PENZI LA WEEZDOM NA MYLEE STAICEY LAVUNJIKA RASMI

PENZI LA WEEZDOM NA MYLEE STAICEY LAVUNJIKA RASMI

Msanii Weezdom  hatimaye amethibitisha kuwa yeye na  mpenzi wake wa siku nyingi Mylee Staicey sio wapenzi tena. Katika kikao cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wa Instagram, shabiki mmoja alimuuliza msanii huyo kama bado ni wapenzi na  Mylee Staicey na ndipo  alipoweka wazi kuwa waliachana zamani. Kutokana na hilo kama ulikuwa unadhani penzi la weezdom na Stacey lilikuwa limefufuka miezi miwili iliyopita nikuambie tu pole kwani ni wazi kuwa penzi lao limeingiwa na ukungu. Hata  hivyo, bado haijebainika kama kuna ukweli wowote kuhusu stori za wawili hao kuachana ila jambo la kusubiriwa. Itakumbukwa taarifa za wawili hao kuachana zilianza kusambaa mitandaoni mwaka wa 2020 ambapo ilidaiwa kuwa weezdom na mchumba wake stacey wamevunja  penzi lao kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutoaminiana

Read More
 TIWA SAVAGE AFUNGUKA JUU YA VIDEO YAKE YA NGONO ILIYOVUJA MTANDAONI

TIWA SAVAGE AFUNGUKA JUU YA VIDEO YAKE YA NGONO ILIYOVUJA MTANDAONI

Baada ya kutangaza mwenyewe kuvuja kwa mkanda wa Video yake ya ngono ikumuonesha akiwa n mpenzi wake wa sasa, mwanamuziki wa kike kutoka nchini Nigeria Tiwa Savage sasa amebainisha kuwa hamtoweza kuziona tena video zake za ngono. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram na kauli aliyo izungumza wakati wa performance yake huko nchini Nigeria imebainisha hilo, huku baadhi ya watu wakiielezea kuwa ameitumia jambo hilo kama Kiki kwa ajili ya kutangaza wimbo wake mpya wa Somebody’s Son alio mshirikisha msanii wa Marekani, Brandy.

Read More
 KENDRICK LAMAR MBIONI KUKATA KIU YA MASHABIKI ZAKE

KENDRICK LAMAR MBIONI KUKATA KIU YA MASHABIKI ZAKE

Mkali wa michano kutoka Marekani Kendrick Lamar anaweza kudondosha album yake mpya kesho Ijumaa. Hii imekuja kufuatia kuvuja kwa ngoma iitwayo “Therapy Session 9” lakini pia mabadiliko ya picha ya Kendrick Lamar kwenye mtandao wa Spotify. Ni miaka minne tangu Kendrick Lamar asikike kwa upana kwenye masikio ya mashabiki zake kupitia album yake ya mwisho iitwayo DAMN iliyotoka mwaka 2017. Hivi karibuni alikuja na tamko la ujio wa album mpya na ya mwisho kwenye label yake ya Top Dawg Entertainment ambayo aliitumikia kwa miaka 17.

Read More
 INSTAGRAM KUWEKA SEHEMU YA KUPOST KATIKA TOVUTI YAKE

INSTAGRAM KUWEKA SEHEMU YA KUPOST KATIKA TOVUTI YAKE

Mtandao wa Instagram unatarajiwa kuweka uwezo wa kupost kwa kutumia tovuti ya Instagram katika kompyuta. Watumiaji wa kompyuta watakuwa na uwezo wa ku-upload videos na picha katika akaunti za Instagram kwa kupitia website ya Instagram. Hii ni feature ambayo watu wengi sana wanaihitaji hasa Account Managers na watu ambao wanatumia kompyuta katika shughuli mbalimbali. Badala ya ku-copy content kwenye simu ili utumia app ya Instagram katika simu, watu watakuwa na uwezo wa kutumia kompyuta kupost Instagram. Feature hii imechelewa sana kuwekwa kwa kampuni ya facebook imekuwa iki-promote app ya Instagram. Facebook imekuwa na full-features katika tovuti  yake lakini bado haikuweka feature ya kupost katika tovuti ya Instagram. Feature hii inaanza kutoka wiki hii kwa baadhi ya watumiaji  ila itatoka taratibu kwa watumiaji wote wa tovuti ya Instagram.

Read More
 WILLY PAUL ATOA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

WILLY PAUL ATOA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki nchini Willy Paul amewapa mashabiki wake orodha nzima ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya  “The African Experience”. “The African Experience” ina jumla ya nyimbo 17, ikiwa na kolabo 5 pekee kutoka kwa wakali kama Juma Jux, Eddy Kenzo,Daphne,Fik Fameica na wengine. Hitmaker huyo wa “Lenga” anatarajiwa kuiachia album hiyo wakati wowote kuanzia sasa kwani ni saa chache tu zimesalia.. Hata hivyo Willy Paul tayari ameachia video ya wimbo mmoja kutoka kwenye album hiyo ambao ni “Ogopa Wasanii”, wimbo namba 11.

Read More
 LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 21, ALIZALIWA MWANASOKA WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED NEMANJA VIDIC

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 21, ALIZALIWA MWANASOKA WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED NEMANJA VIDIC

Siku kama ya leo Oktoba 21 mwaka wa 1981 alizaliwa mwanasoka wa zamani wa Serbia na klabu ya Manchester United, Nemanja Vidic. Vidic alizaliwa huko titovo Yugoslavia ambako alianza soka katika klabu ya Red Star Belgrade  mapema miaka ya 2000 kabla ya kujiunga  ya Sparta Moscow ya nchini Urusi mwaka wa 2004. Akiwa Sparta Moscow Namanja Vidic  alifanikiwa kuichezea klabu ya hiyo mechi 39 huku akitia kimiani magoli manne  kwa misimu miwili aliyoichezea klabu hiyo. Mwaka wa 2006 alitimukia nchini England na kuidaka saini ya klabu ya Manchester United kwa pauni millioni 7 ambapo aliisaidia klabu hiyo kutwaa mataji matano ya Premier,taji la klabu Bingwa Barani Ulaya, Kombe la Fifa na makombe 6 ya Ngao ya Jamii. Akiwa Manchester, Vidic alifanikiwa kuichezea klabu hiyo mechi 211 huku akifunga magoli 15 kwa misimu minane aliyoitumikia klabu ya Manchester United. Baada ya kutumikia klabu ys Manchester United kwa miaka minane Vidic alijiunga na klabu ya Inter Milan inayoshiriki ligi kuu nchini Italia kwa uhamisho wa bure lakini baada kuichezea klabu hiyo mechi 23 na kufanga goli moja, Namanja Vidic alitangaza kustaafu soka ya kimataifa mwaka wa 2016. Katika ngazi ya kitaifa, Namanja Vidic ameichezea timu ya taifa ya Serbia katika ngazi ya vijana na watu wazima ambapo amewaikilisha taifa lake kwenye michuano ya Euro mwaka wa 2004 na kombe la dunia mwaka wa 2006 huku akichezea mechi  56 na kufunga magoli mawili tangu mwaka wa 2002.

Read More
 AROMA ATOA POVU ZITO KWA MASTAA WAKUBWA UGANDA, ADAI WANAUA VIPAJI

AROMA ATOA POVU ZITO KWA MASTAA WAKUBWA UGANDA, ADAI WANAUA VIPAJI

Msanii wa kike kutoka nchini Uganda Aroma amesikitishwa na namna wasanii wakubwa nchini humo wanaendesha tasnia ya muziki. Akiwa kwenye moja ya interview Aroma amedai kwamba mastaa wengi nchini uganda wamehujumu kazi za wasanii chipukizi kwani wamekuwa na mazoea ya kuzihonga vyombo vya habari ili nyimbo zao zichezwe. Hitmaker huyo wa “Yoola” amesema mastaa wengi nchini uganda hawana vipaji kwani wamekuwa wakizitangaza nyimbo ambazo hazina ubora kwa kuwalipa madejaay wa vituo vya redio na runinga. Ikumbukwe pia Juzi kati wasanii kama Naira Ali na Sama Sojah aliwatolea uvivu baadhi ya wasanii wanaolipa vyombo vya habari ili kazi zao zichezwe

Read More
 ESSENCE YA WIZKID YAFIKISHA MAUZO YA PLATINUM MAREKANI

ESSENCE YA WIZKID YAFIKISHA MAUZO YA PLATINUM MAREKANI

Ngoma ya Wizkid akiwa amemshiriki Tems, Essence imefanikiwa kufikisha kiwango cha mauzo ya platinum nchini Marekani. Essence imefanikiwa kuuza jumla ya nakala milioni 1 katika nchini hiyo tangu kuachiwa kwake Oktoba 29, mwaka wa 2020. Lakini pia wimbo huo ulifikisha mauzo ya Gold Septemba 2, mwaka wa 2021 kwa kuuza jumla ya nakala laki 5  nchini Marekani. Wimbo wa Essence  ambao ni wimbo wa nne kwenye album ya ‘Made In Lagos’ iliyotoka Novemba mwaka wa 2020, unakuwa wimbo wa kwanza kutoka Nigeria kuingia kwenye rekodi hiyo nchini Marekani.

Read More
 DIAMOND ATAJWA KWENYE TUZO ZA MTV EUROPE MUSIC 2021

DIAMOND ATAJWA KWENYE TUZO ZA MTV EUROPE MUSIC 2021

Majina ya mastaa mbalimbali yametajwa kuwania tuzo za  Mtv Europe Music mwaka wa 2021 ambazo zitafanyika nchini Hungury mwishoni mwa mwaka huu. Kwenye orodha hiyo staa wa muziki kutoka Tanzania diamond platnumz ndiye msanii anayeiwakilisha Afrika Mashariki na kati. Diamond Platnumz ametajwa kwenye kipengele cha Best African Act ambapo atachuana na wakali wengine kutoka Afrika kama wizkid, tems, focalistic na amaarae kutoka nchini Ghana. Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa November 14,mwaka wa 2021 huko nchini Hungury. Justine Bieber ameongozwa kwa kutajwa kwenye vipengele vingi ambapo ametajwa kwenye vipengele nane.

Read More
 KAMPUNI YA FACEBOOK KUBADILI JINA LA BRAND YAKE

KAMPUNI YA FACEBOOK KUBADILI JINA LA BRAND YAKE

Baada ya miaka 17 ya kuwepo kwa brand kubwa ya mitandao ya kijamii; Facebook inapanga kubadilisha brand na jina lake mwisho wa mwezi huu. Tetesi zilizovuja mtandaoni zinasema kwamba Mark Zuckerberg atatambulisha jina jipya la kampuni ya Facebook Oktoba 28 katika mkutano wa Annual Connect Conference 2021. Malengo mapya ya Facebook ni kuingia katika teknolojia ya Metaverse na kuacha kuwa tu mtandao wa kijamii. Facebook ina malengo ya kukuza huduma za Instagram, WhatsApp na Uculus; kuhamia katika ulimwengu wa Virtual Reality na Augmented Reality. Facebook haitakuwa kampuni pekee ya teknolojia ambayo imebadili brand yake. Mwaka 2015, Google ilibadilisha muunganiko wa kampuni zake na kuziweka chini ya Alphabet Inc na kuacha kuwa Search Engine tu. Facebook itafanya branding mpya ya kampuni yake na kuweka malengo katika teknolojia ya metaverse ambapo watumiaji wake watawasiliana katika mitandao ya kijamii na katika virtual reality. Kampuni hiyo pia inalenga kuingia katika soko la saa, simu, VR, Metaverse na Games. Hakuna anayefahamu jina la brand mpya ya Facebook, hata wakuu na viongozi wengi wa Facebook hawajaambiwa jina la kampuni kuu ambayo itasimamia social media platform na metaverse.

Read More
 BURNA BOY ATAKA BANGI IRUHUSIWE NIGERIA, ADAI HAINA MADHARA

BURNA BOY ATAKA BANGI IRUHUSIWE NIGERIA, ADAI HAINA MADHARA

Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Burna Boy amesema kwamba ni vyema sheria ikaruhusu matumizi ya bangi nchini humo kwani haina madhara kama ambavyo wengi wanasema. Akihojiwa kwenye kipindi cha ‘Home Grown Radio’ jijini Los Angeles, Burna ameeleza kwamba watu wengi wanatumia bangi lakini hawataki kutangaza hadharini lakini kiukweli hamna madhara mabaya yoyote mtu akitumia. “Kila mtu anatumia bangi lakini hakuna anayetaka kusema au kukutwa nayo.” amesema Burna Boy. Lakini pia Hitmaker huyo wa Kilo metre amesema watu wazima na viongozi wamefanikiwa kutoa elimu kwa jamii kwamba endapo mtu akitumia bangi basi atakuwa chizi jambo ambalo yeye amelikataa na kusema kuwa ni uongo,  hivyo ni bora sheria iruhusu matumizi ya bangi.

Read More
 SHATTA WALE ATIWA MBARONI KWA KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO

SHATTA WALE ATIWA MBARONI KWA KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO

Jeshi la Polisi nchini Ghana limemtia mbaroni mwanamuziki Shatta Wale kwa madai ya kusambaza taarifa zisizo za ukweli kiasi cha kuzua hofu na taharuki kwa jamii. Oktoba 19 mwaka huu zilienea taarifa zikidai kuwa mwanamuziki huyo amepigwa risasi mitaa ya East Legon, nchini Ghana. Mtu wa karibu na rapa huyo alienda mbali zaidi na kusema kwamba Shatta Wale amekimbizwa hospitali kwa matibabu. Baada ya taharuki kubwa kwa wananchi kupitia mitandao ya Kijamii, Jeshi la Polisi lilitoa tangazo la kumtafuta Shatta Wale ambaye asubuhi ya leo alifika kituoni na kujisalimisha. Polisi wamethibitisha kukamatwa kwa Shatta Wale kwa kuandika ujumbe kwenye mtandao wa Facebook.

Read More