Ringtone Apoko Atangaza Kuhutubia Umma Baada ya Kuachiwa kwa Dhamana
Msanii maarufu wa muziki wa injili, Ringtone Apoko, amedokeza kuwa atazungumza na umma wiki hii, katika kile kinachoonekana kama hotuba muhimu kufuatia matukio ya hivi karibuni maishani mwake. Katika ujumbe huo aliyouchapisha Instagram, msanii huyo alionesha shukrani kwa marafiki zake waliomsaidia wakati wa kipindi kigumu, na kumshukuru Mungu kwa kupitia changamoto alizopitia. “WILL BE ADRESS THE NATION THIS WEEK. 4 NOW AM THANK FOR MY FRIENDS AND MY GOD.” aliandika Ingawa hakutoa maelezo kamili kuhusu yaliyomo kwenye hotuba hiyo, ujumbe wake umeibua gumzo kubwa mitandaoni. Mashabiki wake wametoa maoni mbalimbali, baadhi wakimuunga mkono na kumtia moyo, huku wengine wakisubiri kwa hamu kusikia atakachosema. Wengine pia walitafsiri ujumbe huo kama dalili ya kurudi kwa kishindo kwa msanii huyo ambaye kwa muda sasa amekuwa kimya kisanaa. Taarifa hii inakuja siku chache tu baada ya Ringtone kuachiwa kwa dhamana na korti, kufuatia kesi inayohusiana na mgogoro wa ardhi. Kesi hiyo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na vyombo vya habari na mashabiki wake, na wengi wanatarajia huenda hotuba hiyo itagusia kwa undani sakata hilo. Kwa sasa, macho na masikio ya wapenzi wa burudani na mashabiki wake yameelekezwa kwake, wakisubiri hotuba hiyo ambayo huenda ikafungua ukurasa mpya katika maisha na safari yake ya muziki.
Read More