Otile Brown Awataka Mashabiki Kumsaidia Kumtafuta Mrembo

Otile Brown Awataka Mashabiki Kumsaidia Kumtafuta Mrembo

Penzi la mjaka mfine, mrembo aliyekutana na Otile Brown katika tamasha la Luo Festival limemkosesha usingizi staa huyo wa R&B. Msanii huyo amekiri waziwazi kwamba alitekwa na mvuto wa mrembo huyo, akidai macho yake na uwepo wake vilimchanganya. Otile Brown, ambaye mara nyingi huweka wazi hisia zake kupitia muziki, safari hii hakuweza kujizuia bali aliamua kutafuta msaada wa mashabiki wake. Kupitia ukurasa wake wa mtandaoni, aliposti picha yake na mrembo huyo wakiwa karibu, akionekana akimnong’oneza kwa upole kana kwamba macho yake yamefungwa na mvuto wa mrembo huyo. Staa huyo wa Dusuma hakuishia hapo, alienda mbali zaidi na kuwaomba mashabiki wake wamfikishie ujumbe mrembo huyo kwa kumtag, ishara kuwa hamtaki kumwachia apotee hivihivi. Mashabiki wake walichangamkia ombi hilo kwa utani na mzaha, huku wengine wakidai huenda Otile anaanza ukurasa mpya wa mapenzi. Kwa upande mwingine, wapo waliotaja tukio hilo kama kiki ya kuitangaza single yake mpya inayokwenda kwa jina la “Not For Me” Kwa sasa macho yote yameelekezwa kwa mjaka mfine huyo, huku mashabiki wakingoja kuona kama utamu wa tamasha la Luo Festival unaweza kugeuka kuwa simulizi jipya la mapenzi kwa Otile Brown.

Read More
 Otile Brown Aumizwa na Habari za Ndoa ya Nabayet, Aandika Ujumbe wa Hisia Kali

Otile Brown Aumizwa na Habari za Ndoa ya Nabayet, Aandika Ujumbe wa Hisia Kali

Mwanamuziki wa Bongo R&B kutoka Kenya, Otile Brown, ameibua hisia mtandaoni baada ya kuonyesha maumivu na mshangao kufuatia habari za aliyekuwa mpenzi wake, Nabayet kutoka Ethiopia, kufunga ndoa. Kupitia Insta Story yake, Otile alionekana kushindwa kuficha hisia zake, hasa kwa kuwa alimtaja Nabayet katika wimbo wake mpya unaotarajiwa kuachiwa. Ameandika:  “How does she go & get married after mentioning her on my new song dropping tomorrow… now I feel dueh…”,  Otile aliandika hisia nyingi Maneno hayo yameibua hisia mseto mitandaoni, huku mashabiki wake wakimfariji na wengine wakihisi kwamba bado ana hisia kwa mrembo huyo. Uhusiano wa Otile Brown na Nabayet ulikuwa wa muda mrefu na wa hadharani, uliovutia mashabiki wengi kutoka Afrika Mashariki na Ethiopia. Wawili hao walionekana kuwa na mahusiano yenye upendo mkubwa kabla ya kuachana kimya kimya miaka michache iliyopita. Kabla ya habari za ndoa ya Nabayet, Otile alikuwa ameonekana kuendelea na maisha, lakini ujumbe huu mpya unaonyesha pengine bado kuna hisia zilizobaki. Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu wimbo mpya wa Otile Brown ili kusikia alivyomzungumzia Nabayet, huku wengi wakijiuliza kama hii itaathiri maudhui au hisia za kazi hiyo.

Read More
 Nabayet, Mpenzi wa Zamani wa Otile Brown, Afunga Ndoa Kwenye Harusi ya Kifahari Ethiopia

Nabayet, Mpenzi wa Zamani wa Otile Brown, Afunga Ndoa Kwenye Harusi ya Kifahari Ethiopia

Mwanamitindo maarufu kutoka Ethiopia,Nabayet, ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa msanii nyota wa Kenya Otile Brown, ameaga rasmi maisha ya u-single baada ya kufunga ndoa kwenye harusi ya kifahari iliyofanyika nchini mwake mwishoni mwa wiki. Harusi hiyo, iliyohudhuriwa na familia, marafiki wa karibu na watu mashuhuri kutoka sekta ya mitindo na burudani, ilifanyika katika hoteli ya kifahari jijini Addis Ababa. Nabayet alionekana mrembo kupindukia akiwa amevalia gauni jeupe la harusi lililobuniwa na mbunifu maarufu wa mitindo wa Ethiopia. Video na picha za tukio hilo zimeenea kwenye mitandao ya kijamii, huku mashabiki wakimpongeza kwa hatua hiyo mpya katika maisha yake. Ingawa hakufichua jina la mchumba wake, mashabiki walionekana kushangilia penzi jipya la mrembo huyo ambaye amekuwa akipunguza sana kuweka maisha yake ya kimapenzi hadharani. Nabayet aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Otile Brown mwaka 2019, na wawili hao walivutia mashabiki wengi kwa mahusiano yao ya kuvutia yaliyokuwa yakisambazwa kupitia mitandao ya kijamii. Hata hivyo, uhusiano huo uliisha baada ya muda kutokana na tofauti zao za kimtazamo. Otile Brown bado hajatoa kauli rasmi kuhusu harusi hiyo ya mpenzi wake wa zamani. Mashabiki wa Nabayet wameendelea kumpongeza kwa hatua hiyo kubwa, wakimtakia heri katika maisha mapya ya ndoa.

Read More
 Otile Brown atangaza ujio wake mpya 2023

Otile Brown atangaza ujio wake mpya 2023

Mwimbaji nyota wa kizazi kipya nchini Kenya, Otile Brown hataki kuwaacha mashabiki wake hivi hivi kabla mwezi huu haujaisha. Hii ni baada ya kutangaza ujio wa ngoma yake mpya ambayo kwa mujibu wake itaingia sokoni Jumanne wiki ijayo, Januari 31. Otile ameitaja ngoma hiyo aliyoipa jina la Shujaa wako kuwa ni kolabo yake ya Kimataifa akiwa na mwanamuziki kutoka nchini Tanzania, Ruby. Hii itakuwa ni Kazi yake ya kwanza kwa mwaka 2023 ikizingatiwa kuwa hajaachia wimbo wowote tangu mwaka jana alipowabariki mashabiki zake na wimbo uitwao Do It alioshirikisha Vivian.

Read More
 Rayvanny na Otile Brown waingia studio kurekodi kolabo yao

Rayvanny na Otile Brown waingia studio kurekodi kolabo yao

Wanamuziki nyota wanaoiwakilisha vyema Afrika Mashariki, wasanii Rayvanny na Otile Brown wameingia studio na wameonekana kwenye upishi wa kazi mpya. Wawili hao wanatajwa kuingia studio usiku wa kuamkia leo katika studio za Next Level Music zilizopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam, zilizo chini ya msanii Rayvanny. Hata hivyo, bado haijafamika kuwa hii itakuwa ni kazi ya nani, tarajia kuipata kazi hiyo kutoka kwa wawili hao siku za usoni.

Read More
 Otile Brown arudishiwa laptop zake zilizoibiwa

Otile Brown arudishiwa laptop zake zilizoibiwa

Msanii kutoka nchini Kenya Otile Brown tayari amepata laptop zake mbili zilizoibiwa alipotua nchini Tanzania siku ya jana. Kupitia video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Otile amethibitisha kupokea laptops hizo aina Mac Book ambayo alizipoteza katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Meneja wa msanii huyo Reginald Noriega amefichua kwamba walifanya uchunguzi walifanikiwa kuzipata kompyuta hizo eneo la kinondoni viungani mwa Jijini Dar es Salaam. Kauli ya Otile Brown imekuja mara baada ya kutoa ahadi ya kuwalipa watakaomrejesha laptops hizo kutokana na stakabadhi zake muhimu ambazo zilikuwa ndani.

Read More
 Otile Brown awaomba mashabiki kumrejeshea laptop zake zilizoibiwa Tanzania

Otile Brown awaomba mashabiki kumrejeshea laptop zake zilizoibiwa Tanzania

Staa wa muziki nchini Kenya Otile Brown ametoa rai kwa mashabiki zake wa Tanzania kumrejeshea kompyuta zake mbili za mkononi zilizopotea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kupitia instagram live amesema yupo radhi kutoa kiasi chochote fedha kwa mtu yeyote atakayemrejeshea laptop hizo kwani zimemkosesha usingizi. Aidha ameahidi kuwa hana mpango wa kufungulia mashtaka mtu yeyote atakajitokeza kumrudishia kompyuta zake aina MacBook kutokana na uhitaji wa stakabadhi zake muhimu zilizomo ndani.

Read More
 Otile Brown aibiwa laptop mbili nchini Tanzania

Otile Brown aibiwa laptop mbili nchini Tanzania

Nyota wa muziki nchini, Otile Brown amedai kuibiwa laptop zake mbili aina ya MacBook akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Kupitia insta story yake Otile ambaye ametua nchini Tanzania asubuhi ya leo kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki ameeleza kuwa walinzi pamoja na watoa huduma walikataa kumpa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuchunguza tukio zima kupitia kamera za CCTV zilizopo eneo hilo. “”So kwenye airport ya Julius Nyerere nimeibiwa Mac/laptop mbili ila walinzi na watoa huduma wamekataa kutusaidia ndani ya masaa 3 wamekataa kuchunguza kwenye cctv … longest night of my life.Tumetoa hadi report ya police ambayo ndio utaratibu lakini wakakataa… nimeumia sana,” Ameandika. Hata hivyo hakufichua thamani ya vifaa vyake vya kielektroniki ambavyo vimetoweka katika uwanja wa ndege.

Read More
 Otile Brown aachia rasmi Extended Playlist yake mpya

Otile Brown aachia rasmi Extended Playlist yake mpya

Mwanamuziki kutoka Kenya Otile brown ameachia rasmi Extended playlist yake mpya baada ya ukimya wa miezi mitatu EP hiyo iitwayo Terminator ina jumla ya nyimbo tano za moto akiwa amewashirikisha wakali kama Vivian, Ilogos na The Ben. Terminator EP ina nyimbo kama Kolo Kolo, Terminator, By My Side, Hatima, Do It na inapatikana Exclusive kwenye majukwaa yote ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni. Hii ni EP ya pili kwa mtu mzima Otile Brown baada ya Uptown Flex iliyotoka mapema mwaka huu ikiwa na jumla ya singles 4 za moto.

Read More
 Otile Brown awajibu waliomjia juu kuhusu Kiswahili

Otile Brown awajibu waliomjia juu kuhusu Kiswahili

Mwanamuziki nyota nchini Otile Brown ameamua kuwajibu wanaoendelea kumponda mtandaoni baada ya kutoa maoni yake kuwa lugha ya Kiswahili inayotumika na wasanii wa Kenya ndio sababu kubwa inayowafanya wasifanye vizuri kimataifa kama wanavyofanya wasaniii wa Nigeria. Kupitia mfululizo wa instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Otile amesema kuwa lugha ya Kiswahili ndio lugha ambayo imempa mafanikio makubwa kisanaa huku akiwataka wanaomkosoa kuelewa kwanza alichokisema kabla ya kuleta ubishi. Hitmaker huyo “I Need You” amesema hakuwa na nia ya kuishusha lugha ya Kiswahili ambayo imemtoa kimuziki ila alikuwa anajaribu kuanzisha mjadala utakaowasaidia wasanii wa Kenya kuchanganya lugha ya Kiingereza kwenye nyimbo ili waweze kupenya kimataifa. Hata hivyo amemalizia kwa kusisitiza kuwa ataendelea kuimba nyimbo zake kwa lugha ya Kiswahili huku akitoa changamoto kwa jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza mjadala wa lugha kwenye nyimbo za wasanii kama njia moja ya kupata suluhu ya kizingiti inayokwamisha muziki wa ukanda huu kufika kimataifa.

Read More
 Otile Brown afunguka kuhusu kujipendekeza kwa mpenzi wake wa zamani Nabayet

Otile Brown afunguka kuhusu kujipendekeza kwa mpenzi wake wa zamani Nabayet

Staa wa muziki nchini Otile Brown amewajibu wanaodai kuwa anajipendekeza kwa mpenzi wake wa zamani Nabayet licha ya mahusiano yao kuvunjika. Otile ambaye amerejea nchini baada ya kukamilisha ziara ya miezi miwili nchini marekani amewashangaa wanaomsema vibaya kuwa bado anamzimia kimapenzi mrembo huyo kwa kusema kuwa hajutii kitendo cha kumtumia salamu za heri kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwake kwani ni moja kati ya watu ambao anawapenda sana. Otile Brown na Nabayet walikuwa kwenye mahusiano kwa kipindi cha miaka miwili lakini mahusiano yalikuja kuvunjika mwaka wa 2020 kutokana na umbali kati yao. Utakumbuka mwaka wa 2019 Otile Brown aliachia wimbo wa kusifia urembo wa Nabayet baada ya penzi lao kunoga.

Read More
 Kiswahili inawakwamisha wasanii wa Kenya kutusua kimataifa – Asema Otile Brown

Kiswahili inawakwamisha wasanii wa Kenya kutusua kimataifa – Asema Otile Brown

Msanii nyota nchini Otile Brown amefunguka kuwa miongoni mwa vitu vinavyowakwamisha wasanii wa Kenya kufanya vizuri kimataifa ni lugha. Katika mkao na waandishi wa habari Otile amedai kuwa endapo wasanii wa Kenya wangekuwa wanaimba kwa lugha ya kingereza basi wangekua na uwanja mkubwa wa kusikika kimataifa zaidi na kupata shows tofauti tofauti za nje ya nchi. Hitmaker huyo wa “Run Up” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa tofauti ya muziki wa Kenya na Nigeria ni lugha pekee na ndio sababu kubwa ambayo hawawezi kushindana na wasanii kutoka taifa hilo la Afrika Magharibi. Hata hivyo ametoa changamoto kwa wasanii nchini kuanza kutumia lugha ya kiingereza kwenye nyimbo zao ili muziki wa Kenya uweze kufika mbali zaidi. Utakumbuka Otile Brown amekuwa nchini Marekani kwa miezi miwili ambako amekuwa akifanya shows kwenye miji mbali mbali nchini humo.

Read More