Harambee Stars Wapoteza Mechi Tatu za Kufuzu Kombe la Dunia 2026

Harambee Stars Wapoteza Mechi Tatu za Kufuzu Kombe la Dunia 2026

Timu ya taifa ya soka, Harambee Stars, ilipoteza mechi yake ya tatu katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026, baada ya kufungwa mabao 3-1 na Gambia uwanjani Kasarani. Kipigo hicho ni pigo kubwa kwa Harambee Stars, ambayo sasa haijaweka wazi nafasi yake ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazoandaliwa mwaka ujao katika mataifa ya Marekani, Canada, na Mexico. Harambee Stars imeshinda mechi moja tu kati ya saba zilizochezwa hadi sasa katika awamu ya kufuzu, na inashikilia nafasi ya tano kwenye kundi F ikiwa na alama 6, alama 12 nyuma ya vinara wa kundi hilo, Gabon. Aidha, Stars sasa itacheza dhidi ya Ushelisheli katika mechi ijayo itakayofanyika tarehe 9 mwezi huu, kabla ya kumaliza mashindano haya kwa kucheza na Burundi na Kodivaa mwezi Oktoba mwaka huu. Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitaanza rasmi tarehe 11 Juni na kuhitimishwa tarehe 19 Julai.

Read More
 Bahati Awajibu Wakosoaji Kuhusu Kuonyesha Utajiri

Bahati Awajibu Wakosoaji Kuhusu Kuonyesha Utajiri

Msanii kutoka Kenya, Bahati, ameibuka na kuwatolea uvivu wakosoaji wanaomshutumu kwa tabia yake ya kuonyesha mali na maisha ya kifahari kupitia mitandao ya kijamii. Kwa mujibu wa msanii huyo, hakuna tatizo lolote katika kuonyesha mafanikio kwani ameyapata kupitia juhudi kubwa na bidii aliyoweka kwa muda mrefu. Anasisitiza kuwa kila mtu ana uhuru wa kuishi maisha anayoyataka na kwamba mafanikio yake ni kielelezo cha kazi ngumu, uvumilivu na imani. Bahati ameendelea kusisitiza kuwa ataendelea kufurahia maisha na kutumia jukwaa lake kuonyesha baraka alizopewa na Mungu, sambamba na mipango ya miradi mikubwa ya muziki na biashara anayotarajia kuzindua siku za usoni. Katika sikiu za hivi karibuni, Bahati amekuwa gumzo baada ya kushiriki picha na video akionekana na fedha taslimu, magari ya kifahari na maisha ya kifamilia yenye mvuto.

Read More
 Trevor: Mungai Eve Anapaswa Kuomba Radhi Kwa Mashabiki

Trevor: Mungai Eve Anapaswa Kuomba Radhi Kwa Mashabiki

Aliyekuwa mpenzi na mshirika wa karibu wa kibiashara wa Mungai Eve, Director Trevor, ameweka wazi mtazamo wake kuhusu sakata linalomkumba mrembo huyo baada ya kutoa kauli tata katika mahojiano akidai kwamba hawezi toka kimapenzi na mwanaume mwenye kipato cha chini. Kwa mujibu wa Trevor, tamko hilo limekuwa na athari kubwa kwa taswira ya Mungai Eve na limepelekea mashabiki wengi kujitenga naye, wakieleza kuwa maneno yake ni kielelezo cha dharau kwa vijana wanaojitahidi kujikimu kwa kipato cha chini. Anasema maneno hayo yamejenga dhana ya kiburi na yamevunja uhusiano wa karibu aliokuwa nao na wafuasi waliomsaidia kufanikisha safari yake ya umaarufu. Aidha, Trevor amesisitiza kuwa hatua ya kuomba radhi inaweza kuwa njia pekee ya kurejesha imani ya mashabiki na kupunguza ukosoaji unaoendelea kumwandama mrembo huyo ambaye juzi kati alikiri kupitia matatizo ya afya ya akili hasa baada ya kujutia maamuzi ya kumkimbia mwanaume ambaye alimpambania hadi kupata umaarufu mkubwa nchini Kenya. Ikumbukwe katika mahojiano na Liz Jackson, Mungai Eve alinukuliwa akisema kuwa hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ambaye kipato chake kiko chini ya shilingi laki tano kwa mwezi. Kauli hiyo ilizua tafsiri kwamba anajiona bora kuliko watu wa kawaida, hali ambayo iliwakasirisha mashabiki na kuibua upinzani mkali dhidi yake.

Read More
 Jovial Aonya Wasichana Kuhusu Safari ya Uzazi

Jovial Aonya Wasichana Kuhusu Safari ya Uzazi

Nyota wa muziki kutoka Kenya, Jovial, amewapa changamoto mabinti wenye mioyo dhaifu kufikiria mara mbili kabla ya kuingia kwenye safari ya ujauzito na kujifungua. Kupitia Instastory, Jovial amefunguka kuhusu changamoto ambazo amekutana nazo wakati wa ujauzito na hata baada ya kujifungua, akisema kuwa ni safari yenye kuhitaji nguvu za mwili na akili. Amesema amekosa usingizi kutokana na usumbufu wa mtoto mchanga, hali ambayo imemfanya atambue kwa undani ugumu wa safari ya uzazi. Lakini pia kipindi hiki kimempa mtazamo mpya juu ya nguvu na uvumilivu unaohitajika na mama katika malezi ya mtoto. Kwa mujibu wake, pamoja na furaha kubwa ya kumpakata mtoto, hatua ya uzazi huambatana na changamoto ngumu kama uchovu wa mwili, mabadiliko ya homoni, na msongo wa mawazo unaoweza kuathiri afya ya mama. Hata hivyo amesema kuwa lengo lake si kuwatisha wasichana, bali ni kuwasisitizia umuhimu wa maandalizi ya kisaikolojia na kifedha kabla ya kuingia kwenye hatua ya uzazi.

Read More
 Police Bullets Yaweka Rekodi Kundi A CECAFA

Police Bullets Yaweka Rekodi Kundi A CECAFA

Police Bullets FC imeanza vyema kampeni ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake, baada ya kuichapa Kampala Queens bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza ya Kundi A iliyochezwa Uwanja wa Nyayo. Bao hilo la ushindi lilifungwa na Emily Moranga mwanzoni mwa kipindi cha pili. Police sasa itamenyana na DenDen FC ya Eritrea katika mechi yao ya pili na ya mwisho ya makundi. Katika matokeo mengine, mabingwa watetezi CBE kutoka Ethiopia walilazwa 2-1 na Rayon Sports ya Rwanda. Michuano ya Kundi C inatarajiwa kuanza kesho kwa pambano kati ya JKT Queens na JKU Princess. Timu zitakazoshika nafasi ya kwanza kila kundi na moja ya pili yenye alama nyingi zitafuzu nusu fainali zitakazopigwa Septemba 14, huku fainali ikifanyika Septemba 16. Bingwa atawakilisha CECAFA kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake.

Read More
 Nyashinski Atangaza Album Mpya ya Kiwango cha Kimataifa

Nyashinski Atangaza Album Mpya ya Kiwango cha Kimataifa

Mwanamuziki kutoka Kenya, Nyashinski, ametangaza ujio wa album yake mpya ambayo kwa mujibu wake itakuwa na kiwango cha kimataifa. Akizungumza kuhusu mradi huo, Nyashinski amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akiwaburudisha mashabiki wa Afrika Mashariki kupitia nyimbo zake, lakini sasa ameamua kupeleka muziki wake kwenye jukwaa la dunia. Msanii huyo amefichua kuwa amekuwa akirekodi album hiyo kwa takribani miezi minane, na kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha video za nyimbo zitakazojumuishwa kwenye kazi hiyo. Kwa mujibu wa tracklist iliyoichapishwa mtandaoni na Nyashinski, album hiyo inatarajiwa kuwa na jumla ya nyimbo 13, ikiwemo ngoma zinazojulikana kama Tai Chi na P.I.C. Amewataka mashabiki wake kujiandaa kwa safari ya kipekee ya muziki, akiwahimiza kuisikiliza album hiyo kuanzia wimbo wa kwanza hadi mwisho, akiahidi itakuwa tofauti na kazi zake za awali. Hii inakuja wiki chache baada ya kujiunga na kampuni kubwa ya muziki, Sony Music, hatua inayotajwa kufungua milango ya kimataifa kwa safari yake ya kisanii.

Read More
 Bahati Amchana Mariga, Asema Binti Yake Ni Maarufu Zaidi

Bahati Amchana Mariga, Asema Binti Yake Ni Maarufu Zaidi

Mwanamuziki Bahati amemchana bila huruma Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Nchini (FKF), McDonald Mariga, akidai kwamba hana jina kubwa la kutumiwa kama chanzo cha kiki. Bahati amesema anamuheshimu Mariga kama gwiji wa soka, lakini akashangazwa na madai kwamba anatafuta umaarufu kupitia jina lake. Amesisitiza kuwa hata binti yake wa mwisho, Malaika, ana umaarufu mkubwa zaidi ukilinganisha na Mariga. Msanii huyo pia ameongeza kuwa kulikuwa na hujuma nyingi dhidi yake kufanikisha mchakato wa kutoa ahadi yake ya shillingi millioni moja kwa Hatambee stars. Kwa mujibu wa maneno yake, waliopanga wanajua ukweli. Kauli hizo zimezua gumzo kubwa, huku baadhi ya mashabiki wakimtetea kwa kusema ana haki ya kulinda heshima yake, na wengine wakimtaka aendelee kuheshimu wachezaji waliowahi kuitumikia Kenya.

Read More
 Shalkido Amuomba Msamaha Terence Creative Baada ya Matusi

Shalkido Amuomba Msamaha Terence Creative Baada ya Matusi

Msanii wa zamani wa kundi la Sailors, Shalkido, ameomba radhi hadharani kwa kumkosea heshima mchekeshaji maarufu Terence Creative, baada ya kumfananisha na mbwa katika kauli zake za awali. Akizungumza baada kulamba dili la ubalozi la Dignity Furniture, Shalkido amesema maneno hayo yalitokana na maumivu na changamoto alizokuwa akipitia, lakini amejitokeza wazi kuomba msamaha, akisisitiza kwamba anajutia matamshi yake na anaamini ni wakati wa kujenga heshima na mshikamano katika tasnia ya burudani. Kwa upande wake, Terence Creative amepokea msamaha huo kwa moyo wa upendo na akaahidi kuendelea kumuunga mkono kijana huyo, akisema kila mtu hupitia makosa na kinachohitajika ni kurekebisha mienendo. Juzi kati Shalkido alitangaza kuwa amefilisika kiasi cha kushindwa kumudu mahitaji ya msingi. Hali hiyo ilisababisha Eric Omondi kujitokeza kumpa msaada wa pikipiki mpya pamoja na mahitaji ya kimsingi, huku pia Wakenya wenye roho ya huruma wakikusanyika kuchanga pesa za kumsaidia kurejea kwenye hali yake ya kawaida

Read More
 Angel Nyigu Apinga Vikali Dansa Bora wa Zuchu

Angel Nyigu Apinga Vikali Dansa Bora wa Zuchu

Dansa maarufu nchini Tanzania Angel Nyigu amefunguka kwa hisia kali baada ya msanii wa Bongo Fleva, Zuchu, kudai kuwa Ashurey ndiye dansa namba moja Afrika Mashariki. Kauli hiyo imeonekana kumkera Nyigu, ambaye amesema Ashurey bado ni mtoto mdogo na hajafikia viwango vya kupewa heshima hiyo kubwa katika tasnia ya densi. Angel Nyigu aliongeza kuwa umaarufu wa Ashurey unatokana zaidi na brand ya Zuchu inayombeba, na si kwa uwezo wake binafsi wa kucheza densi. Ameeleza pia kuwa yeye ndiye aliyemtambulisha Ashurey kwa Zuchu, lakini tangu wakati huo uhusiano wao haujawahi kuwa mzuri baada ya Ashurey kumblock bila sababu za msingi. Kauli hizi zimezua gumzo mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wamejitokeza kumtetea Angel Nyigu kwa kudai ana uzoefu mkubwa na mchango wake hauwezi kupuuzwa, huku wengine wakisema Ashurey amejitengenezea jina kutokana na jitihada zake na ushirikiano wake wa karibu na Zuchu

Read More
 Nicholas Kioko Apinga Madai ya Kuachana na Wambo Ashley

Nicholas Kioko Apinga Madai ya Kuachana na Wambo Ashley

Mtangazaji na content creator Nicholas Kioko amejitokeza wazi kukana tetesi za kuvunjika kwa mahusiano yake na mpenzi wake Wambo Ashley. Kupitia InstaStories, Kioko alifafanua kuwa mapenzi yao bado ni imara na hayatikisiki, akiongeza kwa utani kuwa hakuna uchawi au presha ya mitandaoni itakayomfanya amuache Wambo. Alisisitiza kuwa wao ni moja ya wapenzi wanaoendana zaidi na kwamba wanaotumai kuona wakiachana “watangoja sana.” Uvumi huu ulianza baada ya shabiki mmoja kudai kuwa Kioko na Wambo wangekuwa wanandoa wa pili kuachana, kufuatia misukosuko ya mahusiano iliyoikumba wanandoa wa karibu nao akiwemo Commentator 254 na Moureen pamoja na Vinny Flava na Ng’ang’a. Hata hivyo, Kioko ameweka wazi kuwa yeye na Wambo hawaguswi na tetesi hizo na mapenzi yao yanaendelea kuimarika.

Read More
 Terence Creative Aahidi Msaada wa Kifedha kwa Shalkido Baada ya Kumtusi

Terence Creative Aahidi Msaada wa Kifedha kwa Shalkido Baada ya Kumtusi

Mchekeshaji maarufu Terence Creative ametoa majibu ya busara baada ya kutukanwa na msanii wa Gengetone, Shalkido, kupitia mitandao ya kijamii. Katika ujumbe wake, Terence amemshauri Shalkido kuangalia upya mtazamo wake wa maisha, akisisitiza kuwa namna mtu anavyojipanga kimaisha ndiyo huunda tabia yake, na hatimaye huathiri mustakabali wake. Amemkumbusha kuwa makosa ya zamani hayapaswi kumzuia kusonga mbele, akimtakia heri na baraka katika safari yake ya maisha. Mbali na ushauri huo, Terence ameahidi kumpa Shalkido msaada wa kifedha wa shilingi elfu ishirini pindi atakaporejea nchini, akisisitiza kuwa nia yake ni kumsaidia kuanza upya. Hatua hiyo imepongezwa na mashabiki wengi waliomtaja kama mfano wa hekima na ukarimu licha ya kuchokozwa. Mzozo kati ya Shalkido na Terrence ulitokea baada ya Terence kuwashauri wasanii kuwekeza mapema wakiwa bado wanapata mafanikio katika muziki, jambo ambalo halikumpendeza Shalkido. Shalkido alijibu kwa hasira akimtusi Terence na kudai kuwa anatumia changamoto zake za kuomba msaada kama njia ya kutengeneza maudhui.

Read More
 Mashabiki Wakosoa Diana B kwa Kusample Wimbo wa E-Sir “Saree”

Mashabiki Wakosoa Diana B kwa Kusample Wimbo wa E-Sir “Saree”

Ngoma mpya ya Diana Marua “Bibi Ya Tajiri” imezua mjadala mkubwa baada ya msanii huyo kutumia sample ya wimbo maarufu wa marehemu E-Sir, “Saree”. Ingawa baadhi ya mashabiki waliona hatua hiyo kama heshima kwa nguli huyo wa rap aliyefariki zaidi ya miaka 20 iliyopita, wengi wameibuka na ukosoaji mkali. Wanasema Diana hana uwezo wa kuchana kama E-Sir na kwamba kutumia ngoma hiyo ni sawa na kumvunjia heshima marehemu. Mitandaoni, maoni yamegawanyika. Wapo waliomtaka Diana kuacha kutumia urithi wa wasanii wakubwa kama njia ya kujipatia umaarufu, huku wengine wakimtetea wakidai kila msanii ana uhuru wa kuonyesha ubunifu wake kwa namna tofauti. Hata hivyo, mjadala huu umeonyesha wazi kuwa jina na kazi za E-Sir bado zina nguvu kubwa katika tasnia ya muziki wa Kenya, na zinabaki kuwa urithi unaohitaji kulindwa kwa heshima ya juu

Read More