MENEJA WA OTILE BROWN AFUNGUKA JUU YA KUFUTWA KWA NYIMBO ZA STAA HUYO YOUTUBE

MENEJA WA OTILE BROWN AFUNGUKA JUU YA KUFUTWA KWA NYIMBO ZA STAA HUYO YOUTUBE

Meneja wa otile brown Noriega amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kufutwa kwa nyimbo za msanii huyo kwenye mtandao wa youtube. Akiwa kwenye moja ya interview meneja huyo amesema kama uongozi wa otile brown wameshangazwa na hatua ya nyimbo za staa huyo kufutwa kwenye mtandao wa youtube na aliyezi-upload ambapo ameahidi kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu ili kuhakikisha waliohusika wanakabiliwa kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo Noriega amepuzilia mbali madai yanayotembea mitandaoni kuwa otile brown anatumia suala la nyimbo zake kufutwa kwenye mtandao wa youtube kuupromote kazi yake mpya kwa kusema kwamba suala hilo sio kiki kama inavyodaiwa kwani otile brown huwa hatumii kiki kutangaza muziki wake. Nyimbo ambazo zilifutwa kwenye channel ya youtube ya msanii huyo ni pamoja na Dusuma, Such Kinda of love, Chaguo la moyo wangu, Aiyana na nyingine nyingi.

Read More
 MATATA WAACHIA RASMI UNAWARE EP

MATATA WAACHIA RASMI UNAWARE EP

Kundi la muziki la Matata limeachi rasmi EP yao mpya inayokwenda kwa jina la Unaware. Ep hiyo ina jumla ya mikwaju nne ya moto huku zote zikiwa collabo ambazo wamezifanya na wasanii wa sol generation nviiri the storyteller na Bensoul. Unaware EP ina nyimbo kama Matatu, Pombe na kizungu nyingi, Unaware na tulia nikupange ambapo kwa sasa inapatikana exclusive kupitia digital platforms mbalimbali za kupakulia na kusikilizia muziki duniani. Ikumbukwe kabla ya ujio wa EP hiyo, matata walitusanua kwamba wapo kwenye maandalizi ya album yao mpya na kwanza tangu waanze safari yao ya muziki.

Read More
 KENRAZY KUACHIA ALBUM YAKE MPYA KESHO

KENRAZY KUACHIA ALBUM YAKE MPYA KESHO

Hatimaye nyota wa muziki nchini Kenrazy ameweka hadharani jina na cover rasmi la album yake mpya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kenrazy ameshare artwork ya album yake mpya ambapo amesema album yake hiyo itaitwa Son of God. Hitmaker huyo wa mbilikimo mkora amesema album yake mpya ina jumla ya mikwaju 20 za moto na itaingia sokoni oktoba 13 mwaka huu. Album hiyo ilipaswa kutoka Septemba 27 mwaka lakini kenrazy aliahirishwa kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake. Hii itakuwa ni album ya tatu kutoka kwa mtu mzima kenrazy baada ya Ti-chi ya mwaka wa 2008 na Get it Right from Kenrazy ya mwaka wa 2011.

Read More
 KIM KARDASHIAN AMPA MASHAVU KAMA YOTE KANYE WEST, AMUITA RAPA MKALI WA MUDA WOTE.

KIM KARDASHIAN AMPA MASHAVU KAMA YOTE KANYE WEST, AMUITA RAPA MKALI WA MUDA WOTE.

Kim Kardashian alikuwa Host wa kipindi cha Saturday Night Live (SNL) wikendi hii iliyomalizika ikiwa ni kwa mara ya kwanza. Mengi makubwa yalifanyika na kuwafurahisha watazamaji wa kipindi hicho lakini maneno ya Kim kuhusu Kanye  West yaliwavutia wengi zaidi. Kwenye maneno ya ufunguzi wa kipindi hicho, Kim alizungumzia mumewe Kanye West pamoja na familia yake kwa ujumla “Niliolewa na Rapa mkali wa muda wote. Si hivyo tu, ni Mtu mweusi Tajiri zaidi nchini Marekani. Mtu mwenye kipaji cha aina yake mwenye fikra (genius) ambaye amenipatia watoto wanne wazuri.” alisema Kim Kardashian. Wawili hao wanaendelea kutuweka njia panda kufuatia sakata la talaka ambalo linaendelea baina yao, kwani walionekana wakiondoka hotelini pamoja mjini New York masaa machache kabla ya Saturday Night Live kuanza. Kim pia amekuwa karibu na Kanye West kipindi chote cha uzinduzi wa album ya DONDA.

Read More
 JUSTIN BIEBER ATHIBITISHA MPANGO WA KUPATA MTOTO NA MKEWE HAILEY BALDWIN MWAKA HUU.

JUSTIN BIEBER ATHIBITISHA MPANGO WA KUPATA MTOTO NA MKEWE HAILEY BALDWIN MWAKA HUU.

Staa wa muziki wa Pop duniani Justin Bieber anataka mtoto sasa, amefunguka hadharani.   Kwenye Documentary mpya (Justin Bieber: Our World) iliyoruka kupitia Amazon Prime, Justin Bieber amemwambia mkewe Hailey Baldwin kwamba yupo tayari kuanzisha familia ambapo ataanza rasmi mchakato wa kumpa ujauzito mwaka huu.   “Nia yangu kwa mwaka 2021 ni kuendelea kuweka malengo na kufurahi wakati nikiyafanyia kazi. Kuipa kipaumbele familia yangu ndio jambo la msingi na natumai kwamba tutajaribu kupata mtoto.” amesema Bieber mbele ya Hailey kwenye mkesha wa kuingia mwaka wa 2021.    

Read More
 MAUZO YA MUZIKI WA R.KELLY WAPANDA KWA ASILIMIA 500 BAADA YA KUKUTWA NA HATIA

MAUZO YA MUZIKI WA R.KELLY WAPANDA KWA ASILIMIA 500 BAADA YA KUKUTWA NA HATIA

Mauzo ya muziki wa R. Kelly yameripotiwa kupanda kwa asilimia 517 tangu akutwe na hatia ya mashtaka ya unyanyasaji wa kingono na mengine. Kwa mujibu wa Rolling Stone, mauzo ya muziki wake kwenye majukwaa ya kusikiliza na kupakua muziki mtandaoni (Digital Platforms) yamepanda kutoka millioni 11.2 hadi millioni 13.3 ikiwa ni wiki moja tangu akutwe na hatia ambayo huwenda ikampeleka gerezani miaka 10 au hata kifungo cha maisha. Mitandao kama Apple Music na Spotify ilizima muziki wa R. Kelly, huku wasanii kama Chance the Rapper, Lady Gaga, Ciara na Celine Dion walimfuta kwenye Kolabo za nyimbo ambazo walifanya naye. Mwishoni mwa Wiki iliyopita YouTube ilizifungia akaunti zake mbili za muziki kwenye mtandao huo.

Read More
 SHEEBAH KARUNGI KUZINDUA CHUO CHA KUHAMASISHA WATOTO WA KIKE.

SHEEBAH KARUNGI KUZINDUA CHUO CHA KUHAMASISHA WATOTO WA KIKE.

Mwanamuziki wa lebo ya muziki ya Team No Sleep Sheebah Samali Karungi amefunguka na kusema kwamba ana mpango wa kuanzisha shule ya kutoa ujuzi wa kuwahamasisha watoto wa kike. Hitmaker huyo wa Yolo amesema lengo la yeye kuanzisha chuo hicho ni kuwaona wanawake wanaanza kujitegemea kiuchumi badala ya kukaa nyumbani wakisubiri waume zao wawape pesa na mahitaji ya msingi. Sheebah amedokeza kwamba ataendelea na mpango wake wa kutoa msaada kwa jamii maeneo yote nchini uganda kwa lengo la kuwahimiza watoto wa kike wajenge tabia ya kujitegemea katika maisha. Kauli ya Sheebah imekuja mara baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kuanzisha chuo cha muziki ambacho kitakuza vipaji nchini uganda ili itoe  wasanii wenye tajriba kama yake

Read More
 CAMILA CABELLO AFIKISHA MAUZO YA DIAMOND KUPITIA WIMBO WA “HAVANA”

CAMILA CABELLO AFIKISHA MAUZO YA DIAMOND KUPITIA WIMBO WA “HAVANA”

Wimbo wa msanii camila cabello kutoka nchini Cuba uitwao “Havana” uliotoka mwaka wa 2017 ambao amemshirikisha rappa Young Thug, umefanikiwa kuuza (units) millioni 10 ambayo ni ngazi ya juu kabisa. Camila ambaye ni member wa kundi bora la muziki kuwahi kutoka ulimwenguni la fifty harmony, kutokana na hatua hiyo chama cha Recording Industry Association of America (RIAA) kimekabidhi tuzo maalumu yaani (Plaque) maarufu kwa jina Almasi au (Diamond). Camila Cabello anakuwa msanii wa kwanza kutoka Cuba kufikia mafanikio hayo makubwa kupitia wimbo mmoja. Lingine usilo lijua kuhusu “Havana” ni kuwa, rappa Young Thug ambaye ndiye kashirikishwa kwenye wimbo huo, hakutaka kutia verse yake katika havana kutokana na kutoielewa wimbo huo lakini kwa shinikizo la mama yake mzazi alifanya. Kwenye mahojiano na HipHop DX, Thug ameeleza kwamba hakuamini kama wimbo huo ungefanya vizuri kutokana na kuwa havikua vitu vyake lakini anafurahishwa kuona amekuwa moja ya watu walioshiriki katika wimbo huo ambao umetunukiwa tuzo maalumu ya Diamond na RIAA.

Read More
 ONLY ONE KING ALBUM YA ALI KIBA NDANI YA TIMES SQUARE,NEW YORK.

ONLY ONE KING ALBUM YA ALI KIBA NDANI YA TIMES SQUARE,NEW YORK.

Album mpya ya msanii Ali kiba “Only One King” inazidi kuweka historia mara baada ya cover la album hiyo kuonekana katika Screen za eneo maarufu Times Square huko Jijini New York, nchini Marekani. Album hiyo ambayo ina siku tatu tangu iachiwe, ina kuwa kazi ya kwanza Kwa Ali kiba kuonekana Times Square sehemu ambayo matangazo makubwa duniani huonekana. Sanjari na hilo “Only One King” album imefanikiwa kufikisha jumla ya Streams Milioni 1 katika mtandao wa BoomPlay tangu iachiwe rasmi Oktoba 7. Album hiyo ambaye ni ya tatu kwa mtu mzima Ali Kiba ina nyimbo 16 alizoshirikisha wasanii kutoka Tanzania, Kenya na Nigeria. Miongoni mwa nyimbo zilizoko ni Utu, Let me, Niteke, Bwana mdogo, Happy, na nyingine nyingi.

Read More
 SAUTI SOL MBIONI KUJA NA ALBUM MPYA

SAUTI SOL MBIONI KUJA NA ALBUM MPYA

Kundi la muziki nchini sauti sol wametangaza mwezi ambao wataichia album yao ya sita tangu waanze safari yao ya muziki. Kupitia barua ya wazi waliyoishare kwenye ukurasa wao wa instagram sauti sol wamesema album yao mpya itaingia sokoni mwezi mei mwaka wa 2022. Wakali hao wa ngoma ya Suzzana wamesema kabla ya kuachia album yao mpya, wataachia singo yao mpya mwezi Disemba mwaka huu ambapo wamesema kwamba wataweka wazi tarehe ambayo wataachia project hiyo. Sanjari na hilo wametusanua kwamba wanakuja na documentary yao iitwayo Alone Together ambayo itazungumzia changomoto ambazo wasanii wa kundi la sauti sol wamepitia tangu ujio wa janga la korona. Kauli ya sauti sol inakuja mara baada ya kufanikisha tamasha lao la kimuziki liitwalo UK residency lilofanyika nchini uingereza mapema mwezi huu.

Read More
 K.O AACHIA RASMI FORM NNE EP

K.O AACHIA RASMI FORM NNE EP

Mwanamuziki kutoka lebo ya 001 Music K.O ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Form nne EP. Form nne EP ina jumla ya ngoma nne za moto na bonus track mbili ambapo amewashirikisha wakali kama Susumila, Slyvia Ssaru,Tundaman, na wengine kibao. EP hiyo ina ngoma kama Soba, Waonyeshe akiwa na Sylivia Ssaru,Ngoja akiwa na Tundaman pamoja na Dully Sykess, na Akathope huku bonus tracks zikiwa ni Nimempata akiwa amemshirikisha Susumila na Nitakoma akiwa wanafunzi wa shule ya upili ya Shimo la tewa Form nne EP ni Kazi ya kwanza kwa mtu mzima K.O tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa kukisikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya.

Read More
 KODAK BLACK AOMBA MAHAKAMA RUHUSA YA KUTOKA NJE YA MJI WA FLORIDA.

KODAK BLACK AOMBA MAHAKAMA RUHUSA YA KUTOKA NJE YA MJI WA FLORIDA.

Rapa kutoka nchini Marekani Kodak Black amemuomba Hakimu ruhusa ya kutoka nje ya Mji Atokao wa Florida wakati huu yupo chini ya uchunguzi. Kulingana na taarifa za kuaminika zilizotolewa na Tovuti Ya Tmz,  Muuguzi wa karibu wa Kodak anaamini rapa huyo atafaidika na ratiba ya matibabu atakayopatiwa nje ya Florida katika siku zake 30 za mwisho za kupata matibabu nje ya mji huo. Hata hivyo timu nzima ya Kodak Black wanafikiria kwamba rapa huyo atafanikiwa zaidi na matibabu iwapo atakuwa katika mazingira tofauti kwa muda fulani. Ombi hilo limekuja siku chache tu mara baada ya Kodak Black ku-tweet na kuwashtua mashabiki zake kwamba huenda akawa na matatizo ya akili kwani aliandika kwamba ana huzuni, na anajiona mpweke kabla ya kuzifunga kurasa zake za mtandao wa Twitter & Instagram.

Read More