Spice Diana awajibu wanaoshinikiza aingie kwenye ndoa

Spice Diana awajibu wanaoshinikiza aingie kwenye ndoa

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Spice Diana amedai kwamba hana mpango wa kuingia kwenye ndoa hivi karibuni. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema ana mambo mengi ya kutimiza kabla ya ndoa. Mrembo huyo ambaye hajawahi kumtambulisha mpenzi wake kwa umma, anaamini ndoa ni jambo zuri lakini inapaswa kufanywa kwa wakati sahihi. Hata hivyo amewataka mashabiki zake kuacha kumpa shinikizo zisizo kuwa na msingi na badala yake waendelee kufuatilia kazi zake. “Nitafunga ndoa tu wakati muafaka ukifika. Nina mengi ya kutimiza kabla ya ndoa. Mashabiki zangu wanapaswa kunidai muziki, sihamasishi watu kupitia ndoa,” Alisema. Ikumbukwe Spice Diana kwa sasa yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya tamasha lake ambalo lifanyika Januari 13 mwaka 2023 katika uwanja wa Cricket Oval, Lugogo.

Read More
 Nilitabiri Spice Diana atapata mafanikio makubwa kwenye muziki – Bebe Cool

Nilitabiri Spice Diana atapata mafanikio makubwa kwenye muziki – Bebe Cool

Bosi wa label ya Gagamel, Msanii Bebe Cool anasema alikuwa amemtabiria mema Spice Diana kipindi anatoka kimuziki miaka minane iliyopita. Bebe Cool amesema alikuwa anajua mrembo huyo atakuwa mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi nchini Uganda bila usaidizi wowote wa staa mkubwa nchini humo. Aidha amefafanua sababu za kukataa kufanya kolabo na Spice Diana kwa kusema kuwa ilikuwa njia ya kumpa changamoto aendelee kuipambania brand yake hadi atakapoachia wimbo mkali kama msanii wa kujitegemea. “Miaka minane iliyopita, Spice Diana na meneja wake walikuja kwangu wakiomba kolabo. Tulikutana kwenye baa moja mjini Ntinda. Nilimwambia afanye kazi kwa bidii hadi atakapoachia wimbo mkali bila usaidizi wa mtu yeyote,” Bebe Cool alielezea. Hata hivyo anaamini ikitokea wamefanya kazi ya pamoja na Spice Diana watafaidi wote kwa kuwa mrembo huyo ameacha alama kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda kutokana na nyimbo ambazo amekuwa akiaziachia katika miaka ya karibuni.

Read More
 Spice Diana afunguka kuhusu bifu za wasanii

Spice Diana afunguka kuhusu bifu za wasanii

Msanii kutoka nchini Uganda Spice Diana amedai kwamba ugomvi miongoni mwa wasanii haisaidi kuwajenga kisanaa Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema wasanii wanaojihusisha na bifu kwa lengo la kutanua wigo wao kimuziki, wanaharibu brand au chapa zao  kwenye jamii. Hitmaker huyo wa “Boss” amesema kwa sasa ana muda wa kupishana na wasanii wenzake kwani ameamua kuwekeza nguvu zake kujiboresha kisanaa kwa ajili ya kukuza brand yake. Utakumbuka Spice Diana amekuwa akihusishwa kuwa kwenye ugomvi na wasanii Sheebah Karungi pamoja na Gravity Omutujju jambo ambalo yeye binafsi amekuwa akikanusha kwenye mahojiano mbali mbali.

Read More
 Spice Diana afunguka kuhusu ugomvi wake na walinzi akiwa jukwaani

Spice Diana afunguka kuhusu ugomvi wake na walinzi akiwa jukwaani

Msanii kutoka nchini Uganda Spice Diana amefunguka sababu kutupiana maneno makali na walinzi alipokuwa jukwaani akitumbuiza katika uwanja wa Bugembe huko Jinja. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni mrembo huyo amesema alikerwa na kitendo cha walinzi kuwazuia mashabiki zake kumkaribia licha kuwa walikuwa wamelipa kiingilio cha shillingi elfu 5 kila mmoja. Hitmaker huyo wa “Boss” amesisitiza kuwa ataendelea kuwapigania mashabiki zake wamkaribie akiwa anatoa burudani kwenye majukwaa mbali mbali kwa kuwa wao ndio matajiri wake ambao wamekuwa wakifadhili baadhi ya michongo yake. Hata hivyo vyombo vya usalama vimehoji kuwa hawakutaka kuhatarisha usalama wa mwanamuziki huyo wa Source Management akiwa jukwaani kwa kuwa hawana imani na baadhi ya mashabiki ambao kwa mujibu wao wanaweza kumdhalalisha kijinsia.

Read More
 Spice Diana atishia kuwafungia nje wasanii watakaovalia mavazi  yasiyo na staha kwenye onesho lake la muziki 2023

Spice Diana atishia kuwafungia nje wasanii watakaovalia mavazi yasiyo na staha kwenye onesho lake la muziki 2023

Mwanamuziki kutoka Uganda Spice Diana amedai kuwa hataruhusu wasanii watakaovalia mavazi yanayokwenda kinyume na madili ya jamii kutumbuiza kwenye tamasha lake la muziki mwaka 2023. Katika mkao na wanahabari Spice Diana amesema tamasha hilo itakuwa ya kifamilia zaidi, hivyo kutakuwa na ustaarabu kwenye suala la mavazi. Mrembo huyo amesema tayari ana timu ya watu ambao watakagua wasanii watakaokuwa wanatoa burudani jukwaani kama njia moja wapo ya kuzuia wasanii watakaovalia mavazi yasiokuwa na heshima. Spice Diana anatarajiwa kufanya onesho lake Januari 13 mwaka 2023 huko Cricket Oval, Lugogo na itakuwa mara yake ya kwanza kufanya shoo kwenye ukumbi huo mkubwa zaidi nchini Uganda tangu aanze safari yake ya muziki.

Read More
 SPICE DIANA AZIDI KUMUANDAMA PROMOTA MUTIMA KISA DENI

SPICE DIANA AZIDI KUMUANDAMA PROMOTA MUTIMA KISA DENI

Mwanamuziki kutoka Uganda Spice Diana ameonesha kusikitishwa na hatua ya promota Robert Mutima kukataa kumlipa pesa zake zilizosalia baada ya kutumbuiza kwenye show ya promota huyo huko Masaka. Mrembo huyo amesema licha ya promota huyo kuahidi kumlipa pesa hizo kwa wakati hadi sasa hajatimiza ahadi yake hiyo ambapo amehapa kuwa ataendelea na harakati ya kumshinikiza amlipe haki yake. Utakumbuka mwezi uliopita Spice Diana alikamata vichwa vya habari nchini Uganda alipomkashifu Mutima hadharani akiwa jukwaani baada ya kushindwa kulipa pesa zake, lakini wawili hao walikuja wakakutana ambapo promota huyo aliomba radhi na kuahidi kumlipa.

Read More
 PROMOTA MUTIMA AMVUA NGUO SPICE DIANA KWA KUMVUNJIA HESHIMA

PROMOTA MUTIMA AMVUA NGUO SPICE DIANA KWA KUMVUNJIA HESHIMA

Siku chache baada ya Promota Robert Mutima kumuomba radhi msanii Spice Diana kwa kuchelewesha pesa zake, promota huyo ameibuka tena kumchana msanii huyo kwa kitendo cha kumuahibisha mbele ya mashabiki zake. Mutima amesema alishangazwa na kitendo Spice Diana na huenda mrembo huyo anatumia mihadarati kabla ya kupanda jukwaani kwani njia ambayo alitumia kudai haki yake haikuwa nzuri. Amesisitiza kuwa alikuwa ameshikika na majukumu mengine ambayo yalimkwamisha kutofika kwa wakati kwenye shoo hiyo kukamilisha malipo ya msanii Spice Diana. Utakumbuka baada ya Spice Diana kusimamisha performance yake huko Masaka nchini Uganda alimtuhumu Mutima kwa kutokuwa mwazi kwenye ishu ya malipo ambapo alienda mbali zaidi na kuwataka mashabiki wabebe vifaa vyote vya kielektroniki kama njia ya kumuadhibu promota huyo jeuri.

Read More
 PROMOTA ROBERT MUTIMA AOMBA RADHI KWA SPICE DIANA

PROMOTA ROBERT MUTIMA AOMBA RADHI KWA SPICE DIANA

Promota wa muziki kutoka Uganda Robert Mutima amemuomba msamaha msanii Spice Diana baada ya kushindwa kumlipa pesa zake. Katika taarifa promota huyo amekiri kumvunjia heshima mrembo huyo kwa kusema kwamba hakuweza kumlipa kwa wakati kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake. Hata hivyo Spice Diana amepokea msamaha wa promota huyo kwa mikono miwili huku akisema hana kinyongo naye ila alikuwa anadai haki yake. Wikiendi iliyopita, mashabiki waliachwa na mshangao baada ya Spice Diana kusimamisha show yake ghafla huko Masaka ambapo alianza kumsomea Robert Mutima akitaka amlipe pesa zake.

Read More
 SPICE DIANA MBIONI KUANDAA ONESHO LAKE LA MUZIKI

SPICE DIANA MBIONI KUANDAA ONESHO LAKE LA MUZIKI

Msanii Spice Diana ameripotiwa kuwa yupo mbioni kuja na onesho lake la muziki huko Cricket Oval viungani mwa jiji la Kampala. Chanzo cha karibu na msanii huyo wa Source management kimesema Spice Diana anatarajiwa kufanya onesho lake la muziki katika ukumbu wa Cricket Oval mwakani. Inadaiwa Spice Diana anataka kuweka rekodi ya kujaza ukumbi huo ambao hujaza zaidi ya watu 20, 000 ikizingatiwa kuwa amekuwa akifanyia shows zake kwenye ukumbi wa Freedom City ambao ni mdogo ikilinganishwa na Cricket oval. Utakumba Cricket Oval ni moja kati ya makumbi makubwa ya matamasha nchini uganda na imekuwa ikitumika na mastaa makubwa nchini humo kufanya maonesho yao. Chameolene alikuwa msanii wa kwanza kujaza ukumbi huo na tangu wakati huo wasanii wengine walifuata mkumbo huo akiwemo Gravitty omutujju na Levixone ambao wa pia waliweka historia ya aina yake.

Read More
 TUHUMA ZA MAUJI ZAZIDI KUMUANDAMA SPICE DIANA

TUHUMA ZA MAUJI ZAZIDI KUMUANDAMA SPICE DIANA

Sakata la kijana aliyewauwa nyumbani kwa Spice Diana Henry Nsamba limechukua sura mpya baada ya Mulindwa Lawrence ambaye ni kaka wa mwendazake kudai kuwa ndugu yake alikuwa ana mpango wa kufanya wimbo wa pamoja na msanii huyo. Kulingana na Lawrence, Nsamba alikuwa anafanya vibarua ya kutengeneza matofali mitaani kwa ajili ya kuchangisha pesa za kufanikisha kolabo yake na spice diana kwa sababu alikuwa na ndoto ya kuwa mwiimbaji lakini kwa masikitiko makubwa akakutana na mauti yake. Aidha amedai kuwa Spice Diana na meneja wake Roger Lubega walikula pesa za ndugu yake na waliposhindwa kumrejeshea haki yake wakaamua kumwekelea madai ya wizi ambayo yalimpelekea kupigwa hadi kufa nyumbani kwa msanii huyo. “They are using theft to hide the truth. Nsamba was not capable of robbery. He wanted to collaborate with Spice Diana hence frequenting her residence. He paid Roger Lubega and Spice Diana for the collaboration. They thumped him for demanding it,” amesema Mulindwa Lawrence kaka wa mwendazake Henry Nsamba. Hata hivyo Spice Diana na uongozi wake wamesalia juu ya tuhuma ya mauji ya kijana huyo.

Read More
 FAMILIA YA KIJANA ALIYEUWAWA NYUMBANI KWA SPICE DIANA YATAKA HAKI

FAMILIA YA KIJANA ALIYEUWAWA NYUMBANI KWA SPICE DIANA YATAKA HAKI

Familia ya Henry Nsamba kijana anayedaiwa kupigwa nyumbani kwa Spice Diana na baadae akafariki Hospitalini inashinikiza kukamatwa kwa mwanamuziki huyo kutoka Uganda. Inadaiwa kuwa mwendazake ambaye alikuwa mfanyikazi wa kutengeneza matofali alifumaniwa Juni 30 mwaka huu akitaka kutekeleza kitendo cha wizi wa nyumbani kwa Spice Diana ndiposa akashushiwa kichapo cha mbwa kilichompelekea kufariki. Johnson Matovu,  ambaye ni baba mzazi wa mwaasiriwa ameeleza kuwa alionana na kijana wake huyo siku kadhaa zilizopita lakini alipatwa na mshtuko alipopokea taarifa za kifo chake kwa njia ya simu. Matovu amesema alitofautiana kimawazo na mwanae Nsamba alipotaka kujiunga na muziki jambo ambalo lilimfanya mwanae huyo kukimbia nyumbani na kwenda kutafuta maisha kivyake. Hata hivyo amewataka vyombo vya usalama viharakishe uchunguzi wa kubaini kifo cha mwane Henry Nsamba huku akitoa wito kwa washukiwa wakuu akiwemo Spice diana kukamatwa. Mapema wiki hii Spice Diana alitarajiwa kuhojiwa katika makao makuu ya idara ya upelezi DCI kuhusu tuhuma za mauji yanayomkabili kwa lakini msanii huyo alisusia na kuzima simu zake zote.

Read More
 SPICE DIANA MBIONI KUJA NA TOUR YAKE YA MUZIKI

SPICE DIANA MBIONI KUJA NA TOUR YAKE YA MUZIKI

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Spice Diana inaonekana hataki kabisa kulaza damu kwenye suala la kuupeleka muziki wake kimataifa. Msanii huyo wa Source Managemnent ambaye ameamua kuwapuuza baadhi ya watu wanakosoa muziki wake, ametangaza kuwa yupo kwenye matayarisho ya mwisho kwa ajili ya kuja na tour yake ya muziki nchini uganda. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mbikka” amesema tour hiyo ambayo ni mahususi kwa ajili ya kuwapa mashabiki zake burudani, itang’oa nanga huko Mbale nchini Uganda kabla ya kuelekea kwenye miji mbali mbali nchini humo. Utakumbuka Spice diana amegonga vichwa vya habari nchini Uganda kwa kipindi cha wiki mbili sasa mara baada ya kuachia StarGal EP yenye jumla ya singo 6 ya moto. Utakumbuka juzi kati Pallaso amehitimisha tour yake ya kitaifa ambayo ameifanya kwa kipindi cha miezi 5 iliyopita ndani miji 19 nchini Uganda

Read More