Jay Melody Amtishia Mtu Aliyemvunjia Heshima: Siku Moja Utaishia Jela!”

Jay Melody Amtishia Mtu Aliyemvunjia Heshima: Siku Moja Utaishia Jela!”

Msanii wa Bongo Fleva, Jay Melody, ameacha mashabiki wake wakibaki na maswali baada ya kuandika ujumbe wa mafumbo kwenye Insta Story yake, hatua iliyozua mjadala mkubwa mitandaoni. Katika ujumbe huo, Jay Melody ameandika kwa mtindo wa onyo akimtahadharisha mtu ambaye hakumtaja moja kwa moja kwamba endapo ataendelea na tabia zake za usela anaweza kujikuta matatani na hata jela. Hitmaker huyo wa Mtoto ameongeza kuwa mtu huyo mara kwa mara huonekana akileta miyeyusho na kushindwa kuaminika, hali inayomfanya aonekane kama chizi machoni pa watu. Jay Melody pia amesisitiza kwamba siku moja mtu huyo ataingia katika matatizo makubwa na kuishia kujuta kwa matendo yake. Ujumbe huo uliachwa bila maelezo zaidi, jambo lililoacha mashabiki wake wakijiuliza kama msanii huyo alikuwa anamwandikia mtu maalum au alikuwa akizungumza kwa ujumla kuhusu maisha na tabia za baadhi ya watu. Mashabiki kadhaa mitandaoni wameonyesha hisia tofauti, wengine wakichukulia kama ujumbe wa mafundisho, huku wengine wakihisi huenda ni dongo lililotumwa kwa mtu maarufu.

Read More
 Size 8: Nilitoka Mazingira ya Kishetani Kabla ya Kuokoka

Size 8: Nilitoka Mazingira ya Kishetani Kabla ya Kuokoka

Msanii wa injili kutoka Kenya, Size 8, amefunguka kuhusu maisha yake ya awali akisema alitoka kwenye mazingira ya kishetani. Akipiga stori na podcast ya Mwakideu Live, amesema anaamini kuwa hali hiyo ndiyo iliyochangia kwa kiasi kikubwa kupaa kwake kwa kasi kwenye muziki wa secular na kupata umaarufu mkubwa katika kipindi kifupi. Size 8 ambaye pia ni kasisi, ameeleza kwamba ingawa alipata nafasi na mafanikio ya haraka katika tasnia ya burudani, hakuwahi kufurahia amani ya kweli moyoni mwake. Kwa mtazamo wake, nguvu alizokuwa akizipata zilikuwa za giza na ndizo zilizomsukuma mbele kwa njia isiyo ya kawaida. Baada ya kuokoka na kugeukia muziki wa injili, Size 8 sasa anasema hadithi yake ni ushuhuda wa jinsi Mungu anavyoweza kubadilisha maisha ya mtu yeyote. Anatumia mfano wake kuwatia moyo watu wanaopitia changamoto kuamini kwamba mabadiliko ni kitu cha kweli na kinachowezekana.

Read More
 Brown Mauzo Atangaza Kugombea Kiti cha MCA Kileleshwa 2027

Brown Mauzo Atangaza Kugombea Kiti cha MCA Kileleshwa 2027

Msanii Brown Mauzo, ametangaza rasmi kwamba atawania kiti cha Mjumbe wa Wadi (MCA) wa Kileleshwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Kupitia ujumbe wake kwa wakazi wa Kileleshwa, Mauzo amesema kuwa uamuzi wake umetokana na maombi na ushauri kutoka kwa jamii ambayo amekuwa akiishi nayo. Amesisitiza kuwa sauti ya wananchi wa Kileleshwa ndio imekuwa ikimpa motisha ya kuingia katika siasa. Mauzo ambaye pia ni mume wa zamani wa socialite Vera Sidika, ameongeza kuwa yuko tayari kushirikiana na wakazi wa Kileleshwa kubadilisha ward hiyo na kuboresha maisha ya watu. Hata hivyo, ameshukuru kwa imani na kuungwa mkono na wananchi, akiahidi kuendesha uongozi wa karibu na wananchi na unaolenga maendeleo.

Read More
 Thee Pluto Akana Madai ya Kudate Mwanamke wa Kisomali

Thee Pluto Akana Madai ya Kudate Mwanamke wa Kisomali

YouTuber maarufu wa Kenya, Thee Pluto, amejitokeza kufafanua madai yaliyosambaa mitandaoni kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke wa Kisomali. Akizungumza kupitia mitandao yake ya kijamii, Thee Pluto amesema kuwa si kila mtu anayepigwa naye picha au kuonekana naye hadharani ni mpenzi wake. Amesisitiza kuwa uvumi wa aina hiyo ni wa kupotosha na umekuwa ukiwaweka watu katika hali ya mkanganyiko kuhusu maisha yake ya kibinafsi. Thee Pluto, ambaye ni maarufu kwa majaribio yake ya uaminifu (loyalty tests) mitandaoni, ameomba mashabiki na wafuasi wake kutofautisha kati ya mahusiano ya kirafiki na kimapenzi, akiongeza kwamba si kila anayeonekana naye ana uhusiano wa kindoa naye.

Read More
 Lillian Ng’ang’a Awahimiza Wanawake Kuangalia Ubora wa Wigs Wazotumia

Lillian Ng’ang’a Awahimiza Wanawake Kuangalia Ubora wa Wigs Wazotumia

Mke wa Msanii Juliani, Lillian Ng’ang’a, ameibua mjadala mitandaoni baada ya kutoa ushauri kwa wanawake kuhusiana na matumizi ya wigs. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Lillian amesema wanawake wanapaswa kupunguza matumizi ya wigs, kwani wigs zilizowekwa vibaya zinaweza kuharibu mwonekano mzuri wa make up na mavazi. Mwanamama huyo ameeleza kuwa make up nzuri na vazi zuri vinastahili kuendana na nywele zilizotunzwa au wig iliyowekwa kitaalamu, kwani muonekano wa nywele ni sehemu muhimu ya taswira ya mwanamke. Kauli yake imezua mjadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakikubaliana naye wakisema mara nyingi wigs zisizo bora huondoa mvuto, huku wengine wakimtetea wakidai kila mwanamke ana uhuru wa kujionyesha kwa namna anavyotaka.

Read More
 Msanii wa Elani, Maureen Kunga, Aachia Kazi Mpya kama Msanii wa Kujitegemea

Msanii wa Elani, Maureen Kunga, Aachia Kazi Mpya kama Msanii wa Kujitegemea

Mwanamuziki wa Kenya na mshirika wa kundi maarufu la Elani, Maureen Kunga, ametangaza rasmi kuanza safari yake ya muziki kama msanii wa kujitegemea kupitia wimbo wake wa kwanza aliouachia kwa jina “Majaliwa.” Wimbo huo, ambao tayari umeanza kuvutia mashabiki mtandaoni, ni utunzi wa kipekee wenye kugusa hisia, kwani Kunga ameuandika kama heshima na shukrani kwa mama yake. Akizungumzia kazi hiyo mpya, ameeleza kwamba “Majaliwa” si tu wimbo wa mapenzi ya kifamilia, bali pia ni hadithi ya baraka na imani katika safari ya maisha. Maureen, ambaye amejulikana kwa sauti yake ya kipekee ndani ya Elani, amesema kuwa kuanza kwake kazi ya solo hakumaanishi mwisho wa kundi hilo, bali ni nafasi yake binafsi ya kuchunguza mitindo mipya ya muziki na kueleza hadithi zake binafsi. Mashabiki na wadau wa muziki wamepongeza hatua hiyo, wakimtaja Maureen kama msanii mwenye uwezo mkubwa wa kusimama peke yake katika tasnia ya muziki wa Afrika Mashariki.

Read More
 Commentator 254 Akataa Kufichua Sababu za Kuachana na Moureen Ngigi

Commentator 254 Akataa Kufichua Sababu za Kuachana na Moureen Ngigi

Content creator kutoka Kenya, Commentator 254, amekataa kufichua chanzo cha kuachana na mama ya mtoto wake Moureen Ngigi baada ya kukaa pamoja kwa muda mrefu. Akiwa kwenye channel yake ya YouTube, ameeleza kuwa ingawa amepokea maswali mengi kutoka kwa mashabiki wake kuhusu kilichosababisha kuvunjika kwa penzi lao baada ya miaka mitatu, hatatoa maelezo ya kina bila uwepo wa Moureen. Kauli hiyo imeibua hisia mseto mitandaoni, mashabiki wengine wakihisi kuna zaidi ya kile kinachosemwa, huku wengine wakisifu uamuzi wake wa kuheshimu faragha ya aliyekuwa mpenzi wake. Commentator 254 na Moureen Ngigi walikuwa moja ya wanandoa maarufu mtandaoni, wakijulikana kwa kushirikiana mara kwa mara kwenye maudhui ya YouTube na mitandao ya kijamii, hali iliyowafanya kujizolea mashabiki wengi.

Read More
 Spotify Ya Bure Yapanua Uwezo wa Watumiaji

Spotify Ya Bure Yapanua Uwezo wa Watumiaji

Watumiaji wa Spotify ambao hawalipi ada ya kila mwezi sasa wamepata habari njema baada ya kampuni hiyo kupanua huduma zake. Kwa sasa, watumiaji wa Spotify ya Bure wanaweza kucheza nyimbo wanazozitaka moja kwa moja kupitia playlists, albums, na hata kwenye profiles za wasanii. Hapo awali, mfumo wa bure ulikuwa na vizuizi kadhaa ambavyo vilikuwa vikiwalazimisha watumiaji kusikiliza nyimbo kwa mtindo wa “shuffle” pekee, na hivyo kuwanyima uhuru wa kuchagua moja kwa moja wimbo wanaoutaka. Hatua hii mpya inatazamwa kama jitihada za Spotify kuongeza idadi ya watumiaji wake na kuwapa uzoefu bora zaidi, huku ikishindana na majukwaa mengine ya muziki kama vile Apple Music, YouTube Music na Boomplay. Wataalamu wa teknolojia wanasema mabadiliko haya yanaweza kuongeza mvuto wa watumiaji wapya na kuwashawishi baadaye kujiunga na mpango wa kulipia ili kufurahia huduma za ziada kama vile kusikiliza muziki bila matangazo na kupakua nyimbo. Spotify, ambayo kwa sasa ni moja ya majukwaa makubwa zaidi ya kusikiliza muziki duniani, inaendelea kuboresha huduma zake ili kuendana na mahitaji ya wapenzi wa muziki katika kila kona ya dunia

Read More
 Tokyo 2025: Kipyegon Atetea Ubingwa, Dorcus Ewoi Aipatia Kenya Fedha

Tokyo 2025: Kipyegon Atetea Ubingwa, Dorcus Ewoi Aipatia Kenya Fedha

Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya dunia Faith Kipyegon aliendeleza utawala wake katika mbio za mita 1500, aliposhinda taji yake ya nne mfululizo ya dunia katika siku ya nne ya Mashindano ya Riadha ya Dunia jijini Tokyo Japan. Kipyegon ambaye pia ni bingwa mara tatu wa Olimpiki alitumia muda wa dakika 3 na sekunde 52.15 na kujiongeza taji nyingine ya dunia. Alimaliza mbele ya mwenzake Dorcus Ewoi, ambaye alitumia muda wake bora wa dakika 3 na sekunde 54.92 kunyakua fedha, na Jess Hull wa Australia, aliyenyakua shaba kwa dakika 3 na sekunde 55.16. Kipyegon sasa mwanamke wa pili kushinda taji nne ya dunia katika mbio moja baada ya Shelly-Ann Fraser-Pryce ambaye ameshinda taji tano ya mbio za mita 100. Nelly Chepchirchir alimaliza wa nne kwa dakika 3 sekunde 55.25. Wakati huo huo, matumaini ya Kenya ya kunyakua medali zaidi katika Mashindano ya Riadha ya Dunia yaliboreshwa baada ya bingwa wa Olimpiki Emmanuel Wanyonyi na Kelvin Kimtai kufuzu kwa mbio za nusu-fainali ya mbio za mita 800. Kwa sasa Kenya inashikiliaa nafasi ya pili kwenye jedwali ya medali ikiwa na medali tano, 3 za dhahabu na moja ya fedha, nyuma ya Marekani, ambayo inaongoza kwa jumla ya nishani nane, zikiwemo sita za dhahabu.

Read More
 Willy Paul Ashtumiwa na VJ Patelo kwa Kukaidi Makubaliano ya Malipo

Willy Paul Ashtumiwa na VJ Patelo kwa Kukaidi Makubaliano ya Malipo

Msanii wa Kenya VJ Patelo ameibuka na lawama nzito dhidi ya msanii Willy Paul kwa madai ya kutomlipa baada ya kumshirikisha kwenye video yake mpya ya muziki. Inadaiwa kuwa kabla ya kurekodi, Willy Paul alimuahidi Patelo mafuta ya gari pamoja na kifuta jasho, lakini baada ya kufika kwenye video shoot akiwa na mkewe Diana, msanii huyo alianza kumpuuza na kutojibu simu zake. Patelo amesema vitendo vya aina hiyo vinachangia kudidimiza muziki wa Kenya na kupelekea mashabiki wengi kugeukia muziki wa Tanzania. Kulingana naye, wasanii wa Tanzania wanashinda kwenye chati za muziki nchini Kenya kwa sababu ya nidhamu na uwajibikaji, jambo ambalo wasanii wa Kenya bado wanakosa kuzingatia. Ameonya kuwa hana muda wa kushirikiana na wasanii wasioweza kumlipa ipasavyo na amesisitiza kwamba kazi yake ina thamani inayopaswa kulipwa kwa heshima. Aidha, amewataka wasanii wenzake kuacha tabia ya kutothamini washiriki wanaowaunga mkono katika kazi zao. Mpaka sasa, Willy Paul hajajibu hadharani madai yaliyotolewa dhidi yake, na mjadala kuhusu suala hili unaendelea kushika kasi miongoni mwa mashabiki wa muziki.

Read More
 KRG Afichua Madhaifu ya Mfumo wa Ulipaji Mirahaba kwa Wasanii Kenya

KRG Afichua Madhaifu ya Mfumo wa Ulipaji Mirahaba kwa Wasanii Kenya

Msanii aliyegeukia biashara kutoka Kenya, KRG the Don, amefichua madhaifu ya mfumo wa ulipaji mirahaba kwa wasanii wa Kenya baada ya kuonesha kiasi cha pesa alicholipwa kama royalty za muziki wake na Chama cha Haki za Wasanii wa Utumbuizaji Nchini Kenya (PRISK) Kupitia ukurasa wake wa Instagram stories, KRG alionesha ujumbe wa M-PESA ikibainisha kuwa alipokea KSh 3,214 pekee kama malipo ya mwaka mzima. Akiwa na kejeli, alieleza kuwa hiyo ndiyo mshahara wa mwaka mzima anayopokea kama msanii nchini Kenya, jambo lililozua mjadala mitandaoni. Kauli hiyo imeibua maswali mapya kuhusu mfumo wa ulipaji wa wasanii nchini Kenya, ambapo mashabiki na wanamuziki kadhaa wamekuwa wakilalamikia malipo duni licha ya kazi zao kuchezwa mara kwa mara kwenye redio, televisheni na majukwaa ya kidijitali. KRG, anayejulikana kwa maisha ya kifahari na uwekezaji katika biashara, alitumia kisa hicho kuonesha changamoto kubwa zinazowakabili wasanii wengi nchini katika kupata fidia stahiki kutoka kwa mashirika ya haki miliki.

Read More
 Stevo Simple Boy Ampeleka Mpenzi Wake Mjamzito Likizo Maalum Diani

Stevo Simple Boy Ampeleka Mpenzi Wake Mjamzito Likizo Maalum Diani

Msanii Stevo Simple Boy, ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho baada ya kufanikisha hatua ya kuruka kwa ndege kwa mara ya kwanza. Safari hiyo haikuwa ya kawaida, kwani alichagua kumpeleka mpenzi wake mjamzito kwenye likizo maalum huko Diani. Kupitia mitandao ya kijamii, Stevo alishiriki picha na video wakila bata, wakiburudika katika mandhari mazuri ya ufukweni huku wakionesha furaha na mapenzi ya dhati. Wawili hao walionekana wakifurahia chakula, vinywaji, na wakishikana mikono wakiwa ufukweni, huku wakifurahia mandhari ya bahari na upepo mwanana wa Diani. Furaha ya Stevo na mkewe imeibua mjadala mtandaoni, mashabiki wengi wakimpongeza kwa kuthamini mpenzi wake mjamzito na kuchukua muda wa kuonyesha heshima na mapenzi mbele ya umma. Wengine walieleza kuwa ni jambo la kutia moyo kuona msanii anayekulia mitaani sasa akifikia hatua ya kuonja raha ya maisha kupitia bidii yake ya muziki.

Read More