Msanii nyota kutoka Uganda Spice Diana amewahimiza wanawake kufanya kazi kwa bidii na kujitegemea kifedha badala ya kutegemea wanaume ili kuendesha maisha yao.
Msanii huyo ambaye amedumu kwenye tasnia ya muziki kwa karibu miaka kumi na tano amesema kuwa wanawake wana nafasi kubwa ya kujenga maisha yao na kuchangia maendeleo ya jamii ikiwa watachagua kujituma na kutumia fursa zilizopo.
Akizungumza kuhusu umuhimu wa kujitegemea, Spice Diana amewashauri wanawake kuacha tabia ya kutegemea wanaume na badala yake wajitahidi kujenga mafanikio yao wenyewe.
Msanii huyo ameongeza kuwa wanawake wataendelea kukumbana na changamoto na kudharauliwa iwapo hawatachukua hatua za kudhibiti maisha yao na kutumia fursa zilizopo katika kizazi cha sasa.