Meneja wa Otile Brown awapa mapromota utaratibu mpya wa kumpata msanii wake

Meneja wa Otile Brown awapa mapromota utaratibu mpya wa kumpata msanii wake

Meneja wa Otile Brown, Noriega amewapa utaratibu mpya mapromota wa kimataifa watakaompatia msanii wake shows. Kupitia instastory Noriega amewataka wahakikishe kuwa wanamtumia Otile Brown na timu yake ndege binafsi. Aidha amesema nyakati za Otile brown kugharamikia nauli ya ndege kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya shows zimepita na wakati huku akisema kuwa ni lazima ndege binafsi itajumuishwa kwenye mkataba kati ya uongozi wa Otile na mapromota wa kigeni. ” This before … Sahizi ni Private Jet kwa contract,” Ujumbe wa Noriega unasomeka instastory. Kauli ya Noriega imekuja mara baada ya promota aliyempa mwaliko msanii otile brown nchini marekani kugharamia usafiri wa msaniii huyo kupitia ndege binafsi ya daraja la juu.

Read More
 OTILE BROWN AINGILIA SAKATA LA MSANII FAVE KUDHULUMIWA NA PROMOTA

OTILE BROWN AINGILIA SAKATA LA MSANII FAVE KUDHULUMIWA NA PROMOTA

Nyota wa muziki nchini Otile Brown amefunguka kuhusu sakata la msanii wa Nigeria Fave kudhulumiwa na promota baada ya kukamilisha ziara yake ya kimuziki nchini. Kupitia instastory Otile amesema pana haja ya mapromota wa Kenya kuchukulia biashara kama suala la muda mrefu badala ya kuwadhulumu washirika wao ambao wana mchango mkubwa kwenye mafanikio ya shughuli zao. Hitmaker huyo wa “Celebration” amewakosoa mapromota waliomleta Fave nchini Kenya kwa kutokuwa na mipango mizuri ya kufanikisha show ya msanii huyo huku akisisitiza kuwa mawasiliano ni jambo la msingi kwenye biashara yeyote yenye mafanikio.

Read More
 OTILE BROWN AZUA GUMZO MTANDAONI NA SOKSI YA KSHS. 32,000

OTILE BROWN AZUA GUMZO MTANDAONI NA SOKSI YA KSHS. 32,000

Msanii nyota nchini Otile Brown ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho. Mkali huyo wa “Celebration” kupitia Instastory ametuonesha soksi ambazo kwa mujibu wake zilimgharimu shillingi 32,000 za Kenya. Hatua hiyo imeonekana kuleta ukakasi miongoni mwa mashabiki zake, wengi wakionekana kumkejeli kwa kusema kuwa anatumia suala hilo kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni Hii sio mara ya kwanza kwa Otile Brown kuanika vitu vya thamani anavyovimiliki, mapema mwaka huu alitusanua kuwa alitumia kiasi cha shillingi elfu 80 za Kenya kununua viatu aina Balenciaga Crocs boots.

Read More
 OTILE BROWN AWACHANA WANAOKOSOA MUZIKI WAKE

OTILE BROWN AWACHANA WANAOKOSOA MUZIKI WAKE

Mwanamuziki nyota nchini Otile Brown amewatolea uvivu  baadhi ya mashabiki wanaozidi kumkosoa baada ya kuacha kuimba nyimbo zake kwa lugha ya Kiswahili na kugeukia Kiingereza. Kupitia mfululizo wa insta stories kwenye ukurasa wake wa Instagram, Otile amewataka wanaopinga juhudi zake za kuupeleka muziki wake kimataifa kuanza kujifunza kuhusu mitindo mbali mbali ya muziki huku akienda mbali zaidi na kudai kuwa ataendelea kutoa muziki mzuri kwa lugha ya Kiingereza kwani hatotishwa na maneno ya watu mtandaoni. “Fk the humble shit for a sec … do y’all even to pay to my kizungu songs au kisa mnapenda Kiswahili mnaboeka ata before y’all give it a chance … mimi ukinipa nafasi nakalisha Africa nzima na dunia kwa ujumla kwani ni Siri”, Aliandika Katika hatua nyingine, Hitmaker huyo wa ngoma ya “Celebration” amesema kuwa hana muda wa kuuthibitisha ulimwengu mafanikio yake kisanaa kwa kuwa ana kipaji cha kipekee kwenye tasnia ya muziki barani Afrika na kote duniani. “Na by the way nyimbo za Kiswahili kwangu hamuezi kumaliza msion … sihitaji kuprove chochote uwezo wangu mnaujua … sitochoka kufanya kufanya nyimbo za kimataifa kisa woga … find taste …”  Alisisitiza

Read More
 OTILE BROWN ASHINDWA KUFICHA HISIA ZAKE KWA MICHELE BRAXTON

OTILE BROWN ASHINDWA KUFICHA HISIA ZAKE KWA MICHELE BRAXTON

Mwanamuziki maarufu nchini Otile Brown ameshindwa kuendelea kuficha hisia zake za ndani juu ya mapenzi aliyonayo kwa staa wa muziki wa Rnb kutoka Marekani, Toni Michele Braxton. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Otile ameweka wazi hisia zake  kwa Michele Braxton kwa kudai kwamba amekuwa akimzimia kimapenzi mwanamuziki huyo kwa muda mrefu na bado anaendelea kuhusudu penzi lake. “Still crushing on her,” Otile ameandika. Hitmaker huyo wa ngoma ya Jeraha ameenda mbali zaidi na kumpa maua yake mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 54 kwa kusema kwamba ni moja kati ya wanawake warembo zaidi duniani ambao wapo hai. “One of the sexiest women God ever created,” Amesisitiza. Hata hivyo mashabiki wametoa hisia mbali mbali kuhusiana kauli hiyo ya Otile Brown huku wengi wakisema wameumizwa na kitendo cha msanii huyo kumzimia kimapenzi mtu mwingine licha ya kuwa wamekuwa wakimtamani kimapenzi. Utakumbuka Braxton ambaye anatajwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Rapa Birdman amejaliwa kuwapata watoto wawili ambao ni, Diezel Ky Braxton na Denim Cole.

Read More
 OTILE BROWN AFUNGUKA NAMNA WANIGERIA WANATEGEMEA SOKO LA KENYA KUTANGAZA MUZIKI WAO

OTILE BROWN AFUNGUKA NAMNA WANIGERIA WANATEGEMEA SOKO LA KENYA KUTANGAZA MUZIKI WAO

Staa wa muziki nchini Otile Brown Otile Brown amefunguka jinsi ambavyo Wanigeria wanatumia soko la muziki wa Kenya kutangaza muziki wao Kulingana na Otile Brown wasanii wa Nigeria wanategemea soko la Kenya kufanya nyimbo zao ziwe kubwa zaidi kwa kuwa wanatumia pesa nyingi kuhonga vituo vya redio nchini ili viweze kucheza nyimbo zao. Hitmaker huyo ngoma ya “Woman” amesema nyimbo nyingi za Nigeria zimeshindwa kupenya kwenye soko la muziki hadi pale wakenya kwenye mtandao wa tiktok wanapoanza kuzitumia kwenye video zao. Hata hivyo ametoa changamoto kwa vyombo vya habari  nchini kuunga mkono kazi za wasanii wa humu nchini bila kubagua ili muziki wa kenya uweze kutabulika katika mataifa mengine.

Read More
 OTILE BROWN ATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WAKAAZI WA MIKINDANI, MOMBASA

OTILE BROWN ATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WAKAAZI WA MIKINDANI, MOMBASA

Staa wa muziki nchini Otile Brown ameonesha kuwa na moyo wa shukrani baada ya kutoa Msaada kwa wakaazi Mikindani, Mombasa. Otile Brown ambaye alizaliwa na kukulia Mikindani  ametoa msaada wa vyakula ikiwemo unga,mafuta ya kupikia na mahitaji mengine ya msingi. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Run Up” ameeleza nia ya kufanya hivyo ni kurudisha fadhila kwa jamii kutokana na mchango mkubwa alioupata kupitia muziki wake. Hata hivyo wakaazi wa Mikindani wameonekana kumshuruku mwanamuziki huyo kwa moyo ukarimu wa kurudisha mkono kwa jamii.

Read More
 OTILE BROWN AFUNGUKA SABABU ZA KUACHANA NA NABAYET

OTILE BROWN AFUNGUKA SABABU ZA KUACHANA NA NABAYET

Msanii wa muziki nchini, Otile Brown amesema moja ya sababu ya kuachana na mpenzi wake, Nabayet (Nabii) kutokea Ethiopia ni mrembo huyo kutokuwa tayari kuhamia nchini Kenya. Akizungumza na Presenter Ali, Otile Brown amesema Nabayet alishindwa kuhamia Kenya kwa sababu ya baadhi ya masuala ya kifamilia ambayo yalikuwa muhimu sana katika tamaduni za Waethiopia. Mahusiano hayo ya muda mrefu hayakufaulu kwa sababu zisizoweza kuepukika kwani wakati mwingine Nabii alikuwa akichukua muda mrefu sana kurejea Kenya. Otile ambaye amewahi kuwa na mrembo Vera Sidika kipindi cha nyuma, alisema kuwa wote wawili walikubali na kuamua kuachana, na labda ikiwa imepangwa wao kuoana, inaweza kutokea siku zijazo.

Read More
 OTILE BROWN ALAMBA DILI NONO LA KUWA BALOZI TECNO

OTILE BROWN ALAMBA DILI NONO LA KUWA BALOZI TECNO

Mwanamuziki nyota nchini Otile Brown amelamba dili nono la kuwa balozi mpya wa Simu ya mkono ya Tecno Camon 19 kwa upande wa Kenya. Otile Brown ametangaza habari njema kwa wafuasi wake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ana furaha kubwa kujiunga na familia ya Tecno inayojishughulisha na  uzalishaji na usambazaji wa simu na vifaa vingine vya kielectroniki “I am really thrilled and excited to officially announce my partnership with @tecnomobile @tecnokenya as their Brand Ambassador and the Chief Creative Officer for the TECNO CAMON 19 Series. Super Super Excited for this great partnership #CAMON19BA #TECNO #TECNOKENYA.” Otile Brown ameandika Otile Brown sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za Tecno kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuiongezea kampuni hiyo mauzo.

Read More
 OTILE BROWN AKOSHWA NA KIPAJI CHA ABBY CHAMS, ATHIBITISHA COLLABO

OTILE BROWN AKOSHWA NA KIPAJI CHA ABBY CHAMS, ATHIBITISHA COLLABO

Staa wa Muziki Nchini Otile Brown ameshindwa kujizuia na kufunguka hadharani jinsi anavyomukubali Msanii wa Kike kutoka Tanzania Abby Chams. Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Otile ameonesha kuukubali uwezo wa Mrembo huyo kwa kushare picha ya wimbo wa Rayvanny aliomshirikisha Abby Chams, STAY na kuandika ujumbe unaosomeka ” abby_chams Mashallah  coming to tanzania anytime Inshallah hopn to meet you queen ” Ujumbe huo umewaaminisha mashabiki kuwa huenda wawili wana mpango wa kuja na wimbo wa pamoja hivi karibuni. Iwapo Otile Brown atafanikisha suala la kuachia wimbo wa pamoja na Abby Chams itakuwa ni kazi yake ya tatu kufanya na msanii wa Bongofleva ikizingatiwa tayari ana collabo na Ali Kiba na Harmonize.

Read More
 OTILE BROWN ARIPOTIWA KUNUNUA SUITCASE YENYE THAMANI YA  SHILLINGI 4 ZA KENYA

OTILE BROWN ARIPOTIWA KUNUNUA SUITCASE YENYE THAMANI YA SHILLINGI 4 ZA KENYA

Imekuwa kawaida sasa kwa mastaa Duniani kumwaga mamilioni ya pesa hasa kwenye vito vya thamani, magari pamoja na majumba ya kifahari Staa wa muziki nchini Otile Brown ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho. Mkali huyo wa “Rup Up” ametumia kiasi cha zaidi ya shillingi milioni  485,000 za Kenya kununua Suitcase aina ya Louis Vuiton. Hii ni kwa mujibu wa picha ambazo alizishare kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akitua nchini akitokea Afrika Kusini ambako amekuwa vacations kwa wiki mbili sasa. Hii ni mara ya pili kwa mtu mzima Otile BROWN kununua vitu ya thamani kubwa. Mwezi Machi mwaka huu alinunua pia viatu aina Balenciaga Crocs boots kama zawadi ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake iliyomgharimu kiasi cha shillingi elfu 80 za Kenya.

Read More
 OTILE BROWN AWAKINGIA KIFUA WASANII WA KENYA

OTILE BROWN AWAKINGIA KIFUA WASANII WA KENYA

Staa wa muziki nchini Otile Brown amewajibu baadhi ya watu wanaowakosoa wasanii wa Kenya wakidai kuwa wamefulia kiuchumi. Kupitia Instagram Otile Brown amewakingia kifua wasanii wa Kenya kwa kusema kwamba wana mafanikio makubwa kiuchumi Barani Afrika kuliko wasanii wanaozungumzia sana kwenye vyombo vya habari. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Run Up” amewatolea uvivu wadau muziki nchini akisema kwamba wameshindwa na biashara ya muziki na badala yake wamegeukia kuwatupia lawama wasanii wakenya ambao wanaendelea kutia bidii kupitia kazi zao kila uchao. Utakumbuka Otile Brown amekuwa akiwatetea wasanii wa kenya pindi wanapokosolewa kwenye muziki wao lakini pia amekuwa akiwahimiza wakenya kuunga mkono wasanii wao badala ya kuwasapoti wasanii wa nje.

Read More