Khaligraph Ajibu kwa Utani Madai ya Kuigiza Maisha na Muziki

Khaligraph Ajibu kwa Utani Madai ya Kuigiza Maisha na Muziki

Msanii nyota wa hip hop nchini Kenya, Khaligraph Jones, ameonekana kuguswa na kauli za mtangazaji Rapcha the Sayantist, aliyemshutumu vikali kwa kudai kuwa muziki wake na maisha yake yote ni ya kuigiza. Katika kujibu lawama hizo, Khaligraph ametumia ukurasa wake wa Instagram kwa mtindo wa utani, akionekana kugeuza matusi hayo kuwa fursa ya kumsaidia Rapcha kupata umaarufu zaidi. Amesisitiza kuwa kutajwa kwake ni njia rahisi ya kupata kiki, na akaenda mbali kwa kuwahimiza mashabiki wake wamfuate Rapcha mitandaoni. Pia ametoa dondoo kwamba anajiandaa kuachia freestyle mpya, hatua ambayo mashabiki wameihusisha na majibu ya muziki kwa ukosoaji aliopewa. Mashabiki mitandaoni wamegawanyika, baadhi wakiona kuwa Khaligraph ameonyesha busara kwa kutochukua mambo kwa hasira, huku wengine wakimtuhumu Rapcha kwa kutumia lugha ya matusi na kushusha heshima ya moja ya wasanii wakubwa zaidi wa hip hop Afrika Mashariki. Hayo yote yameibuka mara baada ya Rapcha kwenye moja ya Podcast kudai kuwa kila kitu kuhusu Khaligraph ni cha kubuni kuanzia lafudhi yake, madai ya kutoka Kayole, mtindo wa mavazi hadi muziki anaoutoa.

Read More
 Duru ya Mwisho ya Raga 7s Kuwaka Moto Kisumu Wiki Hii

Duru ya Mwisho ya Raga 7s Kuwaka Moto Kisumu Wiki Hii

Msururu wa kitaifa wa raga ya wachezaji saba kila upande unatarajiwa kuelekea jijini Kisumu mwishoni mwa juma hili kwa raundi ya Dala, huku timu za KCB Rugby na Strathmore Leos zikitajwa kuwa miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kutawazwa mabingwa wa msimu huu. Mashindano haya yamepata msukumo mkubwa baada ya kupokea udhamini wa shilingi milioni 3 kutoka kwa kampuni ya Kenya Breweries, hatua inayolenga kuongeza morali na ubora wa mashindano katika hatua hii ya mwisho. Kwa sasa, KCB inaongoza jedwali kwa alama 104 baada ya kushiriki duru tano. Ili kujihakikishia taji la ubingwa, timu hiyo inahitaji tu kufuzu hadi robo fainali ya duru ya Kisumu. Upinzani mkali unatarajiwa kutoka kwa wapinzani wa kawaida kama Strathmore Leos na Menengai Oilers. Kundi A linajumwisha Kabras Sugar, CUEA Monks, MMUST na Nakuru RFC huku kundi B likijumwisha Daystar Falcons, MSC Rugby, Kenya Harlequin na Nondescripts. KCB Rugby, Mwamba RFC, Homeboyz RFC na Embu RFC wamo kundini C huku kundi D likihusisha Strathmore Leos, Menengai Oilers, Impala RFC na Kisumu RFC.

Read More
 Apple Yazindua iPhone 17, iPhone 17 Pro na iPhone Air

Apple Yazindua iPhone 17, iPhone 17 Pro na iPhone Air

Kampuni ya Apple imezindua rasmi simu mpya ya iPhone 17, ambayo japokuwa muonekano wake unafanana na iPhone 16, imeboreshwa kwa kiwango kikubwa upande wa teknolojia. Sasa inakuja na skrini ya ProMotion inayowezesha refresh rate hadi 120Hz, badala ya 60Hz ya toleo lililopita. Pia, ina kamera kuu ya 48MP, kioo cha Ceramic Shield 2 kilichoimara zaidi dhidi ya michubuko na ajali, pamoja na teknolojia mpya ya kuchaji haraka. Kwa upande mwingine, Apple imezindua pia iPhone 17 Pro, ikiwa na mabadiliko makubwa zaidi. Toleo hili linatumia heat-forged aluminium badala ya titanium, na muundo wa kamera ya nyuma umeboreshwa. Kamera zote ni 48MP, ina zoom ya hadi 8x, na sasa inakuja na lens mpya ya 200mm, ikiwa ni moja ya simu zenye uwezo mkubwa zaidi wa upigaji picha na video kwa sasa. Uzinduzi huu pia umeleta mshangao kwa wengi baada ya Apple kutambulisha iPhone Air, simu mpya kabisa isiyo na jina la namba tofauti na utaratibu wa kawaida. iPhone Air ni iPhone nyembamba zaidi kuwahi kutengenezwa, lakini yenye uwezo wa kifaa cha kiwango cha juu kama iPhone 17 Pro. Inakuja na kamera ya 48MP, lensi za 26mm hadi 52mm, selfie kamera ya 24MP, uwezo wa kurekodi 4K kwa 60fps, na inatumia chip ya iPhone Pro. Kutokana na muundo wake wa kisasa, classic na wa kuvutia, iPhone Air tayari imeanza kushika kasi mtandaoni, huku watumiaji wengi wakionesha kuvutiwa na muonekano wake wa kipekee pamoja na uwezo wa hali ya juu, licha ya mwonekano wake mwembamba. Apple inaendelea kuonesha kwamba teknolojia ya simu janja bado ina nafasi kubwa ya ubunifu.

Read More
 Threads Yazindua Kipengele Kipya cha Maandishi Marefu Hadi Herufi 10,000

Threads Yazindua Kipengele Kipya cha Maandishi Marefu Hadi Herufi 10,000

Mtandao wa kijamii wa Threads, unaomilikiwa na kampuni ya Meta, umetangaza rasmi uzinduzi wa kipengele kipya kinachowaruhusu watumiaji wake kuandika maandishi marefu zaidi hadi herufi 10,000 katika chapisho moja. Hatua hii inakuja kama sehemu ya juhudi za Threads kujiimarisha kama jukwaa la maudhui ya kina na mijadala ya kimaudhui, tofauti na mitandao mingine inayoweka mipaka ya urefu wa maandishi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Meta, kipengele hiki kipya kitawawezesha watumiaji, wakiwemo wanahabari, wanablogu, waandishi wa habari za kisiasa, na wanaharakati wa kijamii, kuchapisha maudhui ya kina bila kulazimika kuyagawanya katika post nyingi au kutegemea viungo vya nje. Hatua hii pia inaashiria ushindani wa moja kwa moja na majukwaa kama X (zamani Twitter), ambalo liliongeza ukomo wa herufi kwa baadhi ya watumiaji wake wa kulipia, pamoja na Substack Notes na LinkedIn, ambayo inawaruhusu watumiaji kuandika maudhui ya kitaaluma. Uzinduzi huu unafanyika wakati Threads ikiendelea kushika kasi kama jukwaa jipya linalowavutia mamilioni ya watumiaji waliokuwa wakitafuta mbadala wa Twitter, kufuatia mabadiliko ya sera na mmiliki wake Elon Musk. Kwa sasa, kipengele hiki kinapatikana kwa watumiaji wote wa Threads waliopo katika toleo jipya la programu hiyo, kwenye Android na iOS, huku wakihimizwa kuendelea kutoa mrejesho kuhusu matumizi yake.

Read More
 Mbosso Ajeruhiwa Akiwa Location ya Video Shoot

Mbosso Ajeruhiwa Akiwa Location ya Video Shoot

Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Mbwana Yusuf Kilungi maarufu Mbosso, ameripotiwa kupata jeraha kwenye mguu wake wa kulia wakati wa shughuli za utayarishaji wa kazi yake mpya ya muziki. Tukio hilo lilitokea akiwa location akirekodi video, ambapo inadaiwa alidondoka ghafla baharini katika harakati za kuhakikisha mashabiki wake wanapata burudani ya kiwango cha juu. Ingawa haijafahamika ukubwa wa jeraha hilo, watu wa karibu na msanii huyo wamesema kuwa hali yake si ya kutia wasiwasi na anaendelea kupata matibabu. Mashabiki wake wameonyesha wasiwasi kupitia mitandao ya kijamii, huku wengi wakimtumia jumbe za kumtakia afueni ya haraka. Mbosso, anayejulikana kwa sauti yake ya kipekee na vibao kama Hodari na Fall, amekuwa akijiandaa na miradi mipya ya muziki, na tukio hili limekuja wakati mashabiki wakingoja kwa hamu kazi yake mpya.

Read More
 Kocha wa Gor Mahia Atangaza Kujiamini Kabla ya Mechi na Simba SC

Kocha wa Gor Mahia Atangaza Kujiamini Kabla ya Mechi na Simba SC

Kocha Mkuu wa Gor Mahia, Charles Akonnor ameelezea imani na kikosi chake huku vigogo hao wa soka humu nchini wakitarajiwa kuchuana na wababe wa Tanzania, Simba SC katika mechi ya kirafiki ya kujiandaa kwa msimu mpya kesho Septemba 10 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Mechi hiyo inatarajiwa kuvutia maelfu ya mashabiki kutoka mataifa yote mawili ni ya kunoa tomi hizo kabla ya kung’oa nanga Kwa michuano ya ligi za nyumbani. Gor Mahia, ambao ni wabambe wa Ligi Kuu ya Kenya waliwasili Tanzania mapema wiki hii na wamekuwa wakiimarisha mazoezi yao. Kocha mkuu Charles Akonnor, ambaye alichukua hatamu mapema mwaka huu anasema kikosi chake kiko tayari kushamiri. Michuano ya ligi msimu huu itang’oa nanga tarehe 20 mwezi huu.

Read More
 Vera Sidika Ajibu Ukosoaji Kuhusu Kumruhusu Brown Mauzo Kuwaona Watoto Wao

Vera Sidika Ajibu Ukosoaji Kuhusu Kumruhusu Brown Mauzo Kuwaona Watoto Wao

Mrembo maarufu kutoka Kenya, Vera Sidika, ameweka wazi msimamo wake baada ya kukosolewa kwa uamuzi wake wa kumruhusu aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki Brown Mauzo, kutumia muda na watoto wao nyumbani kwake. Kupitia Inst story yake, Vera amesema hajawahi kumtegemea Mauzo kwa msaada wa kifedha na kwamba jambo analolipa kipaumbele ni uwepo wake kama baba katika maisha ya watoto wao. Amebainisha kuwa yeye mwenyewe alikulia kwenye familia yenye wazazi wote wawili, jambo lililomfanya atamani watoto wake wapate malezi yenye upendo na uwepo wa baba, bila kujali changamoto za kifedha. Akizungumzia dhamira ya Mauzo kama mzazi, Vera amesema amewahi kushuhudia jinsi alivyovunjika moyo baada ya kuzuiwa kumuona mtoto wake na mama wa mtoto wake kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita. Kwa mujibu wake, hali hiyo ilionyesha wazi jinsi anavyothamini nafasi yake kama baba na hamu yake ya kuwa karibu na watoto wake. Aidha, Vera amekosoa vikali tabia ya baadhi ya akina mama kuwazuia baba kuona watoto wao kwa sababu ya changamoto za kifedha. Alisema kufanya hivyo ni kitendo cha ubinafsi kwa kuwa kinawanyima watoto nafasi ya kupokea upendo na malezi ya baba zao. Kauli ya Vera imezua mjadala mitandaoni, baadhi ya watu wakimsifu kwa ukomavu na mtazamo wake chanya kuhusu malezi ya pamoja, huku wengine wakisisitiza kuwa majukumu ya kifedha nayo ni sehemu muhimu ya malezi ya mzazi.

Read More
 Kelvin Kinuthia Atangaza Mpango wa Kufanyiwa Upasuaji wa Uterus Transplant

Kelvin Kinuthia Atangaza Mpango wa Kufanyiwa Upasuaji wa Uterus Transplant

Mshawishi wa mitandaoni kutoka Kenya, Kelvin Kinuthia, amewashangaza mashabiki wake baada ya kutangaza kuwa ana mpango wa kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza mfuko wa uzazi (Uterus Transplant – UTX). Hii ni aina ya upasuaji wa kibingwa ambapo mfuko wa uzazi kutoka kwa mtoaji (donor) hupandikizwa kwa mpokeaji ili kumpa uwezo wa kubeba mimba Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kwamba maisha yake ni ya faragha na hakuna aliyekuwa akifahamu mipango yake ya kufanyiwa upasuaji huo. Amesema amekuwa akipitia maandalizi ya kimatibabu kwa muda mrefu na amejiandaa kisaikolojia kwa safari hiyo. Pia amefafanua kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo kwa sababu anaamini kila mtu ana haki ya kuwa na familia na kupata mtoto, na ana matumaini makubwa kuwa teknolojia ya kisasa ya tiba itamwezesha kutimiza ndoto hiyo. Kwa mujibu wa Kinuthia, uamuzi wake wa kuzungumzia suala hilo hadharani unatokana na dhamira ya kuwapa ujasiri watu wengine wanaopitia changamoto za kiafya au wale wanaotamani kupata watoto kwa njia zisizo za kawaida. Uterus transplant ni miongoni mwa upasuaji wa hali ya juu unaofanyika mara chache duniani na umewezesha wanawake waliokuwa hawana uwezo wa kubeba ujauzito kupata nafasi ya kujifungua watoto wao wenyewe. Hata hivyo, upasuaji huu unahitaji maandalizi ya kina, usimamizi wa madaktari bingwa, na dawa maalum za kuzuia mwili kukataa kiungo kilichopandikizwa.

Read More
 Nyota Ndogo Amsikitikia Mrembo Aliyedai Hataki Kuolewa Wala Kuzaa

Nyota Ndogo Amsikitikia Mrembo Aliyedai Hataki Kuolewa Wala Kuzaa

Mwanamuziki kutoka Kenya, Nyota Ndogo, ameonyesha masikitiko yake kufuatia kauli ya mrembo wa mtandaoni kwa jina la Lydia Wanjiru, aliyesema hadharani kuwa hataki kuolewa wala kuzaa, akidai ndoa ni mzigo na watoto ni kero maishani. Kupitia ujumbe alioweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nyota Ndogo amesema kuwa kila mtu ana haki ya kuamua namna anavyotaka kuishi, lakini akaonya kuwa mitazamo ya aina hiyo inapochapishwa hadharani inaweza kuwa na athari kwa vijana na wafuasi wanaochukulia kauli hizo kama mwongozo wa maisha. Msanii huyo amesisitiza kuwa watoto ni baraka ya kipekee inayomletea mzazi furaha na msaada mkubwa maishani. Ameongeza kuwa mara nyingi watoto huwa nguzo muhimu hasa katika uzee, kipindi ambacho marafiki na watu wengine huanza kujitenga. Hata hivyo, Nyota Ndogo amemwonya Lydia kwamba anaweza kujutia uamuzi wake huo baada ya miaka mingi, akisisitiza kuwa jamii bado inathamini familia na nafasi ya mzazi ni ya kipekee isiyoweza kuchukuliwa na mtu mwingine. Kauli ya Nyota Ndogo imezua mjadala mitandaoni, huku baadhi ya wafuasi wakimtetea kwa kusimamia maadili ya kifamilia, ilhali wengine wakisisitiza kuwa uhuru wa mtu binafsi unapaswa kuheshimiwa.

Read More
 Shorn Arwa Awapa Somo Wanawake Wanaopost Picha Baada ya Kuvunja Mahusiano

Shorn Arwa Awapa Somo Wanawake Wanaopost Picha Baada ya Kuvunja Mahusiano

Mshawishi wa mitandaoni kutoka Kenya, Shorn Arwa, ametoa somo kwa wanawake kuacha tabia ya kupakia picha nyingi mtandaoni pindi mahusiano yao ya kimapenzi yanapovunjika. Kupitia Insta Story yake, amesema wanawake wengi mara baada ya kuachwa huingia katika harakati za kuonesha maisha ya kifahari, kupendeza na kujiamini kupitia mitandao ya kijamii ili kuthibitisha kuwa bado wako imara. Hata hivyo, Arwa anaona tabia hiyo kama ushamba na jaribio la kutafuta uthibitisho kutoka kwa watu wengine badala ya kujijengea heshima na kuponya nafsi zao. Kwa mtazamo wake, badala ya kutumia mitandao ya kijamii kuthibitisha hali zao, wanawake wanapaswa kuelekeza nguvu katika kujitunza na kujijenga kifedha. Kulingana naye, kuporomoka kwa uhusiano si mwisho wa maisha, bali ni nafasi ya kujifunza na kukua.

Read More
 Eve Mungai Atishia Kutoa Ushahidi Baada ya Kudaiwa Kufilisika

Eve Mungai Atishia Kutoa Ushahidi Baada ya Kudaiwa Kufilisika

Youtuber maarufu nchini Kenya, Mungai Eve, ametoa onyo kali kwa mwanaume asiyejulikana anayedaiwa kuendelea kumtaja na kuingiza jina lake kwenye mabishano ya hadharani mtandaoni. Mungai Eve, kupitia mitandao yake ya kijamii, amesema wazi kuwa hatasita kuwasilisha ushahidi dhidi ya mtu yeyote atakayejaribu kumfanya aonekane duni au kumtuhumu bila sababu. Amesisitiza kuwa utulivu wake wa sasa haupaswi kuchukuliwa kama udhaifu, bali ni ishara ya uthabiti na busara ya kukabiliana na changamoto. Kauli hiyo imetajwa na mashabiki kuwa jibu kwa ex wake, Trevor, ambaye juzi kati alimtaka aombe radhi kwa Wakenya kutokana na matamshi yake kwamba hawezi kuanza uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ambaye kipato chake kiko chini ya shilingi laki tano za Kenya. Trevor alitoa kauli hiyo baada ya wafuasi kumshauri amsaidie Eve, ambaye amekuwa akikabili changamoto mbalimbali za kimaisha tangu kuvunjika kwa uhusiano wao.

Read More
 S2kizzy Ajiita Profesa wa Muziki, Awahimiza  Beatmakers Kujiamini Zaidi

S2kizzy Ajiita Profesa wa Muziki, Awahimiza Beatmakers Kujiamini Zaidi

Mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania, S2kizzy maarufu Zombie, ameweka wazi mtazamo wake kuhusu nafasi ya beatmaker katika tasnia ya muziki. Akipiga stori na The Throne, Zombie anasema hakuna haja mtu yeyote kujisikia vibaya akiitwa beatmaker kwa sababu hiyo ndiyo nguzo muhimu inayoshikilia mchakato mzima wa utayarishaji muziki. Kwa maelezo yake, kutengeneza beat ndiko kunakoipa ngoma uhai kabla ya hatua nyingine za uzalishaji kuingia. Hata hivyo, anasisitiza kuwa safari yake ya kimuziki imemfikisha mbali zaidi ya hatua hiyo, na sasa anajitazama kama profesa wa muziki kutokana na uwezo wake mpana unaojumuisha kuunda beat, kufanya production, kutoa mwongozo na kupanga mashairi. S2kizzy, ambaye amefanya kazi na wasanii wakubwa wa Afrika Mashariki na kimataifa akiwemo Diamond Platnumz, Rayvanny na Harmonize, amekuwa akihusishwa na mageuzi makubwa kwenye sauti ya Bongofleva na kuisukuma kuvuka mipaka ya kanda. Wachambuzi wa muziki wanasema matamshi yake yanaonyesha namna tasnia inavyoendelea kukua na kuhitaji wataalamu wenye ujuzi mpana zaidi ya kutengeneza beat pekee, kwani muziki wa kisasa unahitaji ubunifu, usimamizi wa kiufundi na mtazamo wa kimataifa.

Read More