SHILOLE AMVUA NGUO ALI KIBA

SHILOLE AMVUA NGUO ALI KIBA

Baada ya interview ya Ali Kiba kutrend akizungumzia sakata la kutomualika msanii mwenzake shilole katika uzinduzi wa album yake ya Only One King ,tayari mrembo huyo ameweza kumjibu Ali Kiba kupitia ukurasa wake wa Instagram. Katika maelezo yake Shilole ameonekana kutoridhishwa na kauli ya ali kiba kuwa hakumualika kwenye listening party ya album yake na kudai kuwa yeye hakwenda katika shughuli ile kama mvamizi. Haikushi hapo ameenda mbali na kueleza kuwa Ali Kiba amethibitisha kwa walimwengu kuwa ana kiburi cha ushamba, kuvimba na kupandisha mabega katika namna isiyo stahili. Sekeseke hili limetokea baada ya mjasiriamali Esha Buheti kulalamika kuwa hapewi thamani na Ali kiba licha ya kumuunga mkono kwenye muziki wake kwa asilimia kubwa. Kauli hiyo ya Esha inadaiwa kutolewa baada ya Shilole ambaye hajawahi kuwa shabiki wa Ali kiba kualikwa kupitia ukurasa rasmi wa Alikiba huku Esha akialikwa kupitia ukurasa wa Instagram wa Kings Music.

Read More
 MEEK MILL AIBWATUKIA LEBO YAKE,ADAI KUTOLIPWA PESA ZAKE.

MEEK MILL AIBWATUKIA LEBO YAKE,ADAI KUTOLIPWA PESA ZAKE.

Rapa kutoka nchini Marekani, Meek Mill ameamua kuichana Lebo yake kwa kile anachodai kwamba haijamlipa pesa zake zilizotokana na muziki wake kuuzwa. Kupitia mfululizo wa tweets zake  kwenye mtandao wa Twitter Meek Mill amesema hajalipwa na hafahamu ni kiasi gani cha pesa lebo yake imeingiza kutoka kwenye muziki wake ambapo ameenda  mbali zaidi na kusema kwamba anahitaji Mwanasheria wa kumtetea ili aweze kupata haki yake. Hakuishia hapo, Meek Mill ametishia kuanika wazi mkataba wake ifikapo Jumatatu ijayo ili dunia ione udhalimu wa lebo yake. Hata hivyo Meek Mill ambaye anasimamiwa na Roc Nation, hajaweka wazi jina la Label ambayo anaituhumu, kama ni Maybach Music Group au Atlantic Records

Read More
 EDDY KENZO ATANGAZA KUACHA MUZIKI

EDDY KENZO ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Bosi wa lebo ya muziki Big Talent Eddy Kenzo amejiunga na orodha ya wasanii kutoka nchini Uganda wanaotaka kuacha tasnia ya muziki. Katika mahojiano yake wiki hii , Kenzo ameelezea nia yake ya kuacha kabisa biashara ya muziki na kwenda kujikita kwenye kilimo huko Masaka nchini Uganda. Eddy Kenzo, ambaye amepata mafanikio mengi kwenye muziki wake amesema anataka kusahau kila kitu kuhusu muziki na kuanza kuishi maisha ya utulivu. Hitmaker huyo wa “Sango” amedokeza atakuwa anatumbuiza mara moja baada ya muda  huku akielekeza nguvu zake zote kwenye biashara nyingine ambazo zitamuingiza kipato. Ikumbukwe juzi kati msaniii Winnie Nwagi pia alikiri kuwa amechoshwa na tasnia ya muziki nchini Uganda kutokana na wa kukosoa vikali  kwenye mitandao ya kijamii.

Read More
 MALKIA KAREN NI MJAMZITO,AACHIA VIDEO KWA MARA YA KWANZA

MALKIA KAREN NI MJAMZITO,AACHIA VIDEO KWA MARA YA KWANZA

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Malkia Karen amejibu kwa vitendo tetesi za kubeba ujauzito. Karen ametumia ukurasa wake wa Instagram kupost video ambayo ni kionjo cha video ya wimbo wake mpya alioupa jina la Haina Haja huku akionekana kuwa ni mjamzito wa mimba kubwa. Kwenye kionjo cha wimbo huo Malkia Karen anasikika akimlaumu mwanume ambaye alikuwa naye kwenye mahusiano lakini mwisho wa siku akaja kumtenda vibaya. Tetesi za Malkia Kareen kubeba ujauzito zili trend sana kwenye mitandao ya kijamii wiki kadhaa zilizopita na ujauzito huo ulihusishwa kuwa ni wa staa wa muziki Diamond Platnumz japo hakuna yeyote kati ya wawili hao aliyejitokeza kuthibitisha taarifa hizo.

Read More
 KOEMAN ATIMULIWA BARCELONA

KOEMAN ATIMULIWA BARCELONA

Hatimaye kocha Ronald Koeman amefutwa kazi ya kuendelea kukitumikia kikosi cha FC Barcelona baada ya kuwa usukani kwa miezi 14 pekee. Barca imevuna alama 15 pekee katika mechi 10 za La Liga msimu huu, ambapo tayari wamepoteza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya. Koeman anafukuzwa akiwa kwenye nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi alama sita pungufu ya kinara Sevilla baada ya kupokea kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Rayo Vallecano siku wa kuamkia Oktoba 28. Kipigo kikiwa cha tatu kwa Barcelona katika mechi nne zilizopita kikifuatiwa na kile cha mtani wake Real Madrid mtanange wa El Clasico. Taarifa rasmi ya klabu imesema kuwa “Rais wa klabu (Joan Laporta) amempa taarifa ya kufutwa kazi muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi dhidi ya Rayo Vallecano”.

Read More
 OCTOPIZZO ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA

OCTOPIZZO ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA

Mkali wa muziki wa hiphop nchini Octopizzo amedokeza ujio wa album yake mpya. Octopizzo ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akiwawataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kuipokea album hiyo ambayo kwa mujibu wake ipo njiani. Licha ya kutoweka maelezo zaidi kuhusu ujio wa album yake mpya, hii itakuwa ni Album ya sita kwa mtu mzima Octopizzo baada ya “Jungle Fever” iliyotoka mwaka wa 2020. Kauli ya Octopizzo imekuja mara ya kusherekea mafanikio ya wimbo wake uitwao “Babylon” baada kufikisha zaidi ya views millioni nne kwenye mtandao wa Youtube.

Read More
 KAMPUNI YA FACEBOOK YABADILISHA JINA RASMI

KAMPUNI YA FACEBOOK YABADILISHA JINA RASMI

Kampuni ya Facebook hatimaye ameamua kubadili jina la mtandao wa kijamii wa Facebook na kuwa META. Akizungumza kwenye mkutano wa kila mwaka wa kampuni hiyo, Annual Connect Conference Afisa Mtendaji Mkuu wa mtandao huo Mark Zuckerberg amesema kuwa hatua hii ni sehemu ya mabadiliko katika ruwaza yake kutoka kwenye mitandao ya kijamii na kuelekea katika mfumo wa Metaverse ulimwengu wa kidigitali ambao unaweza kuwa na kizazi kijacho cha mitandao ya kijamii. Mark amewaondoa watu shaka na kwa kusema kuwa mabadiliko hayo hayataathiri mitandao yake binafsi kama vile Facebook, Instagram na Whatsapp bali ni kampuni mama inayozimiliki. Hata hivyo wapo ambao wameibuka kwa kumshutumu Mark kuwa anatupia jicho faida zaidi kuliko usalama

Read More
 DOGO RICHIE AMTIMUA MSANII WAKE

DOGO RICHIE AMTIMUA MSANII WAKE

Msaani Dogo Richie amesitisha kufanya kazi na msanii wake Ruchi Wakanda. Kwa mujibu wa taarifa, wawili hao ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu, kwa sasa hawaonani uso kwa uso. Dogo Richie na Ruchi kwa pamoja wamehusika katika utayarishi wa nyimbo kama Controller na Naringa naye ambayo Ruchi amemshirikisha Dogo Richie. Kulingana na chanzo cha karibu na Dogo Richie, mzozo baina ya wasanii hao umesababishwa na mchongo wa hela ambao ruchi alifaa kutoa kwa dogo richie kutoka na kazi za usimamizi alizokuwa anamfanyia chini ya record lebo yake ya  Riclam.

Read More
 SPICE DIANA: NITAPATA MTOTO BAADA YA SHEEBAH

SPICE DIANA: NITAPATA MTOTO BAADA YA SHEEBAH

Staa wa muziki nchini Uganda Spice Diana,, alisherehekea kumbukizi yake ya kuzaliwa mwishoni mwa juma lilopita katika hoteli ya Serena kwenye hafla ya iliyohudhuriwa na wanafamilia pamoja na marafiki. Sasa akiwa kwenye moja ya interview hitmaker huyo wa body amedai kwamba hana mpango wa kuaanzisha familia hivi karibuni, ikizingatiwa kuwa hakuna wakati maalum wa kuolewa au kupata watoto. Spice Diana ambaye kwa sasa ametimiza umri wa miaka 27 Amebainisha kuwa bado yuko bize na kazi zake za muziki, hivyo ataanzisha familia pindi tu atakapotimiza ndoto zake kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda. Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kumtumia msanii mwenzake Sheebah, ambaye ana umri wa miaka 32, kama role model wake kwenye masuala ya ndoa ambapo amewataka watu kutomshinikiza kuingia kwenye ndoa wakati hayuko tayari kisaikolojia.

Read More
 RAY C ACHUKIZWA NA KITENDO CHA DIAMOND KUZOMEWA MAREKANI

RAY C ACHUKIZWA NA KITENDO CHA DIAMOND KUZOMEWA MAREKANI

Mara baada ya kuwepo kwa kile kinachoonekana ni kubezana kwa watu waliokaribu na Diamond Platnumz na Harmonize kufuatia show za wasanii hao nchini Marekani, Mkongwe wa Bongofleva, Ray C ametaja huo kama Ulimbukeni. Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Ray C amesema kwamba kumbeza harmonize na diamond kutokana shows zao za nchini marekani sio sawa kwani itakuwa vigumu kwa wasanii wa bongo kushindana na wasanii wa nchi nyingine kama Nigeria kwa mtindo huo. Hitmaker huyo wa “Mapenzi yangu” amesema watu waache suala la kumshindanisha harmonize na diamond platinumz  na badala yake wajivunie namna wasanii hao wanavyoiwakilisha vyema nchi ya tanzania kimataifa kupitia kazi zao za muziki.

Read More
 AKOTHEE AWAPA SOMO WAZAZI

AKOTHEE AWAPA SOMO WAZAZI

Rais wa singles mothers nchini Esther Akoth maarufu kama Akothee amewaonya wazazi kukoma kuwatumia watu mashuhuri kama daraja la kulea watoto wao. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Akothee ameweka wazi kuwa mastaa hawatengenezi majina au chapa zao ili kuwa mfano wa kuigwa katika jamii. Hit maker huyo wa ‘Kula Ngoma’ ameongeza kuwa baadhi ya vijana wana tabia ya kuiga maisha ya watu maarufu bila kujua kinachoendelea nyuma ya pazia. Lakini pia amebainisha kuwa mitindo ya maisha ya mastaa kwenye mitandao ya kijamii kumewafanya vijana wengi kuingia kwenye msongo wa mawazo.

Read More
 NBA YOUNGBOY AACHIWA HURU KWA DHAMANA

NBA YOUNGBOY AACHIWA HURU KWA DHAMANA

Baada ya takribani miezi saba kusota rumande, hatimaye rapper NBA YoungBoy ametoka jela kwa dhamana ya shillingi millioni 55.6 baada ya jaji wa Louisiana kumpa dhamana. Rapper huyo ameripotiwa kuachiliwa huru kabla ya kifungo kuisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na tabia nzuri aliyoionesha. Hata hivyo kwa sasa yupo kwenye kifungo cha nyumbani na atahitajika kuvaa kifundo cha mguu, lakini pia hawezi kuondoka katika makazi anayoishi na ni familia yake pekee inayoweza kuishi naye. Rapper huyo ambaye alikamatwa mwezi Machi mwaka huu baada ya kufanyika kwa msako wa polisi na kukutwa na hatia ya kumiliki bunduki na bunduki hiyo kutokuwa na usajili, pamoja na kukutwa na dawa za kulevya. Vikwazo vingine alivyowekewa ni pamoja na kutokuwa na silaha na kutojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambapo pia atatakiwa kuwa anawasiliana na watu wa idara ya kupambana na dawa za kulevya kwa vipimo vya mara kwa mara.

Read More