Stivo Simple Boy Ahitimu Diploma ya Hospitality

Stivo Simple Boy Ahitimu Diploma ya Hospitality

Msanii wa Kenya, Stivo Simple Boy, ameongeza hatua nyingine muhimu katika safari yake ya maisha baada ya kuhitimu masomo yake na kupata Diploma katika kozi ya Hospitality. Stivo ameshiriki furaha yake kupitia mitandao ya kijamii, akipakia picha akiwa amevalia mavazi ya mahafali pamoja na ujumbe mfupi wenye uzito mkubwa unaosomeka “God wins.” Msanii huyo ameahidi kuendelea kutumia elimu yake kujiendeleza zaidi na kuleta mabadiliko katika maisha yake pamoja na jamii inayomzunguka. Kuhitimu huko kunakuja wakati ambapo Stivo Simple Boy ameendelea kujipambanua kama mfano wa uthabiti na kujituma, licha ya changamoto mbalimbali alizokutana nazo katika tasnia ya muziki na maisha binafsi.

Read More
 Stevo Simple Boy Aonyesha Muonekano Mpya wa Gari Lake

Stevo Simple Boy Aonyesha Muonekano Mpya wa Gari Lake

Msanii Stevo Simple Boy ameivutia mitandao baada ya kufichua sura mpya ya gari lake aina ya Nissan March, ambalo sasa limechorwa graffiti kali yenye mandhari ya joka (dragon). Gari hilo limepambwa na michoro mikubwa yenye rangi ang’avu na taswira ya joka, ikitoa mwonekano wa kipekee unaoendana na mtindo wa Stevo Simple Boy na taswira yake kama msanii anayependa utofauti. Muonekano huo mpya wa Nissan March umeweka Stevo Simple Boy kwenye mazungumzo, huku wengi wakimtaja kama msanii asiyeogopa majaribio mapya na mwenye ujasiri wa kuonyesha ubunifu nje ya muziki. Mashabiki wanaendelea kumpongeza kwa hatua hiyo, wakisema kwamba ni ishara ya ukuaji wake binafsi na kujiamini katika kujieleza kupitia sanaa.

Read More
 Stevo Simple Boy Anawishwa Mikono na Pombe ya KSh 100,000

Stevo Simple Boy Anawishwa Mikono na Pombe ya KSh 100,000

Msanii wa muziki wa Kenya, Stevo Simple Boy, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kuposti video ikimuonesha akioshwa mikono na bilionea Chief Godlove kwa kutumia pombe ghali zaidi aina ya Clase Azul kwenye moja ya nightclub Jijini Nairobi. Katika video hiyo iliyosambaa kwa kasi mtandaoni, Stevo anaonekana akifurahia tukio hilo huku akionekana mwenye bashasha. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Stevo Simple Boy ameeleza kwamba, kwa mtazamo wake, matumizi ya pombe au mihadarati hayafai kwa ulevi au matumizi mabaya, bali yanaweza kuwa mfano wa usafi na nidhamu katika maisha. Clase Azul ni moja ya pombe za kifahari duniani, inayotengenezwa nchini Mexico. Nchini Kenya, chupa ya 700 ml ya Clase Azul Plata huuzwa kati ya KSh 24,000 hadi KSh 40,000, huku toleo la Reposado likigharimu kati ya KSh 44,000 na KSh 66,000. Toleo la kifahari zaidi, Clase Azul Gold, linaweza kufikia hadi KSh 159,000 kwa chupa moja, kulingana na maduka ya pombe ya kifahari nchinihumo.

Read More
 Stevo Simple Akodisha Magari ya Kifahari Kumtoa Mke wake Hospitali

Stevo Simple Akodisha Magari ya Kifahari Kumtoa Mke wake Hospitali

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya Stevo Simple Boy anadaiwa kukodisha magari ya kifahari kwa ajili ya kumtoa mpenzi wake hospitalini na kumpeleka nyumbani baada ya kujifungua mtoto wao wa kwanza. Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa mitandaoni, msanii huyo alionekana akiandamana na msururu wa magari ya kifahari, akionyesha furaha kubwa kufuatia ujio wa mtoto wao. Wafuasi wake wengi wamepongeza hatua hiyo wakisema ni ishara ya upendo na heshima kwa mama wa mtoto wake, huku wengine wakikosoa hatua ya kutumia magari ya kifahari wakidai ni maonesho yasiyo ya lazima. Stevo Simple Boy, ambaye amekuwa gumzo kwa maisha yake ya unyenyekevu na uhalisia, bado hajathibitisha wala kukanusha taarifa hizo kupitia mitandao yake ya kijamii.

Read More
  Msanii Stevo Simple Boy Abarikiwa Mtoto wa Kiume na Mpenzi Wake Brenda

 Msanii Stevo Simple Boy Abarikiwa Mtoto wa Kiume na Mpenzi Wake Brenda

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Stevo Simple Boy na mpenzi wake Brenda, wamekaribisha mtoto wao wa kwanza, mvulana waliompa jina Dragon Junior. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Stevo ameshiriki picha akiwa pamoja na Brenda wakimkumbatia mtoto wao mchanga na kufahamisha mashabiki kuwa Dragon Junior amezaliwa salama. Pia ametoa shukrani kwa wafuasi wake kwa sapoti yao na kushiriki nambari yake ya mawasiliano kwa wale wanaotaka kumpa pongezi. Taarifa hii imepokelewa kwa hisia mseto mitandaoni, ikizingatiwa kuwa imekuja siku chache baada ya baadhi ya wafuasi kuhoji uhalisia wa uhusiano wa Stevo na Brenda. Wengine walidai kuwa huenda Brenda hakuwa mke halisi wa msanii huyo, bali ni sehemu ya kiki za kutangaza kazi zake za muziki mtandaoni. Hata hivyo, picha na ujumbe wa Stevo zimeonekana kuthibitisha kuwa wawili hao wamebarikiwa mtoto, hatua ambayo imezima uvumi uliokuwa ukienea kuhusu uhusiano wao. Mashabiki wamemiminika kwenye mitandao ya kijamii kumpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo mpya katika maisha yake binafsi.

Read More
 Stevo Simple Boy Afunga Ndoa Rasmi na Mpenzi Wake wa Muda Mrefu, Brenda

Stevo Simple Boy Afunga Ndoa Rasmi na Mpenzi Wake wa Muda Mrefu, Brenda

Msanii wa muziki nchini Kenya, Stevo Simple Boy, amefunga ndoa rasmi mpenzi wake wa muda mrefu Brenda, katika harusi ya kifahari lakini ya faragha iliyofanyika Jumapili. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Stevo amethibitisha taarifa hizo akisema kuwa ilikuwa siku kubwa na yenye furaha katika maisha yake, akimshukuru Mungu kwa kumbariki na mke mwema. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na ndugu wa karibu, marafiki wachache, na washirika wa karibu wa msanii huyo. Picha na video zilizochapishwa mtandaoni zilionyesha Stevo na Brenda wakiwa wamevalia mavazi ya kifahari, wakionekana wenye furaha tele wakati wa tukio hilo maalum. Mashabiki wengi mtandaoni wamepongeza ndoa hiyo, wakimtakia heri na baraka katika safari yake mpya ya maisha ya ndoa. Wengine wamesema wamevutiwa na unyenyekevu na uhalisia wa msanii huyo, ambaye amekuwa mfano wa kujituma licha ya changamoto alizowahi kupitia.

Read More
 Stevo Simple Boy Ampeleka Mpenzi Wake Mjamzito Likizo Maalum Diani

Stevo Simple Boy Ampeleka Mpenzi Wake Mjamzito Likizo Maalum Diani

Msanii Stevo Simple Boy, ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho baada ya kufanikisha hatua ya kuruka kwa ndege kwa mara ya kwanza. Safari hiyo haikuwa ya kawaida, kwani alichagua kumpeleka mpenzi wake mjamzito kwenye likizo maalum huko Diani. Kupitia mitandao ya kijamii, Stevo alishiriki picha na video wakila bata, wakiburudika katika mandhari mazuri ya ufukweni huku wakionesha furaha na mapenzi ya dhati. Wawili hao walionekana wakifurahia chakula, vinywaji, na wakishikana mikono wakiwa ufukweni, huku wakifurahia mandhari ya bahari na upepo mwanana wa Diani. Furaha ya Stevo na mkewe imeibua mjadala mtandaoni, mashabiki wengi wakimpongeza kwa kuthamini mpenzi wake mjamzito na kuchukua muda wa kuonyesha heshima na mapenzi mbele ya umma. Wengine walieleza kuwa ni jambo la kutia moyo kuona msanii anayekulia mitaani sasa akifikia hatua ya kuonja raha ya maisha kupitia bidii yake ya muziki.

Read More
 Stevo Simple Boy Ajibu Wanaodai Anatumia Magari Kutafuta Umaarufu

Stevo Simple Boy Ajibu Wanaodai Anatumia Magari Kutafuta Umaarufu

Msanii Stevo Simple Boy amenyosha maelezo kuhusu umiliki wa gari aina ya Nissan March aliloinunua hivi karibuni. Hii ni baada ya walimwengu kutilia shaka uhalali wake na kuhoji kwamba msanii huyo amekuwa akitumia magari kutafuta kiki mtandaoni ilhali sio mmiliki halisi. Kupitia Insta Story yake, Stevo amekanusha kutumia magari kutafuta umaarufu, akisisitiza kuwa safari yake ya maisha inachukua mwelekeo mpya. Amewataka mashabiki waamini maendeleo yake kwani ununuzi wa gari hilo ni sehemu ya mafanikio anayojivunia licha ya changamoto nyingi alizopitia. Wiki hii, mjadala uliibuka mitandaoni baada ya Stevo kutangaza umiliki wa gari jipya, mashabiki wakibaki na maswali kuhusu ni magari mangapi anamiliki. Wengine walidai kuwa Nissan March ni gari lake la tatu, wakikumbusha mahojiano ya awali ambapo msanii huyo alikiri baadhi ya magari aliyopiga picha nayo yalikuwa ya kutumia kwa clout pekee.

Read More
 Stevo Simple Boy na Mpenzi Wake Brenda Watangaza Wanatarajia Mtoto wa Kiume

Stevo Simple Boy na Mpenzi Wake Brenda Watangaza Wanatarajia Mtoto wa Kiume

Msanii Stevo Simple Boy na mchumba wake Brenda, wameweka wazi kuwa wanatarajia baraka mpya maishani mwao baada ya kutangaza kuwa wanangoja mtoto wa kiume. Wapenzi hao walifichua habari hizo katika sherehe ya kifahari ya gender reveal iliyofanyika jana, ambapo marafiki na familia walihudhuria kushuhudia tukio hilo la furaha. Tukio hilo lilipambwa na rangi za buluu na pinki, lakini ilipofika wakati wa tangazo rasmi, rangi ya buluu iliibuka ikithibitisha kuwa wanatarajia mtoto wa kiume. Sherehe hiyo imepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa Stevo Simple Boy mitandaoni, wengi wakimpongeza kwa hatua hiyo kubwa ya kimaisha na kumtakia heri katika safari yake mpya ya kuwa mzazi.

Read More
 Stevo Simple Boy Alamba Dili Nono la Ubalozi Skywide Tours & Travel

Stevo Simple Boy Alamba Dili Nono la Ubalozi Skywide Tours & Travel

Msanii wa rap nchini Kenya, Stevo Simple Boy, ameongeza hatua kubwa kwenye kazi yake baada ya kusaini dili la ubalozi na kampuni ya usafiri na utalii, Skywide Tours and Travel. Kampuni hiyo imemteua Stevo kama balozi wake mkuu, hatua ambayo inalenga kuvutia vijana na mashabiki wa muziki wake katika kutumia huduma zao za usafiri na utalii. Uteuzi huu unatajwa kuwa ni fursa kubwa kwa msanii huyo, kwani unamfungulia milango mipya ya ushawishi kibiashara na kuongeza thamani yake nje ya muziki. Vilevile, unasaidia katika kukuza chapa ya Skywide Tours and Travel kwa kushirikiana na jina linalopendwa na vijana wengi nchini. Dili hili linamweka Stevo Simple Boy kwenye nafasi ya kipekee ambapo muziki wake, uhalisia wa maisha yake, na mvuto wake kwa mashabiki vinatumika kama nyenzo ya kutangaza huduma za utalii na usafiri, huku likionekana kama hatua muhimu katika safari yake ya kukuza kipato na ushawishi.

Read More
 Stevo Simple Boy na Brenda Watarajia Mtoto wa Kwanza

Stevo Simple Boy na Brenda Watarajia Mtoto wa Kwanza

Msanii maarufu wa muziki Stevo Simple Boy ametangaza rasmi kwamba yeye na mpenzi wake Brenda wanatarajia mtoto wao wa kwanza. Taarifa hiyo imewavutia maelfu ya mashabiki baada ya Stevo kushiriki picha za kupendeza za mpenzi wake akiwa na ujauzito kupitia ukurasa wake wa Instagram. “Maisha ni safari… sasa kuna kijana au kamrembo anakuja kuendeleza legacy 💯😊 #BabyBump #dragon,” Stevo aliandika katika ujumbe wa kugusa moyo. Picha hizo zilizopigwa na lidstudios ambao walitajwa kama sehemu bora kwa picha za ujauzito, harusi, sherehe za baby shower, na kutangaza jinsia ya mtoto, zimeonyesha upande wa kipekee wa maisha ya msanii huyo anayejulikana kwa unyenyekevu wake na ujumbe wa matumaini katika nyimbo zake. Mashabiki wake pamoja na watu maarufu kwenye tasnia ya burudani wamempongeza kwa hatua hiyo kubwa ya maisha, wakimtakia heri katika safari yake ya kuwa mzazi. Ujio huu mpya unaonekana kuwa mwanzo wa sura mpya kwa Stevo, ambaye amekuwa akivutia wafuasi wengi kutokana na maisha yake ya kweli, unyenyekevu, na msimamo thabiti katika kazi yake ya muziki.

Read More
 Brenda Asema Alimpenda Stevo Muda Mrefu Kabla Ya Kuanzisha Uhusiano

Brenda Asema Alimpenda Stevo Muda Mrefu Kabla Ya Kuanzisha Uhusiano

Brenda, mpenzi mpya wa staa maarufu wa muziki wa Bongo, Stevo, amezua hisia mitandaoni baada ya kufunguka kuhusu mwanzo wa uhusiano wao ulioanzia kama ndoto ya muda mrefu kwake. Katika video aliyoshare mwaka mmoja uliopita, Brenda alikiri wazi kuwa Stevo alikuwa crush wake, jambo lililovutia mashabiki wengi wa msanii huyo. Baada ya miezi michache tu tangu video hiyo kuonekana mtandaoni, Brenda na Stevo walikutana rasmi na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi ambao umeimarika kwa kasi. Sasa furaha yao imeongezeka zaidi kwa kuwa Brenda anatarajia mtoto wa Stevo, jambo lililopokelewa kwa mshangao na furaha kubwa na wafuasi wa wawili hao. Brenda ameeleza kuwa kuishi na Stevo na kujenga familia ni baraka kubwa kwake. Aidha, amempongeza Stevo kwa juhudi zake za kuwa baba mzuri na mwenza mwaminifu. Kwa upande wake, Stevo ameonyesha shukrani na furaha kwa mpenzi wake na amewahakikishia mashabiki kuwa anajitahidi kuwa baba bora na mume mwaminifu. Mashabiki wa Brenda na Stevo wameonyesha mshangao na furaha zao mtandaoni, wakimtakia kila la heri Brenda na kuhimiza wapenzi wote kuwa na matumaini kuhusu maisha ya mapenzi na familia.

Read More