Gossip

Video ya Bahati Akifunzwa Kuvuta Cigar Yazua Gumzo Mtandaoni

Video ya Bahati Akifunzwa Kuvuta Cigar Yazua Gumzo Mtandaoni

Video inayomuonyesha msanii wa muziki kutoka Kenya, Bahati, akifunzwa namna ya kuvuta cigar imezua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusambaa mtandaoni.

Katika video hiyo ya nyuma ya pazia (behind the scenes) ya utayarishaji wa diss track yake inayojulikana kama β€œLost for the Throne,” Bahati anaonekana akielekezwa jinsi ya kushika na kuvuta cigar wakati wakijiandaa kurekodi baadhi ya vipande vya video ya wimbo huo.

Hatua hiyo imeibua mjadala miongoni mwa mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii, hasa kutokana na taswira ambayo Bahati amekuwa akiijenga kwa muda mrefu kama msanii mwenye maadili ya Kikristo. Wapo wanaodai kuwa tukio hilo linaenda kinyume na sura ambayo msanii huyo amekuwa akiionyesha kwa mashabiki wake.

Hata hivyo, wengine wamejitokeza kumtetea wakisema kuwa ilikuwa ni sehemu tu ya uigizaji na ubunifu wa kisanii kwa ajili ya video ya wimbo huo, hivyo haipaswi kuchukuliwa kama tabia yake ya kawaida nje ya kazi ya muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *