Msanii wa muziki kutoka Kenya, Akothee, ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina “Tatu Bora”, kazi ambayo imeimbwa kwa lugha ya Dholuo.
Tatu Bora EP ina jumla ya ngoma tatu kali, ambazo zote amezifanya bila kolabo na msanii yeyote, ikiwa ni hatua inayoonyesha ubunifu na ubora wake binafsi. Nyimbo zilizopo ndani ya EP hiyo ni Bi Mos, Tururu, na Koyo, na zinapatikana exclusive katika majukwaa yote ya kusikiliza na kupakua muziki mtandaoni.
Kupitia ujumbe wake kwa mashabiki, Akothee ameeleza kuwa ameachia kazi hii kama zawadi kwa wafuasi wake na kama msukumo kwa wanawake, akisisitiza kuwa katika ulimwengu wa ndoa na changamoto zake, muziki unaweza kuwa tiba na faraja.
“Tatu Za Bora EP” ni kazi ya kwanza kutoka kwa Akothee tangu atoke hospitalini ambako alikuwa amelazwa kutokana na matatizo ya tumbo.