OTILE BROWN AMVUA NGUO MREMBO MWENYE SHAPE MATATA NCHINI KENYA VERA SIDIKA

OTILE BROWN AMVUA NGUO MREMBO MWENYE SHAPE MATATA NCHINI KENYA VERA SIDIKA

Staa wa muziki nchini Otile Brown amemtolea uvivu mrembo mwenye shape matata Vera Sidika baada ya mrembo huyo kuonekana kulitaja jina lake katika siku za hivi karibuni. Kupitia instagram page yake Otile Brown amemtaka Vera Sidika kuitunza ndoa yake ikizingatiwa kuwa hajawahi kuizungumzia ndoa yake na mumewe brown mauzo sehemu yeyote kutokana na heshima aliyonao kwao. “Jaribu kumheshimu mumeo na kulinda ndoa yako kama ninavyojaribu kunyamaza kila unapotaja jina langu. Dont get comfortable.” Ameandika kupitia insta story yake. Kauli ya otile brown imekuja siku chache baada ya vera sidika kusema kuwa ikitokea otile brown anataka kufanya kolabo na mumwe Brown Mauzo ataunga mkono kikamilifu kolabo hiyo. Hili halikutarajiwa kabisa kutoka kwa Vera Sidika ikizingatiwa kuwa alikuwa kwenye mahusiano na Otile Brown kipindi cha nyuma ambapo walikuja wakaachana vibaya baada ya kuingia kwenye ugomvi mbaya. Kutokana na hilo inaonekana kwamba Vera sidika amepata furaha tena na labda alimsamehe Otile Brown ndiyo maana hajawahi kusema jambo lolote baya kumhusu.

Read More
 OTILE BROWN APOKEZWA TUZO YA DHAHABU NA YOUTUBE KWA KUFIKISHA SUBSCRIBERS MILIONI 1.

OTILE BROWN APOKEZWA TUZO YA DHAHABU NA YOUTUBE KWA KUFIKISHA SUBSCRIBERS MILIONI 1.

Staa wa muziki wa nchini  Otile Brown amepokezwa tuzo ya Golden creators na mtandao wa youtube kwa kufikisha jumla ya subscribers millioni 1. Mkali huyo wa “Jeraha” amewashukuru mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuendelea kufuatilia kazi zake ambazo zinaendelea kuonyesha mafanikio makubwa huku akiahidi kutoa mzuri kwa ajili yao . Otile Brown anakuwa msanii wa kwanza kutokea Kenya kuwa na wafuasi wengi zaidi katika mtandao wa YouTube huku Dusuma aliyomshirikisha Meddy ikiwa ndiyo video yenye watazamaji wengi zaidi ikiwa na views milioni 35 ndani ya mwaka mmoja. Baadhi ya wasanii kutoka Kenya wanaofuata kwa wafuasi wengi ni pamoja na Bahati Kenya  akiwa na subscribers elfu 902K, Willy Paul 877K, Sauti Sol  856K,  Khaligraph Jones 538K, na Nyashinski 473K.

Read More
 OTILE BROWN ATHIBITISHA KUACHANA NA MPENZI WAKE WA SIKU NYINGI NABAYET

OTILE BROWN ATHIBITISHA KUACHANA NA MPENZI WAKE WA SIKU NYINGI NABAYET

Staa wa muziki nchini Otile Brown, ametangaza kuachana na Mpenzi wake raia wa Ethiopia Nabayet baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miaka mitatu. Kupitia ukurasa wake wa instagram  Otile Brown amesema amechukua maamuzi ya kuachana na mpenzi wake huyo baada ya kuafikia makubaliano ya pamoja ambapo amedai kuwa wataendelea kuwa marafiki. Hata hivyo chanzo cha wawili hao kuachana hajaweka wazi ila sio mara ya kwanza kufanya hivyo kwani kipindi cha nyuma wamekuwa na mazoea ya kuachana na kisha mwisho wa siku wanarudiana Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji huenda Otile Brown anatengeza  mazingira ya kumzinguziwa kabla ya ujio wa ngoma yake mpya Ikumbukwe kuwa penzi la Otile Brown na Nabayet lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka 2018  miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Verah Sidika.

Read More
 ALBUM YA OTILE BROWN “JUST IN LOVE” YAWEKA REKODI BOOMPLAY KENYA

ALBUM YA OTILE BROWN “JUST IN LOVE” YAWEKA REKODI BOOMPLAY KENYA

Staa wa muziki nchini, Otile Brown anaendelea kupokea upendo na support kubwa kutoka kwa mshabiki wake kiasi cha kufanya vizuri na album yake  ‘Just In Love’. Hadi kufikia sasa katika mtandao wa boomplay album hiyo imeweza kusikilizwa  zaidi ya mara millioni 17.3 ikiwa ni takriban miaka miwili tangu itokea rasmi. Kwa mafanakio hayo, Album ya just in love  ndio Album iliyosikilizwa zaidi kwenye mtandao wa boomplay kwa wasanii wa humu nchini. Utakumbuka album ya just in love kutoka kwa mtu mzima otile brown iliachiwa rasmi Juni 3 mwaka wa 2020 ikiwa na jumla ya mikwaju 10 ya moto.

Read More
 OTILE BROWN AFIKISHA SUBSCRIBERS MILLIONI MOJA KWENYE MTANDAO WA YOUTUBE

OTILE BROWN AFIKISHA SUBSCRIBERS MILLIONI MOJA KWENYE MTANDAO WA YOUTUBE

Nyota wa muziki Otile Brown anazidi kujikita kileleni kwenye mtandao wa YouTube ambapo kwa sasa amefikisha idadi ya subscribers Milioni 1 kwenye mtandao huo. Hii inamfanya Hitmaker huyo wa “Jeraha” kuendelea kukaa kileleni kama msanii anayeongoza kwa idadi kubwa ya subscribers kwenye Mtandao wa Youtube kwa wasanii wa Kenya. Sanjari na hilo, Mkurugenzi wa lebo ya muziki ya Just in Love na hadi sasa Kupitia channel yake ya YouTube kazi zake zimetazamwa zaidi ya mara milioni  251 tangu ilipofunguliwa rasmi Aprili 20 mwaka 2016. Wasanii wengine kutoka Kenya ambao wapo mbioni kufikisha subscribers millioni moja kwenye mtandao wa youtube ni pamoja na Bahati ambaye ana subscribers laki 9, na Sauti sol ambao wana subscribers laki 8

Read More
 HARMONIZE NA OTILE BROWN WAINGIA LOCATION KUTAYARISHA VIDEO YA WIMBO WAO

HARMONIZE NA OTILE BROWN WAINGIA LOCATION KUTAYARISHA VIDEO YA WIMBO WAO

Msanii wa Bongofleva Harmonize na Otile Brown wameingia location kuitayarisha video ya wimbo wao ambao unahisiwa huenda ukapatikana kwenye EP yao ya pamoja. Harmonize amethibitisha hilo kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram kwa kushare misururu ya picha wakiwa chimbo na mkali huyo kutoka Kenya jambo ambalo limewaaminisha mashabiki muziki mzuri Afrika Mashariki kuwa wawili hao wapo kwenye maandalizi ya video ya wimbo wa pamoja. Kupitia post hiyo Harmonize hajaweka wazi nini hasa wanapika na Otile Brown ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wanahoji huenda Otile Brown akawa mmoja wa wasanii atakaotumbuiza Disemba 31 mwaka huu kwenye listening party ya album yake ya High Schoolhuko Palm Village, Mikocheni, Dar e Salaam. Juzi kati Otile Brown alisifia uwezo wa Harmonize katika verse ya wimbo wao wa pamoja waliofanya kwa mara ya kwanza ambapo alisema msanii huyo wa Bongofleva alifanya vizuri katika ngoma hiyo huku akieleza fahari yake kwa mashabiki wa Tanzania na Kenya ambao watakuwa tayari kusikia kazi hiyo Itakumbukwa Harmonize  akiwa nchini katika ziara yake ya kimuziki alitangaza wazi kuja na ‘EP’ itakayo kuwa na nyimbo 5 za pamoja kati yake na Otile Brown.

Read More
 OTILE BROWN ASIFIA UWEZO WA HARMONIZE KWENYE NGOMA YAO YA KWANZA

OTILE BROWN ASIFIA UWEZO WA HARMONIZE KWENYE NGOMA YAO YA KWANZA

Mkali wa muziki nchini Otile Brown amesifia uwezo wa msanii wa Bongofleva Harmonize katika verse ya wimbo wao wa pamoja waliofanya kwa mara ya kwanza. Otile Brown ametumia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram  kuelezea hilo, ambapo amesema Harmonize amefanya vizuri katika ngoma hiyo huku akieleza fahari yake kwa mashabiki wa Tanzania na Kenya ambao watakua tayari kusikia kazi hiyo. Hivi karibuni Harmonize  akiwa nchini katika ziara yake ya kimuziki alitangaza wazi kuja na ‘EP’ itakayo kuwa na nyimbo 5 za pamoja kati yake na Otile Brown.

Read More
 HARMONIZE & OTILE BROWN KUJA NA EP YA PAMOJA YENYE NYIMBO 5

HARMONIZE & OTILE BROWN KUJA NA EP YA PAMOJA YENYE NYIMBO 5

Nyota wa muziki wa Bongofleva Harmonize ametangaza ujio wa EP ya pamoja mkali wa muziki nchini Otile Brown. Harmonize ameweka wazi hilo akiwa jukwaani kwenye tamasha la Afro Vasha Disemba 12 mwaka huu huko Naivasha ambapo amesema EP hiyo itakuwa na Jumla ya mikwaju 5 ya moto. Hajabainika kama EP hiyo ni ile Harmonize alituahidi atawashirikisha wasanii 5 wa Kenya wenye vipaji bila kuangalia ukubwa wa msanii ila ni jambo la kusubiriwa. Ikumbukwe kabla ya Hitmaker huyo wa Teacher kutua nchini Kenya alidokeza mpango wa kufanya ziara ya kimuziki kwenye miji kumi za Kenya ambapo aliwapa nafasi mashabiki wapendekeze majina ya miji ambayo wangependa afanye tamasha lake la muziki.

Read More
 VIDEO ZA OTILE BROWN ZARUDI YOUTUBE

VIDEO ZA OTILE BROWN ZARUDI YOUTUBE

Hatimaye video za staa wa muziki nchini Otile Brown zimerudi youtube baada ya kuondolewa kwa siku kadhaa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram staa huyo amewajuza mashabiki zake kuwa video hizo zimerudi rasmi baada ya kuondolewa youtube huku akiwashukuru mashabiki wake kwa kumuvumilia yeye pamoja na timu yake wakati walipokuwa wanafuatilia suala la kurejesha nyimbo zake kwenye mtandao huo. Such kinda love, Dusuma, Chaguo la moyo wangu, Regina,Aaiyana ni kati ya video za nyimbo za Otile Brown ambazo ziliondolewa kwenye akaunti yake ya youtube. Kurejeshwa kwa nyimbo hizo kumekuja siku chache baada ya staa huyo kutoa taarifa rasmi, akielezea utata unaozingira suala la kufutwa kwa nyimbo zake. Hata hivyo otile brown hajaweka wazi sababu ya kuondolewa kwa video hizo

Read More
 MENEJA WA OTILE BROWN AFUNGUKA JUU YA KUFUTWA KWA NYIMBO ZA STAA HUYO YOUTUBE

MENEJA WA OTILE BROWN AFUNGUKA JUU YA KUFUTWA KWA NYIMBO ZA STAA HUYO YOUTUBE

Meneja wa otile brown Noriega amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kufutwa kwa nyimbo za msanii huyo kwenye mtandao wa youtube. Akiwa kwenye moja ya interview meneja huyo amesema kama uongozi wa otile brown wameshangazwa na hatua ya nyimbo za staa huyo kufutwa kwenye mtandao wa youtube na aliyezi-upload ambapo ameahidi kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu ili kuhakikisha waliohusika wanakabiliwa kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo Noriega amepuzilia mbali madai yanayotembea mitandaoni kuwa otile brown anatumia suala la nyimbo zake kufutwa kwenye mtandao wa youtube kuupromote kazi yake mpya kwa kusema kwamba suala hilo sio kiki kama inavyodaiwa kwani otile brown huwa hatumii kiki kutangaza muziki wake. Nyimbo ambazo zilifutwa kwenye channel ya youtube ya msanii huyo ni pamoja na Dusuma, Such Kinda of love, Chaguo la moyo wangu, Aiyana na nyingine nyingi.

Read More
 OTILE BROWN APOTEZA ZAIDI YA VIEWS MILLIONI 190 YOUTUBE

OTILE BROWN APOTEZA ZAIDI YA VIEWS MILLIONI 190 YOUTUBE

Staa wa muziki nchini otile brown amepoteza zaidi ya views millioni 190 kwenye akaunti yake ya youtube mara baada ya nyimbo zake tano kufutwa kwenye mtandao huo na aliyezi-upload. Awali Otile brown alikuwa na zaidi ya views millioni 229 ila kwa sasa ana jumla ya watazamaji millioni 35. Nyimbo ambazo zilifutwa kwenye channel ya youtube ya msanii huyo ni pamoja na Dusuma, Such Kinda of love, Chaguo la moyo wangu na Aiyana. Chaguo la Moyo wangu na Dusuma ni video za muziki zenye watazamaji wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube nchini Kenya. Mpaka sasa haijafahamika sababu za kushushwa kwa video hizo za Otile Brown.

Read More