App ya TikTok imefanya mabadiliko mapya katika mwonekano wa sehemu ya Profile za watumiaji wake.
Katika maboresho hayo mapya, TikTok imehamisha taarifa muhimu kama picha ya profile, Bio pamoja na Links na kuziweka upande wa kushoto wa ukurasa wa profile. Mabadiliko haya yamezua mjadala mkubwa, huku watumiaji wengi wakisema muonekano huo unafanana kwa kiasi kikubwa na design ya Instagram.
Aidha, TikTok pia imebadilisha muonekano wa buttons zilizopo kwenye profile. Sasa zimekuwa na kona za mviringo, tofauti na awali ambapo zilikuwa na umbo la boksi.
Mabadiliko haya ni sehemu ya jitihada za TikTok kuboresha uzoefu wa watumiaji na kuendana na mitindo ya kisasa ya teknolojia. Hata hivyo, maoni ya watumiaji bado yanatofautiana kuhusu kama maboresho haya ni bora au la.