RINGTONE ATOA OFA YA KUWASAIDIA WAJANE KENYA

RINGTONE ATOA OFA YA KUWASAIDIA WAJANE KENYA

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Ringtone ametangaza kutoa ofa ya kumlipia karo mwaka ya mmoja watoto wa akina mama wajane waliofanya vizuri kwenye mtihani wa kitaifa wa darasa la nane uliokamilika majuzi. Ringtone amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram ambapo amesema atatoa usaidizi huo kwa mtoto wa mama mjane ambaye alipata alama zaidi ya 400 kwenye mtihani wake wa K.C.P.E Hitmaker huyo wa ngoma ya Zoea mawe amedai atatoa ofa hiyo kwa mjane yeyote ambaye atamtumia ujumbe wa kwanza kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram huku akiwahimiza wasanii wenzake kushindani kwenye masuala ya kurudisha fadhila kwa jamii. “ Nataka kuongea na single mothers, kama uko na mtoto alifanya class 8 na akapata marks over 400, unidm nataka kukusaidia kulipa school fees ya mtoto wako kwa mwaka mmoja. Single mothers wenye mtoto wake alipata maraks over 400 kwa KCPE…nataka kukusaidia . Ule ataniDM wa kwanza ndio ntarushia school fees ya 1 year… ntarrepost hapa hapa na mtsaema naringa …tucompete kufanya mazuri” Ameandika Ringtone. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kupuzilia mbali madai hayo ya Ringtone kwa kusema kwamba msanii huyo anatengeneza mazingira ya kuzungumzia nchini ikizingatiwa kuwa amezoea kutumikia kiki kwenye muziki wake

Read More
 RINGTONE AZUA GUMZO MTANDAONI,AACHIA ORODHAA YA MASTAA 10 TAJIRI NCHINI KENYA

RINGTONE AZUA GUMZO MTANDAONI,AACHIA ORODHAA YA MASTAA 10 TAJIRI NCHINI KENYA

Msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko ameingia kwenye headlines mara baada ya kujitengenezea orodha ya mastaa tajiri nchini Kenya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtone amejiweka kwenye nafasi ya kwanza huku akidai kuwa ana nyumba tano za kifahari katika mitaa ya Runda, Karen na muthaiga huku akieleza anamiliki hoteli na nyumba kadhaa za makazi, magari 7 aina ya Range Rover, Maybach, na BMW. Nafasi ya pili kwenye orodha hiyo ni, amemtaja mbunge wa eneo la Starehe Kaunti ya Nairobi, Charles Njagua Kanyi maarufu Jaguar, ambaye kwa mujibu wake anamiliki nyumba mbili na magari matatu. Kwenye orodha hiyo pia amewataja wasanii kama Akothee ambaye ana Jumba moja la kifahari,na gari aina SUV, pamoja na Bahati ambaye ana magari 3 na majumba 3 ya kifahari. Mastaa wengine ambaye wametajwa ni pamoja na Khaligraph Jones, Arnelisa Muiga, Krg The Don, Betty Kyalo, Huddah Monroe, Otile Brown, na mwisho kabisa Size 8 pamoja na mume wake DJ Mo huku akisisitiza kuwa ana ushahidi wa kutosha kuthibitisha hilo. Hata hivyo mkali huyo wa ngoma ya “Sisi ndio tuko” ameahidi kutoa orodha nyingine ya watu maarufu nchini Kenya ambao amesema ni wapiga kelele ilhali hawamiliki chochote. Orodha ya Ringtone imeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake kwenye mitandao ya Kijamii ambao wameenda mbali zaidi kumtolea uvivu msanii huyo wakidai kwamba kama kweli angekuwa tajiri angeonekana kwenye orodha ya wasanii tajiri iliyotolewa na jarida la Forbes mwaka wa 2021.

Read More
 T-SHIRT YA BEI GHALI YA MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI NCHINI RINGTONE YAZUA GUMZO MTANDAONI

T-SHIRT YA BEI GHALI YA MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI NCHINI RINGTONE YAZUA GUMZO MTANDAONI

Watumiaji wa mitandao ya Kijamii nchini wamemtolea uvivu Staa wa muziki wa Injili  Ringtone Apoko baada msanii huyo kujigamba kuwa anamiliki T-Shirt ya bei ghali aliyodai kuwa ameinunua kwa shilingi milioni moja za Kenya. Kupitia mitandao yao ya kijamii wamemtaka Mwanamuziki huyo akome kuishi maisha ya kuigiza na kuwahada Wakenya kwa kiki zisizo kuwa na mashiko kwani  T-Shirt yake hiyo ni batili. Aidha wameenda mbali zaidi na kumtaka ringtone ache suala la kuendekeza kiki kwenye muziki wake na badala yake aelekeze nguvu zake kwenye suala la kutoa muziki mzuri ambao utajiuza wenyewe. Kauli hiyo ya wakenya imekuja mara baada ya ringtone apoko kusikika kwenye moja ya video inayosambaa mitandaoni akijinadi kuwa licha ya kwamba anamiliki T-Shirt ya shilling millioni moja za Kenya bado ameokoka na anafuata misingi yote ya dini ya Kikristo tofauti na watu ambao vitu vya dunia huwachanganya na kuwapelekea kujihusisha na usherati.

Read More
 RINGTONE APOKO AWEKA WAZI MATAMANIO YA KUINGIA KWENYE NDOA

RINGTONE APOKO AWEKA WAZI MATAMANIO YA KUINGIA KWENYE NDOA

Inaonekana upweke unazidi kumtesa msanii wa nyimbo za Injili nchini Ringtone Apoko mara baada ya kuweka wazi matamanio yake ya kuingia kwenye ndoa. Kupitia Instagram Page yake msanii huyo ameibuka na kutangaza hadharani kwamba anataka mke kwa sasa, maana kifedha anazidi kuwa tajiri tu. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sisi Ndio Tuko” ameenda mbali zaidi na kuwataka mashabiki zake wamsaidie kumtafutia mke wa ndoto yake. Hata hivyo post hiyo haikuwa na uhai wa muda mrefu kwani Ringtone aliufuta ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuwaacha mashabiki na maswali mengi. Hii sio mara ya kwanza kwa Ringtone Apoko kutangaza wazi kuwa anataka kuoa, mwezi Juni mwaka wa 2019 pia alieleza hisia zake kupitia wimbo wake uitwao “Nafuta Bibi.” ambao una zaidi ya views millioni moja kwenye mtandao wa Youtube.

Read More
 BIFU LA RINGTONE NA DJ MO LACHUKUA SURA, HII BAADA YA RINGTONE KUANIKA TUSIYOYAJUA NYUMA YA PAZIA

BIFU LA RINGTONE NA DJ MO LACHUKUA SURA, HII BAADA YA RINGTONE KUANIKA TUSIYOYAJUA NYUMA YA PAZIA

Inaonekana ugomvi wa msanii Ringtone na DJ Mo hautapoa hivi karibuni, hii ni baada msanii huyo kuibuka na kumzushia DJ Mo kashfa zito. Kupitia mitandao yake ya kijamii Ringtone amemtuhumu DJ Mo kuwa yeye ndiye chanzo cha muziki wa injili nchini Kenya kusuasua katika siku za hivi karibuni. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sisi Ndio Tuko” amesema DJ Mo  aliua vipaji vingi kwenye muziki wa injili kwa kuhitisha rushwa ya ngono kutoka kwa wasanii wa kike ili acheze nyimbo zao alipokuwa anafanya kazi kwenye runinga moja hapa nchini. Hata hivyo DJ Mo hajajibu chochote kuhusiana na tuhuma hizo ila ni jambo la kusubiriwa. Utakumbuka ugomvi wa Ringtone na DJ MO ulianza wiki iliyopita kwenye uzinduzi wa album ya msanii Size 8 na hiii ni baada ya Ringtone kukatazwa kujiunga na makasisi waliokuwa wapewa nafasi ya kuibariki album ya Size 8, “Christ Revealed”.

Read More
 SIZE 8 AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA KUHUSU SAKATA LAKE NA RINGTONE

SIZE 8 AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA KUHUSU SAKATA LAKE NA RINGTONE

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Size 8 amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya Ringtone kudai kuwa alifukuzwa kwenye uzinduzi wa album yake wikiendi iliyopita. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Size 8 amesema amemsamehe ringtone kwa kitendo cha kuvuruga shughuli ya uzinduzi wa album yake huku akipuzilia mbali madai ya kumfukuza msanii huyo kwenye hafla ya kuibariki album yake hiyo kwa kusema kwamba haikuwa kiki kama inavyotafsiriwa kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo Ringtone kupitia mitandao yake ya kijamii amesisitiza kuwa Size 8 ni mnafiki na mubaguzi kwenye shughuli zake na kitendo chake cha kumfukuza kwenye uzinduzi wa album yake inaonyesha ni jinsi gani size 8 anawadharau wasanii wa nyimbo za injili.

Read More
 MAHAKAMA YAAHIRISHA KESI ILIYOWASILISHWA NA RINGTONE DHIDI YA MANABLOGU ROBERT ALAI

MAHAKAMA YAAHIRISHA KESI ILIYOWASILISHWA NA RINGTONE DHIDI YA MANABLOGU ROBERT ALAI

Mahakama ya Milimani Jijini Nairobi imeahirisha kwa mara nyingine kesi iliyowasilishwa na mwanamuziki Ringtone dhidi ya mwanablogu Robert Alai ambaye alimshambulia na kumjeruhi vibaya mwaka wa 2021. Akizungumza nje ya mahakama ya Milimani Wakili wa Ringtone Evans Ondiek amesema Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 9 mwezi mei mwaka wa 2022, siku ambayo mahakama itatoa mwelekeo. Kwa upande Mwanamuziki Ringtone amesema ana imani kwamba mahakama itamtendea haki ikizingatiwa kuwa ana ushahidi wa kutosha dhidi ya mwanablogu Robert Alai ambaye alimjeruhi vibaya kichwani kwa rungu. Hii sio mara ya kwanza kesi hiyo kuaahirishwa mwezi Agosti mwaka jana iliahirishwa tena baada ya Mwanablogu Robert Alai kuachiwa kwa dhamana ya shillingi laki tatu za Kenya. Utakumbuka Ringtone na Robert Alai waliingia kwenye ugomvi mwezi Julai mwaka wa 2021 baada ya wawili hao kuhusika kwenye ajali ya barabarani ambapo Ringtone alimtuhumu Alai kwa kumpiga Rungu ya kichwa na kuaharibu gari lake.

Read More
 RINGTONE AOMBA MSAMAHA KWA KUZUA VURUGU KWENYE HAFLA YA UZINDUZI WA ALBUM YA MSANII MWENZAKE SIZE 8

RINGTONE AOMBA MSAMAHA KWA KUZUA VURUGU KWENYE HAFLA YA UZINDUZI WA ALBUM YA MSANII MWENZAKE SIZE 8

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Ringtone Apoko ameibuka na kuwaomba Wakenya msamaha mara baada ya kuzozana na DJ MO kwenye uzinduzi wa album msanii mwenzake Size 8 wikiendi hii iliyopita. Katika mkao na wanahabari Ringtone amekiri kutopendezwa na kitendo cha  kuzua vurugu kwenye shughuli za watu kwa kusema kwamba anajuta kuwaibisha mashabiki zake  kwa kujihusisha na vitendo vya kiuhuni ambavyo vinakwenda kinyume na mafunzo ya kikristo. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sisi Ndio Tuko” ameahapa kutorudia tena  ishu ya kuzua vurugu sehemu yeyote ile kwani jambo hilo imeleta picha mbaya kwa jamii ikizingatiwa kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao watu wamekuwa wakiheshimika kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini. Utakumbuka Februari 13 mwaka huu kwenye uzinduzi wa album ya mwanamuziki Size 8, Ringtone alifurushwa na waandaji wa hafla hiyo baada ya kutaka kujiunga na wahubiri stejini kwa lazima kuibariki album ya Size 8.

Read More
 RINGTONE AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUTAKA KUZICHAPA NA MUME WA SIZE 8, DJ MO.

RINGTONE AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUTAKA KUZICHAPA NA MUME WA SIZE 8, DJ MO.

Mwanamuziki wa nyimbo za injili ringtone ameshika vichwa vya habari wikiendi hii iliyopita mara baada ya kutaka kuzichapa na DJ Mo ambaye mume wa msaniii mwenzake Size 8. Purukushani  kati ya wawili hao ilianza baada ya ringtone kuzua vurugu kwenye hafla ya uzinduzi wa album ya msanii size 8 ambayo imefanyika Februari 13 mwaka huu kwa kutaka kujiunga na wahubiri waliopewa nafasi ya kuibariki album ya size 8, Christ Revealed kabla ya kuingia sokoni. Sasa suala hilo lilimlazimu mume size 8, DJ MO kutumia nguvu kumuondoa ringtone kwenye eneo la tukio kutokana na msanii huyo kutaka kuaharibu hafla ya uzinduzi wa album size 8 kwa kusisitiza kujiunga na wachungaji kwa lazima. Akizungumza nje ya hafla ya uzinduzi wa album size 8 ringtone amesema ameshangazwa na hatua ya DJ Mo kumkataza kujiunga na wahubiri wenzake stejini kuiombea album huku akimsuta vikali kwa hatua ya kumvunjia heshima mbele ya umma licha ya kuwa msanii mkongwe kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini. Kwa upande wake DJ MO amepuzilia mbali madai ya ringtone kwa kusema kwamba hayana msingi wowote kwani msanii huyo anapenda kuleta mzaha kwenye shughuli za watu hivyo hangemruhusu kuaharibu hafla ya uzinduzi wa album ya mke wake Size 8. Hata hivyo  jambo hilo limezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwani walimwengu wameonekana kumshambulia  ringtone kwa hatua kuvuruga shughuli ya yenyewe huku wengine wakihoji kuwa huenda msanii huyo anatengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwa ajili ya wimbo wake na size 8 ambao unapatikana kwenye Christ Revealed album

Read More
 RINGTONE: HUDDAH MONROE ALINITAKA KIMAPENZI NIKAMKATAA

RINGTONE: HUDDAH MONROE ALINITAKA KIMAPENZI NIKAMKATAA

Mwanamuziki wa nyimbo za Injil nchini, Ringtone Apoko amedia kuwa mrembo maarufu mtandaoni nchini, Huddah Monroe aliwahi kumtongoza lakini akamkataa. Kauli yake inakuja mara baada ya Huddah kuibuka na kudai kuwa hajaona mwanaume ambaye amekidhi vigezo vya kuwa naye nchini Kenya. Sasa  Ringtone ameibuka na kusema “Tumekuwa na safari refu sana ya maisha na Huddah Monroe, tunajuana sana kwa vilemba, hawezi sema hivyo, umejuana miaka mingi. Ametoka mbali, labda alikuwa anatafuta kiki ama alikuwa amelewa, huwa anakunywa sana msimhukumu. Ameendelea kwa kusema,  “Hawezi sema mimi sio mtanashati na alikuwa ananililia kitambo, mimi ndio nilimkataa, alikuwa ananililia na kunisumbua sana eti ananitaka nikamkataa” “Alinitongoza nikakataa, nilimwambia lazima aokoke ndivyo tuweze tuzungumzia mambo mengine. Ni msupu. Yeye ni mmoja wa wanawake warembo zaidi barani Afrika. Hata hivyo hawezani nami kwa kuwa lazima aokoke, atubu dhambi na amkiri Yesu. Hapo ndipo tulikosania. Nilimkataa kabisa”. amesema Apoko. Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameonekana kumshangaa sana Ringtone kwa kauli yake hiyo ambayo wamedai hakuna namna ambavyo Huddah Monroe anaweza kumtaka kimapenzi ikizingatiwa kuwa hana vigezo kabisa vya kumshawishi mrembo atokee nae kimapenzi.

Read More
 RINGTONE ASHUTUMIWA KWA KUVAA SAA FEKI AINA YA RICHARD MILLIE

RINGTONE ASHUTUMIWA KWA KUVAA SAA FEKI AINA YA RICHARD MILLIE

Miongoni mwa mijadala mikubwa kwenye kiwanda cha burudani nchini ni saa ya bei ghali aliyonunua Ringtone aina ya Richard Millie mwishoni mwaka wa 2021 aliyodai kuwa ameinunua kwa shilingi milioni 47 za Kenya na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee nchini anayemiliki saa hiyo. Taarifa ikufikie kwamba, ishu hiyo imezua tafrani ya aina yake kwenye mitandao ya kijamii baada ya Kurasa moja mtandaoni maarufu kama Fake Watch Busta kuchapisha taarifa  kuwa msanii huyo alikuwa amevaa saa feki. Kulingana na Fake Watch Busta saa ya Ringtone imekosa baadhi ya nakshi zinazopatikana kwenye saa Original ya Richard Millie. Hata hivyo suala hilo limeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wakihoji kuwa walikuwa wanafahamu saa hiyo ni batili ikizingatiwa kuwa  Ringtone amekuwa akiishi maisha ya kuigiza.

Read More
 RINGTONE AMCHANA ANDREW KIBE KISA NDOA YA MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI GUARDIAN ANGEL

RINGTONE AMCHANA ANDREW KIBE KISA NDOA YA MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI GUARDIAN ANGEL

Msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone amemtolea uvivu mwanahabari mwenye utata nchini Andrew Kibe kwa madai ya kuikosoa ndoa ya msanii Guardian Angel na mke wa Esther Musila. Kupitia instagram page yake Ringtone amemtaka kibe aheshimu maamuzi ya Guardian Angel na mke wake Esther Musila kuhalilisha ndoa kwa njia ya harusi ikizingatiwa kuwa ni watu wazima ambao upendo uliwaleta pamoja licha ya utofauti wa umri wao. Hitmaker huyo wa “Sisi ndio tuko” ameenda mbali na kumshauri Kibe akome kuingilia maisha ya wana ndoa hao wawili na badala yake aelekeze nguvu zake kwenye shughuli itakayomuingizia kipato kwani anapoteza muda wake kuzungumzia jambo ambalo litamsaidia maishani. Kauli ya Ringtone imekuja mara baada ya Andrew Kibe kuonekana kukejeli ndoa ya Guardian Angel na mke wake Esther Musila kwa kusema kwamba haoni ndoa hiyo ikidumu kwani msanii huyo aliwavunjia heshima vijana wa Kenya kwa hatua kumuoa mwanamke mkubwa kiumri.

Read More