ZUCHU ATAKA KUSHINDANISHWA NA WASANII WA KIUME

ZUCHU ATAKA KUSHINDANISHWA NA WASANII WA KIUME

Hitmaker wa “Sukari”, Msanii Zuchu amedai kwa uandishi wake kwenye muziki anafaa kuwekwa kwenye ligi ya wasanii wa kiume. Kupitia ukurasa wake wa twitter Zuchu amesema kupambanishwa na wanawake ni kuwaonea. “Kwa uandiashi wangu yafaa kuwekwa kwenye ligi za wanaume, wadada wenzangu nitawaonea tu,” amesema Zuchu. Kauli ya Zuchu inakuja kipindi anatarajia kuachia nyimbo mbili kwa pamoja. Utakumbuka Zuchu kutoka WCB Wasafi kwa sasa anafanya vizuri na nyimbo zake mbili, Jaro pamoja na Fire na juzi kati alitajwa kuwania tuzo za AFRIMA 2022 kwenye kipengele cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki akichuana vikali na wasanii wengine kutoka ukanda huu

Read More
 ZUCHU KULIPA MILLIONI 500 ZA KENYA KUONDOKA WCB

ZUCHU KULIPA MILLIONI 500 ZA KENYA KUONDOKA WCB

C.E.O wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa Zuchu kuondoka katika Lebo hiyo atalipa takriban shilingi milllioni 500 za Kenya. Kauli ya Diamond inakuja muda mfupi baada ya Babu Tale kutangaza Lebo hiyo itasaini wasanii wapya hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Babu Tale ameandika “Hivi karibuni tutasaini wasanii wawili kujiunga lebo ya Wasafi ila safari hii tumeamua msanii atakua na mashaidi wawili kutoka COSOTA na BASATA” “Music ni biashara yetu na ni jukumu letu kukuza na kusimamia hii kazi, hatuwezi kuacha hata iwe vipi” amesema Tale. Hadi sasa WCB iliyoanza kusaini wasanii tangu mwaka 2015, ina wasanii kama Diamond Platnumz, Queen Darleen, Lava Lava, Mbosso na Zuchu. Utakumbuka WCB Wasafi haijasaini msanii mpya tangu Aprili 2020 walipomtangaza Zuchu ambaye alikuwa msanii wa pili wa Kike ndani ya lebo hiyo.

Read More
 ZUCHU AWEKA HISTORIA BOOM PLAY KUPITIA  “I’AM ZUCH EP”

ZUCHU AWEKA HISTORIA BOOM PLAY KUPITIA “I’AM ZUCH EP”

Extended Playlist ya I’AM ZUCHU kutoka kwa mwanamuziki wa Bongofleva Zuchu imefanikiwa kufikisha zaidi ya streams Million 100′ katika digital platforms zote za kuuza na kusikiliza kazi za muziki. EP hiyo ambayo ndio ya kwanza kwa Zuchu katika safari yake ya muziki, ilitoka Aprili, mwaka 2020 ikiwa na jumla ya nyimbo saba ambazo aliwapa mashavu wasanii wawili pekee kusikika kwenye EP hiyo ambao ni Mbosso na Khadija Kopa ambaye ni Mama yake mzazi. Utakumbuka Zuchu alitambulishwa rasmi kujiunga na lebo ya WCB, Aprili 8, mwaka 2020, ndiye msanii wa kwanza WCB kutambulishwa kwa mtindo wa kuachia EP, wenzake hawakupata bahati hiyo

Read More
 ZUCHU AFIKISHA SUBSCRIBERS MILLIONI 2 YOUTUBE

ZUCHU AFIKISHA SUBSCRIBERS MILLIONI 2 YOUTUBE

Hitmaker wa ngoma ya “Mwambie”, Msanii Zuchu amefanikiwa kufikisha jumla ya subscribers Milioni 2 kwenye channel yake ya youtube. Zuchu anakuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki mwenye Subscribers Milioni 2 na wanne Afrika akiwa ametanguliwa na Sherine (Misri) , Zina Daoudia (Morocco) na Yemi Alade (Nigeria). Katika hatua nyingine Zuchu pia Kupitia channel yake ya YouTube hadi sasa kazi zake zimetazamwa zaidi ya mara milioni 327,652,269 tangu ajiunge na mtandao huo Januari 29 mwaka wa 2019.

Read More
 ZUCHU AKATAA DILI LA SHILLINGI MILLIONI 12 ZA KENYA KISA DINI

ZUCHU AKATAA DILI LA SHILLINGI MILLIONI 12 ZA KENYA KISA DINI

Msanii wa Bongofleva kutoka WCB Wasafi, Zuchu amekataa dili la kutangaza pombe lenye thamani ya Dola 108,000 sawa na shilling milllioni 12,468,600 za Kenya. Kwa mujibu wa mtandao wa Africa Facts Zone, wameeleza Zuchu alikataa dili hilo kutokana na Dini yake, lakini pia ushauri aliyopewa na mama yake mzazi, Khadija Kopa. “Tanzanian Singer, Zuchu rejected a $108,000 endorsement deal offer from an alcoholic brand to preserve her Islamic faith. Her mother, Tanzanian Music Legend, Khadija Kopa warned her against promoting such products earlier” mtandao huo umeeleza. Utakumbuka hadi kufikia Julai mwaka 2021 Meneja wa WCB Wasafi, Sallam SK alieleza kuwa Zuchu anachukua zaidi ya milioni 3 za Kenya kwa ajili ya kufanya kazi ubalozi. Zuchu alitangazwa kuwa chini ya lebo hiyo Aprili mwaka 2020 akiwa ni msanii wa pili ya kike baada ya Queen Darleen.

Read More
 ZUCHU ATAMBA KUWA MSANII WA KIKE ANAYELIPWA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI

ZUCHU ATAMBA KUWA MSANII WA KIKE ANAYELIPWA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI

Mwanamuziki nyota kutoka lebo ya WCB Zuchu ametamba kuwa ndiye msanii wa Kike ambaye alipwa zaidi Afrika Mashariki. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu ameandika tambo hizo huku Twitter akithibitisha kwamba ametoka kufunga dili kubwa zaidi siku ya jana. “I am forever grateful for my fans, Y’all just made me the most paid female artist in East Africa, love ya’ll” .”Just closed one of the biggest deals today, alhamdulillah”. – ametweet Zuchu. Hitmaker huyo wa ‘Sukari’, amedokeza pia ujio wa album yake mpya mwaka huu huku akiwataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuipokea album hiyo. “Promising you an album this Year, you deserved it get ready.” Ikumbukwe Zuchu kwa sasa anafanya vizuri kupitia wimbo uitwao ‘Mtasubiri’ alioshirikishwa na bosi wake diamond platnumz, wimbo unaopatikana kwenye Extended Playlist (EP) mpya ya Diamond iitwayo FOA

Read More
 ZUCHU AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA BOSI WAKE DIAMOND PLATINUMZ

ZUCHU AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA BOSI WAKE DIAMOND PLATINUMZ

Msanii wa Bongofleva Zuchu amekanusha fununu za kuwa amevalishwa pete ya uchumba na Familia ya Diamond Platnumz imepeleka barua ya uchumba kwenye familia yake. Akipiga na Wasafi FM  Zuchu pia Amekanusha madai ya kuishi nyumba moja na Boss wake Diamond Platnumz kwa kusema kuwa kila mtu anaishi nyumbani kwake. Sanjari na hilo amethibitisha kuwa yupo kwenye mahusiano na mwanaume ambaye hajamtaja jina lakini amemtaja kwa mwonekano kwa kusema kwamba ni mrefu ,ana rangi ya maji ya kunde,ni mfanya mazoezi,na mfanyabiashara. Sifa ambazo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamejaribu kuziunganisha na mwonekano wa Diamond Platnumz ambaye  amekuwa akifanya sana mazoezi siku za hivi karibuni.

Read More
 BI KHADIJA KOPA AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMUANDIKIA MWANAE ZUCHU UJUMBE MZITO

BI KHADIJA KOPA AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMUANDIKIA MWANAE ZUCHU UJUMBE MZITO

Mkongwe wa muziki wa Taarab nchini Tanzania Bi Khadija Kopa ambaye ni mama mzazi wa msanii kutoka WCB Zuchu Ameweka ujumbe ambao umewaacha watu wengi na maswali mengi katika mitandao yake ya kijamii. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Khadija Kopa amendika Ujumbe wa kumtakia kheri mwanae Zuchu katika maisha yake mapya ambayo yataanza siku ya Valentine  Februari 14 ambapo amesema kila mwanamke ana ndoto ya kuishi maisha hayo. “Zuhura mwanangu Nimekulea kwenye maadili na Najua wewe ni binti mwenye maamuzi sahihi na mimi kama Mama yako niseme sina budi kukusapoti .Tarehe 14 inaenda kua siku yako kubwa hakuna mwanamke asie na ndoto hii.M/Mungu akakusimamie najua hutoniangusha .siku hii isiwe tu siku yako kubwa duniani basi pia ikawe ndo mwanzo wa maisha mapya yenye Furaha .M/Mungu Akulinde kiziwanda changu Amin” ameandika Bi Khadija Kopa. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameibuka na kuhoji kuwa huenda siku hiyo zuchu akavishwa pete ya uchumba na bosi wake diamod platinumz ambaye katika siku za hivi karibuni amehusishwa kutoka kimapenzi na hitmaker huyo wa “Sukari. Wengine wameenda mbali Zaidi na kusema kuwa huenda Zuchu akaachia album au E yake mpya siku hiyo ya wapendanao duniani ila ni jambo la kusibiriwa.

Read More
 KHADIJA KOPA AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU ISHU YA DIAMOND KUTOKA KIMAPENZI NA ZUCHU

KHADIJA KOPA AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU ISHU YA DIAMOND KUTOKA KIMAPENZI NA ZUCHU

Moja kati ya headlines zinazo gonga vichwa vya habari mtandaoni ni issue inayomtaja mwanamuziki diamond platnumz kutaka kumuoa mwanamuziki mwenzake zuchu , sakata ambalo kila mtu analizungumzia katika namna yake. Sasa mama mzazi wa zuchu, Khadija Kopa amezungumzia kile kinachoitwa penzi jipya mtandaoni kati ya binti yake, Zuchu na Diamond Platnumz. Kwenye mahojiano Kopa  ambaye ni Malkia wa muziki wa Taarab nchini tanzania amepuuzilia mbali madai hayo na kusema aliwasiliana na bintiye na akamueleza hali halisi kuwa huo ni uvumi tu usio na msingi. Zuchu alimhakikishia mama yake kuwa Diamond amekuwa akimuonyesha heshima kubwa na hakuna chochote kinachoendelea kati yao. “Wakati ule Zuhura aliniambia Diamond anamheshimu sana na hajawahi hata siku moja kuniambia vitu vya kipuzi. Nilishtuka maanake watu walikuwa wanavumisha kupita kiasi” amesema na kuongeza; “Nilishangaa mbona walivumisha kupita kiasi, mimi mwenyewe sikushughulika sana, nilimuuliza Zuhura mbona watu walivumisha sana ama kuna kitu chochote. Aliniambia hamna wala hajawahi kuvunjiwa heshima hata siku moja, mimi nilichukulia kama kitu cha kawaida” alisema Khadija Kopa. Aliendelea kwa kusema; “Diamond mimi ananiona kama mama yake kusema ukweli, tangu zamani, kabla hata huyo Zuchu hajaenda Wasafi, amenichukulia kama mama yake”.

Read More
 ERIC OMONDI AMJIBU ZUCHU BAADA YA KUPINGA KAULI YAKE KUWA MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

ERIC OMONDI AMJIBU ZUCHU BAADA YA KUPINGA KAULI YAKE KUWA MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

Mchekeshaji Erick Omondi amejitokeza na kutetea kauli yake kwamba muziki wa Bongofleva umekufa kufuatia baadhi ya wasanii wake kufanya Amapiano. Kupitia mtandao wake wa Instagram, Omondi amemjibu Zuchu ambaye hakukubaliana na kauli hiyo akidai kwamba wanamuziki wa Tanzania wameamua kukumbatia muziki wa Amapiano ambao utawasaidia kujulikana zaidi. “Bongofleva haiwezi kufa, wasanii wanatoka nje ya eneo lao, kutafuta utofauti wa kujaribu sauti mpya. haijawahi shuhudiwa ikiuua tasnia yoyote, tasnia ya muziki ni kubwa sana, acha msanii ajaribu mambo yake. Hayo ni mabadiliko” alisema Zuchu. Kufuatia kauli hio Eric Omondi amejitokeza na kutetea kauli yake huku akimjibu Zuchu na kumweleza kwamba wanamuziki wa Kenya walianza hivyo na muziki wao ukapotea “Dada yangu mpendwa, hivi ndivyo inavyoanza, huwa tunaanza kwa kupoteza uhalisia na utambulisho wetu na kutoa visingizio vyake. Huku Kenya tulianza vivyo hivyo na Muziki wetu ukapotea” “Bongofleva iko SAWAA kabisa na hakuna haja ya kuwaacha Bongo Fleva ati kwa ajili ya ‘diversify’ Amapiano ni Basi tu linapita ila sisi tundapanda bila kujua linaenda wapi, tutashindwa kurudi nyumbani.tutakuwa tunauza sera zao na kushindwa kurundi nyumbani. tutakuwa tunauza tamaduni zao na kuua zetu za nyumbani” Mchekeshaji Omondi alinakiri” “Unapoimba ‘Sukari’ kwa sauti hiyo tamu ya kweli ya bongo na mdundo . unachofanya kimsingi ni kuinua na taifa na Bendera ya Tanzania”alisema Eric Omondi.

Read More
 SUKARI YA ZUCHU, NDIO WIMBO ULIOTAZAMWA ZAIDI KENYA KWA MWAKA 2021

SUKARI YA ZUCHU, NDIO WIMBO ULIOTAZAMWA ZAIDI KENYA KWA MWAKA 2021

Wimbo wa Sukari kutoka kwa mwanamuziki Zuchu umeshika nafasi ya kwanza katika orodha ya nyimbo 10 zilizo tazamwa zaidi nchini Kenya katika mtandao wa youtube. Wimbo huo uliopandishwa katika mtandao wa YouTube Januari 10, mwaka huu pia unashikilia rekodi ya kuwa miongoni mwa nyimbo zilizo tazamwa zaidi Barani Afrika kwa mwaka 2021, ukiwa na zaidi ya watazamaji million 61 katika mtandao wa Youtube. Mbali na Zuchu pia wimbo wa Baikoko wa Mbosso na Diamond Platnumz umeshika nafasi ya pili, ambapo ni wasanii wa 3 tu kutoka Tanzania akiwemo muimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando waliotokea katika orodha hiyo ya nyimbo 10 zilizo tazamwa zaidi nchini Kenya kwa mwaka 2021.

Read More