Entertainment

Diamond Aonyesha Heshima kwa Jose Chameleone, Ataka Ushirikiano wa Mwaka

Diamond Aonyesha Heshima kwa Jose Chameleone, Ataka Ushirikiano wa Mwaka

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ametangaza nia yake ya dhati ya kushirikiana na msanii mkongwe wa Uganda, Jose Chameleone, katika wimbo mpya unaotarajiwa kutoka mwaka huu. Akiwa jukwaani katika tamasha la Coffee Marathon huko Ntungamo, Uganda, Diamond aliwajulisha mashabiki kuwa kolabo hiyo ni ndoto aliyokuwa nayo kwa muda mrefu, na sasa anafanya kila juhudi kuhakikisha inatimia.

Diamond alisema kuwa licha ya mafanikio yake makubwa katika bara la Afrika, hajawahi kusahau mchango wa Jose Chameleone katika muziki wa Afrika Mashariki. Alimuelezea kama msanii aliyeathiri kizazi kizima na kumvutia hata yeye kuingia kwenye tasnia ya muziki.

“Mwaka huu nataka kuhakikisha ninafanya wimbo na Jose Chameleone. Tunamshukuru Mungu kuwa anaendelea vizuri kiafya na tunamshukuru kwa mchango wake mkubwa kwenye muziki,” alisema Diamond mbele ya mashabiki.

Kwa upande wake, Jose Chameleone, ambaye ametamba kwa zaidi ya miaka 20 na kubaki kuwa moja ya nguzo za muziki wa Afrika Mashariki, bado anaheshimika kwa nyimbo zake zenye ujumbe mzito na sauti ya kipekee. Kolabo kati ya Chameleone na Diamond inatarajiwa kuwa ya kihistoria, na tayari mashabiki kote kanda ya Afrika Mashariki wanasubiri kwa hamu kusikia kazi yao ya pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *