ZARI AVUNJA UKIMYA TAARIFA ZA KUOLEWA

ZARI AVUNJA UKIMYA TAARIFA ZA KUOLEWA

Mrembo Zari The Bosslady amewataka mashabiki wake kupuuzia taarifa zinazodai kuwa ameolewa. Zari ambaye ni baby mama wa msanii wa BongoFleva amesema picha hizo zinazodaiwa ni za ndoa yake, zimetoka kwenye kuandaa video ya msanii chipukizi wa muziki wa Injili. Utakumbuka mwaka wa 2020 ilisemekana kuwa Zari pia ameolewa na mwanaume aitwaye ‘King Bae’ lakini baadaye alikuja kuweka wazi hilo halikuwa kweli. Mwanamama huyo wa watoto watano sasa ni miongoni mwa wanawake wenye nguvu ya ushawishi Afrika Mashariki, huku akiwa na followers zaidi ya milioni 9.7 kwenye mtandao wa Instagram.

Read More
 CARDI B AJIWEKA PEMBENI NA MAMBO YA SIASA, ATAJA CHANZO

CARDI B AJIWEKA PEMBENI NA MAMBO YA SIASA, ATAJA CHANZO

Rapa Cardi B alikuwa anapaza sauti yake kwenye mijadala mbali mbali ya siasa za nchini Marekani, lakini kuna muda alikuwa hasikiki tena na watu kuanza kujiuliza maswali. Akijibu swali hilo ambalo aliulizwa na shabiki mmoja kupitia ukurasa wake wa Twitter, Cardi B amesema aliamua kukaa kimya kutokana na kunyanyaswa na kambi ya chama cha Republican ambacho kilikuwa kinaongozwa na Rais Donald Trump. Lakini pia, alikuwa akipokea ukosoaji mkubwa kutoka kwa watu ambao alikuwa akiwapigania kwenye siasa.

Read More
 LAVA LAVA ATANGAZA UJIO MPYA,OKTOBA 23

LAVA LAVA ATANGAZA UJIO MPYA,OKTOBA 23

Msanii wa bongofleva kutoka WCB, Lava Lava ametangaza kuja na project mpya, Oktoba 23, mwaka wa 2021. Lava Lava ambaye hivi karibuni amefuta picha zake zote kwenye ukurasa wake wa Instagram, amechapicha ujumbe kuhashiria Oktoba 23, mwaka huu atakuwa na kitu. Ikumbukwe mwimbaji huyo ambaye mwaka huu ameachia  EP iitwayo ‘Promise’, tayari alitangaza kukamilika kwa albamu yake. Mwaka huu wasanii wa WCB kama Rayvanny na Mbosso wameweza kutoa albamu zao na zinazidi kufanya vizuri.

Read More
 ANGELINA ATANGAZA KUACHA MUZIKI

ANGELINA ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Nyota wa muziki nchini uganda Angelina amedokeza mpango wa kuachana kabisa na masuala ya muziki. Angelina ameweka wazi hayo kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo amesema ataacha muziki mwaka wa 2022 baada ya kuachia project yake ya mwisho ambayo amekuwa akiifanyia kazi kwa muda. Kulingana na mrembo huyo baada ya kuacha muziki ataelekeza nguvu zake kwingine katika suala zima la kujitafutia riziki. Hata hivyo tweet yake hiyo haikukaa kwa muda kwenye ukurasa wake twitter kwani alikuja akaifuta baada ya kuchapisha. Angelina amekuwa kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda kwa muda wa miaka kumi na ametoa hits kali kama Go Down, Ghetto Lovin, Ronaldo na nyingine kibao.

Read More
 HAPPY C AMPA ZA USO WILLY PAUL KWA KUKOSA UBUNIFU

HAPPY C AMPA ZA USO WILLY PAUL KWA KUKOSA UBUNIFU

Mkali wa muziki nchini Happy Chondo maarufu kama Happy C kutoka lebo ya 001 Music amemtolea uvivu staa wa muziki nchini Willy Paul kwa madai ya kukosa ubunifu kwenye uandishi wa nyimbo zake. Happy C ametoa kauli hiyo kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram mara baada ya Willy Paul kuachia wimbo wake mpya uitwao “Ogopa Wasanii” ambao kwa mujibu wake amekopi idea ya msanii wa Bongofleva Diamond Platinumz. Kulingana na Happy C bosi huyo wa Saldido International anajishusha kwenye suala la uandishi wa nyimbo zake ikizingatiwa kuwa kuna wasanii wadogo na hodari ambao wana uwezo wa kuandika nyimbo zenye maudhui ya kumuelisha jamii. Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha “Mariana” ameenda mbali zaidi na kusema kwamba yupo tayari kumuandikia willy paul nyimbo kama ataendelea kutoa nyimbo ambazo hazina mashiko.

Read More
 SNOOP DOGG AINGIZA MABILLIONI YA FEDHA KUPITIA KAMPUNI YA BANGI

SNOOP DOGG AINGIZA MABILLIONI YA FEDHA KUPITIA KAMPUNI YA BANGI

Licha ya kuwa mtumiaji maarufu, Snoop Dogg ni mwekezaji kwenye biashara ya bangi. Kwa mujibu wa Bloomberg, kampuni ya Dutchie ambayo Snoop amewekeza pesa zake tangu mwaka 2018 imepanda thamani na kufikia takriban shillingi billioni 388. Kampuni hiyo iliyopo Oregon nchini Marekani ilianza kufanya vizuri kifedha miezi saba iliyopita kwa kutajwa kuwa na thamani ya shillingi billioni 188 na imeendelea kukua siku hadi siku tangu kuhalalishwa kwa zao la bangi kwenye maeneo mengi nchini Marekani. Ikumbukwe, mapema mwaka huu kampuni nyingine ya “Cannabinoid Technologies” ambayo Uncle Snoop amewekeza ilipanda thamani na kufikia shillingi billioni 7.5. Snoop pia ana bidhaa zake za bangi ziitwazo Leafs By Snoop.

Read More
 RAPA NA PRODYUZA KUTOKA KENYA BIG MIKE AFARIKI DUNIA

RAPA NA PRODYUZA KUTOKA KENYA BIG MIKE AFARIKI DUNIA

Member wa kundi la Nannoma ambalo lilianza muziki mwaka wa 1999  na kujipata umaarufu kwenye tasnia ya muziki nchini kupitia singo iitwayo Kila Saa, msanii Big Mike, amefariki dunia oktoba 17 mwaka huu. Big mike alikuwa rapa na mtayarishaji mashuhuri wa muziki, wakati muziki wa kisasi kipya nchini Kenya ulikuwa kwenye hatua za mwanzo kukua, enzi ambayo kulikuwa na makundi machache ya muziki wa hiphop. Kabla ya umauti kumkuta, Big mike alikuwa anajishughulisha na masuala ya kuzalisha kazi za wasanii na kipindi cha uhai wake alipata fursa ya kufanya kazi na wasanii tajika nchini akiwemo Abass kubaff, wyre na wengine wengi. Big Mike atakumbukwa kwenye kiwanda cha muziki nchini kama muasisi wa mashindano ya kurap ya Wapi Rap Battles ambayo yalikuwa yanawapa  wasanii chipukizi nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kupitia muziki wa hiphop.

Read More
 LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA RAPA KUTOKA MAREKANI LIL DURK

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA RAPA KUTOKA MAREKANI LIL DURK

Siku kama ya leo Oktoba 19 mwaka wa 1996 alizaliwa  staa wa muziki wa Hiphop na mwaandishi wa nyimbo kutoka nchini Marekani Lil Durk. Jina lake halisi ni Durk Derrick na alizaliwa huko Chicago Illinois nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 2009 lakini alikuja akapataa umaarufu mwaka wa 2011 baada ya kuachia ngoma zake mbili ambazo ni Sneak Dissin na Ima  Hitta zilizopokelewa kwa ukubwa nchini Marekani. Mwaka wa 2012 Lil Durk aliachia mixtape yake inayokwenda kwa jina la   Life Aaint No Joke chini ya lebo ya muziki ya OTF  ikafuatwa na mixtape yake iitwayo Signed To The Street ya mwaka wa 2013 ambayo ilitayarishwa na lebo ya muziki ya Def  Jam  Recordings. Mwaka wa 2014 Lil Durk aliachia mixtape nyingine iitwayo The Sequel to Signed to the Streets ikafuatwa na album yake ya kwanza ya mwaka wa 2015 iitwayo Remember My Name, album ambayo ilikuwa na jumla ya ngoma 10 za moto. Mwaka huo huo wa 2015 Lil Durk aliachia mixtape yake inayokwenda kwa jina la 300 days, 300 Nights ambayo ilikuwa ngoma kama My Beyonce ambayo iliweza kufikia viwango vya mauzo ya gold kwa kuuza zaidi ya nakala laki 5. Mwaka wa 2016 Lil Durk aliachia album yake ya pili iitwayo Lil Durk  2X ambayo ilikuwa na jumla ya ngoma 11 akiwa  amewashirikisha wasaani kama young thug,ty dolla sign na wengine kibao. Hata hivyo tangu Lil Durk aanze kujishughulisha na muziki wa hiphop nchini Marekani mwaka wa 2009 amefanikiwa kufanya jumla ya album tano za muziki,Mixtape 12,Singles 20 na album mbili iliyobeba nyimbo zilitoka pamoja na zile hazikutoka. Lil Durk kwa sasa amesainiwa na lebo ya muziki ya Def Jam Records lakini pia yupo chini ya record lebo  ya Coke Boys inayomilikiwa na rapa French Montana ambayo inafanya kazi pamoja na lebo yake ya muziki ya Only the Family.

Read More
 CHID BENZ AACHIA TRACKLIST YA “WA2 WANGU” ALBUM

CHID BENZ AACHIA TRACKLIST YA “WA2 WANGU” ALBUM

Rapa kutoka nchini Tanzania Chidi Benz amewapa mashabiki wake orodha ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya ya “Wa2 Wangu” anayoitarajia kuitoa hivi karibuni. Chid benz ambaye ni mshindi mara nne wa Kill Music Awards kupitia tuzo ya msanii Bora wa Hip Hop nchini tanzania, ameorodhesha jumla ya nyimbo 18 kutoka kwenye album hiyo, huku ikiwa na collabo 5 pekee,ambapo amewapa mashavu wasanii kama Badest 47, Brian Simba kusikika kwenye album hiyo. Hata hivyo, Chidi tayari ameshaachia nyimbo 6 kutoka kwenye album hiyo, ambazo ni Nahamia Bar, Jirani, Walete, One, King of the Jungle na Hilo Ngoma. Ikumbukwe kuwa, hii itakuwa ni album ya pili kutoka kwa mtu mzima Chidi Beenz baada ya Dar Es Salaam Stand Up ya mwaka wa 2010

Read More
 JOSE CHAMELEONE: SINA MPANGO WA KUREJEA TENA KWENYE SIASA

JOSE CHAMELEONE: SINA MPANGO WA KUREJEA TENA KWENYE SIASA

Bosi wa lebo ya muziki ya Leone Island msanii Jose Chameleone ameweka wazi kwamba hana mpango tena wa kuingia kwenye siasa. Chameleone amesema siasa inataka pesa nyingi sana na kwa mantiki hiyo itakuwa vigumu kwake kuwania wadhfa wowote wa kisiasa. Hata hivyo amesisitiza kwamba licha ya watu kutompigia kura kwa wingi kwenye uchaguzi mkuu uliopita nchini Uganda, anaamini hana vigezo vya kuwa kiongozi na ndio maana wananchi walimchagua mpinzani wake. Ikumbukwe Jose Chameolene alipoteza kwenye uchaguzi wa umeya wa Jiji la Kampala mapema mwaka huu na mpinzani wake Erias Lukwago.

Read More
 NYOTA NDOGO AINGIA UBIA WA KUFANYA KAZI NA KAMPUNI YA JOY MILLERS LIMITED.

NYOTA NDOGO AINGIA UBIA WA KUFANYA KAZI NA KAMPUNI YA JOY MILLERS LIMITED.

Staa wa muziki nchini Nyota Ndogo amelamba dili nono la kuwa balozi wa unga wa ugali wa Raha Premium. Nyota Ndogo ametengaza habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram huku akieleza kuwa ana furaha kujiunga na familia ya Raha Premium. Lakini pia ameishikuru uongozi wa kampuni ya Joy Miller Limited kwa kutambua nguvu yake na kuhamua kumpatia dili hilo ambalo litamjengea heshima. Nyota Ndogo sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za Raha Premium kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuongeza mauzo ya unga hiyo ya ugali. Hitmaker huyo wa “Watu na Viatu” anajunga na msanii Bahati pamoja mke wake Diana Marua ambao pia waliingia ubia wa kufanya kazi na kampuni ya Joy millers limited mwezi Agosti mwaka huu. Ikumbukwe nyota ndogo ni mmoja kati ya wasaani ambao wamewekeza kwenye biashara kuuza vyakula na amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kutangaza mgahawa wake ambao ameupa jina la  Nyota Ndogo jikoni.

Read More
 BURNA BOY AKAVA JARIDA LA ES MAGAZINE LA NCHINI UINGEREZA

BURNA BOY AKAVA JARIDA LA ES MAGAZINE LA NCHINI UINGEREZA

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria  Burna Boy ambaye anafanya vizuri kupitia kazi zake mbalimbali, ametokea mbele ya kava la Jarida la Es Magazine la nchini Uingereza. Jarida la Evening Standard Magazine ni jarida kutoka London, Uingereza ambalo hujihusisha kwa kutoa habari za burudani kutoka kwa mastaa wakubwa ulimwenguni. Kwenye Jarida hilo Burna Boy  amefunguka mengi kuhusiana na muziki wake, mpaka kufikia hapo alipo. Uwezo wake mkubwa wa kujaza kwenye Arena, dili mbalimbali alizozipata kama PEPSI, kukutana na mastaa wakubwa, kushiriki kwenye album za wasanii kutokea Marekani. Hata hivyo, Burna boy  anakuwa msanii wa tatu kutoka Afrika kupata nafasi ya kukava jarida la ES, mwaka 2019 WizKid alikava Jarida hilo na mwaka 2020 ikawa zamu ya Davido kutokea kwenye jarida hilo. Ikumbukwe, Burna Boy kupata nafasi ya kukava kwenye jarida hili kubwa ulimwenguni kunampa nafasi ya kuzingatiwa, kuongeza mashabiki na watu kupata nafasi ya kuweza kumfuatilia zaidi.

Read More