Entertainment

Upendo wa Nandy kwa Billnass Wagusa Mioyo ya Mashabiki Mitandaoni

Upendo wa Nandy kwa Billnass Wagusa Mioyo ya Mashabiki Mitandaoni

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Nandy, ameonesha kwa mara nyingine ukubwa wa mapenzi yake kwa mume wake ambaye pia ni rapa, Billnass, kwa kauli ya kugusa hisia iliyoacha wengi wakitafakari juu ya upendo wa dhati.

Kupitia mahojiano ya hivi karibuni, Nandy alieleza kuwa mapenzi yake kwa Billnass ni ya kipekee kiasi kwamba hawezi hata kufikiria kuendelea kuishi endapo angebaki peke yake.

“Nampenda sana Billnass. Ikiwa kuna siku kifo kitatutenganisha, basi ni heri iwe mimi nitaondoka kwanza. Siwezi kuimagine maisha yangu bila yeye,” alisema kwa hisia.

Kauli hiyo imezua hisia mseto mtandaoni, wengi wakiguswa na upendo wao wa dhati, huku wengine wakisifia jinsi wawili hao wanavyoendeleza ndoa yao kwa upendo na heshima, licha ya changamoto za maisha ya mastaa.

Nandy na Billnass, ambao walifunga ndoa yao rasmi mwaka 2022, wamekuwa mfano wa kuigwa katika jamii, wakionesha mshikamano si tu kwenye maisha ya ndoa bali pia katika kazi zao za muziki. Mara kwa mara wamekuwa wakishirikiana kwenye miradi ya pamoja na kuonesha hadharani mapenzi yao, hali ambayo imewavutia na kuwapa matumaini mashabiki wao.

Wakati ambapo ndoa nyingi za mastaa hukumbwa na drama na migogoro, wawili hawa wameendelea kuwa mfano wa kuigwa, huku wakitoa msukumo kwa wengine kuamini katika mapenzi ya kweli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *