KHALIGRAPH JONES AGOMA KUTOA MATUMIZI KWA MTOTO WAKE

KHALIGRAPH JONES AGOMA KUTOA MATUMIZI KWA MTOTO WAKE

Aliyekuwa mpenzi wa msanii Khaligraph Jones,Cashy ameshambulia mwanamuziki huyo akidai kuwa amhudumii mtoto wake wa kiume aliyezaa naye mwaka wa 2018 pindi tu walipoachana. Cashy ameshukuru kufunguliwa kwa nchi ambapo amesema kuwa itakuwa afueni kwa wasanii kupata angalau matamasha ya kuwaingizia pesa kwani wengi wao walikuwa wanategemea matamasha kupata riziki. Kutokana na hilo amesema Papa Jones hatakuwa na sababu zingine za kuepuka majukumu ya kumlea mwanawe mwenye umri wa miaka mitatu kwa sasa ikizingatiwa kuwa tangu ujio wa Corona rapa huyo amekuwa akidai kuwa hakuwa na pesa za kumhudumia mwanae. Hata hivyo khalighraph jones hajetoa tamko kuhusiana na madai yaliyoibuliwa na baby mama wake kuwa amemtelekeza mtoto wake

Read More
 “CRYPTO” WALLET MPYA YA FACEBOOK YAANZA KUFANYA KAZI

“CRYPTO” WALLET MPYA YA FACEBOOK YAANZA KUFANYA KAZI

Baada ya Facebook kusumbuliwa na fedha ya kidigitali ya Libra, iliamua kuipa jina la “Diem” na kuwekeza katika kutengeneza Wallet ya Novi ambayo itatumika kutuma na kupokea fedha na itaunganishwa na crypto, metaverse, mfumo wa matangazo, na apps za Instagram, Facebook na WhatsApp ambapo watumiaji wataweza kutuma na kupokea fedha bure kwa urahisi. Kwa sasa Wallet (pochi ya kidigitali) ina crypto (stable coin) ya Paxos Dollar ambayo ina thamani sawa na Dola. Mkuu wa Idara ya Facebook inayosimamia Novi Wallet, David Marcus amesema kuna zaidi ya watu Bilioni 1.7 ambao hawana akaunti za kibenki na zaidi ya watu Bilioni 1 hawafurahishwi na mfumo wa mabenki hasa katika makato ya kutuma na kupokea fedha. Facebook imeanza kutoa wallet yake ya Novi kuanza kutumika kwa wakazi wa Marekani na Guatemala. Novi Wallet ni wallet ya Facebook ambayo itakuwa haina makato katika kutuma na kupokea fedha. Ni salama,haikusanyi data na Facebook imejaribu kuweka umakini ili kuepusha sifa mbaya katika kusimamia mfumo huo wa kifedha. Wallet hiyo inatumia coin ya Pax Dollar (USDP) na wiki hii imeshirikiana na Coinbase kuwezesha watumiaji kununua na kuuza Pax Coin kwa kutumia wallet hizo mbili. Wallet ya Novi itakuwa haina makato katika kutuma fedha, ni salama  na inatumia mifumo mikubwa ya kuthibiti usalama na urahisi kwa watumiaji. Facebook inajaribu kuifanya iwe “Wallet ya mitandao ya kijamii”.

Read More
 KALIFAH AGANAGA ADAI MUSEVENI AMESHINDWA KUTIMIZA AHADI YA KUMFADHILI KIMASOMO

KALIFAH AGANAGA ADAI MUSEVENI AMESHINDWA KUTIMIZA AHADI YA KUMFADHILI KIMASOMO

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Kalifah Aganaga amefichua kuwa Rais Museveni ameshindwa kutimiza ahadi yake aliyotoa ya kumfadhili kusomea kozi ya uhandisi wa sauti nchini Marekani. Akiwa kwenye moja ya interview, Hitmaker huyo wa “Kiboko” amesema kwamba Museveni alikubali kumfadhili kimasomo nje ya nchi walipokutana katika Ikulu ya rais mwaka wa 2020 ila kwa watu wake wa karibu wamekuwa wakimpa ahadi za uongo. Kalifah Aganaga aliigura chama cha NUP na kutimukia NRM baada ya kushindwa kupata tiketi ya chama hicho ambayo ingemsaidia kuwania ubunge wa eneo la Rubaga Kusini.

Read More
 CHRIS BROWN AMUUNGA MKONO KYRIE IRVING KUKATAA KUCHANJWA

CHRIS BROWN AMUUNGA MKONO KYRIE IRVING KUKATAA KUCHANJWA

Chris Brown amemuunga mkono mcheza Kikapu Kyrie Irving ambaye amegoma kuchanjwa chanjo ya COVID-19. Kupitia Insta Stories yake kwenye mtandao wa Instagram Chris Brown amesema ana simama na nyota huyo wa Brooklyn Nets na kumuita shujaa wa ukweli. Kyrie Irving anaendelea kuvigusa vichwa vya habari duniani kwa kuigomea chanjo ya COVID-19 ambayo imefanywa kuwa lazima kwa wana michezo wote, hivyo kuweka hatiani mustakabali wake wa kucheza kwenye ligi hiyo hasa michezo ya nyumbani kwa sheria za Jiji la New York. Staa huyo ameitaja sababu ya kugoma kuchanjwa, akisema kuwa mtu hapaswi kulazimishwa kufanya jambo lolote kwenye mwili wake, na anasimama na wote ambao wanaamini kipi ni sahihi.

Read More
 DR. DRE AFIKISHIWA NYARAKA ZA TALAKA AKIWA MAKABURINI.

DR. DRE AFIKISHIWA NYARAKA ZA TALAKA AKIWA MAKABURINI.

Sakata la kuvunjika kwa ndoa ya mtayarishaji mkongwe Dr. Dre bado linashika vichwa vya habari duniani, Sasa jipya limeibuka ambapo tovuti ya TMZ imeripoti kwamba Dre amefikishiwa nyaraka za kisheria kuhusiana na mchakato wa talaka, lakini amefikishiwa nyaraka hizo akiwa makaburini. Tunaambiwa Dr. Dre alikuwa akimzika Bibi yake ndipo mtu mmoja alipofika na karatasi hizo kisha kumshikisha Dre ambaye alikuwa amesimama kando ya Jeneza. Taarifa zinasema Dre alikasirika kuona kitendo kama hicho. Tovuti ya TMZ imebaini nyaraka hizo ambazo zilifikishwa kwa Dre zilikuwa zinahusu malipo ya mwanasheria wa aliyekuwa mke wake Bi. Nicole Young kwa ajili ya mchakato huo wa talaka. Kuna mgogoro wa malipo hayo ambapo Dre alilipa takriban shilling million 36.1 badala ya shilling millioni 175 ambayo inadaiwa kwamba Jaji alipitisha akimtaka Dr. Dre ailipe, hivyo karatasi hizo ni agizo la Jaji.

Read More
 MARIOO MBIONI KUJA NA “I’AM MARIOO TOUR”

MARIOO MBIONI KUJA NA “I’AM MARIOO TOUR”

Hitmaker wa Beer Tamu, Marioo ametangaza ujio wa tour yake nchini Tanzania aliyoipa jina la “I’am Marioo tour.” Marioo ameweka wazi ujio wa tour yake hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwaachia mashabiki swali kupendekeza ni mkoa gani nchini Tanzania ambao asiache kukanyaga kwenye tour yake hiyo. Pamoja na kuweka wazi ujio wa tour yake hiyo marioo hajagusia endapo kuna wasanii wengine ambao anatarajia kushirikiana nao kwenye tour hiyo au atakuwa mwenyewe tu. Kauli ya marioo inakuja siku chache baada ya kuwatolea uvivu wasanii wa bongo fleva kwa kuwaita wanafiki pale linapokuja suala la kupeana michongo ya kufanikiwa kwenye muziki

Read More
 WILLY PAUL AHIRISHA TENA TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

WILLY PAUL AHIRISHA TENA TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki nchini Willy Paul ametangaza hataachia album yake mpya iitwayo “The African Experience” kama ilivyokuwa imepangwa. Kupitia ukurasa wake wa instagram Willy Paul amesema hatua ya kuahirisha kutoka kwa album hiyo ni fursa nzuri kwake kujiandaa vilivyo na kuwapa mashabiki wake kazi nzuri. Hata hivyo, bosi huyo wa Saldido records hajasema album hiyo itatoka lini na ni mabadiliko yapi anayafanya. African Experience album ambayo ilipaswa kutoka oktoba 22  ikiwa ni exclusive kwenye jukwaa la boomplay, ina jumla ya nyimbo 17, ikiwa na kolabo 5 pekee kutoka kwa wakali kama Juma Jux, Eddy Kenzo,Daphne,Fik Fameica na Kelly Khumalo

Read More
 BROWN MAUZO AACHIA RASMI V ALBUM

BROWN MAUZO AACHIA RASMI V ALBUM

Mwanamuziki kutoka Kenya Brown Mauzo ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la V. V album imebeba jumla ya mikwaju 12 ya moto huku ikiwa na kolabo 5 pekee. Brown Mauzo amewashirikisha wasanii mbali mbali kama Masauti, Baraka the Prince,Ndovu Kuu, Mwasi, na Kaa La Moto. Kupitia ukurasa wake wa Instagram mauzo amesema ameachia album yake ya v kama zawadi kwa mke wake Vera Sidika ambaye juzi kati amejifungua mtoto wa kike aitwaye Princess Asia Brown. Album ya “V” ni album ya pili kwa mtu mzima Brown Mauzo baada ya Nitulize ya mwaka wa 2019. Hata hivyo Album hiyo inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya  kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay.

Read More
 LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 23,ALIZALIWA STAA WA MUZIKI WA RNB KUTOKA MAREKANI, MIGUEL.

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 23,ALIZALIWA STAA WA MUZIKI WA RNB KUTOKA MAREKANI, MIGUEL.

Siku kama ya leo Oktoba 23 mwaka wa 1983 alizaliwa Staa wa muziki wa RnB kutoka Marekani Miguel. Jina lake halisi ni Miguel Jontel Pimentel na alizaliwa huko San Pedro, Carlifonia nchini Marekani ambako alianza muziki akiwa na umri wa miaka 13 lakini alikuja kupata umaarufu zaidi nchini Marekani mwaka wa 2010 alipoachia album yake ya kwanza iitwayo “All I Want isYou” chini ya lebo ya muziki ya Jive Records Baada ya lebo ya muziki ya Jive Records kuvunjwa,miguel alisaini mkataba wa kufanya kazi na lebo ya muziki ya RCA Records ambayo ilisimamia shughuli zote za album yake ya pili iitwayo Kaleidoscope Dream ya mwaka wa 2012. Mwaka wa 2015 Miguel aliachia album yake ya tatu iitwayo Wildheart ikafuatwa na album yake ya nne inayokwenda kwa jina la “War & Leisure” ya mwaka wa 2017. Hata hivyo tangu aanze muziki miguel ameshafanya jumla ya album nne za muziki,Singles 21,Mixtape nne,na EP nne. Kutokana na mafanikio yaliyopata kwenye muziki wake, Miguel ameteuliwa kunawania tuzo 41 za muziki nchini Marekani na ameshinda tuzo saba za muziki ikiwemo tuzo moja ya Grammy,tuzo mbili za BET Awards, na tuzo nne za Soul Train Music Awards.

Read More
 CATHERINE KUSASIRA AFUNGUKA SABABU ZA KUUZA GARI LAKE

CATHERINE KUSASIRA AFUNGUKA SABABU ZA KUUZA GARI LAKE

Mwanamuziki Catherine Kusasira aliuza gari lake aina ya Toyota Land cruiser V8 ambalo alizawadiwa na rais Yoweri Museveni. Inadaiwa kuwa mwanamama huyo aliuza gari lake kwa sababu alikuwa anaandamwa na madeni. Sasa akiwa kwenye moja ya interview Catherine Kusasira amejitokeza na kukanusha madai kuwa aliuza gari lake kutokana na madeni. Hitmaker huyo “I love you” amesisitiza kwamba alipiga mnada gari  lake kwa sababu watu wake wa karibu walikuwa wanamuonea wivu. Mwimbaji huyo wa zamani wa lebo ya muziki ya Eagles productions amedai kuwa kuna baadhi ya watu waliibua madai hayo kumuaharibia jina kwa sababu anamuunga mkono Rais Museveni. Hata hivyo Amethibitisha kuwa tayari ameagiza  gari jipya aina toyota SUV ambayo haitawafanya watu wawe na wivu

Read More
 JUMA NATURE ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA ALBUM YAKE MPYA

JUMA NATURE ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA ALBUM YAKE MPYA

Msanii mkongwe wa Bongofleva, Juma Nature amesema anajiandaa kuachia albamu yake mpya ambayo imekamilika. Nature amesema anachokifanya kwa sasa ni kutayarisha video kadhaa za nyimbo zinazopatikana kwenye albamu hiyo kabla ya kuingia sokoni hivi karibuni. Hata hivyo Sir Nature hajatuambia jina la album, idadi nyimbo na wasanii aliyowashirikisha kwenye album yake hiyo ila ni jambo la kusubiriwa. Utakumbuka Juma Nature ana historia ya kuwa msanii wa kwanza Bongo kuujaza ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam katika uzinduzi wa albamu yake iitwayo Ugali. Wasanii wengine tanzania ambao tayari wametangaza kukamilika kwa albamu zao ni pamoja na Diamond Platnumz, Harmonize, Marioo, Young Lunya, Lava Lava, Tommy Flavour, Maua Sama, Ommy Dimpoz na wengine wengi.

Read More
 LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 22, ALIZALIWA STAA WA MUZIKI DANCEHALL & REGGAE, SHAGGY

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 22, ALIZALIWA STAA WA MUZIKI DANCEHALL & REGGAE, SHAGGY

Siku kama leo Oktoba 22 mwaka wa 1968 alizaliwa mkali wa Miondoko ya Regge na Dancehall, ambaye pia ni Muigizaji na DJ kutoka Nchini Jamaica, Shaggy. Jina lake halisi ni orville Richard Burell na alizaliwa huko Kingston, nchini Jamaica  ambako alianza muziki mwaka wa 1993 alipoachia  album yake wa kwanza iitwao “Pure Pleasure” ikafuatwa na Original Doberman ya mwaka 1994,Boombastic ya mwaka wa 1996 na Midnite Love ya mwaka wa 1997. Mwaka wa 2000 Shaggy aliachia album yake ya tano iitwayo “HOT SHOT”,album ambayo ilifanikiwa kufika viwango vya mauzo ya Platnumz Mara Sita nchini Marekani lakini  pia ilishika namba moja kwenye  chati ya Billboard Hot 200 japo album zake zilizofuata za Lucky Day ya mwaka wa 2002 na Clothes Drop zilishindwa kufikia mafanikio ya Album ya Hotshot. Hata hivyo tangu aanze muziki mwaka wa 1993 Shaggy ameshafanya jumla ya  12 za muziki, Singles 88 na album 7 za nyimbo zilizotoka pamoja na zile hazikutoka. Kutokana na mafanikio aliyoyapata kwenye muziki wake, Shaggy ameteuliwa kuwania kwenye tuzo mbali mbali na ameshinda tuzo mbili za Grammy kupitia album yake  ya Boombastic ya mwaka wa 1996 na 44/876. Kando na muzik,i Shaggy amewahi kuwa mwanajeshi wa majini nchini Marekani kabla hajeanza muziki lakini pia ni muigizaji kwani ameigiza kwenye filamu nyingi nchini Marekani ikiwemo Blast ya mwaka wa 2004 Game Over Man ya mwaka wa 2018, American Idol ya mwaka wa 2019 na nyingine kibao. Shaggy anakadiriwa kuwa na utajiri wa Dolla Milioni 12, mafanikio ambayo aliyapata zaidi kupitia albums za BOOMBASTIC na HOTSHOT.

Read More