Sports news

Kenya Yatuma Waogeleaji 8 kwa Michezo ya Deaflympics Japan

Kenya Yatuma Waogeleaji 8 kwa Michezo ya Deaflympics Japan

Timu ya taifa ya uogeleaji ya Deaflympics imeboresha mazoezi yake ikijiandaa kushiriki katika makala ya mwaka huu ya michezo ya Deaflimpiki itakayoandaliwa jijini Tokyo Japan baina ya tarehe 15 na 26 mwezi ujao.

Timu hiyo itaongozwa na nahodha Francis Gichuhi ambaye ataongoza kikosi cha waogeleaji wanane wakiwemo Lilian Njeri, Faith Wayua, Jimale Suheib, Salim Mbaraka, Hamadi Ali Juma, Hassan Hamisi, na Yusuf Saddam.

Gichuhi alileleza furaha yake kwa kuchaguliwa kuwakilisha Kenya na kuongeza kusema kuwa ni heshima kuwa kuhudumu kama nahodha wa timu hiyo, jukumu ambalo amekuwa akitamani tangu alipokuwa shuleni mwaka 2019.

Gichuhi atashiriki katika shindano la kuogelea mita 50 na mia moja breaststroke. Waogeleaji wote wanane walifuzu kujiunga na timu hiyo wakati wa mashindano ya majaribio ya kitaifa yaliyoandaliwa tarehe 26 mwezi Agosti katika chuo kikuu cha USIU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *