wake Arrow Boiy uraiani baada ya kutoka hospitali limefanya watu kupigia mstari kuwa mrembo huyo ni mjamzito kwani alikuwa amevaa nguo kubwa (Oversize) Ikiwa ni kweli  Nadia Mukami ana ujauzito kwa sasa, basi huyo atakuwa mtoto wa kwanza kwa staa huyo mwenye umri wa miaka 26 na mchumba wake Arrow Boy

Read More
 NADIA MUKAMI AMCHANA ERIC OMONDI, ADAI ANATUMIA MUZIKI WA KENYA KUJITAFUTIA UMAARUFU

NADIA MUKAMI AMCHANA ERIC OMONDI, ADAI ANATUMIA MUZIKI WA KENYA KUJITAFUTIA UMAARUFU

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami ametolea uvivu Eric Omondi baada ya mchekeshaji huyo kudai wasanii wa kenya wataendelea kudharauliwa hadi pale watakapoacha tamaa na uzembe kwenye kazi zao za muziki. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amemtaka Omondi aache suala la kujipendekeza katika ishu ya kupigania mabadiliko kwenye muziki wakenya ikizingatiwa kuwa ni suala mtambuka ambalo linahitaji kuzungumziwa kwa kina. Hitmaker huyo “Roho Mbaya” ameenda mbali na kuonyosha maelezo kuhusu ya kufukuzwa na promota kwenye tamasha lilofanyika majuzi huko Mombasa kwa kusema kwamba hakutaka kupishana na waandaji wa tamasha hilo kwani hapendi kutumia nguvu kwenye kazi zake. Kauli ya Nadia Mukami inakuja mara baada ya kudaiwa alitimuliwa na msanii  mwenzake Masauti wakiwa jukwaani kumpisha msanii wa bongofleva mbosso kwenye tamasha la Bright Future lilofanyika mombasa wikiendi hii iliyopita.

Read More
 NADIA MUKAMI KUMCHUKULIA HATUA KALI ALIYEFUTA VIDEO YA WIMBO WA TESA YOUTUBE

NADIA MUKAMI KUMCHUKULIA HATUA KALI ALIYEFUTA VIDEO YA WIMBO WA TESA YOUTUBE

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha wimbo wake wa Tesa aliyomshirikisha fena Gitu na Khalighraph Jones kuondolewa kwenye mtandao wa youtube kwa madai ya hakimiliki. Kupitia ukurasa wake wa instagram Nadia Mukami amehapa kupambana na msanii aliyesababisha wimbo wake kuondolewa kwenye mtandao wa youtube kwa kusema kwamba yupo tayari kutumia pesa zote alizochuma kupitia muziki wake kuhakikisha kwamba aliyesusha wimbo wake youtube anachukulia hatua kali za kisheria. Hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” ametoa ya moyoni na kuwataka wanaoendeleza kadhia hiyo kukoma mara moja kwani wamewapelekea wasaniii wengi kupata hasara ikizingatiwa kuwa wasanii hutumia pesa nyingi kuandaa video za nyimbo zao. Kauli ya Nadia Mukami imekuja mara baada ya msanii chipukizi  kudai kwamba mrembo huyo  aliiba idea yake na kuitumia kwenye wimbo wa Tesa bila ya kumshirikisha.

Read More
 VIDEO 4 ZA MUZIKI ZA NADIA MUKAMI ZAFUTWA YOUTUBE

VIDEO 4 ZA MUZIKI ZA NADIA MUKAMI ZAFUTWA YOUTUBE

Video za muziki za msanii nadia mukami zimefutwa kwenye akaunti ya mtandao wa youtube ya msanii huyo.   Ukitembelea kwenye akaunti ya youtube  ya nadia mukami  hautafanikiwa kuziona nyimbo zake kama maombi, Wangu, Radio Love na Kolo kutokana na kuondolewa na aliyezi-upload.   Sanjari na hilo nyimbo za Nviiri the story teller Pombe sigara na niko sawa zimeondolewa pia kwenye mtandao wa youtube.   Hata hivyo chanzo cha music video  za wasanii hao  kuondolewa kwenye mtandao wa youtube haijajulikana mpaka sasa.   Ikumbukwe siku ya jana Msanii otile brown alipata pigo kama hilo baada ya video tano za nyimbo zake kuondolewa kwenye mtandao.            

Read More