LifeStyle

Wapendwa Muziki Watangaza Kuzaliwa kwa Mtoto Wao wa Kiume

Wapendwa Muziki Watangaza Kuzaliwa kwa Mtoto Wao wa Kiume

Wasanii wanaounda kundi la Wapenda Muziki, Nina na Mesh, wametangaza kwa furaha kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza wa kiume.

Kupitia mitandao ya kijamii, wawili hao walishiriki taarifa hiyo njema wakieleza kushukuru Mungu kwa zawadi ya mtoto, hatua iliyopokelewa kwa shangwe na mashabiki wao mitandaoni.

Nina na Mesh wamekuwa wakifuatiliwa kwa karibu kutokana na muziki wao na maisha yao ya kifamilia, na ujio wa mtoto wao wa kwanza umeongeza furaha kwa wafuasi wao.

Kwa sasa, wasanii hao wa ngoma ya Amefanya Mungu, wameomba faragha ili kufurahia kipindi hiki muhimu cha maisha yao, huku wakiahidi kurejea kwa nguvu katika shughuli zao za muziki baada ya mipango yao ya kifamilia kukaa sawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *