Entertainment

Zuchu Amkingia Kifua Diamond Kufuatia Madai ya Kuvuliwa Ubalozi wa Pepsi

Zuchu Amkingia Kifua Diamond Kufuatia Madai ya Kuvuliwa Ubalozi wa Pepsi

Mwanamuziki wa Bongofleva Zuchu ameibuka na kukanusha vikali madai yaliyoenea mtandaoni kwamba mume wake Diamond Platnumz amevuliwa wadhifa wake wa ubalozi wa Pepsi kutokana na kuhusishwa na siasa za CCM.

Katika ufafanuzi wake, Zuchu ameeleza kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote, akisema zimetengenezwa na watu wanaotaka kupotosha umma lakini pia kutafuta kiki mtandaoni.

Hitmaker huyo wa Amanda, ameeleza kuwa Diamond anaendelea kutekeleza majukumu yake kama balozi wa Pepsi bila changamoto yoyote, na mahusiano kati ya WCB na kampuni hiyo bado ni thabiti.

Kauli yake imekuja wakati tetesi hizo zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya mashabiki wakionesha wasiwasi kuhusu mustakabali wa ushirikiano huo. Ufafanuzi huo umeondoa sintofahamu na kuthibitisha kuwa mahusiano kati ya Diamond na Pepsi yanaendelea kuwa thabiti kama ilivyokuwa awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *