Stevo Simple Boy afunguka sababu za kususia show ya Mombasa

Stevo Simple Boy afunguka sababu za kususia show ya Mombasa

Msanii Stevo Simple Boy amewaomba radhi mashabiki zake baada ya kukosa kutumbuiza kwenye tamasha la So Fire Fiesta lilofanyika Nyali, Kaunti ya Mombasa. Kupitia taarifa aliyotoa kupitia ukurasa wake wa Instagram amewalaumu waandaji wa tamasha hilo kwa kushindwa kumlipa pesa zake kabla ya kupanda jukwaani. “Naomba msamaha kwanza kwa mashabiki wangu na kushukuru management yangu MIB Africa mumejaribu Kadri wa uwezo wenu na mnapigania Sana kuniona juu kila wakati..Tunajaribu Sana kama wasani ila wakenya wenzetu ndo wanatudhulumu”, Alisema. Stevo ambaye alikuwa alipaswa kutumbuiza kwenye show hiyo ambaye Ruger wa Nigeria alikuwa msanii kinara amesema kitendo cha kususia kupanda jukwaani kulimpelekea kufungiwa hoteli aliyokuwa amekodishwa na waandaji wa So Fire Fiesta. “Tulifungiwa hotelini kwa sababu tumekataa kuperfom bila kulipwa na kampuni ya sofire fiesta Ni tendo ambalo limenifika kooni kama Msanii na imenikataa moyo Sana ila sikati tamaa kabisa ntazidii kupambana na nawapenda sana wakenya wanao ni support.”, Aliongeza. Hata hivyo mashabiki wamechukizwa na hatua ya waandaji wa So Fire Fiesta kutaka kumdhulumu Stevo Simple Boy huku wakionekana kumnyoshea kidole cha lawama mchekeshaji Eric Omondi kwa masaibu yaliyompata msanii huyo kwa kusema kuwa huenda alishirikiana na wasimamizi wa tamasha hilo kumfanyia mchezo mchafu.

Read More
 Ruger amkataa Stevo Simple Boy

Ruger amkataa Stevo Simple Boy

Hitmaker wa “Girlfriend”, Msanii Ruger amemkataa hadharani Stevo Simple Boy baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kama ana wimbo wa pamoja na msanii huyo wa Men In Business. Ruger ambaye yupo nchini kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki amesema hamjui kabisa msanii huyo huku akithibitisha ujio wa ngoma yake na kundi la Sauti Sol ambayo itapatikana kwenye album yake mpya mwakani. Utakumbuka juzi kati Eric Omondi alithibitisha ujio wa kolabo ya Stevo Simple Boy pamoja na msanii huyo kutoka nchini Nigeria mara tu atakapotua nchini. “At this rate wacha sisi tutengeneze Pesa watu ni Viziwi hawaskii maneno. The only Event happening in Mombasa this December. 28th December Wild waters. Na Stivo Somple boy ashajishindia Collabo na Ruger. GET YOUR TICKETS from my BIO @sofire_53 @sofire_fiesta”, Aliandika Instagram Ruger anatarajiwa kutoa burudani leo kwenye tamasha la So Fire Fiesta litakalofanyika Nyali, Mombasa.

Read More
 Stevo Simple Boy akiri hana mpenzi kwa sasa

Stevo Simple Boy akiri hana mpenzi kwa sasa

Hitmaker wa “Freshi Barida”, Msanii Stevo Simple Boy ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mpenzi na anafurahia maisha yake mapya Msanii wa huyo wa Men in Business ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amefungua milango kwa waliokuwa wanamumezea mate kujaribu bahati yao. “Mapenzi ya siku hizi jamani, sasa niko single naenjoy. Jamani kua single raha, akinipenda baba na mama inatosha, lakini ata mnivunje roho na mbavu, nikipata mwingine napenda tena”, Ameandika. Kauli ya Stevo Simple Boy imekuja siku chache baada ya kuvunjika kwa mahusiano yake na mchumba wake Gee, mahusiano ambayo yalidumu kwa kipindi cha miezi sita.

Read More
 Penzi la Stevo Simple Boy na Jenny Wangui lavunjika rasmi

Penzi la Stevo Simple Boy na Jenny Wangui lavunjika rasmi

Mahusiano ya Stevo Simple Boy na Mrembo Jenny Wangui yamefika mwisho ikiwa ni miezi miwili tangu wawili hao waanze kuchumbiana. Stevo amefuta picha zote akiwa na mrembo huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram siku chache baada ya watumiaji wa mtandao wa Tinder kuibua madai kuwa Jenny Wangui ana akaunti kwenye mtandao huo wa kuwatafuta wapenzi. Utakumbuka jana Jenny Wangui aliibuka na kudai kuwa hakuwahi toka kimapenzi na mkali huyo wa Ngoma ya “Freshi Barida” kwa kuwa mahusiano yao yalikuwa ya kuigiza kwa ajili ya kuutangaza muziki wa Stevo Simple Boy.

Read More
 Gee amuumbua Stevo Simple Boy “Tulipanga tufanye KIKI, Hatuna mahusiano”

Gee amuumbua Stevo Simple Boy “Tulipanga tufanye KIKI, Hatuna mahusiano”

Kama ulidhani mahusiano ya Stevo Simple Boy na Gee yalikuwa ya kweli ni kuambie tu pole, kwa sababu mrembo huyo amejitokeza hadharani na kukiri kuwa hajawahi toka kimapenzi na msanii huyo kama watu wengi wanavyochukulia mtandaoni. Gee ambaye amekuwa akideka sana juu ya huba la Stevo Simple Boy kiasi cha kuwatishia wanawake kutomchumbia hitmaker huyo wa Wedding Day, amesema mahusiano yao yalikuwa ni kiki kwa ajili ya kuutangaza muziki wa Stevo Simple Boy. Hata hivyo kauli ya mrembo huyo imeonekana kuwakera watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii ambao wametoa changamoto kwa wasanii kutoa muziki mzuri badala ya kuishi maisha ya kuigiza mtandaoni. Utakumbuka mapema mwaka huu baada ya Stevo Simple Boy kumtambulisha Gee kama mpenzi wake na kumvisha pete ya uchumba alienda mbali zaidi na kuwaaminisha walimwengu kuwa wao ni mume na mke walipofanya harusi ya kitamaduni maarufu kama Ruracio kwa siri.

Read More
 STEVO SIMPLE BOY AFUNGA NDOA YA KITAMADUNI NA MCHUMBA WAKE JENNY WANGUI

STEVO SIMPLE BOY AFUNGA NDOA YA KITAMADUNI NA MCHUMBA WAKE JENNY WANGUI

Msanii Stivo Simple Boy amefunga ndoa ya kitamudani maarufu kama Ruracio na mchumba wake Jenny Wangui ikiwa ni miezi kadhaa tangu amvishe pete ya uchumba. Kupitia ukurasa wake wa instagram Stivo ameposti ujumbe mrefu wa mahaba kwa mrembo huyo na kusema kwamba amechukua maamuzi hayo kama njia ya kuwathibitishia wazazi wa Jenny Wangui kuwa hafanyi mzaha katika mahusiano yake bali ameamua kwa kauli moja kuingia kwenye maisha ya ndoa. Hitmaker huyo “Freshi Barida” ambaye amepongezwa na mashabiki zake kwa hatua hiyo kubwa maishani, amemuondolea hofu mpenzi wake kwa kumueleza kuwa penzi lake ni la kweli, hivyo asitishwe na watu mitandaoni. Hii ni baada ya mwanamke mmoja kujitokeza na kudai kuwa amemzia kimapenzi Stivo the Simple Boy, kitendo kilichomfanya gee kuwa na wasi wasi juu ya hatma ya mahusiano yake na msanii huyo wa Men in Business.

Read More
 STIVO AKANUSHA TUHUMA ZA KUKIMBIA NA MCHUMBA WA MTU

STIVO AKANUSHA TUHUMA ZA KUKIMBIA NA MCHUMBA WA MTU

Msanii Stivo Simple Boy kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu tuhuma za kumuibia rapa Rapdon mpenzi wake. Katika mahojiano yake ameonyosha maelezo kuhusu na madai hayo kwa kusema kwamba madai hayo hayana ukweli wowote na yameibuliwa rapa huyo kwa ajili ya kujitengenezea mazingira ya kuzungumzia kwenye mitandao ya kijamii. Hitmaker huyo wa “Freshi Barida” amesema uhusiano wake na mpenzi wake ni wa kweli na sio kiki kama namna watu wanavyochukulia mitandaoni. Sanjari na hilo mpenzi wa Stivo amepuzilia mbali madai ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na rapa don kwa kusema walikuwa marafiki kipindi cha nyuma ila hajawahi toka kimapenzi. Kauli yao imekuja mara baada ya rapa Rapdon kujitokeza wazi wazi na kudai kuwa Stivo Simple Boy alimvunjia heshima kwa hatua ya kumunyanganya mpenzi wake.

Read More
 STEVO SIMPLE BOY ATAJWA KUWANIA TUZO ZA ZIKOMO

STEVO SIMPLE BOY ATAJWA KUWANIA TUZO ZA ZIKOMO

Msanii wa Men In Business, Stevo The Simple Boy ametajwa kuwania vipengele viwili katika Tuzo za Kimataifa za Zambia ziitwazo Zikomo Awards. Stevo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na video ya wimbo wake “Fresh Barida”, anawania tuzo hizo kupitia vipengele vya BEST UPCOMING ARTIST OF THE YEAR na BEST SONG OF THE YEAR. Kumpigia kura Stevo The Simple Boy ni rahisi, ingia kwenye tovuti ya tuzo hizo http://www.zikomoawards.com kisha nenda kwenye category iliyoandikwa Music & Film, baada ya hapo unamu-nominate.

Read More
 STEVO SIMPLE BOY AMTOLEA UVIVU EX WAKE PRITTY VISHY KISA MAHARI YA SHILLINGI MILLIONI 2

STEVO SIMPLE BOY AMTOLEA UVIVU EX WAKE PRITTY VISHY KISA MAHARI YA SHILLINGI MILLIONI 2

Msanii Stevo Simple Boy amepuzilia mbali mahari ya shillingi millioni 2 ambayo mpenzi wake wa zamani Pritty Vishy aliweka wazi kwa wanaume wanaotaka kumchumbia. Katika mahojiano na mpasho Stevo amesema mrembo huyo anatumia suala kutafuta mazingira ya kuzungumziwa kwenye mitandao ya kijamii  kwani dhamani yake haiendani na kiwango cha mahari alichodai. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Freshi Barida” ameweka wazi sababu zilizompelekea kuachana na Vishy kwa kusema kwamba mrembo huyo alimsaliti kimapenzi kwa kutoka kimapenzi na wanaume wengine. Hata hivyo amekanusha madai ya Pritty Vishy kuwa amekuwa akimlilia warudiane kwa kusema kwamba  penzi lao lilivunja kitambo na hawezi kumrudia kutokana na tabia zake ambazo hazikumfurahisha hata kidogo. Mbali na hayo msanii huyo ambaye chini ya lebo ya muziki ya Men in Business amedokeza ujio wa tamasha lake la Freshi Barida ambalo linalenga kukuza vipaji vya vijana chini.

Read More
 STEVO SIMPLE BOY APATA HAKIMILIKI YA NEMBO YAKE YA FRESHI BARIDA

STEVO SIMPLE BOY APATA HAKIMILIKI YA NEMBO YAKE YA FRESHI BARIDA

Mwanamuziki Stevo Simple Boy ameripotiwa kusajili jina lake la biashara ambalo ni Freshi Barida. Taarifa hiyo imethibitishwa na lebo ya muziki ya Men In Business kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram ikisema kuwa Stevo kwa sasa ndiye mmiliki halisi wa jina la Freshi Barida kwa mujibu wa sheria ikizingatiwa tayari amepewa hakimiliki za jina hilo na Ofisi ya Patent ya Kenya. Lebo hiyo ambayo inasimamia kazi za Stevo Simple Boy imetoa angalizo kwa atakayetumia nembo hiyo bila ridhaa ya msanii huyo na uongozi wake kwa ajili ya shughuli za kibiashara atachukulia hatua kali za kisheria ambayo itajumuisha kulipa faini. Hii taarifa njema kwa Stevo Simple Boy ambaye juzi kati alizindua bidhaa zake za mavazi za Freshi Barida, siku kadhaa tangu atangaze ujio wa kinywaji chake kiitwacho Freshi Barida Energy Drink.

Read More