RAYVANNY ADOKEZA UJIO WA EXTENDED PLAYLIST YAKE YA FLOWERS 2
Boss wa Lebo ya Next Level Music msanii Rayvanny ametangaza ujio wa EP’ yake ya Flowers 2 katika siku za hivi karibuni. Rayvanny ameshare hilo kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram ,na kuweka wazi kuwa tayari EP hiyo ipo tayari kwa asilimia 100%. EP hiyo itakuwa kama muendelezo wa EP yake ya kwanza ya Flowers iliyotoka mwanzoni mwa mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya nyimbo 8 ikiwemo HitSong yake ya “Teamo”. Utakumbuka Rayvanny mpaka sasa ana jumla ya EP mbili ambazo ni Flowers na New Chui. Lakini pia ana album moja iitwayo Sound From Afrika iliyotoka mwaka wa 2021.
Read More