WINNIE NWAGI AWEKA REKODI INSTAGRAM

WINNIE NWAGI AWEKA REKODI INSTAGRAM

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Winnie Nwagi amefikisha zaidi ya followers millioni moja kwenye mtandao wa instagram. Winnie Nwagi ambaye juzi kati aliweka wazi mpango wa kuacha muziki kutokana na skendo hakuficha furaha yake ya kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao huo kwani ametumia ukurasa wake wa instagram kuwapa shavu mashabiki wake kwa kumpa support kwenye shughuli zake za kimuziki kwani sio jambo rahisi Kushawishi Watu kumfuatilia Kwenye Mitandao Ya Kijamii. Mrembo huyo amepata idadi hiyo ya followers kutokana na picha pamoja na video zenye utata ambayo wajuzi wa mambo nchini Uganda wanadai  inakwenda kinyume na maadili ya jamiii. Hata hivyo hii inamfanya Winnie Nwagi kuingia kwenye orodha ya wasanii Kike na Watu maarufu nchini  Uganda wenye followers wengi kwenye Mtandao wa iNstagram baada ya kufikisha jumla ya Wafuasi Million moja.

Read More
 BOW BOW AJIKUTA AKIWA BABA WA WATOTO WAWILI

BOW BOW AJIKUTA AKIWA BABA WA WATOTO WAWILI

Rapa kutoka Marekani Bow Wow amekuwa akijiita Baba wa mtoto mmoja kwa kipindi cha miaka 10 ambayo amekuwa na binti yake Shai Moss. Hivi karibuni alikuwa akikataa maswali ya kuwa na mtoto mwingine, kupitia ukurasa wake wa twitter, aliwahi kukanusha kwa kusema ana mtoto mmoja tu. Kwa mujibu wa mitandao mbali mbali, Bow Wow alikuwa akimkataa mtoto wa Olivia Sky hadi kushindwa kumpa msaada wa pesa za matunzo hadi pale ambapo Mahakama ilipofikia uamuzi wa kuthibitisha kuwa rapa huyo ni Baba halali wa mtoto huyo wa Kiume, Stone Moss mwenye umri wa mwaka mmoja. Bow Wow mwenye umri wa miaka 34, ameridhia na kuamua Kutangaza rasmi kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa sasa ni Baba wa watoto wawili.

Read More
 MWANAMKE MMOJA AJITOKEZA NA KUDAI KWAMBA NI MTOTO WA DMX

MWANAMKE MMOJA AJITOKEZA NA KUDAI KWAMBA NI MTOTO WA DMX

Vita ya urithi wa mali kwenye familia ya DMX inaendelea kushika kasi, wiki hii amejitokeza mwanamke mmoja na kudai kwamba ni mtoto wa marehemu DMX, hivyo kufanya namba ya watoto wake kufikia 15. Kwa mujibu wa Page Six, wiki kadhaa zilizopita mwanamke huyo aitwaye Raven Barmer-Simmons alimtafuta mtoto mkubwa wa DMX na kumwambia kwamba yeye ni mtoto wa DMX. Hata hivyo kwa mujibu wa mahakama watoto wote 14 akiwemo na mwanamke huyo watafanyiwa vipimo vya DNA kubaini uhalali wao kwa ajili ya kugawa urithi kwa usahihi. Hii yote inatokana na kutoelewana kwa watoto wa DMX juu ya urithi wa mali zilizoachwa na mkongwe huyo wa Hip Hop ambaye alifariki dunia April 9 mwaka huu. Mwishoni mwa juma lilopita Jaji aliwateua watoto watatu; Xavier, Tacoma na Sean Simmons kuwa wasimamizi wa muda wa mali za baba yao.

Read More
 NANDY KUFUNGA MWAKA NA SHOWS ZAIDI YA 15

NANDY KUFUNGA MWAKA NA SHOWS ZAIDI YA 15

Staa wa Bongofleva, Nandy ameweka wazi ratiba ya show zake katika kuufunga mwaka 2021 ambapo anatarajia kufanya show zaidi ya 15 ndani ya nje ya nchi. Show za kimataifa atazifanya Nairobi, Kenya, Lagos, Nigeria, Dubai na Afrika Kusini. Hatua hiyo ya Nandy inakuja baada ya hivi karibuni kutaanza ziara yake ya kimuziki nchini Marekani kuanza Machi hadi Aprili mwaka wa 2022 baada ya kuihairisha kwa mwaka mmoja. Utakumbuka mapema mwaka jana mwimbaji huyo alitangaza ziara yake iliyoipa jina la Nandy USA Tour 2020 ambayo ingeanza Mei 22 hadi Juni 20, mwaka wa 2020, lakini akalazimika kuifutiliwa mbali kufuatia mlipuko wa  virusi vya Corona.

Read More
 WASANII WA P-UNIT WATIA NIA YA KUGOMBEA UONGOZI MWAKA 2022

WASANII WA P-UNIT WATIA NIA YA KUGOMBEA UONGOZI MWAKA 2022

Wasanii wanaounda kundi la P-Unit, Frasha na Gabu wametia nia ya kugombea nyadhifa za uongozi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022. Wawili hao wametangaza kuwa watawania viti vya uwakilisha wadi. Francis Aamisi maarufu kama Frasha amesema atasimama kiti cha uwakilisha wadi huko Athi River huku Gabriel Kagundu maarufu kama Gabu akiwania kiti cha uwakilishi wadi eneo la Kenyatta Golf Course mwaka wa 2022. Wasanii hao wanajiunga na wasanii wengine kama Prezzo na Reuben kigame ambao wametia nia ya kuwania uongozi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.

Read More
 WIMBO MPYA WA MEJJA WAFUTWA YOUTUBE

WIMBO MPYA WA MEJJA WAFUTWA YOUTUBE

Staa wa muziki nchini Mejja amepata pigo nyingine mara baada ya video ya wimbo wake mpya uitwao Maisha tiki kufutwa kwenye mtandao wa youtube. Video ya wimbo huo umeondolewa kwenye mtandao huo siku chache baada ya mejja kuweka wazi kwamba kuna mtu amewasilisha lalama ya hakimili dhidi ya wimbo wake huo kwa uongozi wa youtube. Mejja aliachia wimbo huo Ijumaa wiki iliyopita kusherehekea hatua ya rais uhuru kenyatta kuondoa kafyu na wakati ulifutwa kwenye mtandao wa youtube ulikuwa umefikisha zaidi ya views laki moja. Hata hivyo mashabiki zake kwenye mitandao ya kijamii wameelezea kusikitishwa na kasumba ya watu ambao wamekuwa na mazoea ya kuripoti na kudai umiliki wa nyimbo za Mejja kwenye mtandao wa Youtube huku wakitaka bodi zinazosimamia kazi za wasanii kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaoendeleza kadhia hiyo. Huu sio wimbo wa kwanza kwa mejja kushushwa kwenye mtandao wa YouTube kwani mwezi Juni mwaka huu, nyimbo zake mbili, ‘Tabia za Wakenya’ na ‘Naitwa Mejja’ aliomshirikisha Nasha Travis pia ziliondolewa kwenye mtandao wa YouTube kwa madai ya hakimiliki.

Read More
 OLE GUNNAR BADO YUPO MAN UNITED LICHA KIPIGO CHA 5-0

OLE GUNNAR BADO YUPO MAN UNITED LICHA KIPIGO CHA 5-0

Kocha wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kuendelea kuifundisha klabu hiyo licha ya tetesi za kutimuliwa kushamiri huku Antonio Conte akihusishwa kumrithi. Haya yote yanajiri baada ya kipigo walichokipokea Man Utd juzi Jumapili kutoka kwa Liverpool cha mabao 5-0, dimbani Old Trafford. Ripoti mpya kutoka Sky Sports, inaelezwa kuwa, Uongozi unatarajia kujikita zaidi katika kuboresha hali iliyopo kuliko kumtimua kocha Ole Gunnar Solskjaer.

Read More
 JACK HARLOW ATANGAZA KUWASAINISHA WANAWAKE MKATABA KABLA YA KUTOKA NAO

JACK HARLOW ATANGAZA KUWASAINISHA WANAWAKE MKATABA KABLA YA KUTOKA NAO

Rapa kutoka nchini Marekani Jack Harlow ameweka wazi kwamba ataanza kuwasainisha Wanawake mikataba maalum ya makubaliano kabla ya kuingia penzini. Akizungumza na Jarida la GQ, Jack Harlow amesema itabidi mwanamke asaini makubaliano hayo (Non-disclosure agreement) kwa ajili ya kutoanika mtandaoni kitu chochote ambacho kitafanyika baina yao wakiwa kwenye mahusiano. Jambo kama la ujumbe mfupi wa maandishi ambao watakuwa wakitumiana kwenye simu, ubaki kuwa siri kati yao na sio kwa ajili ya kwenda mitandaoni. Aidha amesema mwanamke ambaye hatapenda kusaini mkataba huo, hatopata nafasi ya kuwa naye.

Read More
 20 PERCENT AMJIBU HARMONIZE

20 PERCENT AMJIBU HARMONIZE

Hatimaye ahadi ya Harmonize ya kuingia studio na kufanya kolabo na 20 percent pindi tu akitua Tanzania kutoka nchini Marekani imepokelewa kwa mikono miwili na mkali huyo wa zamani. 20 Percent ametumia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram kumjibu Harmonize kuwa “Promise is like a debt”  kwa maana yupo tayari hivyo Harmonize atimize alichokiahidi. 20 percent ambaye ni mshindi wa tuzo tano za Kili Music Awards mwaka wa 2010, aliwahi kutamba na ngoma kama Maisha ya Bongo, Mama Neema, Money Money, Tamaa Mbaya na nyingine kibao. Haya yanajiri baada ya usiku wa kuamkia Oktoba 25 kuwa mrefu sana kwa harmonize ambaye alionekana akiburudika na midundo ya 20 Percent na kupelekea kutoa ahadi ya kufanya nae kolabo, sambamba na kueleza kuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.

Read More
 ALBUM YA AZAWI “AFRICAN MUSIC” YACHAPISHWA KWENYE BANGO LA NEW YORK TIMES

ALBUM YA AZAWI “AFRICAN MUSIC” YACHAPISHWA KWENYE BANGO LA NEW YORK TIMES

Nyota  wa muziki nchini Uganda Azawi anazidi kuchana mbuga kimataifa hii baada ya cover ya album yake mpya iitwayo “African Music” kutumika kama art work ya chati  ya new york times  billboard ya nchini Marekani. Kupitia ukurasa wake wa instagram Azawi amewatarifu mashabiki zake  taarifa hiyo njema kwa kushare picha ikionyesha picha yake ambayo ilikuwa imechapisha kwenye chati ya new york times square billboard huku akiwashukuru mashabiki zake ambao wamemshika mkono hadi akafikia mafanikio hayo. Hata hivyo Azawi anakuwa msaani wa pili  kutoka Uganda album yake kutumika kama cover kwenye chati hiyo kubwa ya muziki nchini marekani baada ya Eddy Kenzo. Mafanikio hayo yanakuja siku chache baada ya Azawi kutajwa kwamba atakuwa miongoni mwa wasanii nne wataowakilisha afrika kwenye mpango wa YouTube Black Voice Music  mwaka wa 2022 unaolenga kuhamasisha wasanii, waandishi wa nyimbo,na maprodyuza kote duniani kuhusu namna ya kuboresha kazi zao za sanaa. Ikumbukwe new york times square billboard wamekuwa na utaratibu wa kutumia picha za mastaa wa muziki ambao ngoma zao zinaongoza kwa mauzo kwenye mitandao mbali mbali ya kusikiliza muziki duniani.

Read More
 NAIBOI ATANGAZA TAREHE YA KUACHIA OTERO EP

NAIBOI ATANGAZA TAREHE YA KUACHIA OTERO EP

Mkali wa muziki nchini Naiboi ametoa taarifa muhimu kwa mashabiki zake kuhusiana na ujio wa EP yake iitwayo Otero EP. Akipiga stori na pulse Naiboi amethibitisha EP yake mpya Otero itatoka rasmi Oktoba mwaka huu ikiwa na jumla ya mikwaju kumi ya moto. Awali EP hiyo ilikuwa itoke Oktoba 8 mwaka huu, lakini ilishindikana kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wa Naiboi. Taarifa ya ujio wa Otero EP inakuja wiki kadhaa baada ya naiboi kufunguka kuhusu ukimya wake kwenye muziki akisema kuwa uongozi wake ulikuwa kizingiti kwake kuachia project mpya ikizingatiwa kuwa ana zaidi nyimbo 800 ambazo amesharekodi.

Read More
 MAANDY AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA BREEDER LW.

MAANDY AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA BREEDER LW.

Msanii wa muziki nchini Maandy amekanusha kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na rapa Breeder Lw. Akiwa kwenye moja ya interview Maandy amesema haoni shida yeyote rapa huyo akimzimia kimahusiano ila hawezi chumbiana naye kwani mitindo yao ya maishi ni tofauti. Hata hivyo hitmaker huyo wa Sirudi Home amewataka mashabiki kutofuatilia sana maisha yake ya mahusiano na badala yake waelekeze nguvu zao kwenye muziki wake. Kauli ya mrembo huyo imekuja mara baada ya watu kumhusisha kuwa anatoka kimapenzi na breeder lw kutokana na collabo nyingi ambazo wamezifanya kwa pamoja. Maandy alianza muziki mwaka wa 2016 chini ya lebo ya muziki ya Chuo records ambapo ameenda mbali zaidi na kuachia hits kama Pon  It, Shash na nyingine kibao.

Read More