Entertainment

Ushahidi wa Kid Cudi Dhidi ya Diddy Wamvunja Moyo Kanye West

Ushahidi wa Kid Cudi Dhidi ya Diddy Wamvunja Moyo Kanye West

Rapa maarufu mwenye utata, Kanye West, ametoa hisia zake kuhusu hali inayoendelea kumkumba Sean Diddy Combs, akieleza masikitiko yake juu ya hatua ya Kid Cudi kutoa ushahidi dhidi ya Diddy.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Ye ameonekana kuzungumzia kile anachokiona kama mfumo wa haki unaowakandamiza watu weusi, akisisitiza haja ya jamii ya wasanii na Wamarekani Weusi kwa ujumla kujilinda na kushikamana badala ya kushirikiana na mifumo anayoamini kuwa ya kibaguzi.

“I wish Cudi hadn’t testified against Puff. We need to not be locked in white systems. Praying for Puff and his family. Praying for Puff Daddy and the Family.”Aliandika X

Kauli hiyo imeibua hisia mseto kutoka kwa mashabiki na wanamuziki wenzake, huku baadhi wakimtetea kwa msimamo wake wa kutaka mshikamano miongoni mwa wasanii wa asili ya Kiafrika, na wengine wakimkosoa kwa kudharau mchakato wa haki.

Kid Cudi, ambaye zamani alikuwa rafiki wa karibu wa Ye, anatajwa kuwa miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi dhidi ya Diddy kufuatia madai mazito yanayomkabili kuhusu vitendo vya unyanyasaji na ukiukaji wa haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *