MFUMO WA TWO-FACTOR AUTHENTICATION KUWA LAZIMA KATIKA AKAUNTI ZOTE ZA GOOGLE

MFUMO WA TWO-FACTOR AUTHENTICATION KUWA LAZIMA KATIKA AKAUNTI ZOTE ZA GOOGLE

Mwezi wa tano mwaka huu Google ilitoa tamko watumiaji wote wanaotumia huduma za Google kuweka mfumo wa Two-Factor authentication (two-step verification) ili kuboresha usalama wa akaunti na ilisema mwisho wa mwaka huu itaweka iwe ni lazima kwa watumiaji wake wote. Mfumo wa 2FA unasaidia kuweka ulinzi wa ziada, endapo hacker au mtu akipata Password yako, atashindwa kuingia kwa sababu atalazimika kuandika namba maalum ambayo inatumwa katika simu yako kwa njia ya SMS, au App ya Google Search na Google Authenticator. Google imekumbusha akaunti zote ambazo hazijaweka mfumo wa 2 Factor Authentication zitalazimika kuwekwa mfumo huo kwa lazima. Endapo kama uliweka namba ya simu ya zamani utashindwa kuingia kwenye akaunti yako mpaka ukiweka PIN ambayo itatumwa kwenye namba hiyo. Zaidi ya Akaunti Milioni 150 zikiwemo akaunti za Content Creators Milioni 2 wa YouTube ambao hawajaweka mfumo huo; zitafungiwa na zitalazimika kutumia mfumo mpya kwa lazima. Kuepuka kukosa akaunti ni vyema kuithibitisha namba ambayo imesajiliwa katika 2 Factor na devices zote ambazo umeziunganisha na akaunti yako kabla ya kufungwa rasmi.

Read More
 TIKTOK YAANZA KUPATIKANA KATIKA TV ZA LG

TIKTOK YAANZA KUPATIKANA KATIKA TV ZA LG

TikTok imeanza kupatikana rasmi katika TV zote za LG ambazo zinatumia mfumo wa webOS 5.0 na kuendelea. Hii itasaidia kuweka urahisi kwa watumiaji wa TV kuona videos fupi za TikTok katika TV. Mwaka huu hatua kubwa ambayo mtandao wa TikTok ni kuchukua soko la Smart TV. Tayari ilitoa app kwa watumiaji wa Android TV na mwezi huu imeongeza upatikanaji wake kwa watumiaji wa webOS. Ni mpango mzuri kama ilivyo katika Netflix na YouTube zilivyofanikiwa kuwa na apps katika smart TV.

Read More
 YOUNG LUNYA ATHIBITISHA KUFANYA NGOMA MBILI NA DIAMOND PLATINUMZ

YOUNG LUNYA ATHIBITISHA KUFANYA NGOMA MBILI NA DIAMOND PLATINUMZ

Msanii wa Hip Hop kutoka nchini Tanzania, Yong Lunya amesema yeye na Diamond Platnumz wamepanga kurekodi nyimbo mbili pamoja ambazo kila mmoja atakuwa na yake. Kauli ya Lunya inakuja mara baada ya wawili hao kukutana Afrika Kusini ambapo wote walienda kwa ajili ya maandalizi ya albamu zao na ikasemekana huwenda walirekodi ngoma. Akizungumza katika Podcast ya Swahili Radio, Lunya amesema muda wowote watarekodi. Young Lunya atakuwa Rapa mwingine wa kizazi kipya kufanya kazi na Diamond mara baada ya Young Killer ambaye alishirikishwa kwenye wimbo uitwao Pamela ambao unapatikana kwenye albamu yake, A Boy From Tandale iliyotoka Machi mwaka wa 2018.

Read More
 OTILE BROWN APOTEZA ZAIDI YA VIEWS MILLIONI 190 YOUTUBE

OTILE BROWN APOTEZA ZAIDI YA VIEWS MILLIONI 190 YOUTUBE

Staa wa muziki nchini otile brown amepoteza zaidi ya views millioni 190 kwenye akaunti yake ya youtube mara baada ya nyimbo zake tano kufutwa kwenye mtandao huo na aliyezi-upload. Awali Otile brown alikuwa na zaidi ya views millioni 229 ila kwa sasa ana jumla ya watazamaji millioni 35. Nyimbo ambazo zilifutwa kwenye channel ya youtube ya msanii huyo ni pamoja na Dusuma, Such Kinda of love, Chaguo la moyo wangu na Aiyana. Chaguo la Moyo wangu na Dusuma ni video za muziki zenye watazamaji wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube nchini Kenya. Mpaka sasa haijafahamika sababu za kushushwa kwa video hizo za Otile Brown.

Read More
 AZAWI AACHIA RASMI AFRICAN MUSIC ALBUM

AZAWI AACHIA RASMI AFRICAN MUSIC ALBUM

Mkali wa muziki kutoka nchini uganda Azawi ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la African music.   African Music album imebeba jumla ya mikwaju 16 ya moto huku ikiwa na kolabo nne.   Azawi amewashirikisha wasani kutoka uganda ambao ni Eddy kenzo, A Pass, Fik Fameica na bosi wa lebo ya muziki ya swangz avenue Benon Mugumbya.   Album ya “African Music” ni album ya kwanza kutoka kwa Azawi baada ya kutubariki na EP yake iitwayo Lo-Fit iliyotoka mwaka wa 2020.   Hata hivyo Album hiyo inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya  kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Apple music, Boomplay, na Spotify      

Read More
 EDDY YAWE AWAPA SOMO WASANII WA UGANDA

EDDY YAWE AWAPA SOMO WASANII WA UGANDA

Mkongwe wa muziki kutoka nchini uganda Eddy yawe ametoa changamoto kwa wasanii kutia bidii kwenye kazi zao za muziki ili waweze kutimiza malengo yao maishani. Yawe ambaye ni kaka wa bobi wine amesema kiwanda cha muziki nchini uganda kina fedha nyingi hivyo wasanii wanapaswa kujenga tabia ya kuweka akiba badala ya kutumia pesa zao zote kwenye starehe.. Kauli ya Eddy yawe imekuja mara baada ya kukamilisha ujenzi wa mjengo wake wa kifahari uliomgharimu takriban shillingi millioni 155 viungani mwa jiji la kampala. Licha ya Eddy Yawe kusisitiza kwamba ni bidii yake ndio imechangia kukamilisha mjengo wake wa kifahari baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanahoji kwamba mradi wake huo ulifadhiliwa na serikali.

Read More
 NAIBOI AFUNGUKA CHANZO CHA UKIMYA WAKE

NAIBOI AFUNGUKA CHANZO CHA UKIMYA WAKE

Mkali wa muziki nchini Naiboi amefunguka sababu za kukaa kimya kwenye muziki wake kwa takriban miaka miwill.   Kupitia ukurasa wake wa instagram Naiboi amesema kwa muda sasa mashabiki zake wamekuwa wamkishinikiza atoe nyimbo mpya ila uongozi wake umekuwa kizingiti kwake kufanya hivyo.   Hitmaker huyo wa pesa amesema ameumizwa na kitendo cha kukaa kimya kwenye muziki wake ikizingatiwa kuwa amerekodi zaidi ya nyimbo 800 za moto ambapo amewataka mashabiki zake waendelea kumuombea arejee katika hali yake ya kawaida.   Ikumbukwe Naiboi amekuwa akitangaza ujio wa Ep yake iitwayo Otero ambayo hajeweka wazi itaingia lini sokoni.              

Read More
 MJENGO WA KIFAHARI WA MSANII RINGTONE KUPIGWA MNADA KWA TAKRIBAN SHILLINGI MILLIONI 80

MJENGO WA KIFAHARI WA MSANII RINGTONE KUPIGWA MNADA KWA TAKRIBAN SHILLINGI MILLIONI 80

Mjengo wa kifahari wa msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone ulioko mitaa ya Runda jijini Nairobi imepiga mnada kwa shillingi millioni 80 na kampuni moja ya wanasheria.   Hatua hii inakuja siku chache baada ya Ringtone kupewa notisi ya siku 10 ya kuondoka kwenye mjengo huo wenyewe utata la sivyo ahamishwe kwa nguvu.   Kulingana na barua iliyotolewa na kampuni ya mawakili ya AGN Kamau Advocates,  nyumba ambayo ringtone anaishi kwa sasa ni ya raia wa Sweden kwa jina Mona Ingegard aliyefariki mwaka wa 2007 na Ringtone alinunua nyumba hiyo bila kufuata njia sahihi.   Hata hivyo Ringtone mpaka sasa hajatoa tamko lolote kuhusiana madai ya mjengo wake wa kifahari kupigwa mnada.            

Read More
 KAROLE KASITA ADAI HATAKI KUSIKIA HABARI YA HARUSI KWENYE MAISHA YAKE

KAROLE KASITA ADAI HATAKI KUSIKIA HABARI YA HARUSI KWENYE MAISHA YAKE

Msanii wa muziki wa dancehall kutoka nchini uganda Karole Kasita amefunguka na kudai kwamba hataki kabisa kufunga ndoa kwa njia ya harusi.   Karole kasita amesema hana imani tena na wanaume na hivyo haoni akimtambulisha mwanaume yeyote kwa wazazi wake hivi karibuni.   Hitmaker huyo wa Balance amesema anafadhalisha mahusiano yake yawe ya siri kwani kuna aibu kubwa uibuka wakati mwanamke anapoachwa baada ya harusi.   Kauli yake imekuja mara baada ya kuumizwa kwenye mahusiano yake ya zamani baada ya kuachwa na mchumba kipindi yupo chuo kikuu, hivyo hanawaogopa wanaume wote kwani wanaweza kumkimbia.            

Read More
 LINEX AMCHANA BABA LEVO KWA MADAI YA KUMZUNGUMZIA VIBAYA

LINEX AMCHANA BABA LEVO KWA MADAI YA KUMZUNGUMZIA VIBAYA

Mwanamuziki wa Bongofleva Linex mjeda ameamua kumtolea uvivu baba levo baada ya msanii huyo kuendelea kuongelea maisha yake mara kwa mara kwenye vyombo vya habari Kupitia ukurasa wake wa Instagram Linex amemchana Baba Levo kuwa aache kuongelea maisha yake kwenye redio kwani jambo hilo linamkosesha amani huku akimuomba baba levo msamaha kama amewahi kumkosoa. Linex na Baba Levo ni marafiki wa miaka mingi na Baba Levo ameshawahi kukiri mara nyingi kuwa Linex ni kati ya watu ambao walimsaidia miaka ya hapo nyuma akiwa Dareesalaam akijaribu kuupambania kipaji chake cha muziki. Hata hivyo Baba Levo amekuwa akifunguka matukio na tabia za Linex ambazo walikuwa wanazipitia miaka ya nyuma. Lakini pia amekuwa akilitaja jina la Linex kwenye mifano mbalimbali afanyapo mahojiano na vyombo vya habari jambo ambalo limemfanya Linex kukwazika

Read More
 VIDEO 4 ZA MUZIKI ZA NADIA MUKAMI ZAFUTWA YOUTUBE

VIDEO 4 ZA MUZIKI ZA NADIA MUKAMI ZAFUTWA YOUTUBE

Video za muziki za msanii nadia mukami zimefutwa kwenye akaunti ya mtandao wa youtube ya msanii huyo.   Ukitembelea kwenye akaunti ya youtube  ya nadia mukami  hautafanikiwa kuziona nyimbo zake kama maombi, Wangu, Radio Love na Kolo kutokana na kuondolewa na aliyezi-upload.   Sanjari na hilo nyimbo za Nviiri the story teller Pombe sigara na niko sawa zimeondolewa pia kwenye mtandao wa youtube.   Hata hivyo chanzo cha music video  za wasanii hao  kuondolewa kwenye mtandao wa youtube haijajulikana mpaka sasa.   Ikumbukwe siku ya jana Msanii otile brown alipata pigo kama hilo baada ya video tano za nyimbo zake kuondolewa kwenye mtandao.            

Read More
 ALI KIBA AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA THE ONLY ONE KING

ALI KIBA AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA THE ONLY ONE KING

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba ameachia rasmi albam yake mpya inayokwenda kwa jina la The Only One King.   Album hiyo aliyowashirikisha wasanii tofauti ina jumla ya nyimbo kumi na sita za moto na inapatikana katika platform tofauti na muziki mitandaoni.   Baadhi ya wasanii walioshirikishwa na Alikiba kwenye albam hiyo ni Patoranking kutoka Nigeria, Blaq Diamond, Sauti Sol, Nyashinski, Khaligraph Jones, Sarkodie.   Wengine waliosikika katika albam hiyo ni Mayorkun kutoka nchini Nigeria, Tommy Flavour na K 2ga pamoja na Abdu Kiba kutoka King’s Music.   Ali Kiba ambaye ana miaka zaidi ya 18 kwenye muziki, hii ni album yake ya TATU, ya kwanza ilikuwa ni ‘Cinderella’, iliyotoka mwaka 2006 na ya pili ilikuwa ni ‘Ali K 4Real’,iliyotoka mwaka 2009.                    

Read More