WILLY PAUL AKANUSHA KUIBA IDEA YA WIMBO WAKE MPYA KUTOKA KWA RINGTONE

WILLY PAUL AKANUSHA KUIBA IDEA YA WIMBO WAKE MPYA KUTOKA KWA RINGTONE

Nyota wa muziki nchini Willy Paul amekanusha madai ya kuiba idea ya wimbo wake mpya uitwao “Atoti Jaber” kutoka kwa msanii mwenzake Ringtone Apoko. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Paul amemtaka Ringtone akome kueneza taarifa za uongo kwamba alimuibia wimbo wa “Atoti Jaber” huku akisema madai hayo hayana msingi wowote ikizingatiwa kuwa wimbo huo aliomshirikisha Klons Melody na Jakadalla sio wimbo wa injili. Those of you that know Ringtone know the kind of person he is.. My brother please stop telling your friends that I stole the song atotijaber from you. It has never been a gospel song, enough with your clout chasing bro. It’s 2022, new beginnings. I love and respect you as a big brother who came to this industry before me. To all my fans, keep supporting the song #atotijaber x @klons_melody x @musajakadalla_ ameandika Willy Paul kupitia Instagram yake Hitmaker huyo wa “My Woman” amesema amechoshwa na sarakasi za Ringtone ambapo ameenda mbali na kumtaka msanii huyo aelekeze nguvu zake kwenye ishu ya kutangaza kazi zake za muziki badala ya kutengeneza mitukio ili azungumziwe na vyombo vya habari nchini. Hata hivyo amesema anamheshimu Ringtone kama mmoja wa wasanii waliomtangulia kwenye tasnia ya muziki huku akiwataka mashabiki waendelee kusapoti wimbo wake wa “Atoti Jaber” kwenye digital platflorms mbali mbali za muziki.

Read More
 MR. SEED AMVUA NGUO RINGTONE, AMSHAURI AFUNGE NDOA KWANI UMRI UNAMPA KISOGO

MR. SEED AMVUA NGUO RINGTONE, AMSHAURI AFUNGE NDOA KWANI UMRI UNAMPA KISOGO

Nyota wa muziki nchini Mr. Seed ameibuka na kumtaka staa wa muziki wa nyimbo za injili Ringtone kuoa. Msanii huyo amedai kwamba Ringtone ameshakuwa mtu Mzima, hivyo anaamini kuwa akioa itamletea heshima sana katika jamii. Akiwa kwenye moja ya interview Mr. Seed amesema majukumu ya ndoa pekee ndiyo yatamnyamazisha Ringtone ambaye katika siku za hivi karibu amekuwa gumzo mitandaoni kutokana na sarakasi zake. Hitmaker huyo wa “Dawa ya Baridi” amesema amechoshwa na mienendo ya Ringtone kuingilia ndoa za wasanii wenzake kila mara ikizingatiwa kuwa yeye binafsi ameshindwa kumpata mwanamke wa ndoto yake. Hata hivyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba ringtone ni msherati namba moja ambaye amejificha kwenye muziki wa injili kwani amekuwa na mazoea ya kuzama kwenye  DM za warembo wa  Instagram akiomba penzi. Kauli ya mr seed imekuja mara baada ya ringtone kuonekana kumshambulia kila mara kwenye interviews mbali mbali kufuatia hatua yake ya kuanza kuimba nyimbo za mapenzi tofauti na muziki wa injili ambao ulimtambulisha kwenye kiwanda cha muziki nchini

Read More
 RINGTONE APINGA AZMA YA WILLY PAUL KUJITOSA KWENYE ULINGO WA SIASA MWAKA 2022

RINGTONE APINGA AZMA YA WILLY PAUL KUJITOSA KWENYE ULINGO WA SIASA MWAKA 2022

Baada ya Willy Paul kutangaza azma ya kujiunga na siasa mwaka wa 2022, msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone ameonekana kutofautiana kimawazo na Hitmaker huyo wa “Lenga”. Akipiga stori na Mungai Eve kwenye mtandao wa Youtube Ringtone amesema watu wasichukulie kauli ya Willy Paul kwa uzito kwani msanii huyo anajaribu kushinda na msanii mwenzake Bahati ambaye kipindi cha nyuma alitia nia ya kuwania ubunge wa Mathare. Hitmaker huyo wa “Pamela” amemshauri Willy Paul aachane na siasa na badala yake awekeze nguvu zake kwenye muziki kwani ni mmoja wa wasanii ambao wana kipaji cha kipekee nchini. Sanjari na hilo Ringtone amedokeza kwamba mwaka wa 2022 ataweka wazi azma yake ya kujiunga na siasa kwani amekuwa akipata shinikizo za kuwania ubunge Dagorreti kaskazini kutoka kwa watu wake wa karibu. Ikumbukwe mwaka wa 2011 Ringtine aliwania ubunge katika uchaguzi mdogo wa Kitutu Masaba kupitia chama cha Vijana Progressive Party ambapo aliibuka wanane kwa kupata kura 467.

Read More
 RINGTONE AKATA TAMAA KWENYE SUALA LA KUMTAFUTA MKE WA NDOTO YAKE

RINGTONE AKATA TAMAA KWENYE SUALA LA KUMTAFUTA MKE WA NDOTO YAKE

Msanii wa nyimbo za Injili nchini Ringtone Apoko ni kama amekataa tamaa kwenye mchakato wa kutafuta mke wa ndoto yake. Hii ni baada ya hitmaker huyo wa “Sisi ndio tuko” kukiri hadharani kwamba hana msukumo tena wa kumtafuta mke. Kupitia ukurasa wake wa instagram Ringtone amesema kwa sasa amehamua kuelekeza nguvu zake kwenye ishu ya kueneza injili wakati anasubiri Mungu ajibu maombi yake. Ikumbukwe mwaka wa 2019 Ringtone aliwaacha mashabiki zake na maswali mengi baada ya kuonekana na bango ambalo lilikuwa limeanisha sifa zote ambazo anazitafuta kwa mwanamke wa ndoto yake. Wengi walidhani ni kiki lakini Ringtone mwenyewe alikuja akakanusha madai hayo kwa kusema kwamba alikuwa serious kwenye suala la kumtafuta mke.

Read More
 RINGTONE ATIA NENO SAKATA LA WILLY PAUL NA DIANA MARUA

RINGTONE ATIA NENO SAKATA LA WILLY PAUL NA DIANA MARUA

Baada ya sakata la Willy Paul na Diana Marua kugonga vichwa vya habari nchini Staa wa muziki wa injili Ringtone ameamua kuvunja kimya chake juu ya suala hilo. Akipiga stori na online Media Ringtone ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba Wakenya wamechoshwa na kile ambacho kinaendelea kati ya Willy Paul, Bahati na Diana Marua, hivyo pana haja ya watatu hao kuzika tofauti zao na waelekeze nguvu zao kwenye ishu ya kuupeleka muziki wao kimataifa. Hitmaker huyo wa “Sisi ndio tuko” amewaomba wadau wa muziki nchini kuingilia kati sakata la Willy Paul na Diana Marua ambalo linaendelea huko mtandaoni kwani wasanii hao wakiachwa jambo baya litakuja kutokea. Ikumbukwe Willy Paul na Diana Marua wamekuwa wakirushiana maneno makali mitandaoni mara baada ya Diana Marua kuibua tuhuma za kubakwa na bosi huyo wa Saldido miaka kadhaa iliyopita

Read More
 MJENGO WA KIFAHARI WA MSANII RINGTONE KUPIGWA MNADA KWA TAKRIBAN SHILLINGI MILLIONI 80

MJENGO WA KIFAHARI WA MSANII RINGTONE KUPIGWA MNADA KWA TAKRIBAN SHILLINGI MILLIONI 80

Mjengo wa kifahari wa msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone ulioko mitaa ya Runda jijini Nairobi imepiga mnada kwa shillingi millioni 80 na kampuni moja ya wanasheria.   Hatua hii inakuja siku chache baada ya Ringtone kupewa notisi ya siku 10 ya kuondoka kwenye mjengo huo wenyewe utata la sivyo ahamishwe kwa nguvu.   Kulingana na barua iliyotolewa na kampuni ya mawakili ya AGN Kamau Advocates,  nyumba ambayo ringtone anaishi kwa sasa ni ya raia wa Sweden kwa jina Mona Ingegard aliyefariki mwaka wa 2007 na Ringtone alinunua nyumba hiyo bila kufuata njia sahihi.   Hata hivyo Ringtone mpaka sasa hajatoa tamko lolote kuhusiana madai ya mjengo wake wa kifahari kupigwa mnada.            

Read More