TORY LANEZ ADAI DRAKE NA THE WEEKND WANAMBANIA KOLABO
Rapa Tory Lanez ameweka wazi kwamba Drake na The Weeknd wamekuwa wakimbania kolabo kila anapojaribu kuwacheki. Mkali huyo kutoka Canada kupitia Twitter aliandika ujumbe unaosomeka “Nimekuwa nikiwatumia nyimbo kwa miaka sasa, lakini hakuna hata mmoja aliyekubali.” Tory Lanez amefunguka hayo alipokuwa akijibu swali la shabiki mmoja ambaye aliuliza kama kwenye Album yake mpya kutakuwa na kolabo ya Drizzy au The Weeknd.
Read More