OTILE BROWN ATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WAKAAZI WA MIKINDANI, MOMBASA

OTILE BROWN ATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WAKAAZI WA MIKINDANI, MOMBASA

Staa wa muziki nchini Otile Brown ameonesha kuwa na moyo wa shukrani baada ya kutoa Msaada kwa wakaazi Mikindani, Mombasa. Otile Brown ambaye alizaliwa na kukulia Mikindani  ametoa msaada wa vyakula ikiwemo unga,mafuta ya kupikia na mahitaji mengine ya msingi. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Run Up” ameeleza nia ya kufanya hivyo ni kurudisha fadhila kwa jamii kutokana na mchango mkubwa alioupata kupitia muziki wake. Hata hivyo wakaazi wa Mikindani wameonekana kumshuruku mwanamuziki huyo kwa moyo ukarimu wa kurudisha mkono kwa jamii.

Read More
 OTILE BROWN AFUNGUKA SABABU ZA KUACHANA NA NABAYET

OTILE BROWN AFUNGUKA SABABU ZA KUACHANA NA NABAYET

Msanii wa muziki nchini, Otile Brown amesema moja ya sababu ya kuachana na mpenzi wake, Nabayet (Nabii) kutokea Ethiopia ni mrembo huyo kutokuwa tayari kuhamia nchini Kenya. Akizungumza na Presenter Ali, Otile Brown amesema Nabayet alishindwa kuhamia Kenya kwa sababu ya baadhi ya masuala ya kifamilia ambayo yalikuwa muhimu sana katika tamaduni za Waethiopia. Mahusiano hayo ya muda mrefu hayakufaulu kwa sababu zisizoweza kuepukika kwani wakati mwingine Nabii alikuwa akichukua muda mrefu sana kurejea Kenya. Otile ambaye amewahi kuwa na mrembo Vera Sidika kipindi cha nyuma, alisema kuwa wote wawili walikubali na kuamua kuachana, na labda ikiwa imepangwa wao kuoana, inaweza kutokea siku zijazo.

Read More
 OTILE BROWN ALAMBA DILI NONO LA KUWA BALOZI TECNO

OTILE BROWN ALAMBA DILI NONO LA KUWA BALOZI TECNO

Mwanamuziki nyota nchini Otile Brown amelamba dili nono la kuwa balozi mpya wa Simu ya mkono ya Tecno Camon 19 kwa upande wa Kenya. Otile Brown ametangaza habari njema kwa wafuasi wake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ana furaha kubwa kujiunga na familia ya Tecno inayojishughulisha na  uzalishaji na usambazaji wa simu na vifaa vingine vya kielectroniki “I am really thrilled and excited to officially announce my partnership with @tecnomobile @tecnokenya as their Brand Ambassador and the Chief Creative Officer for the TECNO CAMON 19 Series. Super Super Excited for this great partnership #CAMON19BA #TECNO #TECNOKENYA.” Otile Brown ameandika Otile Brown sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za Tecno kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuiongezea kampuni hiyo mauzo.

Read More
 OTILE BROWN AKOSHWA NA KIPAJI CHA ABBY CHAMS, ATHIBITISHA COLLABO

OTILE BROWN AKOSHWA NA KIPAJI CHA ABBY CHAMS, ATHIBITISHA COLLABO

Staa wa Muziki Nchini Otile Brown ameshindwa kujizuia na kufunguka hadharani jinsi anavyomukubali Msanii wa Kike kutoka Tanzania Abby Chams. Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Otile ameonesha kuukubali uwezo wa Mrembo huyo kwa kushare picha ya wimbo wa Rayvanny aliomshirikisha Abby Chams, STAY na kuandika ujumbe unaosomeka ” abby_chams Mashallah  coming to tanzania anytime Inshallah hopn to meet you queen ” Ujumbe huo umewaaminisha mashabiki kuwa huenda wawili wana mpango wa kuja na wimbo wa pamoja hivi karibuni. Iwapo Otile Brown atafanikisha suala la kuachia wimbo wa pamoja na Abby Chams itakuwa ni kazi yake ya tatu kufanya na msanii wa Bongofleva ikizingatiwa tayari ana collabo na Ali Kiba na Harmonize.

Read More
 OTILE BROWN ARIPOTIWA KUNUNUA SUITCASE YENYE THAMANI YA  SHILLINGI 4 ZA KENYA

OTILE BROWN ARIPOTIWA KUNUNUA SUITCASE YENYE THAMANI YA SHILLINGI 4 ZA KENYA

Imekuwa kawaida sasa kwa mastaa Duniani kumwaga mamilioni ya pesa hasa kwenye vito vya thamani, magari pamoja na majumba ya kifahari Staa wa muziki nchini Otile Brown ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho. Mkali huyo wa “Rup Up” ametumia kiasi cha zaidi ya shillingi milioni  485,000 za Kenya kununua Suitcase aina ya Louis Vuiton. Hii ni kwa mujibu wa picha ambazo alizishare kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akitua nchini akitokea Afrika Kusini ambako amekuwa vacations kwa wiki mbili sasa. Hii ni mara ya pili kwa mtu mzima Otile BROWN kununua vitu ya thamani kubwa. Mwezi Machi mwaka huu alinunua pia viatu aina Balenciaga Crocs boots kama zawadi ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake iliyomgharimu kiasi cha shillingi elfu 80 za Kenya.

Read More
 OTILE BROWN AWAKINGIA KIFUA WASANII WA KENYA

OTILE BROWN AWAKINGIA KIFUA WASANII WA KENYA

Staa wa muziki nchini Otile Brown amewajibu baadhi ya watu wanaowakosoa wasanii wa Kenya wakidai kuwa wamefulia kiuchumi. Kupitia Instagram Otile Brown amewakingia kifua wasanii wa Kenya kwa kusema kwamba wana mafanikio makubwa kiuchumi Barani Afrika kuliko wasanii wanaozungumzia sana kwenye vyombo vya habari. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Run Up” amewatolea uvivu wadau muziki nchini akisema kwamba wameshindwa na biashara ya muziki na badala yake wamegeukia kuwatupia lawama wasanii wakenya ambao wanaendelea kutia bidii kupitia kazi zao kila uchao. Utakumbuka Otile Brown amekuwa akiwatetea wasanii wa kenya pindi wanapokosolewa kwenye muziki wao lakini pia amekuwa akiwahimiza wakenya kuunga mkono wasanii wao badala ya kuwasapoti wasanii wa nje.

Read More
 OTILE BROWN AKOSHWA NA MFUMO WA MUZIKI WA AFRIKA KUSINI

OTILE BROWN AKOSHWA NA MFUMO WA MUZIKI WA AFRIKA KUSINI

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Otile Brown ameusifia mfumo wa muziki wa Afrika Kusini ambao ameutaja kuulinda zaidi muziki wa ndani kwa kutoupa nafasi muziki wa mataifa mengine ndani ya nchi hiyo. Kupitia nstastory yake kwenye mtandao wa Instagram Otile Brown amedai kuwa kwenye kiwanda cha muziki nchini Afrika Kusini kuna hali kujipa kipaumbele zaidi kwani nyimbo za wasanii wa ndani zinapiga sana kwenye maeneo ya umma tofauti na nchini ya Kenya ambayo imewazingatia sana wasanii wa nje huku akieleza kuwa inaweza kuwa moja kati ya sababu za muziki wao kuwa na thamani ya juu yenye maendeleo. Otile Brown ambaye juzi kati amekuwa nchini Afrika Kusini amesema mfumo wa muziki wa Afrika kusini umewapelekea wasanii wengi kuwa na mafanikio makubwa hata wakiwa na kazi chache walizozifanya kwenye career yao ya muziki ambapo ameonekana kutoa changamoto kwa serikali ya kenya kufuata nyayo za nchi ya Afrika kusini ambayo imetengeneza mazingira ya kutumia sanaa kutoa ajira kwa maelfu ya vijana wake. “Soko la muziki la Afrika Kusini halivumi sana lakini lina utajiri. Serikali imewatengenezea mazingirana wanajipenda sana unaweza kuwa na wimbo mkubwa Afrika na hawaujui maana huwezi sikia wimbo wa nje hata mmoja kwenye klabu, Migahawani au kwenye vyombo vya usafiri wowote”. Otile anaendelea kwa kuandika “Ni ubinafsi ila imenifanya nifikirie Je ni bora uwe hivyo na watu wenu wawe vizuri au uwe muungwana waku support nyimbo za nje na kupoteza nguvu na thamani ya sanaa yenu maana jamaa kimya game wanailinda nakuithamini maana inatengeneza ajira 100% kila siku. Jamaa mtu ananyimbo mbili tu lakini mafanikio makubwa sana.” ameandika kupitia Instastory yake

Read More
 OTILE BROWN AJIZAWADI VIATU YENYE THAMANI YA SHILLINGI 80,000 ZA KENYA

OTILE BROWN AJIZAWADI VIATU YENYE THAMANI YA SHILLINGI 80,000 ZA KENYA

Msanii nyota nchini Otile Brown ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho. Hii ni baada ya kutumia kiasi cha shillingi elfu 80 za Kenya kununua viatu aina Balenciaga Crocs boots kama zawadi ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake Machi 21 mwaka 2022. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hitmaker huyo wa ngoma ya “Fed Up” amechapisha video akionekana akizitoa viatu hivyo kwenye boksi huku akiwashukuru mashabiki zake kwa kusapoti muziki wake na kumfanya kuwa namba moja kwenye kiwanda cha muziki nchini.. Otile Brown ambaye kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini kwa ajili kusherekea birthday yake anaungana na rapa Kanye West  kutoka Marekani ambaye hupendelea kuvaa viatu aina ya Balenciaga Crocs Boots

Read More
 OTILE BROWN AIPONDA ALBUM MPYA YA ARROW BOY, ATISHIA KUFUTA WIMBO ALIOSHIRIKISHWA

OTILE BROWN AIPONDA ALBUM MPYA YA ARROW BOY, ATISHIA KUFUTA WIMBO ALIOSHIRIKISHWA

Staa wa muziki nchini Otile Brown ameonesha kukerwa na kitendo cha Arrow Boy kuushirikisha wimbo wao wa pamoja ambao haukuwa umekamilika kwenye album yake mpya iitwayo Focus. Kupitia instastory Otile Brown ametaja Arrow Boy kama mnafiki asiyejali maslahi ya wasanii wenzake kwa hatua yake ya kukwenda kinyume na mkataba wa makubaliano wa kutoachia demo ya wimbo wao wa pamoja huku akisema kwamba kitendo hicho huenda ikamshushia brand yake ya muziki. Hata hivyo wa ngoma ya “Fine By Me” amemtaka Arrow Boy auondowe wimbo wao uitwao “Show Me” kwenye album yake ya Focus kabla hajachukua hatua ya kuishusha mwenyewe wimbo huo kwenye digital platforms mbali mbali za kupakua na kusikiliza muziki duniani.

Read More
 OTIILE BROWN AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE YA MAHUSIANO

OTIILE BROWN AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE YA MAHUSIANO

Nyota wa muziki nchini Otile Brown, amesema licha ya kusumbuliwa na warembo kwa sasa hayupo kwenye mahusiano,yaani yupo ‘Single’. Mkali huyo anayefanya vizuri na EP yake mpya Uptown Flex amedai kwa sasa hataki kukurupuka kuingia kwenye mahusiano ya mapenzi kutokana na matukio aliyopitia kipindi cha nyuma. Otile Brown amefunguka hayo  kwenye Instagram live, mara baada ya mashabiki zake kutaka kujua upande wa maisha yake ya mahusiano baada ya kutangaza kuachana na mrembo mwenye asili ya nchi ya Ethiopia Nabayet wiki kadhaa zilizopita.

Read More
 OTILE BROWN AHITAJI MAOMBI KUHUSU AFYA YAKE

OTILE BROWN AHITAJI MAOMBI KUHUSU AFYA YAKE

Siku chache tu baada ya kufanyiwa upasuaji, mwanamuziki kutoka Kenya, Otile Brown amewaacha mashabiki wake katika hali ya wasiwasi kutokana na chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii. Otile Brown ametoa taarifa fupi kuhusu afya yake akifichua kwamba anashuhudia maumivu makali sana mwili mwake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amewasihi mashabiki wake kumkumbuka katika maombi yao huku akiendelea kuuguza maumivu yanayomkabili. “Nina maumivu makali sana, ombeeni Obizee” Brown ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram. Utakumbuka takriban siku tano zilizopita mwanamuziki huyo alifanyiwa upasuaji katika hospitali moja jijini Nairobi. Hata hivyo,hakueleza sehemu ya mwili wake ambayo ilifanyiwa upasuaji wala kilichokuwa kinamsumbua.

Read More
 OTILE BROWN KUACHIA UPTOWN FLEX EP ALHAMISI HII

OTILE BROWN KUACHIA UPTOWN FLEX EP ALHAMISI HII

Msanii nyota nchini Otile Brown ametangaza kuachia EP mpya chini ya  lebo yake ya muziki ya Just in Love ambayo ni zawadi kwa mashabiki zake kuelekea siku ya wapendanao maarufu kama Valentines Day. EP hiyo inakwenda kwa jina la Uptown Flex itakuwa na jumla ya nyimbo 5 ambazo amezifanya mwenyewe bila kumshirikisha msanii yeyote. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Otile Brown ameshare artwork pamoja na Tracklist ya EP hiyo ambayo ina nyimbo kama  Double up, Realer, Fine By Me,  Run Up na Sempre. Hata hivyo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kuipokea Uptown Flex  EP ambayo itaingia sokoni rasmi Februari 10 mwaka wa 2022. Hii inaenda kuwa EP ya kwanza kwa mtu mzima Otile Brown ikizingatiwa kuwa mwaka wa 202o aliwabariki mashabiki zake na Album iitwayo Just In Love ambayo ilikuwa na jumla ya mikwaju 11 ya moto.

Read More