Entertainment

Eddy Kenzo Awasihi Wasanii Uganda Kupigania Marekebisho ya Sheria ya Hakimiliki

Eddy Kenzo Awasihi Wasanii Uganda Kupigania Marekebisho ya Sheria ya Hakimiliki

Staa wa muziki kutoka Uganda Eddy Kenzo amewahimiza wasanii wenzake kuweka tofauti za kisiasa kando na kushirikiana kupigania marekebisho ya sheria ya hakimiliki nchini humo.

Kenzo, amesema ni muhimu kwa wasanii kuungana ili kuhakikisha sekta ya ubunifu inanufaika kupitia sheria bora zitakazowalinda na kuwahakikishia kipato kutokana na kazi zao.

Msanii huyo anaamini kuwa marekebisho ya sheria hiyo yataboresha kwa kiasi kikubwa sekta ya ubunifu kwa kuhakikisha wasanii wanapata malipo stahiki kutokana na kazi zao.

Kwa mujibu wa Kenzo, muswada wa marekebisho ya sheria ya hakimiliki tayari umewasilishwa katika bunge la kitaifa la Uganda na unaweza kuwasilishwa rasmi kwa mjadala wakati wowote.

Kauli yake inakuja miezi michache baada ya msanii huyo kushiriki kikamilifu katika kampeni za chama tawala cha (NRM). Hata hivyo, sasa anasema wakati umefika kwa wasanii kuangazia masuala ya tasnia badala ya siasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *