KRG THE DON AFUNGUA SHAURI LA TALAKA MAHAKAMANI

KRG THE DON AFUNGUA SHAURI LA TALAKA MAHAKAMANI

Msanii wa muziki wa dancehall nchini KRG The Don amefungua shauri la talaka mahakamani dhidi ya mke wake Linah Wanjiru, shauri hilo limefunguliwa katika Mahakama ya Milimani Jijini Nairobi. KRG ameweka wazi hilo kupitia instagram page yake baada ya kupost  nyaraka za kisheria kuhusiana na mchakato wa talaka na kusindikiza na caption inayosomeka “kwa wale waliyokuwa wanachukulia kwa mzaha, poleni” Hitmaker huyo Giddem alifunga ndoa na mke wake huyo mwaka wa 2014 na wamejaliwa kupata wawili kwa pamoja. Hatua ya KRG kufungua shauri la talaka dhidi mke wake inakuja siku chache baada ya kumsuta vikali mke wake huyo kwa madai ya kujihusisha sana na anasa na kusahau kuwahudumia watoto wao.

Read More
 MOTOROLA YATAMBULISHA TEKNOLOJIA YAKE MPYA YA “SPACE CHARGING”

MOTOROLA YATAMBULISHA TEKNOLOJIA YAKE MPYA YA “SPACE CHARGING”

Motorola imetambulisha teknolojia yake mpya ya “Space Charging” ambayo ipo katika kifaa ambacho kinaweza kuchaji simu nne kwa pamoja katika umbali wa mita tatu. Charging system mpya ya Motorola ina uwezo wa kuchaji simu kwa over-the-air wireless kama ilivyo teknolojia ya Xiaomi Mi Air Charge iliyotoka mwaka huu. Ni teknolojia ambazo zinachaji simu ikiwa karibu na kifaa cha kuchaji kwa mita tatu. Unachaji simu kama unavyotumia Internet au Bluetooth, hakuna ulazima wa kuchomeka cable au kuiweka katika wireless charge ya karibu. Mfumo huu bado upo katika majaribio, itahitajika kukaguliwa na kuhakikisha hakuna madhara kiafya kwa sababu umeme unapita hewani na inaweza kuwa na madhara kiafya.

Read More
 BUCHAMAN ATOA WITO KWA SERIKALI YA UGANDA KUMLIPIA KODI

BUCHAMAN ATOA WITO KWA SERIKALI YA UGANDA KUMLIPIA KODI

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Buchaman alifurushwa nyumbani kwake mapema wiki iliyopita kutokana na malimbikizi ya kodi ya zaidi ya miezi sita. Kutokana na hilo Mwanamuziki huyo kwa sasa ametoa wito kwa serikali ya uganda kumnusuru kwani hana matumaini kama atapata pesa za kulipa kodi bila usaidizi wa serikali. Buchaman ameenda mbali zaidi na kusema  kuwa biashara zake zote ziliathiriwa na msala wa corona, hivyo hana chanzo kingine cha kumuingizia kipato ikizingatiwa kwamba hapati tena riziki kutoka kwa muziki wake kwani tasnia ya muziki nchini uganda bado imefungwa. Buchaman kwa sasa na familia yake wamekita kambi kwa rafiki yake eneo la Luwaffu, viungani mwa jiji la Kampala. Hii sio mara ya kwanza kwa mtu mzima Buchaman kwenye nyumba za kupanga,kwani kipindi cha nyuma alifukuzwa kwa nguvu kwenye nyumba aliyokuwa akiishi huko Namungo, nchini Uganda baada ya kushindwa kulipa kodi.

Read More
 HARMONIZE ATANGAZA TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

HARMONIZE ATANGAZA TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva Harmonize hatimaye ameiweka wazi tarehe ya kuiachia album yake mpya iitwayo “High School”. Album hiyo ambayo ilipaswa itoke mwezi huu wa haitotoka kutokana na sababu mbalimbali hivyo imesogezwa mbele hadi Novemba 5 mwaka huu. Hii ni habari njema kwa mashabiki wa mkali huyo wa “Teacher” ambao wanaisubiri “High School album” kwa hamu kubwa. Ikumbukwe, hii inaenda kuwa album ya pili kwa mtu mzima Harmonize baada ya “Afro East” iliyotoka mwezi Machi mwaka wa 2020.

Read More
 RAPA KODAK BLACK AZUA MJADALA BAADA YA KUMSHIKA MAMA YAKE MZAZI MAKALIO

RAPA KODAK BLACK AZUA MJADALA BAADA YA KUMSHIKA MAMA YAKE MZAZI MAKALIO

Rapper kutoka nchini Marekani, Kodak black ameingia kwenye headlines na kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa video clip inayo muonesha akicheza na mama yake katika mtindo usiopendeza. Katika video hiyo Kodak anaoneka akicheza na mama yake mzazi, kwenye sherehe ya Birthday yake huku akimshika mama yake mzazi makalio (yaani kama anacheza na demu wake hivi) na kuendelea kufanya ujinga mwingi kwa kutaka pia kumkiss mdomoni. Kitendo hiki kimeibua mijadala na kuteka hisia za watu mbalimbali duniani, wengine wakidai Kodak amefanya udhalilishaji wa kijinsia kwa mama yake mzazi.

Read More
 GLORIA MULIRO AFUNGA NDOA NA PASTA EVANS SABWAMI.

GLORIA MULIRO AFUNGA NDOA NA PASTA EVANS SABWAMI.

Msanii wa nyimbo za injili nchini Gloria  Muliro amefunga  rasmi ndoa na mchumba wake wa siku nyingi Evans Sabwami kwenye hafla ya siri iliyohudhuriwa na wanafamilia huko New York chini Marekani. Hii imekuja wiki chache zilizopita baada ya kumvisha pete mchumba wake Evans Sabwami ambapo walienda mbali zaidi na kufunga ndoa ya kitamaduni maarufu kama ruracio mjini Eldoret, kaunti ya Uasin Gishu. Gloria Muliro ameshare picha ya harusi yao kwenye ukurasa wa instagram na kuweka wazi kuwa wao ni mke na mume. Picha hizo za Gloria Muliro na mpenzi wake Evans Sabwami imeibua hisia za mashabiki wake na mastaa wenzake ambao wameenda mbali na kumpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo kubwa maishani. Hii ni ndoa ya pili kwa Gloria Muliro, awali alikuwa kwenye ndoa  na pastor eric ambapo walidumu kwenye ndoa kwa takriban miaka sita lakini walikuja wakaaachana rasmi mwaka wa 2015 baada ya ndoa yao kuingiwa na ukungu.

Read More
 EDY SHEERAN AINASA COVID-19

EDY SHEERAN AINASA COVID-19

Mwanamuziki kutoka nchini Uingereza Edy Sheeran ametangaza kunasa virusi vya Covid-19 ikiwa ni siku chache zimebaki kabla ya kuachia Album yake ya nne inayokwenda kwa jina la Equals Edy Sheeran ametoa taarifa hiyo kupitia ukursa wake wa Instagram ambapo ameandika “Ndugu zangu ningependa kuwajuza kuwa nimepimwa na kukutwa na Covid-191. Kwa hiyo kwa sasa nimejitenga kama vile utaratibu wa serikali unavyosema. Hii inamaana kuwa kwa sasa siwezi kufanya mambo yangu binafsi. Kwahiyo nitafanya mahojiano na kutumbuiza nikiwa nyumbani. Naomba radhi kwa yeyote niliyemkwaza”

Read More
 BEKA FLAVOUR: SIENDEKEZI UTIMU KWENYE MUZIKI WANGU

BEKA FLAVOUR: SIENDEKEZI UTIMU KWENYE MUZIKI WANGU

Mwanamuziki wa Bongofleva, Beka Flavour amedai haweza kujihushisha na timu yoyote katika muziki huo ili kunufaika na mashabiki wa timu fulani kwani yeye anatengenezea kazi nzuri ambazo anajua zinaweza kupendwa na wote. Beka Flavour amesema anafanya muziki mzuri kwa ajili ya mashabiki wake ambao wapo naye kwa ajili ya ubora wa kazi zao na sio timu ambazo kamwe hawezi kujiunga nazo. Kwa miaka ya hivi karibuni wasanii Alikiba na Diamond Platnumz wamekuwa ni washindani wakubwa ambao wametengeneza timu ambazo hadi baadhi ya wasanii wengine wamejiunga nazo. Ikumbukwe Beka Flavour alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliokuzwa na kituo cha Mkubwa na Wanawe chake Mkubwa Fella, na chini ya kundi la Yamoto Band ambalo lilikuwa linaundwa na wasanii Aslay, Enock Bellla na  Mbosso ambaye alichukuliwa na lebo ya WCB Wasafi yake Diamond.

Read More
 BAHATI APEWA TUZO BOOMPLAY

BAHATI APEWA TUZO BOOMPLAY

Nyota wa muziki nchini Bahati ametunukiwa tuzo ya silver Plaque na mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa boomplay Kenya. Hii ni baada hitmaker huyo wa “Pete yangu” kufikisha zaidi ya streams millioni 8 kupitia nyimbo zake zote zilizopakiwa kwenye mtandao  huo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram bahati amewashukuru mashabiki zake kwa kuendelea kufuatilia kazi zake ambazo zinazidi kuonyesha mafanikio makubwa ndani na nje ya Kenya. Tuzo hizo maarufu kama ‘Boomplay Plaques’ hutolewa kutambua jitihada za wasanii wanaofanya vizuri kwenye App ya Boomplay.

Read More
 KESI YA CARDI B KUWASHUSHIA KICHAPO WAHUDUMU WA CLUB KUSIKILIZWA LEO

KESI YA CARDI B KUWASHUSHIA KICHAPO WAHUDUMU WA CLUB KUSIKILIZWA LEO

Rapa kutoka Marekani Cardi B  yuko hatarini kufungwa miaka minne  jela kufuatia mashtaka mawili yanayomkabili,ya kuwapiga na kuwafanyia fujo wahudumu wawili wa club iitwayo Angels-Strip-Club Mwaka 2018 Cardi B alikamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa makosa hayo mawili lakini mwaka wa 2019 alikanusha kwenye mahakama kuu ya queens akiwa kizimbani kwa kumwambia hakimu kuwa hana hatia Inadaiwa Cardi B alitoa maelekezo kwa wasaidizi wake kuwapiga wahudumu hao wawili wa klabu hiyo  na baadaye yeye pia alishiriki kutembeza kipigo, kurusha viti na kupasua chupa mara baada ya kusikia kuwa mmoja kati yao alitoka kimapenzi na mumewe Offset. Hata hivyo usikilizaji wa kesi hiyo umepangwa kufanya oktoba 25, mwaka huu na endapo rapa huyo atakutwa na hatia ya makosa yote mawili basi kifungo cha miaka minne  jela kitamhusu

Read More
 WEASEL AFUNGUKA KWA MARA KWANZA KUHUSU KUMPIGA MFANYIKAZI WAKE WA NYUMBANI

WEASEL AFUNGUKA KWA MARA KWANZA KUHUSU KUMPIGA MFANYIKAZI WAKE WA NYUMBANI

Mwanamuziki kutoka Uganda Douglas Mayanja maarufu kama Weasel Manizo kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya kile kilichotokea kati yake na mfanyikazi wake wa nyumbani ambaye aliripotiwa kupigwa na msanii huyo. Akiwa kwenye moja ya Interview, Weasel amekanusha kumshushia kichapo mfanyikazi wake wa nyumbani huku akisema kwamba alisikia uvumi huo kutoka kwa vyombo vya habari na majukwaa mengine. Hitmaker huyo wa “Magnetic” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa vyombo vya habari vilirusha taarifa hiyo bila kujua kiini cha kupigwa kwa mfanyikazi wake wa nyumbani. Hata hivyo amesema licha ya mfanyikazi wake wa nyumbani kueleza upande wake wa stori,anasubiri apate nafuu ili aweze kuweka wazi kilichotokea kati yao kwa kina.

Read More
 DIAMOND AINGIA STUDIO NA MOHAMMED RAMADAN KUANDAA WIMBO WA PAMOJA

DIAMOND AINGIA STUDIO NA MOHAMMED RAMADAN KUANDAA WIMBO WA PAMOJA

Mwanamuzi kutoka Tanzania,Diamond Platnumz ameingia studio kurekodi wimbo na staa wa muziki kutoka nchini Misri, Mohamed Ramadan. Diamond ameingia studio na staa huyo ambaye ni mbabe wa youtube afrika kwa upande wa wasanii kwani anazaidi ya subscribers zaidi ya milioni 13.3 kwenye mtandao huo huku akiwa amevuna jumla ya watazamaji zaidi ya bilioni 4.3 kwenye mtandao huo wa youtube. Diamond na Mohamed wamekutana jijini Dubai ambapo wote walikuwa wamealikwa kwenye tamasha la All Africa Festival lililofanyika usiku wa kuamkia October 22,mwaka wa 2021. Ikumbukwe Diamond Platnumz ndiye alikuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki na kati kufikisha jumla ya watazamaji bilioni 1 kwenye mtandao wa youtube lakini pia ndiye msanii mwenye subscribers wengi kwa wasanii wa wanaopatikana kusini mwa Jangwa la Sahara.

Read More