WILLY PAUL APOTEZA TAKRIBAN SHILLINGI MILLIONI 96 BAADA YA TUHUMA ZA UBAKAJI KUIBULIWA DHIDI YAKE

WILLY PAUL APOTEZA TAKRIBAN SHILLINGI MILLIONI 96 BAADA YA TUHUMA ZA UBAKAJI KUIBULIWA DHIDI YAKE

Staa wa muziki nchini Willy Paul amedai kwamba amepoteza takriban shillingi millioni 96 tangu diana marua amtuhumu kuwa alijaribu kumbaka. Kupitia waraka aliyochapisha kwenye ukurasa wake Instagram Willy Paul amesema amepoteza matangazo ya takriban shillingi millioni 10 kutoka kwa kampuni moja ya mawasilioni, shillingi milioni 4 kutoka kwa kampuni ya magodoro na dili la kurekodi na kusambaza muziki la takriban shillingi millioni 82 . Ameenda mbali zaidi na kutoa onyo kwa Diana Marua na baadhi ya watu wanaolenga kumshusha kimuziki kwa kusema kwamba mrembo huyo amewalipa baadhi ya wanawake watoe ushahidi wa uongo dhidi yake.  Hitmaker huyo wa “My Woman” katika taarifa yake amesema hatorusu baadhi ya watu wamharibie chapa yake ya muziki huku akidokeza kwamba atafungua kesi dhidi ya Diana Marua ambaye kwa mujibu wake analenga kumharibia kazi ya muziki kwa tuhuma za uongo. Hata hivyo baadhi ya wadau wameonekana kutofautiana na Wiily Paul ambapo baadhi wamedai msanii huyo ameghushi kiasi hicho cha fedha huku wengine wakidai kwamba yeye ndiye alianzisha sakata hilo hivyo apambane nalo hadi mwisho.

Read More
 WILLY PAUL AMALIZA BIFU YAKE NA ERIC OMONDI

WILLY PAUL AMALIZA BIFU YAKE NA ERIC OMONDI

Hatimaye staa wa muziki nchini Willy Paul ametangaza kumaliza bifu yake na mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi baada ya wawili hao kurushiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii kwa muda. Kupitia ukurasa wake wa instagram willy paul amemtaka Eric Omondi kuwa waache matukio yasioyokuwa na msingi na badala yake waupambanie muziki wa kenya uweze kusikilizwa zaidi kimataifa. Hitmaker huyo wa “My Woman” amesema bifu kwenye muziki hazisaidii kwani zinarudisha tasnia ya muziki nchini ambapo amemtakia Eric Omondi kila la kheri kwenye harakati za kuupambania muziki wa Kenya. Ikumbukwe bifu kati ya Willy Paul na Eric Omondi ilianza wakati mchekeshaji huyo alimshauri bosi huyo wa Saldido kubadilisha jina la msaani wake mpya Queen P huku akisisitiza kuwa Miss P ambaye alikuwa msanii wa Willy Paul atasalia kuwa mmoja.

Read More
 WILLY PAUL AHIRISHA TENA TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

WILLY PAUL AHIRISHA TENA TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki nchini Willy Paul ametangaza hataachia album yake mpya iitwayo “The African Experience” kama ilivyokuwa imepangwa. Kupitia ukurasa wake wa instagram Willy Paul amesema hatua ya kuahirisha kutoka kwa album hiyo ni fursa nzuri kwake kujiandaa vilivyo na kuwapa mashabiki wake kazi nzuri. Hata hivyo, bosi huyo wa Saldido records hajasema album hiyo itatoka lini na ni mabadiliko yapi anayafanya. African Experience album ambayo ilipaswa kutoka oktoba 22  ikiwa ni exclusive kwenye jukwaa la boomplay, ina jumla ya nyimbo 17, ikiwa na kolabo 5 pekee kutoka kwa wakali kama Juma Jux, Eddy Kenzo,Daphne,Fik Fameica na Kelly Khumalo

Read More
 WILLY PAUL ATOA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

WILLY PAUL ATOA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki nchini Willy Paul amewapa mashabiki wake orodha nzima ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya  “The African Experience”. “The African Experience” ina jumla ya nyimbo 17, ikiwa na kolabo 5 pekee kutoka kwa wakali kama Juma Jux, Eddy Kenzo,Daphne,Fik Fameica na wengine. Hitmaker huyo wa “Lenga” anatarajiwa kuiachia album hiyo wakati wowote kuanzia sasa kwani ni saa chache tu zimesalia.. Hata hivyo Willy Paul tayari ameachia video ya wimbo mmoja kutoka kwenye album hiyo ambao ni “Ogopa Wasanii”, wimbo namba 11.

Read More
 HAPPY C AMPA ZA USO WILLY PAUL KWA KUKOSA UBUNIFU

HAPPY C AMPA ZA USO WILLY PAUL KWA KUKOSA UBUNIFU

Mkali wa muziki nchini Happy Chondo maarufu kama Happy C kutoka lebo ya 001 Music amemtolea uvivu staa wa muziki nchini Willy Paul kwa madai ya kukosa ubunifu kwenye uandishi wa nyimbo zake. Happy C ametoa kauli hiyo kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram mara baada ya Willy Paul kuachia wimbo wake mpya uitwao “Ogopa Wasanii” ambao kwa mujibu wake amekopi idea ya msanii wa Bongofleva Diamond Platinumz. Kulingana na Happy C bosi huyo wa Saldido International anajishusha kwenye suala la uandishi wa nyimbo zake ikizingatiwa kuwa kuna wasanii wadogo na hodari ambao wana uwezo wa kuandika nyimbo zenye maudhui ya kumuelisha jamii. Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha “Mariana” ameenda mbali zaidi na kusema kwamba yupo tayari kumuandikia willy paul nyimbo kama ataendelea kutoa nyimbo ambazo hazina mashiko.

Read More
 WILLY PAUL: SIHITAJI SUPPORT YA WASANII WA KENYA KWENYE THE AFRICAN EXPERIENCE ALBUM

WILLY PAUL: SIHITAJI SUPPORT YA WASANII WA KENYA KWENYE THE AFRICAN EXPERIENCE ALBUM

Hitmaker wa Lenga msanii Willy paul ametoa ya moyoni baaada ya baadhi ya wasanii nchini kuzuzia kumpa support kwenye album yake ijayo  iitwayo The African Experience. Kupitia ukurasa wake wa instagram Willy Paul amewatolea uvivu wasanii ambao amewataja kama wanafiki kwa kusema kwamba ahitaji watu wa sampuli hiyo kumuunga mkono wakati huu anajianda kuiachia album yake mpya. Bosi huyo wa Saldido ameenda mbali zaidi na kusema kwamba alizaliwa na atakufa pekee yake hivyo haitaji support ya mtu yeyote kwani Mungu yupo upande wake. The Africa Experience album kutoka kwa mtu mzima Willy paul inatarajiwa kuingia sokoni rasmi Oktoba 24 mwaka ingawa hajatuambia  idadi ya nyimbo ambazo zitapstikana kwenye album hiyo. Hii itakuwa ni Album yake ya pili, baada kuachia  album yake ya kwanza mwaka wa 2020 iitwayo songs of solomon ikiwa na jumla ya mikwaju kumi ya moto.

Read More