LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA MKALI WA RnB KUTOKA MAREKANI USHER

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 14, ALIZALIWA MKALI WA RnB KUTOKA MAREKANI USHER

Siku kama ya leo Oktoba 14 mwaka wa 1978 alizaliwa Staa wa muziki RnB kutoka nchini Marekani Usher. Jina lake halisi ni Usher Raymond IV na alizaliwa huko Dallas, Texas nchini na kukulia Atlanta, Georgia nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 1994 alipoachia album yake ya kwanza iitwayo Usher. Lakini mwaka wa 1997 ndipo Usher alipopata umaarufu baada ya kuichia albamu yake ya pili iitwayo MY WAY,ambayo ndani yake kulikuwa na wimbo uitwao NICE & SLOW ambao ulishika namba moja kwenye Billboard hot 100. Hakuishia hapo,albamu yake tatu ya mwaka wa 2001 iliyoitwa 8701 ilitoa wimbo ambao wengi leo tunaimfahamu kwa jina la U REMIND ME ambao nao ulishika namba moja pia kwenye Billboard hot 100. Mwaka 2004 alitoa albamu ya nne iliyoitwa CONFESSIONS albamu iliyouza zaidi  ya nakala million 10 kwa marekani pekee na kupewa hadhi ya viwango vya mauzo ya DIAMOND,ndani yake kulikuwa na vibao vikali kama YEAH,BURN na MY BOO. Mwaka 2008 usher alitoa albamu ya tano iitwyo HERE I STAND ndani kukiwa na hits kali kama LOVE IN THIS CLUB ambayo nayo ilishika namba moja kwenye chati ya Bllboard hot 100. Hata hivyo mpaka sasa usher ameshafanya jumla ya album 8 za muziki, EP 8, Singles 79 na album 10 za nyimbo zilizotoka pamoja na zile hazikutoka akiwa chini ya lebo ya muziki ya La Face,Arista, Jive na RCA Records. Kutokana na mafanikio ambayo aliyapata kwenye muziki wake nchini marekani Usher ameteuliwa kushiriki kwenye tuzo mbali mbali za muziki na ameshinda tuzo 8 za Grammy, 18 za Billboard music Awards, 34 za ASCAP Awards, 9 za Soul train music na nyinngine kibao Kando na muziki, usher ni mmiliki wa record lebo iitwayo vanity records na pia ameigiza kwenye filamu mbali mbali nchini marekani ikiwemo the Faculty ya mwaka wa 1998, Light it up ya mwaka wa 1999, Hustlers ya mwaka wa 2019 miongoni mwa nyingine kibao.

Read More
 LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 13, ALIZALIWA MKALI WA RnB NA HIPHOP KUTOKA MAREKANI ASHANTI

LEO KATIKA HISTORIA OKTOBA 13, ALIZALIWA MKALI WA RnB NA HIPHOP KUTOKA MAREKANI ASHANTI

Siku kama ya leo Oktoba 13 mwaka wa 1980 alizaliwa staa wa muziki wa RnB na Hihop kutoka nchini Marekani Ashanti.   Jina lake halisi ni Ashanti Shequoiya Douglas na alizaliwa huko Glen Cove, New York nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 2001 kipaji chake kilipotambuliwa na prodyuza mkali kutoka marekan Irv Gotti ambaye alimshirikisha kwenye wimbo uitwao Whats Luv  wake Fat Joe na always on time wa Jah Rule.   Kutokana na uwezo ambao alionyesha kwenye collabo hizo Ashanti alisaini mkataba wa kufanya kazi na lebo ya muziki Murder Inc ambayo ilisimamia kazi zote za album yake ya kwanza iitwayo Eponymous ya mwaka wa 2002,album ambayo iliweza kufikia viwango vya mauzo ya Platinum kwa kuuza zaidi ya nakala milllioni 6 nchini Marekani.   Mwaka wa 2003 ashantia aliachia album yake ya pili iiitwayo Chapter II ambayo ilifanikiwa kushika namba moja kwenye chati ya billboard 200 lakini pia ikafanikiwa kufikia viwango vya mauzo ya platinum kwa kuuza nakala millioni 1.5.   Mwaka huo huo Ashantia aliachia ya tatu iiitwayo Christmas ikafuatwa na Concrete Rose ya 2004, Declaration ya mwaka wa 2008 na Braveheart ya 2014 album ambazo hazikufanya vizuri kwenye soko la muziki ikilinganishwa na album zake za awali.   Hata hivyo mpaka sasa ashanti ameshafanya jumla album 6 za muziki, singles 24,  na video 21 za muziki wake akiwa chini lebo ya muziki  Murder Inc,Def Jam na Motown.   Kutokana na mafanikio ambayo aliyapata kwenye muziki wake nchini Marekani Ashanti ameteuliwa kushiriki kwenye tuzo 89 za muziki na ameshinda tuzo 35 ikiwemo  8 za Billboard Music Awards, 3 za American Music,moja ya Grammy na nyinngine kibao.   Kando na muziki, Ashanti ni muigizaji ana ameshiriki kwenye filamu nyingini nchini marekani ikiwemo  Coach Carter,John  Tucker Must Die na nyingine kibao.

Read More
 “MADE IN LAGOS” YAFIKISHA ZAIDI YA STREAMS BILLIONI MOJA

“MADE IN LAGOS” YAFIKISHA ZAIDI YA STREAMS BILLIONI MOJA

Album ya msanii WizKid kutoka Nigeria, “Made in Lagos” Deluxe Edition iliyotoka Agosti 27 mwaka huu yenye hitsong kama Essence Remix, imefanikiwa kufikisha jumla ya streams Bilioni Moja. Made in Lagos” imefikisha jumla ya streams hizo ikiwa ni mjumuisho wa streams zote za (Deluxe Edition) katika Platform mbalimbali za muziki duniani kama Apple Music (millioni 322.75), Spotify (millioni 229.33), Youtube (millioni 227.82), Audiomack (millioni 178.25), Boomplay (millioni 40.17) na Pandora (millioni 20.1) WizKid ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake ya kimuziki ya “Made In Lagos Tour”, aliyoianza Septemba 10 mwaka huu, anaendelea pia kufanya vizuri kwa kupata idadi kubwa ya mashabiki kwenye show zake.

Read More
 AZIZ AZION MBIONI KUJA NA ONE DECADE CONCERT

AZIZ AZION MBIONI KUJA NA ONE DECADE CONCERT

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Aziz Azion, ametangaza kwamba  ana mpango wa kuja na tamasha la muziki la One Decade Concert kuadhimisha miaka 10 ya uwepo wake kwenye muziki baada ya katazo la kufanya matamasha ya muziki litakapoondolewa nchini uganda. Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 37 amedokeza kuwa kiingilio cha tamasha hilo litakuwa shillingi laki tano za kenya katika sehemu ambayo ataweka wazi hivi karibuni baada kukamilisha taratibu za kuandaa tamasha hilo. Hitmaker huyo wa My Oxygen amesema alipaswa kufanya tamasha hilo mwaka wa 2019 lakini kwa sababu ya maswala kadhaa ambayo yalikuywa nje ya uwezo wake, alilazimika kuahirisha hadi  mwaka wa 2020. Mwaka wa 2020 bado, tamasha hilo lilifeli kufanyika kufuatia kuzuka kwa janga la Corona ambayo ililemaza shughuli zote za kibiashara ulimwenguni kote.

Read More
 PROFESSOR JAY ATANGAZA UJIO WA EP MPYA

PROFESSOR JAY ATANGAZA UJIO WA EP MPYA

Staa mkongwe wa muziki wa rap nchini Tanzania, Professor Jay ameweka wazi kuachia EP mpya yenye jumla ya ngoma 5 hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa instagram Professa Jay ameandika ujumbe unaosomeka “Badala ya kuwapa chakula cha ubongo kwa single moja naona kama niwape chakula cha EP ya nyimbo 5 au mnasemaje Maboss wangu” Professa Jay amebainisha hilo ikiwa ni takribani miezi 6 imepita tangu alipoachia hitsong yake iitwayo “Utanambia Nini”.

Read More
 VIDEO ZA OTILE BROWN ZARUDI YOUTUBE

VIDEO ZA OTILE BROWN ZARUDI YOUTUBE

Hatimaye video za staa wa muziki nchini Otile Brown zimerudi youtube baada ya kuondolewa kwa siku kadhaa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram staa huyo amewajuza mashabiki zake kuwa video hizo zimerudi rasmi baada ya kuondolewa youtube huku akiwashukuru mashabiki wake kwa kumuvumilia yeye pamoja na timu yake wakati walipokuwa wanafuatilia suala la kurejesha nyimbo zake kwenye mtandao huo. Such kinda love, Dusuma, Chaguo la moyo wangu, Regina,Aaiyana ni kati ya video za nyimbo za Otile Brown ambazo ziliondolewa kwenye akaunti yake ya youtube. Kurejeshwa kwa nyimbo hizo kumekuja siku chache baada ya staa huyo kutoa taarifa rasmi, akielezea utata unaozingira suala la kufutwa kwa nyimbo zake. Hata hivyo otile brown hajaweka wazi sababu ya kuondolewa kwa video hizo

Read More
 INSTAGRAM KULETA FEATURE MAALUM YA KUTOA TAARIFA ZA MATATIZO YA KIUFUNDI YANAYOJITEKEZA

INSTAGRAM KULETA FEATURE MAALUM YA KUTOA TAARIFA ZA MATATIZO YA KIUFUNDI YANAYOJITEKEZA

Kufuatia taharuki ambayo imekuwa ikijitokeza kwa watumiaji pale ambapo mtandao wa Instagram unakuwa umekumbwa na matatizo ya kiufundi, sasa mtandao huo umeanza majaribio ya ‘feature’ mpya ambayo itakuwa ikitoa taarifa pale linapojitokeza tatizo hilo. Taarifa hiyo itakuwa ikitokea kwa mfumo wa notification kwenye ukurasa wa mtumiaji wa mtandao huo kumjulisha kuwa limejitokeza tatizo la kiufundi.

Read More
 OS SSUNA AFUNGUKA SABABU ZA KUBADILI DINI

OS SSUNA AFUNGUKA SABABU ZA KUBADILI DINI

Bosi wa lebo ya muziki ya White House Music Entertainment  Emmanuel Suna maarufu kama Os Suna amefunguka sababu za kubadilisha dini kutoka ukristo kwenda uislam. Akiwa kwenye moja ya interview Suna amesema alipata wito wa kubadili dini kutoka kwa mwenyezi mungu na hakuna jinsi hangezuia jambo hilo kufanyika. Hitmaker huyo wa Siri Gambler amekanusha madai yanayotembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa alibadili dini na kuwa muislamu kwa sababu alilazimishwa na mwanamke aliyetaka kumuoa kipindi hicho. Suna amesema wakati aliacha dini ya ukristo alirudi kwa wana familia wake na kuwaomba msamaha kwa hatua ya kubadili dini bila ya kuwataarifu. Hata hivyo amejinadi kwa kusema kwamba kipindi anakumbatia dini ya kiislam alikuwa na mafanikio makubwa kimuziki kwani nyimbo zake zilifanya vizuri kwenye chati mbali mbali nchini uganda.

Read More
 HANSTONE AACHIA RASMI THE AMAZING EP

HANSTONE AACHIA RASMI THE AMAZING EP

Msanii wa muziki wa kizazi kipya  nchini Tanzania Hassan Ramadhani Masanja maarufu kama ‘Hanstone’ ameachia EP yake mpya aliyoipa jina “The Amaizing” yenye jumla ya nyimbo 7. Mkali huyo ambaye alikuwa akihusishwa kuwa ni msanii mpya ajae kutoka lebo ya WCB, ameachia EP hiyo nje ya WCB. “The Amaizing EP” tayari inapatikana kwenye mitandao mbalimbali ya ku-stream muziki duniani. Hanstone ni mtoto wa pekee wa marehemu Banza Stone, alijipatia umaarufu kupitia ngoma ya Iokote aliyoshirikishwa na Maua Sama mwaka wa 2018.    

Read More
 MENEJA WA OTILE BROWN AFUNGUKA JUU YA KUFUTWA KWA NYIMBO ZA STAA HUYO YOUTUBE

MENEJA WA OTILE BROWN AFUNGUKA JUU YA KUFUTWA KWA NYIMBO ZA STAA HUYO YOUTUBE

Meneja wa otile brown Noriega amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kufutwa kwa nyimbo za msanii huyo kwenye mtandao wa youtube. Akiwa kwenye moja ya interview meneja huyo amesema kama uongozi wa otile brown wameshangazwa na hatua ya nyimbo za staa huyo kufutwa kwenye mtandao wa youtube na aliyezi-upload ambapo ameahidi kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu ili kuhakikisha waliohusika wanakabiliwa kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo Noriega amepuzilia mbali madai yanayotembea mitandaoni kuwa otile brown anatumia suala la nyimbo zake kufutwa kwenye mtandao wa youtube kuupromote kazi yake mpya kwa kusema kwamba suala hilo sio kiki kama inavyodaiwa kwani otile brown huwa hatumii kiki kutangaza muziki wake. Nyimbo ambazo zilifutwa kwenye channel ya youtube ya msanii huyo ni pamoja na Dusuma, Such Kinda of love, Chaguo la moyo wangu, Aiyana na nyingine nyingi.

Read More
 MATATA WAACHIA RASMI UNAWARE EP

MATATA WAACHIA RASMI UNAWARE EP

Kundi la muziki la Matata limeachi rasmi EP yao mpya inayokwenda kwa jina la Unaware. Ep hiyo ina jumla ya mikwaju nne ya moto huku zote zikiwa collabo ambazo wamezifanya na wasanii wa sol generation nviiri the storyteller na Bensoul. Unaware EP ina nyimbo kama Matatu, Pombe na kizungu nyingi, Unaware na tulia nikupange ambapo kwa sasa inapatikana exclusive kupitia digital platforms mbalimbali za kupakulia na kusikilizia muziki duniani. Ikumbukwe kabla ya ujio wa EP hiyo, matata walitusanua kwamba wapo kwenye maandalizi ya album yao mpya na kwanza tangu waanze safari yao ya muziki.

Read More
 KENRAZY KUACHIA ALBUM YAKE MPYA KESHO

KENRAZY KUACHIA ALBUM YAKE MPYA KESHO

Hatimaye nyota wa muziki nchini Kenrazy ameweka hadharani jina na cover rasmi la album yake mpya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kenrazy ameshare artwork ya album yake mpya ambapo amesema album yake hiyo itaitwa Son of God. Hitmaker huyo wa mbilikimo mkora amesema album yake mpya ina jumla ya mikwaju 20 za moto na itaingia sokoni oktoba 13 mwaka huu. Album hiyo ilipaswa kutoka Septemba 27 mwaka lakini kenrazy aliahirishwa kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake. Hii itakuwa ni album ya tatu kutoka kwa mtu mzima kenrazy baada ya Ti-chi ya mwaka wa 2008 na Get it Right from Kenrazy ya mwaka wa 2011.

Read More