Vera Sidika atumia shape kama kiki

Vera Sidika atumia shape kama kiki

Baada ya kuchafua hali ya hewa siku chache zilizopita, Mrembo Vera Sidika ameachia rasmi wimbo wake mpya kupitia mtandao wa Youtube. Inawezekana mpaka sasa watu wengi wameamini kilichosemwa na Vera Sidika juu ya kutoa shepu yake, lakini ukweli umejidhihirisha baada ya kuachia wimbo wake mpya, unaokwenda kwa jina la “POPSTAR”. Wimbo wa Vera Sidika ameuimba kwa miondoko ya Hiphop na baadhi ya comment za Wakenya zimemtaadharisha Diana B kuwa Vera amekuja kumpindua kimuziki.

Read More
 Brown Mauzo avunja kimya chake kuhusu muonekano mpya wa Vera Sidika

Brown Mauzo avunja kimya chake kuhusu muonekano mpya wa Vera Sidika

Msanii Brown Mauzo amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya baby mama wake Vera Sidika kukiri kufanya upasuaji wa kupunguza makali yake kutokana na matatizo ya kiafya. Kupitia mtandao wa Instagram ameandika waraka mrefu akipongeza mrembo huyo kwa hatua ya kujitokeza wazi na kuweka mapungufu yake kwa umma huku akisema itakuwa funzo kwa wadada ambao kwa njia moja au nyinngine wataka kubadilisha miili yao kwa upasuaji. Katika hatua nyingine Mauzo amekiri kutamani maungo ya mrembo huyo kabla hajafanyiwa surgery ambapo ameenda mbali zaidu na kuhapa kwamba hatokuja kumkimbia Vera Sidika kutokana na muonekano wake mpya kwani alivutiwa na utu wake. Hata hivyo baadhi ya mashabiki wametafsiri ujumbe huo wa Brown Mauzo kuwa ni njia msanii huyo kutengeneza mazingira ya kuachia wimbo mpya huku wakienda mbali zaidi na kuhoji kuwa hatua vera sidika kutangaza hadharini kufanya upasuaji wa kupunguza makalio ilikuwa ni mkakati wa kumtoa kisanaa. Utakumbuka Brown mauzo na vera sidika ambaye walihalalisha mahusiano yao Septemba, 24 mwaka wa 2020 wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwae Amina Brown.

Read More
 Vera Sidika Afichua Kufanyiwa Upasuaji wa Kupunguza Makalio

Vera Sidika Afichua Kufanyiwa Upasuaji wa Kupunguza Makalio

Mrembo maarufu na mjasiriamali wa mitandaoni, Vera Sidika, amezua gumzo mitandaoni baada ya kufichua kuwa alifanyiwa upasuaji wa kupunguza makalio kutokana na matatizo ya kiafya aliyoyapata kufuatia mabadiliko ya awali ya mwili wake. Kupitia ujumbe aliouandika kwenye Instagram, Vera amesema alilazimika kupitia hatua hiyo baada ya kupitia kipindi kigumu sana kiafya, hali iliyomlazimu kufanya maamuzi ya kubadili muonekano wake kwa mara nyingine. Mama huyo wa mtoto mmoja ameongeza kuwa safari hiyo haikuwa rahisi, na imeacha athari kubwa katika maisha yake. Vera amewashauri wanawake kujikubali jinsi walivyo na kutokubali kushawishiwa na shinikizo la mitindo au marafiki kuingia kwenye upasuaji wa kubadilisha miili yao. Amesisitiza kuwa hatua kama hizo zinaweza kuwa na madhara ya muda mrefu kiafya na kiakili. “Wanadada tafadhalini, mjue kujipenda mlivyo na msikubali shinikizo la rika liwafanye mkimbilie kufanya mambo ambayo yatawaharibia maisha yenu huko mbeleni,” aliandika Instagram Haya yanajiri miaka kadhaa baada ya Vera kuwa gumzo kwa mara nyingine kwa kuonekana akiwa na muonekano tofauti wa ngozi, ambapo alidai kuwa ameachana na bidhaa za kubadilisha rangi ya ngozi. Hata hivyo, madai hayo baadaye yalitafsiriwa na wengi kuwa yalikuwa mbinu ya kiki kwa ajili ya kutangaza mradi mpya. Vera Sidika, ambaye ni miongoni mwa watu maarufu wenye ushawishi mkubwa mitandaoni nchini Kenya, ameonekana kuchukua mwelekeo mpya wa maisha kwa kutoa tahadhari na elimu kwa mashabiki wake, hasa wanawake, kuhusu hatari za kubadilisha maumbile kwa njia za upasuaji.

Read More
 VERA SIDIKA AWAPA SOMO MABINTI WANAOTOKA KIMAPENZI NA MASPONSA

VERA SIDIKA AWAPA SOMO MABINTI WANAOTOKA KIMAPENZI NA MASPONSA

Mwanasosholaiti maarufu nchini Kenya, Vera Sidika ameshauri kina dada kuchukua fedha za Sponsa na kuwekeza. Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, mmoja wa mashabiki wake alimuuliza ushauri wake kwa wasichana ambao wanatoka na watu wazima. “Ushauri wako kwa msichana anayechumbia wababa,” Shabiki aliuliza. “Kula pesa yake mzuri, lakini cha muhimu wekeza,”Alijibu Vera. Utakumbuka Vera alipata umaarufu nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla mara baada ya kutokea kwenye video ya kundi la P Unit, You Guy.

Read More
 OTILE BROWN AMVUA NGUO MREMBO MWENYE SHAPE MATATA NCHINI KENYA VERA SIDIKA

OTILE BROWN AMVUA NGUO MREMBO MWENYE SHAPE MATATA NCHINI KENYA VERA SIDIKA

Staa wa muziki nchini Otile Brown amemtolea uvivu mrembo mwenye shape matata Vera Sidika baada ya mrembo huyo kuonekana kulitaja jina lake katika siku za hivi karibuni. Kupitia instagram page yake Otile Brown amemtaka Vera Sidika kuitunza ndoa yake ikizingatiwa kuwa hajawahi kuizungumzia ndoa yake na mumewe brown mauzo sehemu yeyote kutokana na heshima aliyonao kwao. “Jaribu kumheshimu mumeo na kulinda ndoa yako kama ninavyojaribu kunyamaza kila unapotaja jina langu. Dont get comfortable.” Ameandika kupitia insta story yake. Kauli ya otile brown imekuja siku chache baada ya vera sidika kusema kuwa ikitokea otile brown anataka kufanya kolabo na mumwe Brown Mauzo ataunga mkono kikamilifu kolabo hiyo. Hili halikutarajiwa kabisa kutoka kwa Vera Sidika ikizingatiwa kuwa alikuwa kwenye mahusiano na Otile Brown kipindi cha nyuma ambapo walikuja wakaachana vibaya baada ya kuingia kwenye ugomvi mbaya. Kutokana na hilo inaonekana kwamba Vera sidika amepata furaha tena na labda alimsamehe Otile Brown ndiyo maana hajawahi kusema jambo lolote baya kumhusu.

Read More
 SOCIALITE MAARUFU MTANDAONI VERA SIDIKA KUFANYA TENA UPASUAJI WA MATITI

SOCIALITE MAARUFU MTANDAONI VERA SIDIKA KUFANYA TENA UPASUAJI WA MATITI

Mrembo maarufu mtandaoni nchini Kenya na Afrika Mashariki, Vera Sidika amesema atafanya tena upasuaji wa matiti yake ili kuboresha muonekana wake baada ya kumaliza kuzaa. Kupitia Instagram page yake Vera Sidika amesema anatamani kupata matiti yenye umbo la mviringo na ambayo yamesisima ila kwa sasa anataka kwanza aikuze familia yake. “Kunyonyesha hakujawahi kunisumbua hata kidogo, inafanya hivyo kwa kujivunia na nina furaha nyingi. Mara tu baada ya kumaliza kupata watoto, hakika nitafanyiwa upasuaji wa kubadilisha umbo la matiti yawe ya kuvutia, ya mviringo na yaliyoinuka,” amesema Vera. Ikumbukwe Vera Sidika ambaye miaka michache iliyopita alifanyiwa upasuaji wa kuongeza ukubwa wa matiti yake pia ameweka wazi kwamba amekuwa akijivunia sana kumnyonyesha binti yake, Asia Brown.

Read More
 BROWN MAUZO NA VERA SIDIKA MBIONI KUFUNGA NDOA

BROWN MAUZO NA VERA SIDIKA MBIONI KUFUNGA NDOA

Tutegemee ndoa kutoka kwenye couple ya mwanamuziki Brown mauzo na mrembo mwenye shape matata Vera Sidika mapema week ijayo. Hayo yamebainishwa kutoka kwa Instagram page ya mwanamuziki brown mauzo ambaye ameShare picha ya mrembo huyo na kuandika ujumbe unao ashiria kuwepo kwa ndoa kati yao huku akiweka wazi tarehe husika ya tukio hilo kuwa ni Januari 18 mwaka wa 2022. Hata hivyo walimwengu wameibuka kupitia mitandao ya kijamii na kuhoji kuwa brown mauzo anajianda kuachia kazi yake mpya ila anajaribu kutengeneza mazingira ili azungumziwe kwenye vyombo vya habari. Utakumbuka brown mauzo pamoja na vera sidika wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwae Amina Brown

Read More